Kijana akiendelea na kazi yake ya unyonyoaji wa kuku.
Kuku wakisubiri kunyonyolewa.
Muonekano wa ndani ya soko.
Eneo la ovyo lililohifadhiwa kuku.
Ndoo mbovu ndizo hutumika katika kuchotea maji.
Vijana wakiendelea na kazi yao.
Sehemu ya kuhifadhia kuku ni chafu.
Kijana akiendelea na kazi zake…
Kijana huyu akijifuta uchafu kwa kutumia nguo aliyovaa huku akiendelea na kazi jambo ambalo si salama Habari/Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imetakiwa kuweka kipaumbele katika soko la Kinondoni Manyanya ili kuboresha afya za watumiaji.
Utafiti uliofanywa na Kajunason Blog ndani ya soko hilo, ulionyesha soko limekuwa chafu hasa wakati wa mvua na upande wa machinjio ya kuku.
Ukiangalia jinsi wale wachinjaji walivyovaa nguo zao hakika ni watu wachache wanaoweza kwenda kupata huduma japo kuku wanazochinja hupelekwa masupermakert.
Katika mahojiano na wananchi wachache waliokuwa eneo la soko hilo walilalamika kwa kusema, ‘Kiukweli soko limekuwa ni kichefu chefu japo hakuna jinsi ni lazima uje kununua mahitaji, binafsi sitamani kwenda upande wa machinjio maana sitaweza hata kumla huyo kuku bora nimkute tayari dukani nitanunua,” alisema mwananchi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe.