Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19874 articles
Browse latest View live

SHAMSA FORD NA CHIDD MAPENZI WAFUNGA NDOA LEO

$
0
0
HONGERENI SANA MUNGU MUNGU AWAPE BARAKA KWENYE MAISHA YENU MAPYA YA NDOA @shamsaford @chiddimapenzi.

KIWANDA CHA SARUJI CHAIPIGA TAFU SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU YA ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Rasilimawatu kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas mhasibu.
Tangakumekuchablog Tanga,

KIWANDA Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.

Akizungumza wakati wa halfa fupi ya makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

Alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.

‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule yako ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu” alisema Malambugi

Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school , Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla

Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA PEMBA KATIKA UWANJA WA GOMBANI YA KALE KISIWANI PEMBA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wanchi wa Pemba katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuhutubia mkutano wa katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuhutubia mkutano wa katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba. PICHA NA IKULU

RAIS DKT MAGUFULIA ALAKIWA KWA SHANGWE MJINI ZANZIBAR AKITOKEA KISIWANI PEMBA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba ambako aliweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hayati Dkt Omar Ali Juma, na kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye ndege ya ATCL katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akivishwa shada la maua ya asumini baada ya kutelemka kutoka kwenye ndege ya ATCL katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na makamanda wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri  wa Ujenzi, Mawasilaino na usafirishaji wa Zanzibar Balozi Ali Abeid Karume katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni   katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mhe. Mohamed Raza Hassanali  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na  Waziri wa Afya Mhe.  Mahmoud Thabit Kombokatika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohamed Seif Khatib katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mratabu wa Diaspora,Ofisi ya Rais Ikulu na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Ndugu Hassan Hafidh katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na mmoja wa makada waandamizi wa CCM katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na mmoja wa viongozi  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiakisalimiana na mmoja wa viongozi katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na mmoja wa wazee mashiuhuri katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said  katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia ngoma ya utamaduni ya Kilua katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiangalia ngoma ya Msewe baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Zanzibar leo jioni akitokea kisiwani Pemba. Picha na IKULU

CCTV YAPIGA HODI JIJINI ARUSHA, KILA KITU KWENDA 'LIVE'

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akizungumza aliyeambatana na Wabunge toka Sweden walipotembelea Ofisini kwake mapema leo.
Kiongozi wa ujumbe toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns (kushoto) akikabidhi zawadi yao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
Kutoka kushoto ni Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnite akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mashaka Gambo pamoja na Kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Bi. Matilda Irnkarns kwenye picha ya pamoja baada ya Kikao
Katika picha ya pamoja ni kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Kwitega, Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnite , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, kiongozi wa msafara wa wabunge toka Sweden Bi. Matilda Irnkarns, ujumbe toka Sweden pamoja na viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Baadhi wa wabunge toka Sweden wakifuatilia kikaa wakati walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema leo.
---
Nteghenjwa Hosseah –Arusha

MKOA wa Arusha umeanza kujipanga katika utaratibu wa kulinda mji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya CCTV – Camera ili kuimarisha usalama wa mji  “Safe City”, Mfumo huu utawezeshya Mji kulindwa masaa 24 dhidi ya  uhalifu kwa raia, wawekezaji na watalii.

Kauli hiyo ilitolewa  leo mjini hapa na Mkuu wa Mkoa huo Mrisho Gambo ofisini kwake mara baada
ya kutembelewa na Balozi wa Sweden nchini, Bi. Katarina Rangnite  aliyeambatana na Ujumbe wake wa Wabunge kutoka Nchini Sweden.

Akizungumza na ujumbe huo RC Gambo alisema, mkoa huo tayari umekwisha kuonyesha nia
ya kuwekeza katika mfumo huo ili kuwaongezea wananchi na mali zao  usalama zaidi.

“Nia yetu ni kuona hali ya usalama katika mkoa  wa Arusha ikiwa ya juu sana ili kuendelea kuwavutia watalii zaidi  kutoka nchi mbalimbali Duniani. Malengo yetu ni kuwa na mifumo  itakayoulinda mkoa wetu kwa Saa 24 na mwaka mzima,” alisema RC Gambo na kuongeza:

“Hatua hii itaongeza ulinzi kwa raia na mali zao,  pia kwa wawekezaji waliopo mkoani kwetu na watalii wanaokuja kutembelea  hifadhi na vivutio mbalimbali kwani Arusha ndio kitovu cha utalii hapa  nchini,” alisema.

