Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19851 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WA CUBA NA INDIA IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na balozi wa India nchini Mhe.Sandeep Arya aliyekutana naye na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiangalia Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara akisalimiana na balozi wa Cuba nchini Mhe Jorge Lopez Tormo kabla ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na balozi wa Cuba Mhe Jorge Lopez Tormo nchini Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 30, 2016

PICHA NA IKULU.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AMJULIA HALI MTOTO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI JIJINI DAR

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akimjulia hali mwanafunzi wa Darasa la 4 wa Shule ya Msingi ya Mount Kibo ya Mbezi Beach ya Jijini Dar es Salaam, David Kamoga , anayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba, Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Baada ya kujeruhiwa kwa kugongwa na Gari aina ya Hiace eneo la Tegeta Namanga, kulia ni baba wa mtoto huyo, Hudson Kamoga. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

SERIKALI HAIJAKURUPUKA KUNUNUA NDEGE ZA BOMBADIER Q400: PROFESA MBARAWA

$
0
0
Serikali imesema kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT)

Mbarawa alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
“Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali halisi ya Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa baadhi, huku lengo ni kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa Mbarawa.

Mbarawa aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo mbalimbali ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.

Aliongeza kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.

Prof. Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa ndege hizo katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa safari moja.
Na Abushehe Nondo na Sheila Simba - MAELEZO - Dar es Salaam.

Waziri Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na Kampuni hiyo.

Mpaka sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa asilimia 40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19 septemba mwaka huu ambapo zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15 septemba mwaka huu kupitia nchini Uingereza.

Akizindua mafunzo hayo ya wakufunzi wa marubani, Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.

“Hatutaki kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu, hakikisheni mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika sekta hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro lakini bado anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof. Mbarawa.

Aidha amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za urubani ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini.

JWTZ KUADHIMISHA SIKU YAO SEPTEMBA MOSI KWA KUFANYA USAFI NA WANANCHI NCHI NZIMA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) juu Maadhimisho ya kilele cha miaka 52 ya jeshi hilo.
Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kazi mbalimbali watakazozifanya katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi hilo.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akisalimiana namakamanda wa Jeshi la Ulinzila Wananchi wa Tanzania JWTZ, alipokutana nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016. JWTZ itaadhimisha miaka 52 kwa kufanya usafi kote nchini.

Na Bakari Issa Madjeshi, Globu ya Jamii

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ linatarajia kuadhimisha siku ya  kilele cha miaka 52 tangu kuzaliwa kwake kwa kufanya usafi wa mazingira  sambamba na uchangiaji wa damu.

Akizungumza na Waandishi wa  Habari wakati alipokutana na Maafisa wa Jeshi hilo Mkuu wa Mkoa wa Dar  es Salaam, Paul Makonda amesema JWTZ inapotimiza miaka 52 ni fahari  kubwa hivyo tunapaswa kuwapongeza kwa kudumisha amani na  mshikamano,kusaidia mataifa mbalimbali pamoja na kulinda mipaka ya nchi.

Makonda amesema kuwa Wananchi wanapaswa kuungana nao katika kazi mbalimbali wanazofanya katika mkoa wa Dar es Salaam.

"Wakuu wa Wilaya wamejipanga kuainisha maeneo ambayo yatafanyiwa usafi hivyo kama kuna mwananchi anataka kushiriki nao usafi na Wanajeshi siku ya  kilele, Septemba mosi basi asubuhi na mapema waripoti kwa Wakuu hao wa  Wilaya na watapangiwa jinsi gani wataweza kushirikiana nao"amesema  Makonda.

" Pia wamekubali kuchangia Damu hii itasaidia kutokana  na mahitaji ya Damu ni makubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na pia hospitali za Mwananyamala, Temeke na Amana"ameeleza Mkuu wa Mkoa  huyo wa Dar

Pia ametoa wito kwa wananchi wapenda amani kujitokeza kwa wingi kuchangia damu katika maeneo ya Lugalo, JKT Kawe na maeneo mengine ya kambi yenye vituo vya uchangiaji damu.

Akithibitisha kuwepo kwa Maadhimisho ya kilele cha miaka 52 ya JWTZ, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema Mkuu wa Majeshi amefarijika  kushiriki kikamilifu katika shughuli zao za kuadhimisha miaka 52 ya Jeshi hilo.

