Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19828 articles
Browse latest View live

ASASI YA FEDHA YAWAKUMBUSHA WANACHUO UMUHIMU WA KUWEKA AKIBA

$
0
0
Mkurungezi mtendaji wa Asasi ya Fedha Jafari Selemani akisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha iliyofanyika katika Chuo cha Kilimanjaro Insitute college na kuwakutanisha wanavyuo zaidi ya mia 2 hapa jijini Dar es salaam ambapo alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa na tabia ya kuweka akiba na kujiandaa na maisha ya uzee ambapo Moto wa asasi hiyo ni "UHURU WA KIFEDHA NI WAJIBU WAKO " kulia kwake ni mtaalamu wa biashara na mhamasishaji wa vijana Fasili Boniface mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Mhamasishaji wa vijana Mussa Mashauri akitoa mada kuhusu Vijana na Utendaji kazi katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Asasi ya Fedha iliyofanyika katika chuo na Kilimanjaro Insitute college na kuwakutanisha wanachuo zaidi ya 200 toka chuo cha UDSM, Ustawi wa jamii, Teku , St Joseph na Kilimanjaro Insitute college na kushoto kwake ni Murungezi Mtendaji wa KONCEPT na Mhamasishaji wa Vijana Krantz Mwantepele mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Mmoja wa wanachuo waliohudhuria warsha hiyo akiuliza swali kwa mwongoza Mada Musa Mashauri.
Mtaalamu wa Biashara na Mhamasishaji wa vijana Fasili Boniface akiongoza mada kuhusu "Siri za jinsi ya kupata Ajira " katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Asasi ya Fedha mapema mwishoni mwa wiki iliyopita katika chuo cha Kilimanjaro Insitute college na kukutanisha wanachuo zaidi ya mia 200 hapa jijini Dar es salaam.
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT na mhamasishaji wa vijana Krantz Mwantepele akisitiza jambo wakati akiongoza mada kuhusu "Siri za uhuru wa kifedha na fursa ambazo zipo nchini vijana wanaweza kujiajili na kutengeneza thamani kwa jamii inayowazunguka ,katika warsha iliyofanyika mapema mwishoni mwa wiki iliyopita katika chuo cha Kilimanjaro Insitute college,
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisiliza kwa makini mada toka kwa Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele mapema mwa wiki iliyopita.
Mkurungezi Mtendaji wa Koncept akiongoza washiriki wa warsha hiyo kula kiapo kuwa wanaamini nguvu ya mafanikio ipo ndani yao na ni wajibu wao kutafuta fursa na kutimiza ndoto zao
Mkurungezi wa Asasi ya Fedha Jafari selemani akitoa neno la kufunga warsha hiyo iliyofanyika katika chuo cha kilimanjaro na kukutanisha zaidi mia mbili kutoka vyuo vya UDSM , TEKU, USTAWI WA JAMII , ST JOSEPH NA KILIMANJARO INSITUTE COLLEGE mapema wiki iliyopita katika chuo cha Kilimanjaro Insitute college.

JUMAPILI NJEMA; BEATRICE MWAIPAJA - KUMBE NI KWA NEEMA TU

$
0
0

FLYDUBAI INASHIRIKI KATIKA ONYESHO LA KWANZA LA UTALII WA DUBAI KUFANYIKA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
flydubai Boeing 737-800
---
Shirila la ndege lenye makao yake Dubai watashiriki katika maonyesho ya huduma zake nchini Uganda na Tanzania liikiangazia safari zake za bei nafuu za moja kwa moja kwenda Dubai na idadi ya safari zake zilizoongezeka

Shirika la ndege lenye makao yake Dubai, flydubai litashiriki katika maonyesho ya Utalii yatakayofanyika kwa mara ya kwanza kabisa Afrika Mashariki, litaungana na washirika wake wengine 14 kutoka Dubai katika kuonyesha huduma na vivutio mbalimbali vinavyoibukia. Flydubai imeshiriki katika maonyesho ya Kampala mnamo Agosti 24, ambapo maonyesho hayo yatahamia Dar es Salaam manamo Agosti 30.

Maonyesho haya ni fursa kwa watoa huduma wa ndani kukutana moja kwa moja na viongozi wa shirika hili na kujifunza kuhusu huduma na chaguzi ambao wasafiri wanafanya pale wanapotaka kusafiri moja kwa moja kwenda Dubai kwa ajili ya biashara au mapumziko.

Akitoa maoni yake, Issam Kazim, Mkurugenzi Mtendaji katika idara Utalii wa Dubai, alisema: “Uwezo wa Uganda na Tanzania kama soko kubwa ni mzuri, na maonyesho haya yanatupatia fursa ya kutangamana moja kwa moja na watoa huduma wa ndani na kuonyesha kile ambacho Dubai inatoa. Tunatazamia kuwa na mahusiano ya kibiashara ya muda mrefu na yenye kuzaa matunda wakati wa ziara yetu katika kukuza zaidi soko la utalii nchini Uganda kwa manufaa ya wote.”

Flydubai ilizinduliwa mwaka 2009 ili kusaidia uendeshaji wa biashara na utaliii bila vikwazo na kusaidia zaidi njozi ya Dubai kuwa kitovu cha utalii na usafiri wa anga unaotambulika kimataifa. Bidhaa za ubora wa juu, nafuu na zinazoaminika za flydubai zinazotolewa kwa madaraja yote ya biashara na ya kati, zimewawezesha watu zaidi kusafiri mara nyingi kwenda Dubai.
Sudhir Sreedharan (pichani), Anayehusika na Operesheni za Kibiashara katika flydubai (GCC, Afrika na India), alisema: “Tulifurahia sana kushiriki katika maonyesho ya kwanza ya Utalii wa Dubai kufanyika Afrika Mashariki na kuonyesha chapa Dubai na flydubai. Tumejizatiti kufungua masoko hayapati huduma na kufungua vituo ambavyo awali havikuwa au vilikuwa na safari chache za moja kwa moja kwenda Dubai. Afrika Mashariki ni soko muhimu zaidi ambalo limeonyesha ukuaji mkubwa katika miaka michache iliyopita. Kwa sasa tunafanya safari 82 kila wiki kwenda vituo 11 barani Afrika, hii inajumuisha safari 3 kwenda Entebbe na safari 4 kwenda Dar es Salaam na Zanzibar. Safari hizi za kujirudia za kila wiki zitaongezeka hadi kufikia safari 4 kwenda Entebbe na safari 7 kwenda Dar es Salaam na Zanzibar kuanzia Oktoba.”

