Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19839 articles
Browse latest View live

PSPF YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete.

Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la
Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko
huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.

“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,

“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha
Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo.

Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi.

Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego

Njaidi akikagua timu ya soka ya Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo
 
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza

Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi)

Pambano la masumbwi likiendelea.

Pambano la masumbwi likiendelea.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo

Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo.

Wanamichezo wakishangilia hotuba.

Onyesho la Judo.

Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu

Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
Picha ya pamoja.

AIRTEL YAWAWEZESHA MAWAKALA MKOANI ARUSHA KUKOPA NA KUONGEZAA MITAJI YAO

$
0
0
 Meneja wa kampuni ya Jumo Tanzania, Rweb Mutahaba akizungumza na Mawakala wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel mbinu za kukuza biashara na kuongeza mtaji kupitia huduma ya Airtel Timiza katika semina iliyofanyika jijini Arusha.
Mmoja wa mawakala wa kampuni ya Airtel jijini Arusha, David Lima akiuliza swali wakati wa semina iliyotolewa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na washirika wake Jumo kuhusu huduma ya Airtel Timiza inayowapatia wateja na mawakala nchi nzima mikopo isiyona dhamana kupitia simu zao za mkononi.
Mmoja wa mawakala wa kampuni ya Airtel jijini Arusha, Chihiyo Malick akizungumza wakati wa semina iliyotolewa na kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na washirika wake Jumo kuhusu huduma ya Airtel Timiza inayowapatia wateja na mawakala nchi nzima mikopo isiyona dhamana kupitia simu zao za mkononi.

MAONI YA MSOMAJI; NINGEKUWA MIMI NI RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.....

$
0
0
Sehemu ya kwanza

UKUTA NI MATOKEO YA UCHAGUZI ULIOPITA.

Na Peter Sarungi (Next Speaker).

Uchaguzi uliopita 2015 ulikuwa ni uchaguzi wa kihistori toka siasa ya vyama vingi ulipoanza nchini. Ulikuwa ni uchaguzi ambao tulishuhudia maajabu mengi ambayo hatukuwahi kuyaona katika chaguzi zilipita. Tuliona miiko ya vyama ikivunjwa, vigogo maarufu wakihama kambi zao za miaka mingi na wengine kustaaf gafla siasa kwa shinikizo mbalimbali, tuliona mbwembwe nyingi na maigizo mengi ya jukwaani, tuliona kejeli na kashfa nyingi, tuliona misukosuko mingi ya polisi dhidi ya wanasiasa, tuliona matamko mengi ya makundi mbalimbali ya jamii juu ya wagombea, tulishuhudia usaliti mkubwa, tuliona kampeni zilizo andaliwa kwa kiwango cha juu na za garama za juu kabisa kuwahi kutokea Tanzania, tulishuhudia kambi zikifanya kazi isiyokuwa na malipo usiku na mchana bila kulala, tulishuhudia mafuriko ya kila aina kwa kambi zote, tulishuhudia mbinu chafu na safi zilizotumika, tulishuhudia uvumilivu na ustaimilivu mkubwa kwa wananchi wa kambi zote, tulishuhudia vifo vya gafla na vya mshituko kwa baadhi ya wanasiasa wakubwa (R.i.p all), tulishuhudia kesi tata na kuntu za kutafsiri katiba, tulishuhudia upindishwaji wa baadhi ya vifungu na makatazo, tulishuhudia mihemko na hari kubwa ya vijana na wanawake kwenye siasa, tulishuhudia matumizi makubwa ya teknohama na mitandao ya kijamii, tulishuhufia idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura lakini vilevile tulishuhudia matokeo ya kura tulizopiga (CDM 6M, CCM 8M).

Bila kupepesa macho na mdomo, uchaguzi huu 2015 ulikuwa wa mnyukano mkali sana uliotikisa nchi kwa kila nyanja ya uchumi, siasa, jamii na kimataifa. Ni uchaguzi ulifuatiliwa na mataifa mengi ya nje na majirani zetu, wengi walitaka kuona ukomavu wa kidemokrasia kwa nchi yetu hasa kigogo mmoja alipoamua kupambana na kambi aliyo lelewa tangu aanze siasa. Kambi zote zilikuwa na imani na mategemeo makubwa ya kushinda uchaguzi. Tume na mabadiliko yake ya mara kwa mara nayo ilijinasibu kwa watanzania kuwa itatenda HAKI.

