Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19795 articles
Browse latest View live

KANUNI 30 KWA WANAWAKE NDANI YA NDOA

$
0
0
1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima.

2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako.

3). Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha.

4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.

5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo.

6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako.

7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe.

8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha.

9). Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo.

10). Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu.

11). Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.

12). Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la mwanaume ni heshima.

13). Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo.

14). Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.

15). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo.

16). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa.

17). Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu.

18). Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake.

19). Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.

20). Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu.

21). Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu.

22). Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi.

23). Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula.

24). Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake.

25). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli.

26). Usisuhubiane na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa.

27). Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa.

28). Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri.

29). Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa.

30). Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako.

Ninakutakia ndoa njema. Usisahau ku share na wenzako kusambaza ujumbe huu muhimu.

Na Kenneth Magoma Jr.

BURUDANI YA LEO; SIJIWEZI - TOPAZZ MILLENIUM

$
0
0

MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA JWTZ, JKT MGULANI YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR

$
0
0
Meja Dora Kawawa wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa 831 KJ Mgulani (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula, Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, Dar es Salaam leo jioni , ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambapo kilele chake kitakuwa Septemba Mosi mwaka huu.
Maofisa wa Jeshi wa kikosi hicho wakifurahi na watoto wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wao.
Msaada ukitolewa.
Hapa ni furaha pamoja na watoto hao.
Watoto wakipata msaada huo.
Watoto wakipokea msaada.
Hapa ni furaha tupu kwa watoto kwa kupokea msaada kutoka kwa wazazi wao hao.
Picha ya pamoja na watoto hao na viongozi wao.

Na Dotto Mwaibale.

JESHI la Kujenga Taifa Kikosi 831 Kj Mgulani limetoa msaada wa vyakula na sabuni kwa watoto waishio Makao ya Taifa ya Watoto Wenye Shida Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo kwa niaba ya mkuu wa kikosi hicho Dar es Salam , Meja Dora Kawawa alisema ni moja ya sehemu ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

"Tumeamua kushiriki shughuli za kijamii kama kutoa msaada na kufanya usafi ikiwa ni kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa jeshi letu ambapo kilele chake kitakuwa Septemba mosi mwaka huu" alisema Kawawa.

Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance alishuru JKT kwa msaada huo na kueleza ni muhimu sana kwa watoto hao na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora la kesho.

MWANARIADHA ALPHONCE FELIX SIMBU ALA MKATABA WA MWAKA MMOJA TOKA DSTV TANZANIA

$
0
0
Mwanariadha Alphonce akisaini mkataba mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande wakati wa hafla ya kumtangaza mwanariadha huyo kuwa balozi wa DSTV Tanzania.
Mwanariadha Alphonce abadilishana mkataba na Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande mara baada ya kusaini na mkumtangaza kuwa balozi wa DSTV Tanzania pambeni ni Rais wa Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka (Kushoto) na kulia ni Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Furaha Samalu.
---
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imesaini mkataba wa mwaka mmoja na mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliyeshiriki mashindano ya Olympic ya Rio 2016 yaliomalizika hivi karibuni huko nchini Brazil na kushika nafasi ya 5 kati ya wanariadha 157 kwenye mbio za Marathon za wanaume.

Katika Mkataba huu, Kampuni ya Multichoice Tanzania imemzawadia Alphonce Simbu shilling za Kitanzania 1,000,0000 ambazo atalipwa kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni kumsadia katika maandalizi yake ya mashindano yajayo ya IAAF WORLD CHAMPIONSHIP yanayotarajiwa kufanyika mjini London Uingereza August 2017.

Vile vile bwana Alphonce Simbu atapatiwa vifaa maalumu vya kumuwezesha kufanya mazoezi yake vyema. Vifaa hivi ni kama vile, viatu na nguo za mchezo wa Riadha.

Si hivyo tu bali Kampuni ya MultiChoice itamtengenezea makala yenye kuonyesha matukio mbalimbili aliyopitia ya Kimichezo na Familia siku za nyuma. Vile vile watarekodi mazoezi atakayokuwa anafanya akiwa katika kambi ya riadha Chuo cha Wakala wa Mistu Fiti kilichopo West Kilimanjaro eneo la Ngarenairobi Wilaya ya Sia Mkoa Kilimanjaro. Makala hii itarushwa kwenye DStv hapo baadae.

Katika Kipindi hicho cha mkataba huu Alphonce Felix Simbu atakuwa Balozi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambapo atashiriki katika promosheni mbalimbali kutangaza huduma zake.

Alipokuwa akisaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande mbele ya Rais wa Riadha Tanzania na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, mwalimu wa wake Alphonce Nd. Francis John Marcially pamoja na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Furaha Samalu, alisisitiza kuwa “Kuu ni mwanzo na kadri mafanikio yanavyo ongezeka Multichoice itakuwa tayari kuwa mstari wa mbele kushirikiana na chama cha riadha Tanzania katika kunyanyua riadha Tanznaia na kurudisha heshma ya taifa kwenye mchezo huo”.

'NIMEUPOKEA UTEUZI' - JULIUS MTATIRO

$
0
0
Imeandikwa na Julius S. Mtatiro

Ndugu zangu, nimepokea majukumu niliyokabidhiwa na Baraza Kuu la chama changu. Siwezi kuepuka majukumu haya muhimu kwa wakati huu ambapo chama kinahitaji mchango wangu. Niko IMARA sana, natambua nimepewa majukumu wakati gani na nianze na mguu upi kwenda mbele.

Uongozi ni MZIGO na si kazi nyepesi, nahitaji kusaidiwa, kushauriwa, kuombewa na kuungwa mkono na watu wenye nia njema na siasa za mabadiliko ya kweli hapa nchini, walio ndani na nje ya CUF.

Natambua kuwa wapo wana CUF wenye sifa, uwezo, vigezo na busara kunishinda, lakini kwa sasa chama kimeona naweza kuuungana na wenzangu kukisimamia. Naahidi kuwa ntatoa uongozi wa KISASA wenye kushughulikia MASUALA. Ntatimiza wajibu wangu bila hofu yoyote kama kawaida yangu na ntatoa UONGOZI WA PAMOJA (Collective Leadership) kwa kila mwenye nia safi na CUF na mabadiliko.

Nitakuwa mhimili imara katika kipindi hiki cha mpito, kuhakikisha CUF inafanya kazi zake na inaimarika ili kujenga uwezo wa ndani, kulinda mtandao wake na kujitanua katika maeneo yote ya Bara na Zanzibar - lakini pia, ntahakikisha ushirikiano wa CUF na vyama vyote vyenye nia njema ya kupigania mabadiliko hapa Tanzania, unazidi kuimarika ili mwisho wa siku watanzania wafaidike na juhudi za mabadiliko hayo.

Mtanzania yeyote anaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa njia za ujumbe mfupi na WHATSUP kwa namba +255787536759, na Barua Pepe: juliusmtatiro@yahoo.com, na atajibiwa. Tutaendelea kuwa karibu kwa hali na mali.

Nakishukuru chama changu kwa kuniamini. Nawashukuru wanachama wote na watanzania wenzangu walionitumia salamu za pongezi ambazo sina uwezo wa kuzijibu zote.
Mungu awabariki sana.

Julius Mtatiro,
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi,
The Civic United Front (CUF).

MWANDISHI SIMON KIVAMWO ANAHITAJI DAMU KUOKOA MAISHA YAKE, SHIMYE WANAHABARI NA WADAU

$
0
0
Bw. Simon Kivamwo
Waandishi wa habari wakitoa damu ili kuwezesha matibabu ya Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Ocean Road iliyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo Bw.Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na maradhi leo hii na kukimbizwa kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari walihitaji kumuongezea damu. 