Flydubai kwa sasa inafanya safari kwenda katika vituo 11 Afrika Kaskazini na Afrika Mashariki: Addis Ababa, Alexandria, Asmara, Dar es Salaam, Djibouti, Entebbe, Hargeisa, Juba, Khartoum, Port Sudan na Zanzibar.

Daraja la Biashara linapatikana katika njia nyingi katika mtandao wa flydubai na ndege zake hivi karibuni zimeanzisha huduma ya WiFi na Live TV kwa baadhi ya safari zake.

Shirika hili ambalo ni la pili kwa ukubwa kufanya safari za kimataifa nje ya Dubai, limejenga mtandao wa vituo 90 katika nchi 44 na hufanya safari zaidi ya 1,700 kwa wiki nje ya Dubai International (DXB), Temino namba 2 na Temino nyingine mpya iliyofunguliwa hivi karibuni Al Maktoum International- Dubai World Central (DWC).

MAGAZETINI LEO; MKAPA AWAKUTANISHA MAGUFULI NA LOWASSA ... KILICHOJIFICHA HAFLA MAGUFULI, LOWASSA

$
0
0

SHEREHE YA JUBILEI YA DHAHABU (MIAKA 50) YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA

$
0
0
 Ukumbi wa sherehe
 Msafara ukielekea ukumbini
 Viongozi waalikwa
 Viongozi wastaafu
 MC Angela Bondo kazini
 Sehemu ya waalikwa
 Taswira ya mbele
 Meza ya wana familia
 Burudani ya muziki
wakielekea jukwaani kukata keki
 Ni wakati wa keki
 Wakikata keki
 Wakilishana keki huku wakishuhudiwa na msimamizi wa ndoa yao miaka 50 iliyopita Balozi  Anthony Nyaki
 Wajukuu, watoto, wakwe wakilishwa keki
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Maria Nyerere na Mama Shadya Karume.
 Wanafamilia wakijadiliana jambo
 Taswira ya ukumbi
 Bw. Nicholaus Mkapa akimimina champagne isiyo na kilevi  meza kuu
 Bw. Nicholaus Mkapa akijianda kumimina champagne isiyo na kilevi  kwa Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) Mstaafu Mhe. Joseph Rugumyamheto akiwatakia wote maisha marefu kwa kuongoza toast
  Meza kuu wakigonganishiana glasi na Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Meza kuu wakigonganishiana glasi na Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akigongesha glasi na Mama Maria Nyerere, Mama Shadya Karume na Mama Salma Kikwete
   Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akigongesha glasi na Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi na Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi, Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman, Spika Mstaafu Mamam Anne Makinda
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi viongozi  wastaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM na katibu Mkuu wake
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi viongozi  wastaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM na katibu Mkuu wake
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi viongozi  wastaafu
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakigongesha glasi na mawaziri wakuu wastaafu

 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na MKUU wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mstaafu, Jenerali George Mwita Waitara na mkewe Mama Waitara
 Rais Dkt. Magufuli akisaini kitabu cha sherehe hizo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana akisalimiana na Waziri mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa
 Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Mhe. Alnoor Kassumna mkewe Mama Kassum.
 Watoto kutoka Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Kibaha (Kibaha The EOTF Orpham Centre) wakiwaimbia babu na bibi Mkapa
 Brigedia Jenerali  mstaafu Francis Mbena akikabidhi zawadi yake
 Brigedia Jenerali  mstaafu Francis Mbena akikabidhi kadi maalumu aliyotengeneza
 Brigedia Jenerali  mstaafu Francis Mbena akikabidhi kwa Nicholaus Mkapa na mkewe zawadi yake
 Bw. Kambona aliyesoma darasa moja na Mzee Mkapa akionesha zawadi ambao baadhi ya waliosoma naye waliileta kumkabidhi
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakipokea zawadi ya waliosoma na Mzee Mkapa
 Msemaji wa familia ya Mzee Mkapa Bw. William Erio akitoa shukurani kwa wote waliofika na pia waliofanikisha sherehe hizo

 Sheikh wa mkowa wa Dar es salaam Ahaj Alhad Mussa Salum akisema machache
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani zake kwa wote waliohudhuria na waliofanikisha sherehe hizo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani zake kwa wote waliohudhuria na waliofanikisha sherehe hizo
 Rais Dkt. Magufuli na mkewa Mama Janeth Magufuli wakiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
  Rais Dkt. Magufuli na mkewa Mama Janeth Magufuli wakiwapongeza Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
  Rais Dkt. Magufuli na mkewa Mama Janeth Magufuli wakiwakabidhi zawadi Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Edward Lowassa. Kushoto ni Mama Regina Lowassa

  Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Bishop Eusebius Nzigilwa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipozi na viongozi wa dini. Kutoka kushoto ni Sheikh Alhad Mussa Salum, Shekhe wa mkoa wa Dar es salaam, Rais Magufuli, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo, Mama Janeth Shoo na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Bishop Eusebius Nzigilwa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa pamoja na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete  wakipozi na wajukuu wa Mzee Mkapa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Mama Maria Nyerere

Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa pamoja na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Mama Salma Kikwete wakipozi na wajukuu wa Mzee Mkapa. Picha zote na IKULU.

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA YA MOYONI BAADA YA KUKUTANA NA MHE. LOWASSA JANA KATIKA JUBILEI YA MIAKA 50 YA MZEE MKAPA NA MAMA ANNA MKAPA

$
0
0

KIFAHAMU KIPINDI KIPYA CHA 'CHUKUA HATUA' KINACHOHUSU VIJANA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Watangazaji wa kipindi kipya cha CHUKUA HATUA Happy Balisidya na Mohammed Hammie, siku ya kwanza walipokutana wakati wa maandalizi ya kutengeneza kipindi hicho.
Mohammed Hammie na Happy Balisidya wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kufahamu watakuwa wakiendesha kipindi cha CHUKUA HATUA.
---
Chukua Hatua ni kipindi kipya cha radio kitakachowashirikisha vijana, wakizungumza na kujadili kwa pamoja masuala yanayowahusu hasa ya kujikwamua na maendeleo mkoani Dodoma na maeneo jirani.

Hiki ni kipindi ambacho kinatarajiwa kujadili kwa kina changamoto za ajira kwa vijana kupata mwelekeo wa maendeleo kwa vijana wa kike na kiume.

Lengo kuu la kipindi hiki ni kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira na changamoto wanazokutana nazo katika mihangaiko yao, kipindi kitapaza sauti za vijana ambazo hazikupata nafasi ya kusikika hapo kabla.

Si kipindi tu, bali pia ni jukwaa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi, mawazo, uzoefu na pia kujifunza kutoka kwa wengine, ni mahala pekee ambapo kijana atayaona matarajio na uzoefu kutoka fani na taaluma mbalimbali.

Kipindi pia kinatarajiwa kuimarisha ujuzi na kuelekeza upya akili za vijana kufanya kazi na kuchangamkia fursa za ajira kwa ujasiriamali, kujiajiri na kuukwepa umaskini uliokithiri miongoni mwao.

Kipindi kitaanza kuruka hewani siku ya Alhamisi ya tarehe 01/09/2016 kupitia kituo cha RASI FM RADIO inayopatika masafa ya 103.7 Dodoma.

Pia kipindi kitakuwa kinapatikana kupitia mtandao wa Youtube ukurasa wa CHUKUA HATUA, pia mijadala itakuwa inaendelea kupitia ukurasa wetu wa facebook ambao ni CHUKUA HATUA, Instagram ni KIJANA CHUKUA HATUA, na Twitter ni CHUKUA HATUA1

Kipindi hiki kimewezeshwa na mpango wa pamoja wa ajira kwa vijana wa Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kazi Duniani (ILO) kwa udhamini wa SIDA.

MAGAZETINI LEO; LOWASSA, JPM WAIBUA MAZITO ... MBOWE ASEMA 'UKUTA UPO PALE PALE'

$
0
0
 

WANANCHI WA KANDA YA ZIWA ZAIDI YA 750 WAPATA MAFUNZO KILIMO BIASHARA JIJINI MWANZA

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) na Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia) pamoja na wajumbe wengine kutoka UNDP wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano Rock City Mall lilipofanyika kongamano la Kilimo Biashara jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumzia malengo ya Kongamano la Kilimo Biashara kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) kufungua rasmi.
Mwakilishi Msaidizi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akitoa salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akitoa hotuba ya kufungua Kongamano la Kilimo Biashara kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk. Charles Mahika akielezea mikakati iliyowekwa na wizara ya kuhakikisha sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo inafanikiwa.
Mwezeshaji ambaye pia ni Rais wa vijana wajasiriamali na wataalamu wa miradi ya maendeleo mkoa wa Singida, Philemon Kiemi akitoa mafunzo ya ufugaji kuku wa kisasa kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Mratibu wa Kongamano kutoka ESRF, Abdallah Hassan akizungumza jambo kwenye kongamano hilo.
Mwezeshaji Bi. Kalega akitoa mafunzo ya ufugaji Kuku na matumizi ya Azolla kwa washiriki wa Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.
Baadi ya wakazi wa Kanda ya Ziwa akiwemo mke wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bi. Mongella waliohudhuria Kongamano la Kilimo Biashara lililofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Na Mwandishi wetu.

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limesema litaendela kuinua fursa za kiuchumi zinazopatikana hapa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa zinazoendelea kuibuliwa.

Kauli hiyo imetolewa na Programme Specilist- Inclusive Growth UNDP Tanzania, Ernest Salla wakati wa Kongamano la Kilimo Biashara kanda ya ziwa lilofanyika katika ukumbi wa Rocky City Mall Agosti 27 mwaka huu Jijini Mwanza.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na UNDP/UNEP lililolenga kuzitambulisha fursa katika kilimo biashara, lilihudhuriwa na wananchi mbalimbali zaidi ya 750 kutoka mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza wenyewe.

Katika kongamano hilo Salla alisema kilimo kina fursa nyingi hivyo watanzania hawana budi kuzitumia fursa hizo kwa kuwakumbatia wataalamu ili kiwe mkombozi wa maisha yao.

Akizungumza katika Kongamano hilo la siku moja, Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida alisema licha ya uchumi wa taifa kutegemea kwa kiasi kikubwa kilimo, lakini kilimo hapa nchini bado kipo nyuma hivyo kuchangia kiasi kidogo katika kumuendeleza mkulima.

“Kwa kutambua upungufu huu, ESRF ikishirkiana na UNDP/UNEP imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi na taifa kwa ujumla kujikwamua katika vizingiti mbalimbali vya maendeleo ukiwemo umasikini wa kipato,” alisema Dk Kida

Alisema kukua kwa teknolojia duniani, kumeongeza fursa nyigi za kimaendeleo ikiwamo kilimo, kwani wakulima wengi hivi sasa hawategemei mvua na hutumia eneo dogo kwa ajili ya kilimo.