Kanali Lubinga amesema wamefarijika kuona Mkoa wa Dar es Salaam umeshiriki nao katika shughuli mbalimbali za Jeshi hilo  ikiwemo shughuli za usafi.

"Siku hiyo ya kilele shughuli zetu  zitakuwa ni utoaji damu, kufanya usafi kutokana na usafi ni afya na ni  amani" amesema Kanali Lubinga

Amesema kutakuwa na Madaktari wa  Jeshi watakao toa huduma za ushauri kwa magonjwa mbalimbali kama  Kisukari pamoja na Shinikizo la Damu sambamba na kushiriki Michezo.

Pia amesema Ndege za kivita zitakuwa zitapita kuashiria siku ya kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi hilo.

UJUMBE WA LEO; SIASA NI MAJIRA - HAYATI SHAABAN HAMIS MLOO - CUF

$
0
0
Wanaolazimisha mambo yasiyowezekana katika SIASA kwa kuwa tu nafsi zao zinayapenda au wana maslahi binafsi hata kama hayana tija, hawajajifunza majira ya siasa. Mwanasiasa yeyote asiyejifunza majira ya siasa hawezi kuyadhibiti. Siasa ni MAJIRA, tujiandae kabla hayajafika maana huja na upepo wake na hayadhibitiki."

Hayati Shaaban Hamis Mloo,
Makamu Mwenyekiti wa CUF,
Februari 2004.

MAGAZETINI LEO; LOWASSA SASA ATUMA WARAKA POLISI, CCM ... MAKUSANYO KODI ZA SIMU YAPANDA MARA 5

$
0
0
 
 

CHEKA UNENEPE; MJINI SHULE ... JIFUNZE NAMNA YA KUDAI DENI LAKO

$
0
0
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp...!

Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang'oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri.

Kisha nikaituma ile message

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake... Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

Akatuma message akiniuliza...

Hao wanawake unawajuwa, ...mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli...!

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa...!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa...! Akaniandikia message nyingine....

...Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe... Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri...!

Nami nikamjibu...

Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo...!


Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai...!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa.... Kama sio mie!

MAONI YA MSOMAJI; WOSIA WANGU KWA WANAHABARI KUELEKEA SEPTEMBA MOSI

$
0
0
Tunaelekea siku ya Septemba Mosi siku ni ambayo wanasiasa nchini kama wanataka kututumia ngazi kwa maslahi yao ya kisiasa.

Nashauri mambo yafuatayo;

(1). Kamwe tusikubali kutumika ama kutumiwa kwa ajili ya kuwakweza wanasiasa kwa kuwa siku zote furaha yao imekuwa mauti yetu.

(2). Tufanye kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma yetu bila kushabikia upande wowote wa kisiasa ili kuwa salama kwa kuwa STORI nzuri ni ile itakayokuacha ukiwa HAI.

(3). Tutambue kuwa hata tukiwa kimbelembele namna gani siku hiyo hakuna tija wala maslahi tutakayopata zaidi ya kubaki na maumivu, majeraha na hata vifo na kuziacha familia zetu zikihangaika na wengine wakibaki wajane na yatima.

(4). Siasa sio kila kitu katika taaluma ya habari kwani tunaweza kuandika habari za kijamii zinazoweza kusaidia kuibua kero na matatizo ambayo hatimaye yatasaidia chachu ya maendeleo kwa jamii husika.

(5). Tutumie kalamu na kamera zetu kuwaangazia akina mama na watoto wanaokosa huduma za afya na baadhi yao kufa kwa kukosa dawa ama huduma nzuri katika vituo vya Afya.

(6). Tuibue na tutafiti sababu za kukwama kwa maendeleo katika maeneo yetu na kuwamulika watendaji wanaojifanya miungu watu ambao wanasababisha nchi yetu na wananchi wake waendelee kuwa maskini na kuishi kwa mlo mmoja kwa siku.

(7). Nasisitiza hatutasifiwa kwa kuwa kimbelembele kukaa kwenye taget na kulegwa shabaha kwa kudhani kuwa kwa kufanya hivyo tutasifiwa.

RASHID MKWINDA,
-MSHINDI WA NNE WA TUZO YA HABARI ZA RUSHWA NA UTAWALA BORA 2008/MAZINGIRA(2013).

'TUNATAFUTA HELA MUDA WA KUANDAMANA HATUNA': BODABODA WA ARUSHA

$
0
0
Na Aron Msigwa.

"Mimi ni Bodaboda, nikuambie ukweli tu brother sitaandamana kabisa, nikose kutafuta hela nikalie kuandamana, watakaoandamana watajuta maana polisi wa hapa Arusha wamejifua vya kutosha tumewaona mtaani waandamane hao hao wasio na kazi sio mimi"

Hayo ni maneno ya kijana Omary dereva wa Bodaboda jijini Arusha wakati akitoa maoni yake kuhusu maandamano ya UKUTA ya Septemba Mosi.

Anasema vijana watakaokubali kutumika na kuingia mtaani wasivumiliwe kwa kuwa wakazi wa Arusha muda huu wako busy na kazi kutafuta hela.

" Kama unavyoniona mimi na jamaa zangu hawa tuko barabarani na bodaboda zetu tunafanya kazi, tukianza kuandamana kushindana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa maandamano yaliyopigwa marufuku na Serikali afu tupata madhara nani atalisha familia zetu? Lazima tutumie akili hatukubali " Anasisitiza Omary.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA TAASISI YA AFRICA MATTER LIMITED YA UINGEREZA MHE. LYNDA CHALKER

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalkeraliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimkaribisha kuketi Mwenyekiti wa  Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker aliyemtembelea kwa mzungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli akimsindikiza Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya mzungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016.
 
"Hapa kazi tu..." anaonekana kusema Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited ya Uingereza Mhe. Lynda Chalker baada ya mzungumzo yake na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 31, 2016.

BEI YA MADAFU LEO AGOSTI 31, 2016

$
0
0

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA BW. DOTTO JAMES KUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

$
0
0
Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto M. James.

MAMA WA MITINDO NA YASIN KAPUYA KUIWAKILISHA TANZANIA MAREKANI

$
0
0
Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin kutoka Tanzania anategemea kuiwakilisha Tanzania kwa kuonesha mitindo yake katika jukwaa kubwa la biashara nchini Marekani katika mji mkuu wa California, Sacramento.

Show hiyo inatambulika kama 'The African Trader Show', Tamasha litafanyika siku 3 kuanzia Tarehe 2 mwezi wa 9/2016 - 4/9/2016. Mbali na Asya pia Mr. Yasin Kapuya atawakilisha Tanzania kwa kutoa mada na kuonesha ufundi wa kazi zake katika onesho hilo.

AIRTEL NA VETA KUENDELEA KUELIMISHA VIJANA KUPITIA VSOMO APPLICATION

$
0
0
Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mafanikio ya mafunzo ya stadi za ufundi yanayotolewa na VETA kupitia mtandao wa simu ya mkononi wa Airtel yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO katika ofisi za makao makuu ya Airtel Tanzania zilizoko Moroco jijini Dar es Saalam hapo jana.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa kijamii wa Airtel FURSA ikishirikiana na Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) imeendelea kuwawezesha vijana kupata kozi mbalimbali zinazotolewa katika vituo vya VETA nchini kupitia application ijulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO.

Akiongea na waandishi habari afisa Uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema, “vijana wameufurahia sana mpango huu unaowawezesha kusoma masomo kutoka VETA kwa urahisi zaidi na kuchochea kukua kwa elimu kwa vijana wengi na kuwawezesha kupata ujuzi wa ufundi na biashara itakayoongeza ufanisi wao”.

“Mafunzo kwa njia ya mtandao ni rahisi na yatapatikana kwa wateja wa Airtel wenye simu zenye mfumo wa android. Mteja atatakiwa kupakua application ya VSOMO kwenye orodha ya menu yake ya simu sehemu ya google play store na kujiandikisha bure. Mara baada ya kumaliza masomo yake kwa 40% mwanafunzi atatakiwa kwenda kwenye kituo cha VETA kilichopo karibu nae na kujiandikisha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo ambayo yatachukua muda wa wiki 2 kumaliza ikiwa ni sawa na masaa 60 na ndipo atakapokaa kwaajili ya mtihani na kutakiwa kufaulu kwa 60% “alisisitiza Kaniki.