Benjamin Thomspon ametoa wito kwa wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwandidhi mwenzetu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

SIMBA KUKIPIGA NA POLISI DODOMA SEPTEMBA 3, 2016 UWANJA JAMHURI MJINI DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara akizungumza na Waandishi wa habari leo kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli za kuhamia Dodoma na kuridhia timu yake kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Polisi Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoani Dodoma (DOREFA) Mulamu Nghambi.
---
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Simba imekubali mwaliko wa kwenda kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Polisi Dodoma ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Raisi Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli za kuhamia Mkoani Dodoma.

Mwaliko huo umeletwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma. Mwenyekiti wa Mulamu Nghambi amesema kuwa wao kwa pamoja wanaunga mkono juhudi za Raisi za kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani kwao kwani zitaleta maendeleo makubwa.

Nghambi amesema, walituma maombi yao kwa uongozi wa klabu ya Simba na waKaonesha nia ya kushirikiana katika harakati hizo kwani mkoa wa Dodoma una mashabiki wengi wa timu ya Simba na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Septemba 03 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wa Simba Haji Manara amesema kuwa wamefurahi kupata mwaliko huo na kwa kuwa hakuna ratiba ya ligi wikiend hii nawaahidi mashabiki wa Simba mkoani Dodoma kusubiri ujio wetu kwa shangwe zote.

"Katika kuhakikisha tunaunga hoja za Raisi John Pombe Magufuli za kuhamishia makao makuu ya nchi Mkoani Dodoma  na Chama cha Mpira wa Miguu mkoani humo kutupatia mwaliko tumeupokea kwa mikono miwili na tunawataka wanachama na mashabiki wa timu ya Simba kuja kushuhudia mchezo wetu na Polisi Dodoma siku ya Jumamosi Septemba tatu mwaka huu,"amesema Manara.

Kikosi cha Simba kitaondoka Alhamisi wakiwa na wachezaji wao wote waliosalia baada ya wengine kuwepo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa.

WATOTO WENYE USOJI (AUTISM) WANAOSOMA SHULE YA MSINGI MBUYUNI WAPATIWA VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
Pamoja na kuwa bora utoaji wa huduma za kibenki lakini pia benki ya NMB imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora katika kusaidia jamii na katika kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa vya kutumia darasani na vya michezo kwa watoto walio na usonji (autism) ambao wanasoma katika shule ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Akielezea kuhusu msaada huo, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo alisema wameamua kutoa msaada kwa shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye usonji kusoma katika mazingira mazuri hasa kutokana na hali zao jinsi zilivyo.
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya shuleni kwa wanafunzi wa usonji katika shule ya Msingi Mbuyuni.

"NMB kila mwaka tunatenga asilimia moja ya faida ambayo tunaipata katika kusaidia jamii, tumeshatoa misaada mingi kama madawati na sasa tuliona tuwasaidie watoto hawa na tunaamini msaada wetu utaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa," alisema Bi. Bishubo.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi aliwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia shule ya Mbuyuni na kuwataka kuendelea kuwa na moyo huo kwa kutoa msaada katika shule zingine zilizo na mahitaji.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akiwashukuru NMB kwa msaada ambao wamewapatia ambao unakadiriwa kuzidi Milioni 7.

Alisema licha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali lakini bado inahitaji wadau wengine wa kusaidiana na kama kunakuwa na wadau kama NMB ambao wanajitoa kusaidia jamii basi wanakuwa wadau wa ukweli ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo.

"Kwa nia yenu ya kusaidia jamii basi nyie mnaipatia kabisa serikali sababu inajitahidi kuleta elimu bora na hata kwa watoto hawa ambao bado kuna changamoto ya vifaa kwahiyo sisi tuwashukuru kwa msaada wenu na msisite tena kutusaidia siku tukiwafata kwa kuomba msaada," alisema Mushi.

Na Rabi Hume, MO BLOG
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dorothy Malecela akitoa neno la shukrani kwani niaba ya uongozi wa shule na wanafunzi. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akimshukuru Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa msaada ambao wamewapatia.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi na Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo wakicheza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mwonekano wa baadhi ya vifaa vya michezo ambavyo NMB imetoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbuyuni.

MAONESHO YA BASHARA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA JIJINI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, hii leo akifungua Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.

Maonesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, yalianza Agosti 26,2016 na yanatarajiwa kufikia tamati Septemba 04,2016 katika viwanja wa Rock City Mall.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mara, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.

Wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamehimizwa kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko la pamoja la nchi hizo kutokana na soko hilo kuwa na idadi kubwa ya wateja.

Akifungua maonesho ya 11 ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema soko lililopo kwenye nchi hizo lina zaidi ya wateja milioni 140 na hivyo likitumika vizuri litatoa fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe kwa wenyewe.

Kwenye hotuba ya ufunguzi iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt.Leonard Massale,mkuu huyo wa mkoa amesema badala ya wafanyabiashara hao kutegemea masoko ya nje yanayofikika kwa gharama kubwa,wanapaswa kuuziana bidhaa ndani ya nchi za Afrika Mashariki na hivyo kuinua uchumi wa nchi hizo.

Aidha amewahimiza waandaaji wa maonesho hayo chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo nchini, TCCIA, kuyatangaza zaidi ili yavutie makampuni mengi kutoka nchi zingine.

Katika hotuba yake Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, amesema licha ya kuandaa maonesho hayo kwa miaka 11 mfululizo bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na eneo linalofaa kwa ajili ya maonesho hayo na hivyo kulazimika kuhama mara kwa mara na kuiomba serikali kuharakisha upimaji wa eneo la maonesho Nyamuhongolo ili kujenga majengo ya kudumu.

Maonesho ya mwaka huu yanashirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, China na wenyeji Tanzania ambapo kuna mabanda ya bidhaa mbalimbali pamoja na wanyama hai.

WAZIRI NAPE AZINDUA MICHEZO YA UMOJA WA VYAMA VYA WALIMU WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
Rais wa Chama cha Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.
---
Lorietha Laurence - WHUSM.

Michezo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuimarisha ushirikiano na mahusiano baina ya nchi na nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ufunguzi wa michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) ambayo imeanza rasmi leo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa ni fahari kubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa kuwa inatoa fursa kwa wageni na wenyeji kujumuika kwa pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kimichezo.

“Kuunganisha nchi na nchi si kazi rahisi lakini kupitia michezo imekuwa ni jambo rahisi kwa kuwa inawafanya kuwa na umoja uliothabiti na hivyo kuimarisha mahusiano baina ya nchi husika” alisema Mhe. Nnauye

Aidha Mhe. Nnauye aliwataka washiriki wasiishie kwenye michezo tu bali pia watumie fursa ya kuwepo nchini kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika Jijini la Dar es Salaam ikiwemo Makumbusho ya Taifa pamoja na Bagamoyo ambako kuna historia kubwa ya nchi.

Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba ameeleza kuwa mashindano hayo ni muhimu kwa walimu kwa kuwa yanawasiadia kuimarisha afya pamoja na kushirikiana katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

“Kupitia michezo hii tunaimarisha afya pamoja na kujadili changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo walimu ikiwemo ukosefu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi na namna ya kutatua tatizo hilo “ alisema Bw. Mukoba.

Kwa upande wake Rais wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda amesema kuwa kupitia michezo hiyo walimu hujifunza tamaduni mbalimbali baina yao ukizingatia elimu ndio msingi wa maendeleo.

Mashindano haya ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) yanafanyika kwa mara ya sita huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza ikihusisha nchi za Namibia, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika ya Kusini, Swizland na Tanzania.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 36 WA SADC MJINI MBABANE SWAZILAND

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa leo kwenye ukumbi wa Mandvulo uliopo Lozitha, Swaziland.
Mfalme Mswati wa III (kushoto) akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwenye ukumbi wa Mandvulo, Lozitha Swaziland.
Binti akionyesha bendera ya Tanzania wakati wa kuimba shairi maalum ya ufunguzi wa mkutano wa 36 wa SADC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini ubao wa kumbukumbu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wenye majina ya viongozi waliohudhuria mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika Lozitha, Mbabane Swaziland.
Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 36, Lozitha Swaziland.
---
Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC- ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dkt. Seretse Khama Ian Khama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Rais huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI anawakilishwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.

Amesema ana Imani kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani, uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.

Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.

Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika).

Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

SHUKRANI ZA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED MTATURU MKONONGO

$
0
0
Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake

Familia ya marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo (pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi, kwa ajali ya gari.

Familia inapenda kuwashukuru kipekee Wakwe wa marehemu - familia ya Mzee Edriss Mavura; Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Prof Elifas T. Bisanda pamoja na uongozi wa chuo na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT);

Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Afya duniani (WHO) Uganda na Tanzania; Dr Harvinder Palaha wa Aga Khan Hospital, na madaktari wenzie, wauguzi na wafanyakazi wote wa Aga Khan Hospitali kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU);

Mzee wetu Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi; Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania na Bw. Ziya Kaharan, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki; Prof. Fatmahan Atalar, Mkurugenzi wa MUHAS Genetic Laboratory ya Chuo Kikuu cha Muhimbili; Wanajumuiya wa Ikungi Development Association (IDEA); Umoja wa Wanafunzi waliosoma Uturuki, Masheikh wa Dar es Salaam na Ikungi; na Majirani wote wa Dar es Salaam na Singida.

Kwa kuwa si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, tunaomba wote mlioguswa na msiba huu mpokee shukrani zetu za dhati.

Tunapenda kuwataarifu kuwa Dua ya arobaini (40) ya marehemu itasomwa Jumamosi, tarehe 03 Septemba 2016, Makiungu-Ikungi, Singida, saa 5 asubuhi Wote mnakaribishwa.

INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUU.

MKUTANO WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA NCHINI MAURITIUS

$
0
0
Viongozi Wakuu pamoja na Sekretieti ya Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wake, katikati mwenye suti Waziri Mkuu wa Mauritius Sir Anerood Jugnauth.
Ujumbe wa Tanzania walioshiki Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid katikati kulia Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mussa Zungu na kushoto Dk Raphael Chegeni.Kutoka kushoto Maryam Rajab, Mbarikiwa Masinga, Mhe,Maria (MB) Mhe. Raphael Chegeni (MB)Mhe Juma Hamad Omar (MB) Mhe Simai Mohammed Said (BLW) Aziza Makwai.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akibadilishana mawazo na Wajumbe kutoka Tanzania kabla ya kuaza kwa Mkutano huo.
Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said, akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo inayozungumzia Suala la Nishati kwa Bara la Afrika, uliofanyika nchini Mauritius Balaclava.
Spika wa Baraza la Wawkilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe kutoka Tanzania wakishirika katika Mkutano huo wakifuatilia Mada zinazowasilishwa na Wajumbe wakati wa Mkutano huo nchini Mauritius.
Mtoto wa Mfalme wa Lesotho HRH Prince Seeiso B Seeiso, Raisi wa Senate na Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara kutoka Bunge la Falme ya nchi ya Lesotho akichangia mada iliyowasilishwa na Tanzania inayohusiana na nishati ya umeme.
Mjumbe wa Sekterieti kutoka Tanzania Aziza Mwakwai kushoto akimsaidia Spika wa Rwanda wakati wa Kikao hicho za kuwasilisha Mada kwa Nchi husika.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakipitia makabrasha yao kabla ya kuaza Kikao cha Kanda ya Afrika Mashariki. katika ukumbi wa Hoteli ya Meridian Mauritius
Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Spika wa Bunge la Mauritius na Rais wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Hon Mrs. Santi Bai Hanoomanjee. kulia kwake Katibu wa Bunge la Mauritius.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Kenya Mhe.Justin Muturi, Spika wa Uganda Mhe Rebecca Kadaga na Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akimwakilisha Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndungai.
Spika la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid (katikati) akifurahia jambo wakati wakibadilishana mawazo na Wajumbe wa Mkutano huo, kushoto Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebecca Kadaga na Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar, wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania ambaye pia Katibu wa Nchi za Jumuiya ya Madola Dk Thomas Kashillilah (wa tatu kutoka kulia mwenye suti), akizungumza na Wajumbe wa Sekterieti ya Jumuiya ya Kanda ya Afrika wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano huo uliofanyika Nchini Mauritius.
Mwakilishi kutoka Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano huo, pamoja na Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi mwenye kaunda suti pamoja wa Wawakilishi kutoka Kisiwa cha Rodrigues Mauritius.
Waziri wa Afya kutoka Nchini Botswana Hon Dorcas Makgato akiwa na Mjumbe kutoka Tanzania Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiwa na Mhe Simai Mohammed Said wakiwa katika eneo maarufu la Kitalii nchini lijulikanali kwa jina la Trou Aux Cerfs (Valcano in Vacoas - Phoenix, Mauritius).
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe wa Mkutano huo wakitembelea Kiwanda cha Kufulia Umeme na Sukari Nchini Mauritius wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kiwanda hicho cha Omnicane Limited.
Msanii wa Sanaa za kutengeneza Boti kwa ajili ya Watalii wanaotembelea Nchi hiyo akiwa katika harakati za kutengeza za boti zinazopatika katika eneo la Curepipe Mauritius hutengenezwa kwa mbao kama majahazi ya Zanzibar.
Sanamu la pili refu duniani baada la Nchini India lijukanali kwa jina Lord Shiva Nchini Mauritius likiwa katika maeneo ya Ganga Talao.
Mandhari ya kutoka juu ya bustani ya Trou Aux Cerfs.

