Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19870 articles
Browse latest View live

CHADEMA WASITISHA 'UKUTA' KESHO SEPTEMBA 1, 2016 KUPISHA MALIDHIANO YA VIONGOZI WA DINI

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kusitisha maandamano na mikutano nchi nzima iliyokuwa imepangwa kufanyika kesho (Septemba 1) waliodai ni uzinduzi wa Oparesheni ya kile walichokiita Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA).

Chadema wamesema wameahirisha UKUTA kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo ili kutoa nafasi ya mazungumzo iliyoombwa na wadau na viongozi wa dini nchini.

Akizungumza muda mfupi uliopita na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na viongozi wa dini kuwapa angalau wiki tatu.

“Viongozi wa dini walituambia tupeni wiki mbili au tatu, sisi tukawaongeza nyingine moja,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa chama hicho kimepata wakati mgumu kufikia uamuzi huo baada ya wadau mbalimbali kuwasihi kutofanya maandamano, badala yake watoe nafasi ya kuzungumza na Serikali ili kufikia muafaka kwa amani.

KATUNI YA LEO

$
0
0

CHUO CHA UDEREVA CHA NYATO'S CHAWATUNUKU VYETI MADEREVA WALEMAVU 19

$
0
0
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kulia), akimkabidhi cheti, Mpoki Mwasunga, baada ya kuhitimu mafunzo ya udereva ya mwezi mmoja katika chuo cha udereva cha Nyato's kilichopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala Dar es Salaam leo. Wahitimu 19 ambao ni walemavu walihitimu mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga, akiangalia alama ya usalama barabarani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Mossi Ndozero.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mshairi, Kiiza Amani akitoa burudani kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (katikati), akihutubia kwenye hafla hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu, Kabateke Jutoram na Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero.
Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Mossi Ndozero, akitoa neno kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Usalama Barabarani Wilaya ya Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Peter Mashishanga (kushoto), akimkabidhi cheti, mhitimu, Subira Semsimbazi.
Hapa James Hizza akipokea cheti chake.
Sikujua Mbwembwe, akikabidhiwa cheti chake.
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
Stafu Sajeni, Enock Machunde akitoa darasa kwa hitimu hao kuhusu sheria za usalama barabarani.
Koplo, Faustina Ndunguru, akizungumza kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

WATU Jamii ya walemavu ambao ni maderava wa vyombo vya moto wametakiwa kujitokeza kwenye shule mbalimbali za udereva ili kupata mafunzo ya udereva ikiwa pamoja na kupata leseni kabla ya kutumia vyombo hivyo.

Wito huo umetolewa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi wa Ilala,Peter Mashishanga wakati akiwatunuku vyeti walemavu 19 ambao wa mefunzo ya mwenzi mmoja katika shule ya udereva ya Nyato's iliyopo Majohe Bomba mbili Manispaa ya Ilala.

Alisema kuwa ipo haja ya walemavu ambao wanamiliki vyombo vya moto na kuendesha vyombo hivyo kabla hawajaingia barabarani ni vema wakapata mafunzo ya kujuwa alama,kanuni na sheria za usalama barabarani.

"Ni muhimu kwa kundi hili ambalo leo mmepata vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva kwenda kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata fursa ya kupata mafunzo kama nyie kwenda kuwahamasisha ili wajiunge katika vyuo vya udereva ikiwamo chuo hiki cha Nyato's ambacho kimeaza mpango wa kutoa mafunzo haya kwa nchi nzima kwa kushirikiana Kamati ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu Wenye Ulemavu."alisema Mashishanga

Aidha aliwaeleza wahitimu hao kuwa wahakikishe wanakwenda kupata majaribio kwa wa kufunzi wa kikosi cha Usalama barabarani ili wapate leseni zitakazo wafanya waweze kuendesha vyombo vya vya moto.

Kwaupande wake Mkurugenzi wakitengo cha Elimu kwa Umma kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP),Mossi Ndozero alisema kuwa ni muhimu kwa wahitimu hao kwenda kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuvaa kofia ngumu,na kutozidisha abiria.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Wilfred Nyato alishukuru kwa ushirikiano uliopo kati ya Jeshi hilo na taasisi yake ambapo pia ametoa ofa ya kusoma bure kwa mlemavu Thomas Kone ambaye hivi karibuni alipata msaada wa bajaji kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli.

Nyato alisema kuwa kimeazisha mpango wa kutoa mafunzo ya udereva kwa kushirikiana na kamati ya Taifa ya usalama kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kukabiliana na matukio ya ajali za barabarani.

MKUU WA MKOA WA ARUSHA, MHE. GAMBO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA DINI

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na Askofu wa Kanisa la Anglikan, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Stanley Hotay (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo nae akiwa ameambata na Mbunge wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki (Eala) Mheshimiwa Angela Kizigha.
Askofu wa Kanisa la Anglikan, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, StanleyHotay(kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro, Stanley Hotay (kulia) baada ya mazungumzo yao.

Nteghenjwa Hosseah – Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.

Mhe. Gambo amekutana na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Mchungaji Solomon Masangwa, Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT) mkoa wa Arusha, Leonard Mwizarubi na
Askofu Stanley Hotay wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mount
Kilimanjaro.

Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.

Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Joseph Magufuli kutaka kuwainua wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani halmashauri zimetenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake na Vijana wajasiriamali zitakazowawezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Amewataka wawajulishe waumini wa dini zote na serikali iko tayari kupanga utaratibu wa maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na kutoa  elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini wala kisiasa.

Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Aidha alishauri kutokana na idadi ya watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) pekee.

Mhe. Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili watoe mawazo yao katika kuiboresha na kuifanya itekelezeke kwa wepesi zaidi.

MAGAZETINI LEO; SIRI YA MBOWE KUAHIRISHA 'UKUTA' YAJULIKANA ... LOWASSA: NITAMTAFUTA MAGUFULI

$
0
0

NHC YAWAONDOA WADAIWA SUGU OFISI ZA FREEMEDIA WACHAPISHAJI WA GAZETI LA TANZANIA DAIMA

$
0
0
Katika kutekeleza agizo la wadaiwa sugu, Madalali wa shirika la nyumba la Taifa la - (NHC) mapema leo wamevamia ofisi za Freemedia wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na kutoa vitu.

Mwisho wa mwezi uliopita shirika la nyumba la Taifa - (NHC) kupitia Mkurugenzi Mkuu, Nehemia Mchechu, lilitangaza kuwaondoa wadaiwa wote sugu wanaoishi katika nyumba zao.

KAULI YA MKURUGENZI MKUU WA NHC, NEHEMIA MCHECHU.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa mwezi uliopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanas pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema na kwamba sasa zimesalia wiki tatu.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadaiwa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

WAKUU WA MIKOA YA MBEYA NA SONGWE WAONGOZA WANANCHI KUSHUHUDIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA RUJEWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa wakiangalia kupatwa kwa jua kwa miwani maalum katika eneo la Tazara Relini Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo wageni na wananchi kutoka maeneo mbalimbali na mikoa ya jirani wakiwemo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka ulaya wamekuja kushuhudia tukio hilo linalotokea kwa nadra. (PICHA NA JOHN BUKUKU - FULLSHANGWE-RUJEWA, MBEYA).

Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii TTB Bw. Geofrey Meena akiangalia tukio la kupatwa kwa jua kwa miwani maalum wakati wa kushuhudia tukio hilo katika eneo la Taraza Relini Rujewa wilayani Mbarali.

Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena kulia pamoja na pamoja na wafanyakazi wenzake wa TTB kutoka kulia Gladstone MlayMkuu wa Utalii Kanda ya Ziw , Irene Mvile Afisa Utalii Habari na ErnestMususa Mhasibu wakishuhudia tukio hilo kwa pamoja.
Mkurugenzi wa Fullshangwe Bw. John Bukuku hakuwa nyuma ili kushuhudia tukio hilo pia
Mkuu wa Mawasiliano TTB Geofrey Tengeneza akizungumza na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika eneo hilo ili kushuhudia tukio hilo.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala akiwa pamoja na viongozi wa mkoa huo Katikati Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw William Ntinika na Mbunge wa jimbo la Mbarali.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Mh. Chiku Galawa akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa Mstaafu Bw.Eraston Mbwilo.
Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia tukio hilo.
Mwananchi wa Rujewa Kennedy Lutambi akishuhudia tukio hilo.
Mwandishi wa Gazeti la Uhuru Issa Mohammed naye hakuwa nyuma kushuhudia tukio hilo adimu.
Hivi ndivya hali ilivyokuwa baada ya juwa kupatwa matukio tofauti yakionyesha lilipokuwa likipatwa na kuachiwa.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-RUJEWA-MBEYA).

SHULE NNE ZA WILAYANI GEITA ZALA NEEMA YA MADAWATI NA TIGO FIESTA 2016

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga (kushoto)akipokea moja kati ya madawati 185 yenye thamani ya shillingi milioni 31 jana, toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande ikiwa ni mpango wa kampuni ya simu za mkononi Tigo kutoa madawati kupitia kauli mbiu “ Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora fiesta 2016 kwa kishindo cha Tigo imooo”
Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga(katikati) akiwa ameketi kwenye dawati mara baada ya kukabidhiwa madawati 185 toka kampuni ya simu za mkononi Tigo hafla iliyofanyika shule ya msingi Mwatulole jana mkoani humo, Wengine pichani kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande na Afisa elimu mkoa wa Geita, Catheline Mashala.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga akiwa ameketi na wanafunzi wa shule ya msingi Mwatulole mara baada ya kukabidhiwa madawati 185 toka kampuni ya simu za mkononi Tigo hafla iliyofanyika shule ya msingi Mwatulole jana mkoani humo, Pembeni mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi.

Kampuni ya Tigo Tanzania leo imekabidhi madawati 185 yenye thamani ya shilingi milioni 31 yatakayogawiwa shule nne katika mkoa wa Geita ikiwa ni sehemu ya mkakati wake unaoendelea nchi nzima wa kutoa msaada wa madawati ambayo yatainufaisha mikoa 14 bega kwa bega na tamasha la Tigo FIESTA 2016.

Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’

Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo zilizofanyika katika Shule ya Msingi Mwatulole, Meneja wa Kikanda wa Tigo Kanda ya Ziwa Edgar Mapande, alisema umekuwepo uhitaji mkubwa wa madawati katika shule za msingi na kutokana na kuwepo kwa uhaba wa madawati imebainika kuwa ni moja ya sababu zinazoathiri uwezo wa kujifunza pamoja na ufanisi wa masomo miongoni mwa wanafunzi katika shule zetu nyingi za msingi.

“Lengo letu kama kampuni ni kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi na tunayo furaha kwamba msimu wa FIESTA 2016 unaleta mabadiliko kwa kizazi cha baadaye ambacho ni wanafunzi walio katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai tena chini sakafuni,” alisema Mapande.

Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyingu ambaye alisema kuwa madawati hayo 185 yataboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya kujifunza kwa watoto katika mkoa huo na kutoa witom kwa watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mashule mkoani humo.

Kyingu alizitaja shule zitakazonufaika na madawati hayo na idadi yake katika mabano kuwa ni Mwatulole (50), Nyankumbu (45), Ukombozi (45), na Kivukoni (45).

“Tunawashukuru sana Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza idadi ya uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Geita. Tunaamini madawati haya 185 yatatufikisha mbali katika kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio katika kuelekea kuwa viongozi wa baadaye,” alisema Kyingu.

Mradi mkakati wa madawati wa Tigo Fiesta ulianzia mkoani Mwanza na hadi sasa Tigo imeshatoa madawati wilayani Kahama na mkoani Kagera.

TPSF YATOA WAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI MKOANI GEITA

$
0
0
Katibu Tawala wa wilaya ya Geita Thomas Dimme akifungua semina ya wajasiriamali ya taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation iliyofanyika wilayani humo
Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali kutoka kutoka mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha (FSDT) akiongea wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mwandamizi kutoka ofisi ya RAS ya Geita akiongea wakati wa mafunzo hayo.
Ni meneja Mradi wa mafunzo kutoka TPSF, Celestine Mkama,akitoa maelekezo kwa wanasemina
Baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria mafunzo mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wakufunzi.
---
TPSF yatoa wafunzo kwa wajasiriamali mkoani Geita.

Wajasiriamali waliopo mkoani Geita wametakiwa kutumia raslimali mbalimbali zilizopo mkoani humo na firsa zinazojitokeza kwa sasa kuibua miradi ya biashara na kuendesha biashara yao kitaalamu wakiwa na malengo ya kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Tawala wa wilaya ya Geita,Bw.Thomas Dimme aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo kama mgeni rasmi wakati wa mafunzo maalumu ya mbinu za kuendeleza wajasiriamali yaliyoandaliwa na taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation.

Bw.Dimme alisema kuwa serikali imefungua milango ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa kutumia fursa zilizopo hivyo aliwataka kuibua miradi ya biashara na kuwa na utayari wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika biashara kwa kipindi hiki mojawapo ikiwa ni ushindani mkubwa na kufanya biashara kwa kufuata njia halali zinazotakiwa ikiwemo kulipa kodi za serikali kwa mujibu wa sheria.

Aliipongeza taasisi ya TPSF kwa kuendesha miradi ya mafunzo kwa wajasiariamali sehemu mbalimbali nchini “Nawapongeza kwa kuwafikishia mafunzo wajasiriamali wa ngazi za chini katika ngazi ya mikoa na wilaya kwa kuwa wafanyabiashara wakipata mafunzo kama haya kwa vyovyote wataweza kupata mafanikio katika shughuli zao”.Alisema Dimme.
 
Kwa upande wake Meneja Mradi wa Mafunzo kutoka taasisi ya TPSF,Celestine Mkama alisema kuwa taasisi hiyo inaendesha mradi wa kuwapatia mafunzo wajasiriamali kuhusiana na mbinu mbalimbali za kufanya biashara kwa lengo la kupata mafanikio.

“Mafunzo haya yamelenga kuwapatia maarifa wafanyabiashara wadogo ili yawajengee uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo katika biashara “Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya biashara kutokana na kukosa elimu ya biashara ndio maana tumeona tuwasaidie katika eneo hili la kuwajengea uwezo kupitia kuwapatia elimu ya ujasiriamali”.Alisema Bw.Mkama.

Mkama alisema baadhi ya masuala yanayofundishwa kupitia mafunzo haya ni utunzaji wa mahesabu ya biashara, nidhamu katika matumizi ya fedha,utunzaji wa kumbukumbu za biashara na jinsi ya kupanga miradi.

Akiongea kwa niaba ya wajasiriamali wenzake,Bi.Elizabeth Bigambo ,aliishukuru taasisi ya TPSF kwa kuwafikishia elimu ya ujasiriamali. “Tuna imani mafunzo haya tuliyoyapata yatatusaidia katika kukuza biashara zetu na kukua kibiashara na kuchangia pato la taifa kwa njia ya kodi”.Alisema Bigambo.

MWANARIADHA MADUMLA AAHIDI KUREJEA NA MEDALI KUTOKA OLIMPIKI, BRAZIL

$
0
0
 Kaimu katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja akimkabidhi bendera mshiriki wa mashindano ya walemavu ya Paralympiki Ignas Madumla akiwa na kiongozi wa msafara Tuma Dandi walioondoka leo mapema asubuhi kuelekea Nchini Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki.
Mwanariadha wa Tanzania, Ignas Madumla anayekwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa walemavu, PARA LYMPIKI, yatakayofanyika jijini RIO DE JANAIRO, nchini BRAZIL ameahidi kurejea na medali

Akizungumza baada ya kukabidhi bendera ya taifa kwa mwanariadha huyo, kaimu katibu mkuu wa baraza la michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja amemtaka mwanaridha huyo kucheza kwa bidii ili arudi na medali.

Kwa upande wao, mwanariadhi Ignas Madumla, na kiongozi wa msafara, Tuma Dandi wamesema wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi katika mashindano hayo.

Madumla atashiriki katika mchezo wa kurusha kisahani na tufe.mashindano ya PARALYMPIKI yanafanyika baada ya mshindano ya olympiki kumalizika huku wawakilisha wa watanzania wakirejea na mikono mitupu.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKABIDHI TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU 2015 KWA MKURUGENZI WA KAJUNASON BLOG

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna (kulia) akikabidhiwa vitabu vyenye Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 na Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Mohamed Seif ambaye alimkabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kajunason Blog, Bw. Cathbert Angelo Kajuna akionyesha vitabu vyenye Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA RIPOTI YA HALI YA HEWA BARANI AFRICA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Kutoka kwa Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimaina na Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu, Benjamin Mkapa katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya The Investment Climate Facility for Africa (ICF), Neville Isdell na Katikati ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyekiti wa Masula ya Uhusiano wa Kimataifa wa ICF, Ris Mstaafu, Benjamin Mkapa katika hafla ya kuzindua Ripoti ya Hali ya Hewa Barani Afrika, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar Septemba 1, 2016.
Picha ya pamoja. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Afrika wajiulize wanaweza kuchangia kitu gani katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wakazi wa bara hilo.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Alhamisi, Agosti 31, 2016) wakati akizungumza na wawakilishi wa taasisi za kimataifa waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya Taasisi ya Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji barani Afrika (ICF) uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alisema taasisi hiyo imesaidia kukuza uwekezaji kupitia miradi katika nchi mbalimbali za Afrika kwa kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi, usajili wa biashara za wajasiriamali na upatikanaji wa leseni za biashara.

“Kutokana na kazi inayofanywa na taasisi hii, hali ya uwekezaji katika nchi nyingi imeimarika na bara la Afrika limekuwa mbia kwa wawekezaji kutokana na ushirikiano baina ya Serikali za nchi husika na sekta binafsi. Uchumi wa nyingi za Afrika umeimarika kuliko hapo awali,” alisema.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema zaidi ya wajasiriamali 500 kutoka Tanzania walipatiwa mafunzo kwa ushirikiano baina ya ICF, Serikali na ESAURP ili kuwajengea uwezo waweze kufanya biashara zao kwa tija zaidi. “Mafunzo hayo yaliwalenga wajasiriamali wadogo na wa kati ambao wanajihusisha na uvuvi, biashara za rejereja na jumla kutoka mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam”.

“Kupitia mafunzo hayo, wajasiriamali hao waliweza kusajili biashara, kurasimisha biashara zao, kuongeza mitaji na kujua namna ya kutunza taarifa za biashara zao,” alisema.

Mapema, Mwenyekiti Mwenza wa taasisi hiyo ambaye pia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin Mkapa alisema kuna haja ya wananchi kubadili mitazamo yao juu ya sekta binafsi kwani nayo ni muhimu katika ujenzi wa uchumi kwa nchi yoyote ile.

“Watu wengi wanahisi kwamba wawekezaji ni wabaya. Hii si kweli. Tunapaswa kujenga mazingira ya kuwakubali kwa sababu wanakuja na mitaji yao na wao wanawakilisha michango kutoka kwa mamilioni ya wafanyakazi kutoka kwenye nchi zao. Hatupaswi kuwaona kwamba ni maadui,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa kukubali kuiruhusu taasisi hiyo ya ICF iweke makao yake makuu hapa nchini wakati ilikuwa imeshakataliwa kufanya hivyo katika nchi nyingi ambako ilipeleka maombi yake.

Aliwataka viongozi mbalimbali watumie uzoefu uliowekezwa na taasisi hiyo kwenye uboreshaji wa mifumo ya mahakama na ukusanyaji kodi, utoaji wa leseni, urasmishaji wa biashara za wajasiriamali wadogo.

“Tunayo maeneo mengi ambayo tumefanya vizuri iwe ni katika TEHAMA, miundombinu, mahakama au mambo ya forodha. Uamuzi ni wenu juu ya jambo lipi muanze nalo katika kuboresha huduma ili kuharakisha maendeleo ya bara hili,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, SEPTEMBA MOSI, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMWAPISHA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO IKULU JIJINI DAR

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango Doto James mara baada ya kuapishwa. PICHA NA IKULU

WIZARA YA AFYA KUFANYA UZINDUZI WA KONDOMU MPYA MKOANI MWANZA

$
0
0
Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni.

Baada ya juzi Agosti 30, 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuzindua aina mpya ya Kondomu iitwayo Zana Kondomu mkoani Mbeya, Uzinduzi kama huo unatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza Septemba 05,mwaka huu.

Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (pichani), jana alisema mkoa wa Mwanza unatarajia kupokea ugeni kutoka wizara hiyo ambao utajumuisha wataalamu mbalimbali wa afya watakaokuwa wakitoa semina na elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari, wakielezea juu ya uzinduzi wa kondomu hiyo.

Alisema miongoni mwa dhumuni la kuzindua aina hiyo mpya ya Kondomu, ni kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambapo Wizara itakuwa ikigawa bure kondomu hizo zenye ubora kwa wananchi, kote nchini.

RAIS DKT. MAGUFULI KUBADILI FEDHA ILI KUWAKOMOA WALIOZILALIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua Mkutano  Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016

---
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kwa mamlaka aliyonayo kikatiba anaweza kubadili fedha za Tanzania ili watu waliozificha hivi sasa wakose mahali pa kuzipeleka.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika Mkutano wa 14 wa Wahandisi, uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wapo watu ambao wamekuwa wakificha fedha zao majumbani kwao hali inayosababisha zisiingie kwenye mzunguko. Hivyo, amewataka watu hao kuacha mara moja tabia hiyo inayopelekea kukosekana kwa fedha kwenye mzunguko.

Pia amewataka wananchi kufanya kazi kwani katika kipindi chake cha utawala ni vigumu kwa mwananchi asiyefanya kazi kupata fedha kwani awali fedha nyingi zilizokuwepo zilitokana na wizi serikalini.

MAGAZETINI LEO; MAGUFULI: WANAOLIA NJAA NI WAPIGA 'DILI' ... MAALIM SEIF, LIPUMBA WAIFIKISHA CUF PATAMU

$
0
0

WAZEE WATAKA USHIRIKI WA WAZI KATIKA SERA NA MIPANGO YA MAENDELEO

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akiongoza na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za ESRF kufungua warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.

Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati). Wengine kushoto ni Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha na Mkurugenzi Mkazi Msaidizi wa Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Smart Daniel (wa pili kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na washiriki wa warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Jukwaa la Wazee Tanzania, Samson Msemembo (85) akizungumzia changamoto wanazokutana nazo wazee katika vituo vya huduma za afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Kaimu Kamishna Ustawi wa Jamii Bw.Rabikira Mushi kutoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida waliopo meza kuu.

Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) na Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Oswald Mashindano akizungumzia nafasi ya wazee katika sera ya kitaifa kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros akishiriki kutoa maoni kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi Shirika la kimataifa la kusaidia wazee (Help Age International), Amleset Tewodros.

Mshauri wa Masuala ya Ushirikiano wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kati na Magharibi wa Shirika la Help Age International, Roseline Kihumba akizungumzia hali ya uzee na wazee duniani na ushirikishwaji wa wazee katika maendeleo endelevu kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.

Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha akichangia mada kwenye warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mudith Cheyo akifafanua jambo kwa washiriki wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Watu Waishio na Virusi vya Ukimwi Tanzania (SHDEPHA), Joseph Katto akizungumzia changamoto zinazowakabili wazee wanaoishi na VVU katika kupata huduma mbalimbali nchini kwenye warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.



Sehemu ya washiriki waliohudhuria warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mikutano wa ESRF wakati wa warsha kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Shirika la Help Age International.

Picha ya pamoja

Na Mwandishi wetu

SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kuhakikisha kwamba kunakuwapo na ushirikishaji wa wazi wa wazee katika sera na mipango ya maendeleo.

Aidha imetakiwa kutoa nafasi kwa wazee katika utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo, jamii na mazingira.

Kauli hizo zimetolewa na washiriki wa warsha ya nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambayo imeingizwa katika mipango ya maendeleo ya taifa.

Wakiongozwa na mada mbalimbali zilizotolewa na wataalamu mbalimbali kama Dk Oswald Mashindano, Danford Sango, Ahmed Makbel, Dk. Ntuli Kapologwe washiriki walisema kwamba ingawa Tanzania ina sera nzuri kuhusu wazee utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kutokana na kukosekana kwa utashi.

Aidha walisema kwamba kukosekana kwa sheria ya wazee kunawafanya wazee hao kunyanyasika hasa katika masulaa ya kiuchumi na kiafya.

Joseph Kato (62) ambaye alisema kwamba amekuwa akiishi na UKIMWI tangu ujana wake hadi sasa ameingia rasmi katika rika la wazee, anasema kwamba sera za nchi hasa za afya haiztoa umuhimu kwa magonjwa kama Ukimwi.

Aidha alisema kwamba wazee wakiwa na afya zao wamekuwa wakipuuzwa katika suala la uchumi kwani ukiwa unaishi na Virusi vya Ukimwi ukienda benki hupewi mikopo na pia ukiwa mzee hupewi mikopo.

Alisema kama sera ni kuhakikisha hakuna anayeachwa katika safari za utekelezaji wa maendeleo endelevu ipo haja kwa serikali kuhakikisha kwamba wazee hawanyanyaswi na wanasaidiwa kuwezeshwa kiuchumi.

Mshiriki mwingine aliyejitambulisha kama Mama Koku alisema kwamba ngazi za chini za utekelezaji zimekuwa hazitoi kipaumbele kwa wazee japo serikali kuu katika mipango yake imeonesha nini kinachotakiwa kufanywa na kila mmoja katika nafasi ya kuhudumia wazee.

Alisema upo mkakati wa mwaka 2007 hadi 2025 ambao umeonesha utekelezaji wa huduma kwa makundi tete lakini wakurugenzi wa halmashauri hawaweki wazee kama kipaumbele chao wakisingizia serikali kuu.

Hata hivyo amesema wakati umefika kwa serikali kufuatilia mkakati huo kwa lengo la kuwabana wahusika ili kipaumbele kwa wazee kiwepo.

Amesema maofisa mipango wengi wanakwepa kuweka kipaumbele kwa dai kuwa fedha wanazoletewa ukomo wake hauruhusu kuwaingiza wazee huku wengine wakidanganya kwamba serikali kuu ndio imeondoa msaada kwa wazee.

Naye Ishaka Msigwa kutoka Ruvuma alisema kwamba tatizo kubwa la kuhudumia wazee sio sera kwani ipo ila dhamira ndio haipo. Alisema wazee wanataabika sana katika suala la uchumi na kwamba ipo haja sheria ya wazee ikatungwa ili kuwasaidia kuondokana na adha ya kukataliwa wakati wa kutafuta mikopo ya kuwainua kiuchumi.

Alisema asilimia 50 ya mayatima wanakaa na wazee vijijini na kitendo cha kuwanyima ushiriki wa uwezeshaji unawatesa.

Pamoja na malalamiko hayo ya wazee ambayo yalijikita katika kuwa na kipato cha uhakika na suala la upatikanaji wa matibabu, serikali ilisema imekamilisha utaratibu wa utoaji wa pensheni kwa wazee Tanzania bara na kinachosubiriwa kwa sasa ni utekelezaji wake.

Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua warsha hiyo kuhusu nafasi ya wazee katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) alisema hata hivyo serikali itaanza kutoa posho hizo kwa wazee wa miaka 70 kwenda juu na badae watashuka hadi katika umri unaokubalika.

Alisema wamejifunza kutoka Zanzibar na wanaona hapo ni eneo jema la kuanzia.

Aidha alisema kwamba bado anaendelea na juhudi zake za kutaka sheria ya wazee itungwe kwa kuwa ipo sera inayohusu wazee.

Kwa hesabu za karibuni Tanzania inawezee zaidi ya milioni 2.

Pamoja na kuzungumzia suala la malipo ya pensheni ambapo alisema suala hilo kwa sasa lipo Hazina, waziri huyo alirejea msisitizo wake wa kutaka wazee watibiwe bila malipo.

Alisema serikali ya awamu ya tano ni serikali ya utekelezaji na kwamba suala la tiba bure kwa wazee ni suala la sera na wala si utashi.

Akizungumza kwa kina masuala yanayogusa wazee kama yalivyotolewa kwa sauti na mzee Samson Msemembo (85), Waziri Ummy alisema kwamba serikali inatambua changamoto zinazowakumba wazee na itazifanyia kazi kuhakikisha kwamba zinapatiwa majibu.

Mzee Msemembo kutoka Jukwaa la wazee Tanzania, alisema kwamba wazee wamekuwa wakinyanyasika katika sekta ya afya na uchumi wakibaguliwa na kunyimwa fursa za kuishi kwa furaha.

Akizungumza kuhusu kero zilizoelezwa katika warsha hiyo iliyoendeshwa kwa pamoja katika Taasisi za Tafiti za Kiuchumi na Kijamii nchini (ESRF) na taasisi ya kimataifa ya kusaidia wazee Help Age, Waziri Ummy alisema serikali inataka wazee wawe na kipato cha uhakika na kupewa matibabu.

Amesema hakubaliani na suala la wazee kukosa matibabu na kutaka wakurugenzi wote wa halmashauri kuhakikisha kwamba wazee wanaingizwa katika mfumo wa matibabu wa CHF au wanapewa kadi maalumu ya matibabu bure.

Alisema kwamba haingii akilini kuona kwamba wazee sita katika watu 100 wanakosa kutibiwa kwa dai la kukosekana kwa fedha wakati sera zipo zinazotaka watibiwe bure.

Akizungumzia tatizo la Hospitali ya Taifa Muhimbili kutotibia wazee alisema kwamba atalishughulikia tatizo hilo kwani haliingii akilini mwake:“Watumishi, vifaa, kila kitu ni cha serikali inakuaje wazee wasitibiwe” alihoji Waziri Ummy .

Akizungumzia suala la kukuza uchumi wa wazee alisema kwamba atamwandikia barua Rais Magufuli ili aweze kutoa agizo la asilimia 2 katika mapato ya ndani ya halmashauri kuchochea uchumi kwa wazee.

Alisema kuna asilimia 5 zimetengwa kwa vijana na wanawake pia 5 na haoni sababu zisitengwe asilimia 2 kwa ajili ya wazee.

Katika warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba warsha hiyo imelenga kusaidia wadau mbalimbali kutambua masuala ya wazee katika mipango ya maendeleo kuanzia ngazi za chini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia.

TAARIFA YA JWTZ KUFUATIA HABARI ILIYOANDIKWA KWENYE GAZETI LA TANZANIA DAIMA JANA SEPTEMBA MOSI

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa kwake na shughuli za kisiasa.

Tunapenda kuwataarifu wananchi kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya juu, hivyo lisihusishwe na propaganda zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye maadili ya kitaasisi ya hali ya juu.

Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi. Inaombwa kuwa makini katika utoaji wa maelezo au malalamiko, iachwe mara moja vyama vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi.

Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita vya Kagera.

Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria, ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa wekeni kumbukumbu zenu vizuri.

Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri wakasoma vema historia ya nchi wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno yanayotolewa na viongozi wa kisiasa wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na kiungulia, awe makini kuongea vitu ambavyo haelewi na kutokuwa makini zaidi aelewe madhara yanayoweza kutokea kutokana na upotoshaji.

Jeshi letu linafanya shughuli zake ki weredi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

MATUKIO YA RAIS DKT. MAGUFULI NA ASKARI WA JWTZ KATIKA KUAZIMISHA MIAKA 52

$
0
0
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwaunga mkono na kuwatumia wahandisi wa ndani wenye ujuzi mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, reli, barabara na miundombinu mingine.
Hayo yamesema na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alipokuwa akifungua Mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 01 Septemba, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Magufuli amesema atafurahi kuona miradi inayohusisha kazi za kihandisi na hasa wakati huu ambapo nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda inatekelezwa kwa kutumia wahandisi wa ndani na hivyo amewataka kujipanga sawasawa ili kukabiliana na changamoto hiyo.
“Nyinyi wahandisi mkiamua nchi hii iende kwenye uchumi wa kati tutafika, mkiamua nchi hii iende kwenye uchumi wa viwanda tutafika, na msipoamua hatutafika.

“Sasa hivi kuna ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) kwani nyinyi mnashindwa kujenga?” Amehoji Rais Magufuli huku akisisitiza kuwa Serikali yake ipo tayari kuwaunga mkono pale watakapohitaji msaada.
Hata hivyo Dkt. Magufuli amewakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa ubora, ushirikiano na upendo miongoni mwao huku akielezea kusikitishwa kwake na baadhi ya wahandisi ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo kushirikiana na wakandarasi na wazabuni kuzidisha viwango vya makadirio ya gharama za miradi na manunuzi ya Serikali ili kujipatia fedha isivyo halali na kupitisha miradi iliyojenga chini ya viwango.
Rais Magufuli ameongeza kuwa Serikali yake itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaotumia vibaya fedha za umma na amesisitiza kuwa hatua zaidi za kuhakikisha kunakuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali zitachukuliwa.
“Kuna watu wanasema mzunguko wa pesa umepungua na hali imekuwa ngumu, hizo pesa zilizokuwa zinachezewa huko mitaani zilikuwa pesa za Serikali, mimi nataka pesa ziende kwenye miradi ya maendeleo na ndio maana bajeti ya maendeleo tumeongeza kutoka asilimia 26 hadi asilimia 40” Amesisitiza Rais Magufuli.
Katika tukio jingine, Rais Magufuli amewatembelea Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 603 (Air Wing) kilichopo Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuwapongeza kwa kuadhimisha miaka 52 ya tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo.
Katika kuadhimisha miaka 52 ya JWTZ Askari wa Jeshi hilo wamefanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Pamoja na pongezi hizo Rais Magufuli amekagua baadhi ya ndege zinazotumiwa na Jeshi hilo na amewahakikishia Wanajeshi kuwa Serikali yake itaendelea kuliimarisha Jeshi hilo kwa vifaa na maslai ya Askari ili kuendelea kuwa na Jeshi bora, la kisasa na lililo tayari kuilinda nchi wakati wote.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI PEMBA KWA SAFARI YA KIKAZI

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamewasili leo Septemba 2, 2016 Pemba kwa safari ya kikazi visiwani humo. Rais Dkt. Magufuli amelakiwa na ngoma na shamra shamra.

Ngoma za mapokezi ya rais visiwani humo.
Viewing all 19870 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>