Kwa hayo yote yaliyofanyika kipindi cha uchaguzi ni dhairi na ukweli usiopingika kuwa Uchaguzi huu umeacha VIDONDA ambavyo mpaka sasa bado ni vibichi kabisa vinavyohitaji kutibiwa haraka ili walau vibadilike na kuwa makovu yanayotoweka taratibu. Na vidonda hivi ndivyo vinavyozalisha operation kama hii ya UKUTA. Maranyingi tunapoenda msibani utakuta watu wengi wanalia kwa uchungu wa misiba ya wapendwa wao waliotangulia kabla ya msiba huo, yaani unakuta mtu anaenda kwenye msiba wa jirani yake lakini analia kwa uchungu huku akikumbuka mpendwa wake aliyefariki miaka ya nyuma. Vivyo hivyo katika operation hii ya UKUTA wengi watashiriki kuandamana kwa maumivu waliyoyapata katika uchaguzi uliopita. Hii ni kawaida kabisa ya binadamu kupata sehemu ya kutoa hisia zake na kuelezea maumivu yake ili awe huru na maisha yaendelee.

Ningekuwa mimi ni Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kama alivyo JPM, Ningeanza na kutibu vidonda vilivyosababishwa na uchaguzi maana ni wengi walio umia na matokeo ya kushindwa. Unapokuwa Raisi wa nchi maana yake unakuwa Raisi wa raia wote bila kujali itikadi zao na bila kujali kama walikuchagua ama laa. Na kwa sababu hii ni siasa basi ukiwa kama raisi unapata nafasi nzuri ya kuwarudisha na kuongeza imani kwa wale ambao hawakukuchugua.

Mimi Ningeunda baraza ama kamati ya kutibu haya maumivu yaani chombo cha usuluhishi na kujenga umoja wa kitaifa. Chombo hichi kingekuwa na kazi kuu mbili, 1. Kurejesha umoja wa kitaifa kuanzia juu kwa viongozi hadi chini kwa wananchi, 2. Kushugulika na mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi kwa kila idara. Naamini hii ingesaidia sana utawala wa JPM maana sio afya hata kidogo kudharau na kubeza kura 6M za upande wa pili kwa mamlaka uliyopata kwa kura 8M. Hizi kura 6M ni watu wa makundi mbalimbali ya jamii na wa rika tofauti na ni watanzania wenye haki katika nchi yao, kuwaweka kando na kubeza uwepo wao ni kosa kubwa kisiasa kiuchumi na kwa ustawi wa jamii.

#MyTake Mhe. John Pombe Magufuli nakushauri uunde chombo hicho cha usuluhishi na kujenga umoja wa kitaifa ili kuondokana na vikwazo kama hivi katika utawala wako maana yawezekana haya yakajitokeza kwa wingi mbeleni. Unaweza kukiunda kabla ya UKUTA ama baada ya UKUTA.

Tupo wengi tunaopenda aina ya uongozi wako maana madhaifu ni machache kuliko mazuri na tungependa kuendelea kula matunda ya uongozi wako kwa kipindi chote bila kikwazo.

Asanteni sana.

U.S. ARMY AND NATIONAL GUARD TRAIN 50 TANZANIAN GAME SCOUTS

$
0
0
Major General Greg Lusk, Adjutant General for the North Carolina National Guard, speaking with U.S. Ambassador to Tanzania Mark Childress, Permanent Secretary of the Ministry of Natural Resources and Tourism (MNRT) Major General Gaudence Milanzi, and game scouts. The game scouts are participating in training conducted by U.S. military experts and funded by the U.S. government to increase their capacity to combat wildlife poaching and trafficking. (Photo Courtesy of U.S. Embassy)
---
Rungwa Game Reserve, TANZANIA. On Wednesday, Ambassador Mark Childress observed a training demonstration of field techniques learned by Tanzanian game scouts to increase their capacity to combat wildlife poaching and trafficking in Rungwa Game Reserve. The game scouts have been participating in a training conducted by U.S. military experts from U.S. Army Africa Combined Joint Task Force - Horn of Africa and the North Carolina National Guard Special Forces, and funded by the U.S. government.

During two three-week training sessions between July 25 and September 9, 50 Tanzanian game scouts are being trained in surveillance and patrol techniques, arrest and detention procedures, search and seizure, crime scene investigation, first aid, human rights and rules of engagement.

Major General Greg Lusk, Adjutant General for the North Carolina National Guard, traveled to Tanzania to observe the training. Wednesday’s demonstration of field techniques was also attended by the Permanent Secretary of the Ministry of Natural Resources and Tourism (MNRT) Major General Gaudence Milanzi, the Project Manager of Rungwa Game Reserve Saidi Kabanda, and the Country Director of the Wildlife Conservation Society (WCS), Tim Davenport.

This training program was initiated after Ambassador Childress visited Rungwa Park in 2015. Seeing the need for capacity building and improved infrastructure to stop the alarming rates of poaching in the Game Reserve, the Ambassador pledged to take quick action and, within a year, marshalled support from a variety of partners to assist the game scouts. He highlighted that an infusion of support from The Wyss Foundation provided equipment and light gear to game scouts at a post that had been taken over by poachers, enabling the game scouts to patrol this post during the rainy season for the first time in more than a decade. At the event on Wednesday, the Ambassador remarked, “This program highlights the strong collaboration that the United States has with Tanzania and is a model of what can be achieved when we all work together: government, security forces, the international community, NGOs, the private sector, and Tanzanian citizens across the country.”

This program is one part of a major effort by the U.S. Government and other partners to protect the elephant and wildlife corridor between Rungwa and Katavi, thus conserving a critical link between the Ruaha-Rungwa and Katavi ecosystems. The U.S. Agency for International Development (USAID), in partnership with WCS, is supporting the $8.5-million five-year Southern Highlands and Ruaha-Katavi Protection Program (SHARPP). SHARPP is focused on four key areas: wildlife management areas (WMAs); livelihoods; habitat management; and elephant monitoring and protection. In addition to this capacity training for the game scouts in Rungwa, WCS, with support from both USAID and private funds, has also conducted training with Tanzanian game scouts on crime scene management, the Spatial Monitoring and Reporting Tool (SMART), and rapid reaction.

DADA MKALI WA KURUKA SARAKASI

$
0
0

KAMPUNI YA UDALALI YA YONO YAINGIA MKATABA WA KIMATAIFA NA KAMPUNI YA BIDDERS CHOICE YA AFRIKA KUSINI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart & Co. Ltd, Scholastika Christian Kevela (kushoto), akiwaonesha waandishi wa habari Dar es Salaam leo (hawapo pichani), mkataba wa kimataifa walioingia na Kampuni ya Bidders Choice ya Afrika Kusini wa ushirikiano kwa ajili ya kufanya mnada wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Stanley Kevela.
---
Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart imeingia mkataba wa ushirikiano na Kampuni ya Bidders Choice ya Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya mnada wa mitambo ya kampuni ya uchimbaji ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu Bulynhulu uliopo mkoani Shinyanga .

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Scholastika Kevela alisema wameingia mkataba huo Agosti 24 mwaka huu ambapo watafanya minada ya kuuza mitambo ya zamani ya kampuni ya Acacia kwa njia ya mtandaoni.

Alisema kampuni ya Bidders Choice imewapa tenda ya kufanya minada ya mitambo ya zamani ya madini mbalimbali ambayo inatakiwa kutolewa na kuwekwa mipya.

“Hivyo tunategemea kwenda kwenye mgodi wa dhahabu Bulynhulu kuangalia ni mitambo gani inatakiwa kupigwa mnada ili iwekwe mingine,”alisema Kevela.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo,Stanley Kevela alisema kampuni yake ilipata tuzo ya ufanyaji kazi kwa ubora ambayo imesaidia nchi ya Afrika Kusini kutoa mkataba huo wa kimataifa ambao haujawahi kufanyika nchini kwa kampuni nyingine ya udalali isipokuwa ya Yono.

Alisema kutokana na utendaji wao kuwa mzuri hivyo wanatarajia kuanzisha chuo cha madalali kitakachosaidia serikali kukusanya mapato ya kutosha.

“Hiki chuo cha madalali kikianzishwa kitaleta maendeleo kwenye jamii yetu na jamii wataelewa umuhimu wa kukusanya kodi hivyo taifa litapata mapato mengi, alisema Kevela.

KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YATEMBELEA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart, Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.

Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.

Na Dotto Mwaibale.

Kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa leo asubuhi imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea mradi wa Udart yenye lengo la kujua jinsi mradi huo unavyoendeshwa pamoja na kujua changamoto zake ambapo wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba vijijini.

Katika hatua nyingine ya ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa wafanyabiashara katika Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa haraka (Udart)

Simbachawene alitoa agizo hilo wakati akizungumza na uongozi wa Udart baada ya kufanyika majuisho ya ziara ya kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.

"Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart" alisema Simbachawene.

Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart.

Alisema changamoto waliyonayo ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila mwananchi anaipata jambo litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata huduma bora.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi.

Kamati hiyo ilitembea mradi wa udart katika vituo vikuu vya Kimara mwisho, Moroco makao makuu ya Udart Jangwani, Gerezani na Kivukoni.

