Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

TIGO YADHAMINI WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO KUUZA BIDHAA COCO BEACH KILA MWEZI

$
0
0
 Meneja Mawasiliano wa Tigo Bw. John Wanyancha (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo kuhusu udhamini wa gulio la wafanyabiashara kutoka Kariakoo liitwalo 'Kariakoo at Coco Beach' litakalofanyika kila mwisho wa mwezi kuanzia wikiendi hii ya 29-30 Machi 2014 katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Miradi kutoka Hazina Capital, Bi. Rachael Ndauka, ambao ni waandaji wa gulio hilo.
Meneja wa Miradi kutoka Hazina Capital, Bi. Rachael Ndauka, ambao ni waandaji wa gulio hilo akizungumza na waandishi wa habari mapema leo. Mpaka sasa wafanyabiashara zaidi ya 50 wameweza kujiandikisha katika maonyesho hayo yatakayofanyika 29-30 Machi 2014 kuanzia asubuhi mpaka saa 12 katika fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam.
---
Tigo Tanzania leo imetangaza udhamini wake kwa maonyesho ya biashara yajulikanayo kama ‘Kariakoo Coco Beach Shopping Festival’ yenye malengo ya kuinua biashara za wafanyabiashara kutoka Kariakoo.

Akitangaza udhamini huo kwa waandishi wa habari kutoka ukumbi wa Coco Beach jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha, alisema maonyesho hayo ambayo yatafanyika kila mwisho wa mwezi yana malengo yakuleta bidhaa zenye gharama nafuu kutoka Kariakoo mpaka ufukwe wa bahari wa Coco kwa ajili ya kuwaondolea wateja usumbufu wa kwenda mpaka mjini na kero ya msongamano wanayoipata wakiwa huko.

“Ukiondoa mazingira mazuri ambayo maonyesho haya yatawapatia wateja, pia tunaamini ya kwamba kupitia maonyesho haya wafanyabiashara wa kati na wadogo wote watafaidika na kutokana na wateja watakaokuja kununua bidhaa zao, hivyo kuwasaidia kuongeza mauzo yao na hatimaye kukuza biashara zao,” alisema Wanyancha.

Wanyancha aliendelea kusema kwamba wauzaji na wanunuzi watapata urahisi wa kuuza au kulipia bidhaa na huduma mbali mbali kupitia Tigo Pesa na kwa gharama ile ile ya bila makato yoyote.

Kutokana na maelezo ya waandaji wa maonyesho hayo, Hazina Capital, uzinduzi utafanyika Jumamosi na Jumapili wikendi ijayo ya tarehe 29 na 30 Machi 2014, na kufuatiwa na maonyesho kama hayo yatakayofanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi.

“Zaidi ya wafanyabiashara 50 wamiliki wa biashara mbali mbali wamejisajili kushiriki mpaka sasa. Mbali na mazingira yasiyokuwa na bughudha kwa wauzaji na wanunuzi, tunatarajia wateja kufika na kukuta bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na kwa gharama nafuu,” alisema Rachel Ndauka kutoka Hazina Capital.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>