Kwa upande wake Balozi Rangnite ambaye  kiongozi wa msafara huo uliojumuisha pia wabunge kutoka Bunge la Sweden  wanaowakilisha Kamati ya Kilimo na Mazingira, alikubaliana na nia ya  kuwekeza kwenye mfumo wa usalama wa mkoa wa Arusha.

Balozi  Rangnite alimueleza Mkuu wa Mkoa Gambo kwamba, nchi ya Sweden inayo  wataalamu waliobobea katika mifumo hiyo ya usalama wa miji hivyo  alimuomba Gambo kuwasilisha kwake maandiko ya vitu vinavyohitajika ili  kuwezesha mradi huo kutekelezwa.

“Tukipata maandiko mbalimbali  ya mradi tunaweza kuangalia ni wapi Serikali ya Sweden inaweza kuwekeza  ikiwamo kusaidia kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili,” alisema  Balozi Rangnite.

Aidha Gambo alitoa ombi kwa Balozi wa Sweeden  kushirikiana na Mkoa wa Arusha kwenye Kampeni ya Kulinda vyanzo vya Maji ili kuwezesha mradi mkubwa wa maji unaosimamiwa na mamlaka ya maji safi na maji taka (AUWSA) kutekelezwa kwa mafaniko makubwa. Itakumbukwa  kwamba imepatiwa Bil 476 ili kumaliza tatizo la maji Jiji hapa.

Katika ziara ya ujumbe huo pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo la  kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji katika Kilimo, Mazingira na  maeneo muhimu kutoka mkoani Arusha.

Ujumbe huo kutoka Sweden ukiongozwa na Balozi Rangnite uliridhishwa na kuvutiwa na maeneo ya
utalii yaliyopo katika mkoa huo yakiwamo pia mazingira rafiki  yanayoruhusu uwekezaji kwa jamii yao.

TANZANIA URUSI ZABADALISHANA UZOEFU WA KUDHIBITI UHALIFU

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAHITIMU 1365 WAMALIZA MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT, SONGE

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge wa pili kulia,akikata utepe jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha Internet Cafe katika kikosi cha 842 KJ Mlale kilichopo wilayani Songea,kulia ni mkuu wa kikosi hicho meja Absolomon Shausi. Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema,mwakilishi wa mkuu wa jeshi la Kujenga taifa Kanali John Mbungo na kushoto ni kaimu mkuu wa Brigedi ya 401 Songea, Meja Absolomon Shausi
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge akikagua gwaride rasmi la vijana 1365 waliojiunga na mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu katika kikosi cha 842 Kj- Mlale Jkt kwa mujibu wa sheria operesheni Magufuri 2016 kilichopo wilayani Songea
Baadhi ya vijana wa operesheni Magufuri 2016 waliojiunga na mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu katika kikosi cha 842 Mlale Jkt wakipita kwa mwendo wa kasi mbele ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge(hayupo pichani) wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo jana.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge katikati akizindua Jarida la Mlale leo linalochapishwa na kikosi cha 842 KJ Mlale JKT kilichopo katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni kaimu mkuu wa kikosi hicho Meja Absolomon Shausi,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Songea Mhe. Palolet Mgema na mwakilishi wa mkuu wa Jkt Kanal John Mbungo.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilth Mahenge katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa baraza la ulinzi na usalama la mkoa wa Ruvuma na maafisa wa mbalimbali wa JWTZ NA JKT mara baada ya kufunga rasmi mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu kwa vijana 1365. Picha zote na Muhidin Amri.

DIANA EDWARD NDIYE LETE RAHA MISS KINONDONI 2016

$
0
0
Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
Warembo hao wakiserebuka wakati wakijitambulisha.
Wadau wakifuatilia kwa karibu shindano hilo.
Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika vazi la ubunifu. Kutoka kushoto ni Catherine Liston, Hafsa Mahamoud na Mariana Charles.
Washiriki hao waliofanikiwa kuingia 10 bora.
Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora. Kutoka kulia ni Hafsa Mahamoud, Diana Edward ambaye ndiye Miss Kinondoni 2016. Regina Ndimbo, Sia Pius na Jackline Kimambo.
Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.
Mgeni rasmi wa shindano hilo, Gift Msuya (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo.
Hapa ni sebene kwa kwenda mbele.
Wakina mama wakimtuza mwanamuziki Christian Bella wakati akiimba wimbo wa Nani kama mama.
Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.

Na Dotto Mwaibale.

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Lete Raha Miss Kinondoni 2016 imemtangaza Diana Edward kuwa mlimbwende wa wilaya hiyo baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana.

Edward aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 20 waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Regina Ndimbo huku ya tatu ikichukuliwa na Sia Pius ambapo Happyness Munisi akishinda nafasi ya utanashati.

Akizungumza wakati wa mchakato wa kutoa zawadi Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George alisema asilimia 10 ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo yatakwenda Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa ikiwa ni kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure katika mazingira bora.

Katika shindano hilo washindi waliofanikiwa kuingia tano bora wataingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia bia ya Windhoek Lager na Draught pamoja na Gazeti la Lete Raha na wadhamini wengine.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya alisema Serikali itaendelea kuunga mkono mashindano hayo ambayo yamekuwa yakitoa ajira na kuibua vipaji vya watoto wa kike.

Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa mwanamuziki wa muziki wa dansi Christian Bella na kundi la sanaa la Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd.

MAGAZETINI LEO; MAGUFULI: SHEIN RAIS HALALI ZANZIBAR ... JPM ASEMA 'JECHA APEWE TUZO'

$
0
0

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI MARA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa akiongea na wazazi,walimu na wanafunzi wa shule ya msingiUtegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa shule hiyo jana. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa mkoa huo. Pichani kutoka kushoto Meneja waTigo Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo,Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande ,Mkuu wa wilaya ya Rorya, Simon Chacha na Mwenyekiti wa Halmashauri mka Mara, Albert Machiwa
Meneja wa Tigo Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa shule hiyo jana.
Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi madawati kwa shule hiyo jana, Wengine pichani kushoto kwake ni mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwana Mkuu wa wilaya ya Rorya, Simon Chacha.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa akipokea madawati 235 kwa mkoa wa Mara toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande kwenye hafla iliyofanyika shule ya msingi Utegi wilayani Rorya jana.
Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt. Charles Mlingwa na Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande wakinyanyua mikono juu mara baada ya makabidhiano ya madawati 135 kwa wilaya ya Rorya na jumla ya madawati 235 kwa mkoa wa Mara, hafla iliyofanyika shule yamsingi Utegi wilayani Rorya jana
Wanafunzi wa shule ya msingi Utegi wakiwa wameketi kwenye madawati waliopewa na kampuni ya simu za mkononi Tigo jana.

NENO LA LEO

$
0
0

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA POLE NYUMBANI KWA MAREHEMU MZEE ABOUD JUMBE MWINYI, AWEKA SHADA LA MAUA KABURINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa Bw. Mustapha Aboud Jumbe na Rajabu Aboud Jumbe alipokwenda kutoa mkono wa pole kwa familia ya Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimu wanafamilia alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka sahihi kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekezwa jambo na Rajabu Aboud Jumbe alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016. Nyuma yao ni Mama Janeth Magufuli na wanafamilia wa Mzee Jumbe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kaburini na kutoa heshima zake alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na ujumbe wake wakishiriki dua alipokwenda kutoa mkono wa pole nyumbani kwa Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kutoa mkono wa pole nyumbani kwa Rais wa awamu ya Pili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi nyumbani kwao Migombani Zanzibar mjini leo Septemba 3, 2016

PICHA NA IKULU.

KILOLO FC KUKIPIGA NA TIMU YA WABUNGE MJINI DODOMA

$
0
0

Venance Mwamoto
---
Na Matukiodaima Blog

KOCHA wa timu ya Bunge Venance Mwamoto ametoa mwaliko kwa timu ya Bodaboda Kilolo kwenda bungeni kucheza mchezo wa kirafiki na wabunge

Mwamoto ambae ni mbunge wa Kilolo mkoani Iringa alitoa mwaliko huo wakati wa kikao chake na vijana hao wa bodaboda mjini Ilula Jana.

Alisema kuwa kabla ya kwenda bungeni vijana hao watashindana kupata bingwa wa
mashindano hayo ambaye atakwenda Dodoma kucheza na wabunge

Hivyo alisema lazima kujipanga vema kwa kujiandaa ili kuepuka aibu ya kichapo kutoka kwa wabunge.

"Nawaomba timu itakayoshinda iwe bungeni kutangaza wilaya getu ya Kilolo kisoka pia kuanza rasmi kwa mashindano ya Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia  Abdalah na mimi mbunge wenu nitadhamini "

Hata hivyo alisema kabla ya mashindano hayo atatoa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama njia ya kuondoka kero ya vifaa vya michezo.

Mwamoto alisema lengo ni kuona vijana Kilolo wanakuwa na timu na kupitia michezo wanapata ajira kwa kuchezea timu mbali mbali kubwa nchini.

WATOTO WA KITUO CHENYE MAHITAJI MAALUM CHAMANZI WAPATIWA MSAADA WA MAGODORO

$
0
0
Meneja wa kitengo cha Masoko wa Benki ya Diamond Trust (DTB), Sylvester Bahati (kulia), akikabidhi magodoro 50 kwa Mkuu wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo Chamazi, Bi. Winfrida Rubanza. Pichani chini ni Bi. Winfrida Rubanza akihojiwa na mwandishi wa habari. Tukio hili liliratibiwa na Benki ya Diamond Trust ikishirikiana na Bi Lorna Dadi ambaye ni mwandishi wa kitabu cha Vipande Vya Maisha.

PICHA YA LEO; RAIS DKT. MAGUFULI AKIDUMISHA MILA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma katika uwanja wa Gombani ya Kale Chake chake kisiwani Pemba mara baada ya kumaliza kuhutubia mamia ya wananchi wa kisiwa hicho jana. Kulia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiangalia. PICHA NA IKULU.

ABRAHAM MOSSI NA RACHEL KISSUI WAFUNGA NDOA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Bwana Harusi Abraham Mossi akiwa na mkewe Rachel Kissui katika nyuso za furaha mara baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa la Boko jijini Dar es Salaam leo Septemba 3, 2016.
 

RAIS DKT MAGUFULI AZURU KABURI LA MAREHEMU SHEIKH ABEID AMANI KARUME, AWEKA SHADA LA MAUA

$
0
0

SIMIYU YAJIPANGA KUANZA KUTENGENEZA CHAKI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akionesha aina tofauti za maboksi yatakayotumika kufungashia chaki nyeupe na za rangi ambazo zinatarajiwa kuanza kuzalishwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa, Mkoani humo wakati alipohitimisha Mafunzo ya Teknolojia ya Utengenezaji wa Chaki kwa vijana hao, (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa, Mhe. Peter Bunyongoli.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe akizungumza na vijana na wadau wengine wakati wa kuhitimisha mafunzo Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwa Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa, katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi (aliyesimama) akizungumza na vijana na wadau wengine wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika hilo kwa Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa.
Baadhi ya Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiangalia sampuli za maboksi yaliyopendekezwa kutumika kufungashia chaki pindi uzalishaji utakapoanza wakati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) akihitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO kwa vijana hao, wilayani humo.

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Serikali Mkoani Simiyu imetangaza azma yake ya kuanza kutengeneza Chaki ambazo zitauzwa
katika Wilaya za Mkoa huo na nchi nzima kabla ya Oktoba 14 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony John Mtaka wakati alipohitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa Chaki kwa vikundi vya vijana Wajasiriamali wilayani Maswa, yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga.

Mtaka amesema shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali Mkoani humo zinatumia jumla ya katoni 1200 za chaki ambazo zinagharimu shilingi 25,000,000 kwa kila mwezi, hivyo kama Vijana wa Wilaya ya Maswa wakizalisha Chaki na kusambaza katika mkoa mzima watajipatia kipato na kuondokana na umaskini.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na
Tanzania ya Viwanda, Mkoa huo umejipanga kuimarisha uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo ambavyo vitazalisha mahitaji ya kila siku ya wananchi, hivyo wamedhamiria kuwa na uzalishaji wa bidhaa moja kwa kila wilaya ( one district one product), ambapo Wilaya ya Maswa itakuwa ikizalisha chaki.


“Wilaya ya Maswa imepokea shilingi 38,000,000 Meatu 31,000,000 kwa ajili ya vijana kutoka
Wizara yenye dhamana na Vijana, sasa hivi tumepeleka maombi ya wilaya zilizobaki. Tumedhamiria kuutambulisha Mkoa kwa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe, tumeanza na Chaki wilaya ya Maswa, Wilaya ya Meatu wao watazalisha maziwa, tutaendelea kutengeza utambulisho(brand) wa wilaya nyingine kwa kuzalisha bidhaa zinazoendana na malighafi zilizopo” alisema Mtaka.

Akizungumza katika hitimisho la Mafunzo hayo kwa Vijana, Meneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi ametoa wito kwa vikundi vya vijana kuwa na mipango itakayowasaidia kutangaza bidhaa zao na kupata soko la bidhaa hizo ndani na nje ya Mkoa ili kujiongezea kipato.

“Mtakapoanza kuzalisha chaki, kulingana na tathmini iliyofanyika kama mtauza kwa Mkoa wa Simiyu tu mtakuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya shilingi 8,000,000 kila mwezi, hiyo si fedha ndogo mkiwa na mipango thabiti mkazalisha chaki bora mtaweza kuuza chaki zenu nchi nzima na hata nje ya nchi” alisema Moshi.