Katika warsha hiyo zilitolewa mada mbalimbali; pamoja na kilimo cha Foda (Hydroponic fodder), kilimo cha mbogamboga (Hydroponic and Aquaponic Vegetables), shamba kitalu (Green house), Azolla na ufugaji wa samaki na nyuki kutoka kwa wakufunzi mbalimbali waliotoa ufafanuzi kuhusu fursa mpya za kilimo biashara.

Alisema kilimo cha kisasa au “smart farming” ambacho hakihitaji maeneo makubwa kinaweza kufanyika katika maeneo ya mjini tofauti na izaniwavyo kuwa kilimo lazima kiwe vijijini.

Alisema ESRF imeshiriki katika utekelezaji wa miradi ya majaribio inayotegemea teknolojia ya kisasa katika wilaya za Bunda, Bukoba vijijini, Sengerema, Nyasa, Ikungi na Ileje kupitia miradi ya PEI na CDRBM kwa kipindi cha miaka mitatu.

Pamoja na mambo mengine, alisema matokeo ya miradi hiyo ya majaribio yamethibitisha fursa katika kilimo biashara yanayoweza kuwasadia wananchi katika kujikwamua na ndio miongoni mwa sababu ya kuandaa warsha hiyo.

Akifungua kongamno hilo ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alisema kilimo pekee ndicho chenye fursa pekee rahisi kuliko sekta nyingine duniani kote.

Mongela aliipongeza ESRF, UNDP, na wadau wengine wa maendeleo, kwa tafiti hizo na kwamba hatua hiyo itasaidia kuinua uchumi wa watanzania na taifa kwa ujumla.

Licha ya Mongella kupongeza hatua hizo, lakini alizitaka taasisi mbalimbali kupitia wataalamu wake kuonyesha gharama halisi za kutekeleza miradi hiyo.

“Hizi tekonolojia ni rahisi, watu wakianza nazo kidogokidogo baadaye watapanda na kufika juu, tatizo la wataalamu wanasema gharama ni kubwa za teknolojia, hivyo kuwaogopesha watu,” alisema Mongella

Amoni Manyama kutoka UNDP, alisema kuzingatia maelekezo ya wataaalamu ndio njia pekee ya kufanikisha katika kubuni fursa za kilimo na biashara.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Dk Charles Mahika alisema wizara yake ikishirikiana nan chi zinazozunguka Ziwa Victoria wanaandaa mwongozo wa kuanzisha ufugaji wa samaki katika vizimba na kwamba mwongozo huo unatarajiwa kukamilishwa jijini Mwanza hivi karibuni.

Katika kongamano hilo wapo baadhi ya wananchi waliotoa shuhuda mbalimbali walionza kunufaika na fursa za kilimo biashara chini ya ufadhili wa UNDP ikishirikiana na ESRF.

WAZIRI JENISTA ATOA SOMO KWA MABENKI

$
0
0

Sekta za kifedha zinazohusika na utoaji wa mikopo nchini zimetakiwa kutenga utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wa wadogo, kati na wakubwa ili kuleta unafuu wa masharti ya ukopaji. Hayo yalisemwa katika kilele cha mafunzo ya Wiki ya Huduma ya Kifedha na Uwekezaji na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama alipokuwa anafunga siku ya mwisho ya mafunzo hayo Agosti 27.

Mhagama alisema kuwa mafunzo kwa wajasiriamali yamekuwa yakitolewa mara kwa mara ila kikwazo kimekuwa ni mkopo hususani kwa wajasiriamali wanaoenda kukopa masharti wanashindwa yakiwemo uwekaji wa hati ya nyumba kama dhamana na riba kubwa.

“Tanzania kuna takribani wajasiriamali milioni tano, ila wengi wao wanashindwa kupiga hatua kutokana na masharti mazito ya mikopo, mfano mama anauza vitumbua unamwamabia alete hati ya nyumba na wakati kapanga chumba kimoja” Alisema Mhagama.

Alieleza kuwa banki na wadau wote wa maendeleo wakutane ili kujadili ni namna gani wanavyoweza kupunguza masharti kwa wajasiriamali wadogo ili kuwakomboa na kupunguza tatizo la ajira na umasikini nchini. Mhagama ambae pia ni Mbunge wa Peramiho alisema kuwa Serikali itakuwa tayari kufanya majadiliano kuona namna ya kumsaidia mjasiriamali mdogo na wa kati huku akiwapongeza Banki ya Finca kwa kupunguza gharama za ukopaji kwa wananchi.

Meneja Masoko na Afisa Mahusiano wa Bank ya Finca, S pacio Aboubakar alisema walijitahidi kufatilia vikwazo vyote vinavyowakwamisha wajasiriamali na kuvifanyia kazi na kwa sasa kuna unafuu mkubwa wa masharti kwa mkopaji na ulipaji wa riba. Banki ya Finca imekuwa mkombozi kwa wajasiriamali nchini katika maonyesho hayo walifanikiwa kusajili zaidi ya wajasiriamali 4000 wapya.

Katika mafunzo hayo wajasiriamali kutoka vikundi mbalimbali vilishiriki ikiwemo Vikoba pia washindi walikabidhiwa fedha taslimu laki tano ili kuwapa motisha wajasiriamali wengine kushiriki miaka inayofata. Nuru Salim ni mmoja wa washindi wa zoezi lililofanywa na banki ya Finca na kuibuka mshindi alisema wamama wajitokeze kwa wingi kujifunza na kupata elimu ya uwekezaji na ujasiriamali ili kuepukana na tatizo la kuwa tegemezi.

“Mimi najihusisha na uuzaji wa nguo za wanawake Kariakoo, ila hapohapo nauza vitafunwa ninavyotengeza mwenyewe kama vitumbua ila nimekuja hapa kuongeza vitu vipya” Aleleza Nuru.

Maonyesho hayo yalikuwa ya tano na huwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta za banki, bima na uwekezaji kutoa elimu kwa wajasiriamali zaidi ya 20,000 na muitikio mkubwa ulikuwa wa wamama kuliko vijana na wanaume

Mwandishi: Muyonga Jumanne (Mwananchi).

BONANZA LA MISS KINONDONI 2016 LAFANA JIJINI DAR

$
0
0
Wanyange wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 wakionesha moja ya shoo katika Bonanza walioandaliwa na Mdhamini wao Mkuu Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd lililofanyika ufukwe wa Jangwani Sea Breeze Mbezi jijini Dar es Salaam jana lenye lengo la kuwaweka fiti kabla ya shindano lao litakalofanyikaa Septemba mbili Hoteli ya Denfrances Sinza jijini Dar es Salaam.
Wanyange hao wakiwa na waandaaji wa shindano hilo litakalofanyika Septemba 2, 2016 Hoteli ya Denfrances iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Shindano hilo, Rahmat George ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Rahmat Entertainment iliyoandaa shindano hilo, akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya shindano hilo.
Burudani zikiendelea katika bonanza hilo.
Wanyange hao wakishiriki kucheza mpira wa mkono kwenye bonanza hilo.
Wadau wa Windhoek wakicheza soka la ufukweni katika bonanza hilo.
Soka la ufukweni likiendelea.
Mchezo wa kuogelea ukiendelea ndani ya kiota cha Jangwani Sea Breeze huko Mbezi jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

MDHAMINI Mkuu wa Lete Raha Miss Kinondoni 2016 Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd imewaandalia Bonanza wanyange wa shindano hilo ili kuwaweka fiti kuelekea shindano lenyewe litakalofanyika Septemba 2 Ukumbi wa Denfrances uliopo Sinza.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Abdallah Ngoma alisema wameamua kuwa andalia bonaza hilo ili kuwafanya wawe fiti kabla ya kuingia kwenye shindano lenyewe Sptemba 2.

"Katika bonaza hilo warembo hao wameweza kushiriki mpira wa miguu, mikono na kucheza" alisema Ngoma.

Mratibu wa shindano hilo Rahmat George alisema maandalizi yote yamekwisha kamilika ambapo warembo 20 watapanda jukwaani kuwania nafasi ya Miss Kinondoni 2016.

Alisema kama kawaida warembo hao watapanda jukwaani wakiwa katika vazi la ufukweni, ubunifu na kujibu maswali wata kayoulizwa na majaji.

AIRTEL MONEY TIMIZA YAFANYA SEMINA NA MAWAKALA MKOA WA MWANZA

$
0
0

Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitia msisitizo zaidi katika semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.
Mawakala toka viunga mbalimbali ndani ya jiji la Mwanza wamekusanyika hapa ndani ya ukumbi wa Gold Crest Hotel kwa nia ya kupata mafunzo.
Msimamizi mkuu wa uelimishaji wa huduma ya Airtel Money Timiza, Rwebu Mutahaba akitoa semina kwa Mawakala wa mihamala ya fedha za mtandao jijini Mwanza juu ya mikopo hiyo ya mtando wa Airtel ambayo imekuja kama sehemu ya maboresho ya huduma na kuwarahisishia wananchi wa Tanzania linapokuja suala la mtaji.



'MUDA NI MALI' = Jinsi Airtel Money Timiza inavyokomboa muda huku ikimkuza na kumnyanyua mwananchi toka lindi la umasikini.
David Wankuru ambaye ni Meneja wa Airtel Mkoa wa Mwanza akifafanua kilichofanyika ndani ya semina kwa mawakala, masharti na masuala yote juu ya Airtel Money Timiza.
Ni sifa zipi zitampa mteja fursa ya kuweza kukopeshwa na Airtel Money Timiza? Joel Laizer ambaye ni Meneja wa Mauzo Airtel Mwanza anafunguka zaidi.
Mawakala - Kalunde Kafiti na wenzake hapa wanafunguka mengi juu ya
1.Wazo la Airtel Timiza linamanufaa gani kwa wenye kufanya kazi ya miamala?
2. Nini Tahadhari kwa matapeli wanaoweza kuitumia Airtel Money Timiza kufanya yao?
3.Jeh Mikopo itawasaidiaje wajasiliamali ambao suala la mtaji limekuwa changamoto kubwa kwao?

MZEE PIUS MSEKWA ASEMA 'WATANZANIA WAACHE KUFUATA MKUMBO'

$
0
0
Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa.

Na Fatma Salum na Sheila Simba, MAELEZO

Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pius Msekwa amewaasa watanzania kuacha kufuata mkumbo wa kisiasa badala yake watii mamlaka ili kuepuka kuvunja sheria na kuleta madhara kwao binafsi na taifa kwa ujumla.

Msekwa aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia masuala mbalimbali kuhusu mwenendo wa siasa za hapa nchini na utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi
wa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Alieleza kuwa watu wengi wana hulka ya kufuata mkumbo kwenye mambo fulani bila ya kuchunguza na kufahamu ukweli wake kabla ya kushabikia.

“Ni hulka ya watanzania kushabikia mambo wasiyoyafahamu ilimradi tu yanawafurahisha masikioni
au machoni mwao kwani hata huko mitaani wanakimbilia ngoma bila ya kujua inatokea wapi au inaelekea wapi, hivyo nawasihi wajaribu kuwa makini na mbinu za siasa zinazotumiwa na baadhi ya vyama kwa kuwa nyingine zina madhara ndani yake.” Alisema Msekwa.

Akifafanua mwenendo wa siasa  za hapa nchini, Mzee Msekwa alisema kuwa bado wanasiasa wengi hawafuati kanuni za ushindani wa kisiasa katika kutafuta madaraka badala yake wanatumia mbinu ambazo zinavunja sheria za nchi na hatimaye wanapambana na mamlaka.

“Ushindani wa kisiasa ni jambo la kawaida na linalokubalika ingawa ushindani huo ni lazima ufuate sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ili kufikia lengo, hivyo kubuni vitu ambavyo vinachochea utovu wa nidhamu na uvunjifu wa amani sio jambo zuri, ' alisisitiza.

Aidha, Msekwa alieleza kuwa utendaji wa Mhe. John Magufuli ni wa kuridhisha na wa aina yake kwa kuwa amekusudia kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania na kuondoa mfumo wa utendaji kazi kwa mazoea jambo ambalo limesaidia kurudisha nidhamu kwa watumishi wa Serikali.

Akizungumzia uzoefu wake katika masuala ya kuongoza Bunge, alieleza kuwa tofauti ya Bunge la zamani ni kwamba lilikuwa na nidhamu kubwa na linaheshimika lakini Bunge la sasa halina utii na hicho ndio chanzo cha malumbano yanayojitokeza mara kwa mara katika vikao vya Bunge.

Aliongeza kuwa tangu awali wapinzani kazi yao ni kuipinga Serikali iliyo madarakani lakini kwenye Bunge la uongozi wake walikuwa wakipinga kwa kutumia hoja na kufuata kanuni bila ya kudharau mamlaka ya Spika wala Serikali iliyoko madarakani.

“Kanuni zinatoa nafasi kwa mbunge asiyeridhika na maamuzi ya Spika kushitaki kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge, na kamati hiyo itasikiliza na kutoa uamuzi kama mahakama inavyosikiliza lakini wabunge wa sasa hawataki kutumia utaratibu bali hutumia mbinu za tofauti ili waweze kupata sifa ambazo hazina tija kwa wananchi waliowachagua,” alisema.

Msekwa pia amewaasa vyama vya upinzani kutumia mbinu nzuri katika kutafuta madaraka bila ya kuvunja sheria au kuhatarisha amani ya nchi kwani waliowachagua wanategemea zaidi matokeo ya kazi waliyoahidi kuwatumikia kuliko malumbano yasiyo na tija kwa ustawi wao na taifa.

RADIO 5 NA MAGIC FM ZAFUNGIWA KWA MUDA USIOJULIKANA

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mapela leo, wakati akitangaza kuzifungia radio mbili Magic Fm ya Dar es Salaam na Radio 5 ya Arusha kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi na kuvirusha hewani ambavyo vinaashiria uchochezi.

---
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo vimerushwa hewani vinavyoashiria uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia vituo hivyo umefikiwa baaa ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo cha utangazaji cha Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.

Nape amesema kuwa kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.

Wakati vituo hivyo vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa jukuu la kuviita na kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua gani zaidi ya kuchukua dhidi yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za utangazaji.

Nape ameendelea kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoshawishika kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda heshima ya tasnia yetu na wakati huo kuhakikisha nchi inabaki na Amani, Mshikamano na Umoja.

WAKAZI WA MULEBA WALIPOKEA KWA SHANGWE TAMASHA LA TIGO FIESTA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Muleba Bwa. Richard Ruyango , akifungua rasmi tamasha la Tigo fiesta kwenye uwanja wa David Zihimbile wilayani humo usiku wa jana, Kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya ziwa Edgar Mapande na kushoto mkurugenzi wa vipindi clouds Ruge Mutahaba na mwakilishi kutoka wilayani.
Msanii Christian Bella akipagawisha kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.
Msanii Joh Makini akiwarusha mashabiki wa hip hop kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.
Msanii Raymond akionyesha umahiri wake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile.
Msanii Shilole akiwa na shabiki wake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta wilaya Muleba usiku wa jana lililofanyika uwanja wa David Zihimbile. 
Msanii wa bongofleva Maua Sama, akitumbuiza kwenye uwanja wa Kahama Stadium Mkoani Shinyanga kwenye tamasha la Tigo Fiesta.
Wasanii kutoka kundi la Navy Kenzo, wakiburudisha kwenye uwanja wa Kahama Stadium Mkoani Shinyanga kwenye tamasha la Tigo Fiesta.
Msanii chipukizi wa super nyota aliyebahatika kushiriki fiesta ya mwisho litalofanyika jijini Dar es salaam.
Sehemu ya umati uliohudhuria tamasha la Tigo fiesta Muleba

MCHIMBA KISIMA AFIA NDANI YA KISIMA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Mchimbaji wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani baada ya kutumia moto wa mkaa.

Alisema marehemu huyo aliwasha moto wa mkaa kulainisha mwamba ili aweze kupata maji, Pia alisema kisima hicho akichokuwa anachimba chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha.

"Kilichotokea ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika , "alisema

"Mwili wa marehemu haujakutwa na jera lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda.

Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha.

MPINGA CUP 2016 YAKONGA NYOYO ZA WAKAZI WA KITUNDA

$
0
0
 WP 7627 PC Sharifa Ismaili, Polisi Konsitebo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, akigawa vipeperushi kwa moja ya timu zilizoshiriki kwenye michezo ya MPINGA CUP 2016, makundi raundi ya kwanza kutoka kundi C iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kitunda, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam. (Picha na Traffic Makao Makuu). 
WP 7627 PC Sharifa Ismaili, Polisi Konsitebo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, akikabidhi mipira kwa moja ya timu zilizofanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo ya MPINGA CUP 2016, makundi raundi ya kwanza kutoka kundi C iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kitunda, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam. (Picha na Traffic Makao Makuu).
Mkaguzi wa Polisi Aghata Mashayo akizikagua timu za kundi C zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi siku za Jumamosi na Jumapili, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam. (Picha na Traffic Makao Makuu).
 Staff Sajent wa Polisi, Enock Machunde akifundisha jambo kwa madereva wa Boda boda wakati wa michezo ya Mashindano ya MPINGA CUP 2016 kundi C zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi siku za Jumamosi na Jumapili, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam. (Picha na Traffic Makao Makuu).
 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eric Ndidi akifundisha kuzijua Alama za Barabarani kwa wachezaji wa timu za kundi C kabla ya kuingia uwanjani kwenye Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi siku za Jumamosi na Jumapili, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam. (Picha na Traffic Makao Makuu).
Staff Sajent wa Polisi, Enock Machunde akikabidhi Mpira kwa timu za Waendesha Piki Piki (Boda boda) wakati wa michezo ya Mashindano ya MPINGA CUP 2016 kundi C zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi siku za Jumamosi na Jumapili, Lengo la Mashindano haya ni kutoa Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Pikipiki ususani waendesha Boda Boda katika mkoa wa Dar es Salaam. (Picha na Traffic Makao Makuu).

Na: Traffic Makao Makuu.

Mashindano ya Kombe la MPINGA CUP 2016 hatua ya makundi inayoendelea kwenye Mkoa wa Kipolisi ILALA iliyopangwa kwenye makundi sita tayari makundi matatu yamekamilisha ratiba baada ya kupata washindi wa michezo yao ya awali kutoka kundi C, timu hizo zimechuana kuwania nafasi ya kusonga hatua ya pili baada ya jana kukamilisha ratiba hiyo na kuwa kundi la tatu kuungana na kundi A na B ambayo michezo yake imeshakamilika.

Mchezo wa kwanza wa kundi C ulianza majira ya saa nne asubuhi katika Uwanja wa Kitunda Shule ya Msingi ikiwa ni siku ya Jumamosi tarehe 27/8/2016 ambapo timu ya Chakenge F.C iliweza kucheza dhidi ya timu ya Mara fc ikifuatiwa na Mchezo wa pili ambao timu ya Kivule C.C.M (A) ilipata Ponint za mezani baada ya timu ya Polisi Kitunda kushindwa kutokea Uwanjani na kukabidhiwa Mpira mmoja kwa ajili ya kujinoa kwa kinyang’anyiro cha mzunguko wa pili.

Mchezo mwingine ilikuwa ni kati ya timu ya Mwembeni Fc Kivule iliyoshindwa kutumia vyema nafasi walizopata kipindi cha kwanza ambapo waliambulia kupata goli 1 dhidi ya wenzao wa Amani fc wakati timu ya Matembele Kivule walishinda kwa kupata magoli mawili (2) katika mchezo wa tatu huku mchezo wan ne (4) Njia Panda Msikitini fc Kitunda ilitolewa kwenye mashindano na timu ya Relini Kitunda iliyoibugiza kwa jumla ya mabao 3-2 na kuzawadiwa mpira ili wakajiweke vema na mzunguko wa pili.

Mwendelezo wa Mashindano haya ya MPINGA CUP 2016, ilifuata siku ya 28/8/2016 Siku ya Jumapili na michezo iliyochezwa ilikuwa ni mitano (5) ikiwa na jumla ya timu kumi zilizokutana kwenye kutafuta nafasi ya kusonga mbele hatua ya kwanza mtoano, Katika Mchezo huo mgumu kwa timu zote mbili, Matembele fc (KIPUNGUNI) dhidi ya timu ya Pentagini Fc ambapo mshindi alikuwa ni Matembele Kipunguni kwa njia ya Penalt -4-3 na kuzawadiwa mpira kwa ajili ya kwenda kujiandaa na mchuano wa dulu la pili.

Mchezo mwingine ulizikutanisha timu za Kitunda fc Kivule iliyocheza na timu ya Mwembeni fc Kivule na timu ya kitunda Fc ilifanikiwa kuibuka na Ushindi wa mnono wa mabao 3-1 dhidi ya wenzao wa Mwembeni Fc na kuzawadiwa Mpira moja kwa ajili ya kwenda kujiandaa na raundi inayofuata.

Na mchezo wa Tatu uliokuwa na mshikemshike mkubwa dhidi ya timu zote kwa Mashabiki wao, Timu ya MACHIMBO F.C walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MUSOMA BUCHA F.C MACHIMBO ambayo hata hivyo mchezo huo ulimalizika kila timu ikiwa na mashike mshike mkubwa na ulikuwa ni mchezo wa kusisimua kutokana na ulivyochezwa kwa ufundi mkubwa na wachezaji wa timu zote mbili hata ivyo mshindi alizawadiwa mpira kwa lengo la kwenda kufanya maandalizi mazuri ya mzunguko wa pili.

Michezo yote hiyo iliongzwa na Mafunzo Muhimu kwa Walimu wa Masuala ya Elimu ya Usalama Barabarani ambao walitoa Mafunzo hayo kwa timu zote kabla ya kuingia uwanjani huku wakifundidishwa pia Alama za Barabarani na Kuulizwa Maswali na Washindi mbali mbali walizawadiwa Furana kutoka kwa wadhamini Mbali Mbali wa Mashindano haya ya MPINGA CUP 2016 yanayofanyika kwenye Mkoa wa Kipolisi ILALA.

Ambapo timu ya Kitunda Sabato Fc ilifanikiwa kuifunga timu ya Kipunguni Relini kwa jumla ya mabao 2-0 katika mchezo ambao ulikuwa wa Upande mmoja huku wachezaji wa timu ya Kipunguni Relini wakisingizia Uwanja kuwa na Michanga wakilinganisha na Beach Soccer, pamoja na yote lakini hatimaye washindi walipatikana na kufnikiwa kijipatia zawadi ya mpira mmoja kila timu iliyoibuka Kidedea.

Mchezo wa Mwisho Timu ya Kivule Silali ilipepetana na timu ya Nyantila fc, timu mbili ambazo ni wapinzani wa jadi walijikuta wakimaliza dakika 90 kwa kutoshana nguvu baada ya kumaliza wakiwa wamefungana bao moja kwa moja 1-1. Lakini hata hivyo kutokana na Sheria ya Mashindano mshindi ni lazima apatikane, walikwenda kwenye mikwaju ya Penalti na mshindi kuwa timu ya Nyantila Fc waliopata mikwaju ya Penali nne (4) huku wenzao wa timu ya Kivule Silali wakiambulia kupata mikwaju miwili (2) ya Penalti na hivyo kumaliza Kundi hilo na Sasa Mashindano Haya ya MPINGA CUP 2016 yatafanyika Kiwalani wiki hii kama ratiba inavyoonyesha.

RATIBA YA MASHINDANO YA BODABODA KUNDI D:

Uwanja ni Chuo cha Walemavu Kiwalani Tarehe 3/9/2016.

1. Mafundi Fc Vs PANDA KIWALANI F.C

2. BOMBOM F.C vs KIJIWE SAMLI KIWALANI

3. YOMBO HOSPT.KIWALANI vs MORNING STAR KIWALANI

4. KIPAWA FC vs KIPAWA SHELI FC

5. VINGUNGUTI SCANIA vs KIZOTA F.C VINGUNGUTI

6. MORNING STAR F.C vs WASHAWASHA F.C

7. KIWALANI BEACH F.C vs BODABODA GARDEN

KAtika UWanja huo huo tarehe 4/9/2016

1. VINGUNGUTI RELINI vs MAZIZI F.C

2. MTI PESA vs MASHUJAA F.C

3. TABATA DARAJANI F.C vs BALAKUDA HIGHLAND FC

4. GOGOVIVU F.C vs BODABODA F.C

5. MANDEZE F.C vs YOMBORELI F.C

6. VIPAJI FC vs GOLAN F.C

Inavyoonekana kwenye kundi hili kutakuwa na ushindani mkubwa sana kutokana na timu nyingi kujitokeza kujiandikisha kutoka maeneo ya kundi D, ambapo jumla ya 14 zitacheza siku hiyo ya jumamosi na siku inayofuata jumla ya timu 12 zitacheza na kupata washindi pekee watakaosonga mbele hatua inayofuata ya mashindano haya a kusisimua na yenye mafunzo mazuri kwa madereva wa Boda boda.

Wadhamini mbali mbali wamejitokeza kudhamini na kuweza kufanikisha michezo hii kuwa ya aina yake mwaka huu ikiwa ni pamoja na Udhamini Wa G.S.M wauzaji wa Piki waliotoa zawadi ya Pikipiki kwa Mshindi, Cool Blue Tanzania ambao kwa hakika wameonyesha Sapoti nzuri kwa kutuhakikishia Maji kwa wachezaji wakati wote wa michezo sambamba na kampuni ya Coca Cola,Big Bon, NMB, Zantel, Haki Elimu, Star Times, Windhoek, Red Bull, NHIF, PUMA, Yono, Dar City Promotions, TBL, Milcom, E.F.M Radio, T-Marc Tanzania, Michuzi Blogs, Mwananchi Communications, Dira Tv, My Way Entertainment, Mashujaa Band, MpaluleBlogs: Miss Demokrasia Tanzania, Balozi wa Demokrasia Tanzania, na Jeshi la Polisi Tanzania.

DALADALA LAGONGA MAGARI MATATU MAJI MATITU TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
Daladala hili likiwa limegonga gari namba T 458 CAN.
Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.

Na Dotto Mwaibale

MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.

Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.

Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.

" Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema Juma.

Alisema baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.

Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.

Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.

AKINAMAMA WAJAWAZITO WAJIFUNGUA KWA TOCHI ZA SIMU MONDULI - ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza, Arusha.

Wajawazito katika zahanati ya kijiji cha Selela kata ya Selela wilaya ya Monduli mkoani Arusha wamelazimika kujifungua kwa kutumia tochi za simu pamoja na taa ya chemli kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme kwa takribani mwezi mmoja na wiki mbili.

Kinamama wa kijiji hicho tumaini shirima na mwasiti hemedy wameeleza kuwa wamekua wakiwapeleka wajawazito kwenye zahanati hiyo kwa ajili ya kujifungua na kushuhudia wauguzi wakitumia tochi za simu kutoa huduma kwa wajawazito jambo ambalo linawafedhesha hivyo wameiomba serikali isaidie upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme ili waweze kupata huduma bora.

“Tunapata shida hata tunapowapeleka Wajawazito zahanati hakuna umeme wauguzi wanatumia tochi za simu, juzi tulimpeleka mwenzetu akajifungue tuliona hilo likijitokeza kwa sababu umeme hakuna”

Mganga wa zahanati hiyo Michael Msalu alisema kuwa nyakati za usiku wanalazimika kutumia tochi jambo ambalo linaweza kuathiri afya ya mama mjamzito na mtoto, vile vile wameshindwa kufanya baadhi ya vipimo maabara kutokana na kukosa huduma ya umeme .
 
Msalu anaeleza kuwa si jambo zuri kiafya kushika simu huku unamhudumia mama mjamzito unaweza kusababisha maambukizi kwani huduma hiyo inahitaji uangalifu mkubwa ili kulinda afya ya mama na mtoto pamoja na mtoa huduma.

Diwani wa kata ya Selela, Cathbert Meena amesema kuwa licha ya zahanati hiyo shughuli za kiuchumi na kijamii zimesimama katika kata hiyo ikiwemo biashara, mashine za kusaga nafaka kwa muda wa mwezi mmoja na wiki mbili baada ya transfoma iliyowekwa na Tanesco kupata hitilafu baada ya kuwasiliana na mamlaka hiyo imekua ikitupiana mpira kati ya Rea katika maboresho hayo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Mkoa wa Arusha Tanesco ambaye ni Mhandisi Mkuu Donasian Shamba amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo linasababishwa na masuala ya kitaalamu yanayopelelekea transfoma kuungua mara kwa mara hivyo wametuma timu ya wataalamu na mapema wiki hii watarekebisha tatizo hilo ili wananchi wapate huduma.

Wakazi wa Selela wamelazimika kusimamisha shughuli zao za uchumi zinazotegemea nishati ya umeme hivyo wanaiomba serikali ichukue hatua ili waweze kurudi katika shughuli za uzalishaji zinazowaingizia kipato.

MAGAZETINI LEO; LOWASSA, MBOWE WAKAMATWA DAR ... CUF SI SHWARI

$
0
0
Viewing all 19828 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>