Imetayarishwa na Zanzinews.com

KATUNI YA LEO

$
0
0

INTERNET SOCIETY STUDY POINTS TO REASONS FOR SLOW INTERNET GROWTH IN AFRICA

$
0
0

*Launches “Promoting Content in Africa” at African Peering and Interconnection Forum in Tanzania

DAR ES SALAAM, Tanzania, August 30, 2016/ -- Internet access and availability are not enough to get people online, says a new Internet Societystudy released today at the African Peering and Interconnection Forum (AfPIF) taking place 30 August - 1 September in Tanzania. The “Promoting Content in Africa” report reveals that while significant improvements have been made in Internet infrastructure, most notably in mobile networks, Internet adoption rates are slowing in many countries because users lack compelling reasons to connect.

According to the study, content and services are the main factors in making the Internet desirable, especially when the subject matter is relevant and in a language that users can easily understand. A lack of local content and services is affecting the number of new online users in Africa. In Sub-Saharan Africa in particular, local language content is key to bringing new users online, as many are not comfortable reading in English or French.

“Promoting Content in Africa” outlines the barriers to the development of local content and offers recommendations to improve local content availability and distribution.

In the Sub-Saharan countries studied by the Internet Society, the majority of international and locally developed content is hosted outside the country, typically overseas. This results in slow Internet speeds and higher access costs. In Rwanda for example, of all websites using the .RW domain name, only a small fraction are hosted in Rwanda. The majority of sites are hosted in Europe and the U.S. Hosting content locally is key to making the Internet faster and more affordable for users.

As mobile financial services are becoming increasingly available in the African continent, monetizing mobile content is still a major challenge. “Faster and better Internet access can help entrepreneurs create new local content including services and apps, but developers face barriers when it comes to payment mechanisms in order to monetize content,” said Bastiaan Quast, Internet Society Fellow and co-author of the report.

The region faces a combination of barriers, including the inability to pay and receive payments for mobile apps, which serve as a major channel for content distribution in most African countries.

Detailed results of the report will be presented at the seventh annual AfPIF which begins today in Dar es Salaam, Tanzania. Hosted by the Internet Society in partnership with the Tanzania Internet Service Providers Association (TISPA), the event serves as a platform to expand Internet infrastructure and services across Africa by bringing together key players to address the opportunities in interconnection, peering, and traffic exchange on the continent.

Internet peering is a business relationship whereby two Internet service providers agree to provide access to each other’s customers at no cost. Internet users throughout Africa benefit from peering, which enables faster and more affordable access.

“Removing barriers to content availability and distribution will have significant impacts on the Internet ecosystem in Africa. It will help to make existing international content more accessible,” explained Dawit Bekele, Internet Society Regional Bureau Director for Africa. “AfPIF is the only event in Africa focused on building the Internet by building relationships. It plays a key role in bringing together different parties to increase local traffic exchange across the continent,” he added.

AfPIF aims to build cross-border interconnection opportunities by facilitating discussions on Internet infrastructure challenges including capacity building, development of Internet Exchange Points (IXP) and local content.

Previous editions of AfPIF have been held in Kenya, Ghana, South Africa, Morocco, Senegal and Mozambique. Last year’s event featured 232 participants from 57 countries and an online participation of 978 people in 77 different countries.

FACEBOOK CEO GOES TO NIGERIA TO WITNESS AFRICA'S TECH REVOLUTION

$
0
0
 *Zuckerberg is in Nigeria to listen and learn and take ideas back to California on how Facebook can better support tech development and entrepreneurship across Africa

Facebook CEO Mark Zuckerberg is visiting Nigeria this week on his first trip to Africa, using his time in the country to visit the Yaba technology hub in Lagos, meet with developers and partners, and explore Nollywood.

Zuckerberg is in Nigeria to listen and learn and take ideas back to California on how Facebook can better support tech development and entrepreneurship across Africa.

One of his first stops on the trip was to visit a 'Summer of Code Camp' at the Co-Creation Hub (CcHub) in Yaba, known as the Silicon Valley of Nigeria.

CcHub opened in 2011 and at the time didn't even have an office. Five years later they fill three floors and the roof of a building. At CcHub people can learn how to code, developers can get help launching their first products, and find mentors and funding.

At CcHub Zuckerberg met with developers like Temi Giwa, who runs a platform called Life Bank (http://www.LifeBank.ng) that makes blood available when and where it is needed in Nigeria. Life Bank saves lives by mobilizing blood donations, taking inventory of all blood available in the country, and delivering blood in the right condition to where it is needed.

After visiting CcHub Mark Zuckerberg, CEO of Facebook, said:

“This is my first trip to sub-Saharan Africa. I'll be meeting with developers and entrepreneurs, and learning about the startup ecosystem in Nigeria. The energy here is amazing and I'm excited to learn as much as I can.

“The first place I got to visit was the Co-creation Hub Nigeria (CcHUB) in Yaba. I got to talk to kids at a summer coding camp and entrepreneurs who come to CcHub to build and launch their apps. I'm looking forward to meeting more people in Nigeria.”

IKUNGI HALF MARATHON 2016 KUANZA KURINDIMA WILAYANI IKUNGI JUMAMOSI WIKI HII

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielezea dhamira ya kuanzishwa kwa
---
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielezea dhamira ya kuanzishwa kwa Ikungi Half Marathon ofisini kwake

Na Mathias Canal, Singida.

Ni kama vile kuwa na kiu kizito kinachohitaji maji ya kunywa na kisha maji yakakutikana kusikojulikana, ndivyo itakavyokuwa Wilayani Ikungi Mkoani Singida mara baada ya kutangazwa mashindano ya riadha yanayojulikana kama Ikungi Half Marathon 2016.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika Vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi.
Akizungumzia dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa itakuwa ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Alisema kuwa Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yatafanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 200, mita 400 na mita 800.

Mashindano hayo yataanzia katika ngazi ya Vijiji Septemba 3, 2016, ngazi ya Kata itakuwa ni Octoba Mosi, Ngazi ya Tarafa ni Octoba 15, 2016 na kwa ngazi ya Wilaya itakuwa ni Octoba 29, 2016.

Dc Mtaturu alisema kuwa kuanzishwa kwa kuzinduliwa kwa mashindano hayo ni katika kuhakikisha Wilaya ya Ikungi inaibua changamoto katika sekta ya michezo nchini hivyo hiyo ni fursa muhimu kwa washiriki kujitokeza ili kuonyesha uwezo wao katika kusakata riadha.

Mtaturu alisema kuwa mwaka 2017 panapo majaaliwa wamejipanga kufanya mashindano ya Ikungi Marathon yatakayohusisha mbio ndefu za kilomita 42 ambapo jambo hili itakuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Ameeleza kuwa mashindano hayo pia yamedhamiria kuitambulisha Wilaya hiyo Kitaifa na Kimataifa kupitia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo mbalimbali hususani mashindano ya Riadha.

Aidha amewaomba vijana wote wenye umri uliofikia miaka 17 kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ili kuimarisha afya zao na kuachana na mawazo ovu yakiwemo yale ya kujihusisha na wizi na ujambazi, Ngono zembe pamoja na ubakaji.

Kwa upande wake Afisa michezo Wilayani Ikungi Abubakary Kisuda alisema kuwa mashindano ya ngazi ya Vijiji yatafanyika kwa lengo la kupata vijana watakaoshindana ili kushiriki mashindano ya ngazi ya Kata, ambapo mashindano ya Kata yatafanyika kwa lengo la kupata vijana watakaoshindana ili kushiriki mashindano ya ngazi ya Tarafa.

Kisuda alisema kuwa hili ni tukio la awali kabisa kuanzishwa Wilayani humo tangu kuanzishwa kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo miaka mitatu iliyopita hivyo litaibua hisia chanya na kuigwa na Taifa zima.

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akipokea msaada wa madawati 235 kwa mkoa wa Kagera toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande jana kwenye shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Vijijini Deodatus Kinawiro akihutubia wakazi wa Bukoba baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi Kagera makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba
Meneja wa Tigo kanda ya ziwa , Edgar Mapande akitoa hotuba kwa wageni waalikwa na wanafunzi mara baada ya makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi za mkoa wa Kagera ,katika hafla iliyofanyika katika shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakishuhudia makabidhiano ya madawati 235 kwa shule za msingi mkoani Kagera toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Katoro wilayani Bukoba wakiwa wameketi kwenye moja ya dawati kuonyesha kuwa wamepokea madawati toka kampuni ya simu za mkononi Tigo.

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI, JANETH JIMMY AMSHUKURU MUMEWE JIMMY NA MARAFIKI ZAKE KWA KUMFIKISHA ALIPO

$
0
0
Naikumbuka sana hii siku nilijifunza sana na nikagundua Kumbe Nina uwezo wa kufanya vitu vingi sana! Nawashukuru sana rafiki zangu na ndugu zangu Lenick Joackim pamoja na Neema Alex #DadaMeneja kwa kuniamini na kunipa nafasi siyo kila mtu anaweza kufanya hivyo Nina #WAPENDASANA sana sana sanaa Ninaheshimu mchango wa kila mtu hata kama ni mdogo kiasi gani kwa sababu ninajua udogo huo huo ndo unatengeneza ukubwa wa kesho!

Ninawaheshimu sanaa!

Mume wangu Jimmy Charles kwa namna ya pekee sana naomba nikushukuru wewe na mchango wako kwangu, siku zote umeniamini na umeniruhusu kuyafanya haya bila kigugumizi huku ukinikosoa kunielekeza na kuniongoza namna ya kufanya wewe ni mmoja kati ya mamilioni Mungu aendelee kukutunza anisaidie ili niendelee kukuheshimu na kukutii siku zote!

My gratitude from the very bottom of my heart.

MBWEMBWE ZA WATANI WA JADI YANGA

$
0
0
Viewing all 19795 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>