MKurugenzi wa Msama Promotions Ltd, ambao ndio waandaji wa tamasha la krismass na Pasaka B wa. Alex Msama amesema kuwa maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar mnamo April, 20 mwaka huu yamekamilika.
Aakizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar leo katika viwanja vya Karimjee, Msama amebainisha kuwa kila kitu kimekwishakamilika, wakiwemo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza siku hiyo, aidha amesema kuwa pamoja na wanamuziki wa nyumbani kushiriki tamasha hilo, pia kutakuwepo na wanamuziki wengine kutoka nje ya nchi.
Msama amesema kuwa katika kuhakikisha washabiki na watazamaji wanalifurahia tamasha hilo lenye kujaa nyimbo za kumsifu na kumuabudu Mungu, kutakuwepo na wanamuziki nyota kutoka nchini Afrika kusini, ambao watalipamba vyema tamasha hilo.
"Katika tamasha hilo kutakuwepo na wanamuziki kutoka Afrika kusini,akiwemo Rebecca Malope mbaye atatumbuiza kwenye hitimisho la tamasha hilo jijini Mwanza, pamoja na Mwanamuziki Kekeletso Phoofolo ambaye atatumbuiza hapa jijini Dar,wakiwemo na wanamuziki wengine wengi wa hapa nyumbani kama vile Rose Muhando,Upendo Nkone, Bon Mwaitege,John Lisssu, Upendo Kilahilo na wengineo wengi" alisema Msama.
Msama amesema kuwa Tamasha hilo litazunguka mikoa isiyopungua tisa,ameongeza kuwa pia katika kuisadia jamii, Kamati ya maandalizi ya tamasha la pasaka itaandaa fungu Maalum kwa ajili ya kuwapa Mayatima na watoto waishio katika mazingira magumu.
Sisi kama Msama Promotions tutaandaa fungu rasmi kwa ajili ya kusaidia watoto Yatima,lengo likiwa ni kuwapa fungu maalum kwa ajili ya kujitegemea, mfano kuwaanzishia biashara ambayo itakuwa endelevu na yenye kuwasaidia badala ya kupewa vitu vya kupita tu kila wakati" alisema Msama.
Amesema kuwa watatoa fungu maalum kwa kila kituo kwa kuwapa kiasi cha shilingi Milioni tano kwa kila kituo ili kujiendeleza zaidi,na tunalitoa kutokana na mapato ya Pasaka,na mapato mengine yatatumika kuendeleza ujenzi wa kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu, Kituo cha Watoto kiitwacho Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa wasiojiweza.