Aliendelea kusema kuwa “vijana zaidi ya 19000 wamejisajili kusoma kozi mbalimbali kutoka VETA kupitia simu zao za mkononi. Kwasasa masomo yanayopatikana ni Ufundi pikipiki (bodaboda), Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium, utaalamu wa maswala ya urembo na ufundi wa kuchomelea vyuma.”

Akibainisha hayo Kijana Saleh Shomari anayesoma kozi ya ufundi umeme kupitia application ya VSOMO alisema “ VSOMO imekuwa msaada kwangu maana nilikuwa natamani kusoma kozi VETA lakini sikuwa na mda wa kufika chuo cha VETA kutokana na mihangaiko ya biashara zangu, lakini nawashukuru Airtel na VETA kulionahili na sasa najisomea mafunzo haya ya umeme jioni nikishafunga biashara yangu na kuweza kufikia malendo yangu ya kupata cheti kutoka VETA.”

Dangio alimalizia akisema” Mwanafunzi atatahiniwa na kisha kuandikishwa na kutakiwa kulipia kiasi shilingi 120,000/= kwa kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kama gharama ya mafunzo hayo. Tunatoa wito kwa vijana kutumia fursa hii ya kipekee ili kupata mafunzo ya ufundi kwa urahisi na gharama nafuu kwani gharama ya masomo iko chini zaidi.”

MASAUNI AZINDUA PROGRAMU YA “TUNZA AMANI IKUTUNZE” JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO) , Kulia ni Mkurugenzi wa shirika hilo, Askofu Nason Ngoy Ngoy. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO). Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba akizungumza mara baada ya uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Askofu Nason Ngoy Ngoy, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Goodluck Ole Medeye, mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)

MNEC MUFINDI AWATAKA WANANCHI KUJIANDAA NA MILIONI 50 ZA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

$
0
0
Na MatukiodaimaBlog

WANANCHI wilayani Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kuanza maandalizi ya kunufaika na milioni 50 kwa kila kijiji zilizopangwa kutolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanza kujiunga vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili.

Wito huo umetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa kutoka wilaya ya Mufindi, Marcelina Mkini (Pichani) wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utaratibu huo mzuri ulioahidiwa na Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni.

Alisema kuwa ili wananchi kuweza kunufaika na utaratibu huo ni lazima kujiunga katika vikundi vya watu wenye malengo yanayofanana na kuvisajili ili pindi pesa hizo zitakapotolewa kuweza kuzipata.

Mkini alisema kwa utaratibu wa fedha hizo hazitatolewa kwa mtu mmoja mmoja hivyo kwa wale ambao wanazitamani fedha hizo ni lazima kuanza kujiunga katika vikundi ambavyo vimesajiliwa.

"Lengo la Rais wetu ni kuona wananchi wananufaika na matunda ya nchi hii ndio sababu ya kuahidi kusaidia vijiji fedha hizo shilingi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo ni nyingi sana na zitasaidia wananchi kujikwamua katika dimbwi la umasikini ... lazima tumpongeze sana kwa mtazamo huu ambao haujapata kutokea"

Hivyo alitaka vijana, wanawake na wazee kujiunga makundi yenye malengo yanayofafa yakiwemo ya ufugaji kwa wazee ama kilimo na makundi mengine ambayo yatapelekea vijiji kuwa na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) zao.

Mkini ambae pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (CWT) wilaya hiyo ya Mufindi aliwataka viongozi wote wa UWT ngazi zote kusaidia kuhamasisha wanawake kuonyesha mfano katika kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali .

Huku akiwataka kwa kipindi hiki cha kuelekea kupata fedha hizo kuwa makini na matapeli ambao baadhi ya mikoa wameanza kujipitisha kudanganya wananchi kuwa fedha hizo zitapitia katika NGOs zaO.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd. Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, atayeshuhulikia masuala ya Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na Nd. Hassan Khatib Hassan,baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshughulikia Idara Maalum za SMZ,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini hati ya kiapo ya ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimkabidhi hati ya kiapo ACP Sida Mohamed Himid baada ya kumuapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, anayeshuhulikia Idara Maalum za SMZ, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Makamanda Wakuu wa Vikosi vya SMZ walihudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi, walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Baadhi ya Mawaziri wa Wizara za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi katika taasisi mbali mbali walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo. Picha na Ikulu ya Zanzibar.

TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA KASKAZINI KUFANYIKA SEPTEMBA 11, 2016

$
0
0
Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma akiongea na waandishi wa habari.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Chama cha waandishi wa habari za michezo na Burudanimkoa wa Arusha (TASWA ARUSHA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Arusha Media wameandaa tamasha la 11 la waandishi wa habari za michezo na burudani kanda ya Kaskazini ambalo litafanyika Septemba 11 katika uwanja wa Generat Tyre.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma alisema zaidi ya watu 2500 wanatarajiwa kushiriki Tamasha hilo, ambapo kutakuwa na michezo ya Soka, Kuvuta kamba, Mbio za magunia ,Kukimbiza kuku na muziki kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.

Juma alizitaja timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, timu ya Radio ORS kutoka mkoa wa Manyara, timu ya Sunrise Radio, Timu ya chuo cha uandishi habari Arusha, timu ya MJ Radio na timu ya Triple a Radio.

Katika tamasha hilo, pia kutakuwa na timu za vyuo vya uandishi habari vya mkoa wa Arusha, chuo cha habari Maalum, Tasisi ya habari na mawasiliano iliyopo maji ya chai, TASWA Arusha.

“Tamasha litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoani Arusha juu ya masuala ya michezo, Utalii wa ndani na umuhimu wa Uwekezaji katika taifa”alisema

Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alifafanua kuwa pia kuna timu ambazo zimealikwa ambazo ni Kitambi Noma, Timu ya TANAPA,timu ya TBL Arusha, timu ya PEPSI na Coca Cola na Wenyeji timu ya Wazee Klabu.

Ngobole alisema Septemba 3, TASWA na Arusha Media watatangaza zawadi kwa washindi, wadhamini wote na Mgeni rasmi.

CHRISTIAN BELLA KUPAMBA SHINDANO LA MISS KINONDONI 2016, KESHO KUTWA UKUMBI WA DENFRANCES SINZA JIJINI DAR

$
0
0
Warembo hao wakiwa mbele ya ghala zinamo hifadhiwa bia za Windhoek wakati wa ziara hiyo.
Mshauri wa Miss Kinondoni, Boy George (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo. Kutoka kulia ni Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo,Constantine Mwafulilwa, Andrea Missana, Mratibu wa Shindani la Miss Kinondoni Rhamat George na Mwalimu wa warembo hao, Neema Chaky.
Mratibu wa shindano hilo, Rhamat George (katikati), akizungumza katika mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale.

Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi hapa nchini Cristian Bella anatarajiwa kuwasha moto katika shindano la kumsaka Malkia wa Ulimbwende

Kanda ya Kinondoni linatarajiwa kufanyika kesho kutwa Ijumaaya katika Ukumbi wa Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwa kutanisha warembo hao na wadhamini washindano hilo ambao ni Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambao ni wasambaji wa kinywaji cha Windhoek Dar es Salaam jana, Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo, Andrea Misama alisema maandalizi ya shindano hilo yanaendalea vizuri ambapo aliwashukuru warembo wote waliojitokeza kwenye shindano hilo kwa mwaka huu na kuwa mwanamuziki huyo akishirikiana na kundi la sanaa la kampuni hiyo watapamba jukwaa kwa kutoa burudani la kukata na shoka.

"Mwaka huu washiriki waliojitokeza ni wengi ukulinganisha na mwaka jana, hivyo tunatoa pongezi kwa wazazi waliowaruhusu watoto wao kushiriki, malengo yetu ni kukuza vipaji na kutoa ajira kwa wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao”, alisema.

Kwa pande wao warembo watakaoshiriki shindano hilo wameahidi kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuwaomba wadau na mashabiki waurembo kujitokeza kwa wingi siku ya shindano ili wawezekusapoti Miss Kinondoni.

Shindano hilo linashirikisha warembo 20 kutoka vitongoji mbalimbali vya Kanda ya Kinondoni ambapo kiingilio kitakuwa sh 10,000 na 20,000 kwa VIP huku shindano hilo likipambwa kwa burudani kutoka kwa mkali wa masauti Christian Bella.

RAIS DKT. MAGUFULI AMEMTHIBITISHA BW. GERSON MSIGWA KUWA MKURUGENZI WA KITENGO CHA MAWASILIANO YA RAIS (DIRECTOR OF PRESIDENTIAL COMMUNICATION-DPC)

$
0
0

Viewing all 19851 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>