Naye mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya utengenezaji wa chaki, Kelvin Steven ametoa wito kwa Wananchi wa Simiyu na Watanzania kwa ujumla, kuunga mkono juhudi za Vijana Wajasiriamali na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuinua uchumi wa Vijana hao na Taifa kwa jumla.

Aidha, Bi. Specioza Fundikira ambaye pia amepata mafunzo hayo amesema matarajio ya Vijana waliopata mafunzo ni kuwa uzalishaji wa chaki utakapoanza kutakuwa na soko la uhakika kwa Shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali mkoani humo na mikoa ya jirani, vijana watapata ajira na kuachana na shughuli zisizo halali kama wizi na ulevi.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe vijana kutoka vikundi 8 vya Wajasiriamali ambao wameunda kikundi kimoja cha ‘Maswa Youth Enteprises’ wamepatiwa mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa chaki na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kuanzia tarehe 29/08/2016 hadi tarehe 03/09/2016.

RAIS DKT MAGUFULI ALIPOHUTUBIA WANANCHI UWANJA WA DEMOKRASIA ZANZIBAR JUMAMOSI

$
0
0

Viongozi mbalimbali wakiwa wamejipanga kumsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khatib alipowasili   kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Uchumi na Ushiriuka.Mhe Haroun Ali Suleiman  kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA  Mhe. Juma Ali Khatib  kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa kabla  kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba   kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akioungia umati kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Mafundi mitambo wa AZAM TV  wakiongozwa  na Mehboub Al Hadad wakiwa tayari kurusha live mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Shekhe akitoa mawaidha kabla Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuhutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na viongozi wengine wakiwa  katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru Shekhe wakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Shekhe akipongezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe.  January Makamba na waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi
Jukwaa kuu
Wasomautenzi walisisimua umati
Wasoma utenzi wakipongezwa jukwaa kuu
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Sehemu ya viongozi mbalimbali wakifuatilia mkutano
Jukwaa kuu
Risala 
Pongezi kwa msoma risala
Bendi ya vijana
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisoma muhtasari wa shughuli na kutambulisha wageni
Sehemu ya umati mkubwa uliojitokeza
Umati
Nyomi
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitambulishwa
Mke wa Rais wa Zanzibara Mama Mwanamema Shein akitambulishwa
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akitambulishwa
Mawaziri wakitambulishwa
Viongozi wa vyama mbalimbali wakitambulishwa
Bw. Hafidh Ameir, mume wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Abdulhamid Yahya Mzee akitambulishwa
Viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa wakitambulishwa
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud akisoma muhtasari wa shughuli na kutambulisha wageni
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akisalimia viongozi
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha akitambulishwa jukwaani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakiongea
Mama Fatma Karume akitambulishwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakiongea, Kushoto ni  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisalimia
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akisalimia wananchi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ, Mhe. Haji Omar Kheri akisalimia
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe Vuai Ali Vuai akisalimia
Umati ukshangilia
Furaha
Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA  Mhe. Juma Ali Khatib  akisalimia
Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA  Mhe. Juma Ali Khatib  akipongezwa 

Mwananchi akifurahia hotuba
Umati ukifuatilia hotuba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikaribishwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuhutubianmkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Jukwaa kuu wakifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe akihutubia Magufuli mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016 
Jukwaa kuu likifurahia hotuba
Viongozi wakifurahia
Umati wa wnanchi  ukimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja Jumamosi Agosti 3, 2016
Umati ukisikiliza kwa makini hotuba hiyo

KARIAKOO KUWA MKOA MAALUMU WA KODI- KAYOMBO

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Kuhusiana na mikakati mbalimbali waliyojiwekea Mamlaka ya Mapato(TRA) ili kuhakikisha Mapato yanakusanywa ipasavyo.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo

Baadhi ya waandishi wa Habri wakimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
---
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

ENEO la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini eneo hilo litasaidia kwa kila mfanyabiashara kuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Amesema kuwa hiyo ni moja ya Mkakati wa harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati.

Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka huu wa fedha.

Kayombo amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti Mwaka 2015 TRA ilikusanya Billion 923.

Pia Kayombo ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo TRA vilivyo karibu kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo.

Amesema kuwa vituo vya kuhakiki taarifa zao ni pamoja na vitua vya

• Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)

• Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara

• Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu

• Wilaya ya Kigamboni - Ofisi za TRA Kigamboni

Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji.

Kayombo pia amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla Septemba 30 mwaka huu kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe Oktoba 1 na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

Na walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.
Viewing all 19874 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>