WATANZANIA TUPAZE SAUTI KUKATAA MAANDAMANO YA SEPTEMBA MOSI – CHEYO

$
0
0
Mwenyekiti wa UDP Mh. John Cheyo akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar, akiwaomba viongozi wa chama cha CHADEMA, Kusitisha maandamano yao waliyoyapa jina la UKUTA, wanayotarajia kuyafanya Septemba Mosi nchi nzima, Mhe. Cheyo amekiomba chama hicho kutofanya maandamano hayo kwa lazima na badala yake watumie njia ilio sahihi ambayo ni ya mazungumzo ya mezani na kuendelea kuitunza amani ya nchi iliopo, pia amewaomba Watanzania kupaza sauti zao kuyakataa maandamano hayo yanayoweza kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu.Pichani kulia ni Kaimu Katibu MKuu wa chama hicho Mhe. Goodluck Ole Medeye.

"Ukitaka kufanya maandamano,vyombo vya usalama vikikukatalia, basi usitumie  nguvu,jaribu kutafauta njia nyingine ambayo itakuwa ya amani zaidi kuliko kulazimisha,jambo ukililazimisha bila kufuata taratibu na sheria za nchi, matokeo yake hayatakuwa mazuri, yataleta machafuko na kutia doa  amani ya nchi yetu ambayo tumekuwa tukijivunia,hivyo nawasihii ndugu  zangu wa CHADEMA bado kuna njia nzuri za kufuata na kufikia muafaka wa  jambo hilo bila kusumbua amani ya nchi yetu iliopo kwa sasa" alisema Mhe. Cheyo.
Mhe. Cheyo akisitiza jambo wakati alipokuwa akijiabu maswali mbalimbali ya  waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kukitaka chama cha  CHADEMA kusitisha maandamano yake, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara  ya Habari MAELEZO,Vicent Tinganya.PICHA NA MICHUZI JR.

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo amewataka Watanzania kupaza sauti na  kukataa maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu ambayo yameandaliwa na  Chama cha Demokrasia (CHADEMA).

Cheyo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake juu ya maandamano hayo.

“Watanzania wenzangu jambo la kuwaacha watoto wetu kwenda kupambana na Polisi si  jambo zuri, wote tupaze sauti zetu na kusema hapana kwa maandamano ya  Septemba Mosi,” alisisitiza Cheyo.

Alisema kuwa, ziko njia mbalimbali ambazo Chadema wanaweza kuzitumia kutatua  migogoro, kama vile meza ya mazungumzo na kuachana na maandamano ambayo  yanachochea vurugu na hata kutishia amani ya nchi.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linapotoa katazo la maandamano ni lazima utii  uwepo, kwani Polisi wapo kwa mujibu wa Sheria na Katiba. Ikiwa Chama  hicho hakikuridhika na katazo hilo basi wanatakiwa kuonana na Waziri anayehusika na Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi alisema kuwa Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua za makusudi za kutatua matatizo mbalimbali kama vile kupambana na ufisadi, ambapo  viongozi wengi wa Serikali wamesimamishwa kazi au kufukuzwa kutokana na  kujihusisha na masuala ya rushwa.

Mwenyekiti huyo wa UDP amewataka watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Magufuli ili  aweze kutimiza ndoto zake na yale ambayo ameyaahidi kwa ajili ya nchi ya Tanzania.

Aidha Cheyo aliwasifu viongozi wa Dini ambao walikaa na Viongozi wa Umoja wa  Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kukubali kurudi bungeni bila pingamizi  lolote. Amewataka viongozi hao wa dini kuendelea kuzungumzia suala la  amani kwa Watanzania na Viongozi wa kiasa ili kudumisha amani ya nchi.

MKUU MKOA WA DAR, MAKONDA ATUMIWA BARUA YA WITO NA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

$
0
0

MWANARIADHA SIMBU AREJEA NCHINI TANZANIA AKITOKEA KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI, BRAZIL

$
0
0
 Mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania Alphonce Felix Simbu (24) jana amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam akitokea nchini Brazil kwenye michuano ya Kimataifa ya Olimpiki.

Simbu alitia fora kwa kushika nafasi ya 5 kwenye siku ya mwisho ya michuano ya Olimpiki katika mashindano ya marathon jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Alitumia saa 2:11:15, sekunde 11 nyuma ya mshindi wa nne Ghirmay.

MHE. LUKUVI AZINDUA RASMI MIRADI YA UPATIKANAJI WA PICHA ZA ANGA (BASEMAP) NA MFUMO UNGANISHI WA TAARIFA ZA ARDHI (ILMIS)

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akizindua rasmi Miradi ya upatikanaji wa picha za anga (Basemap) na mfumo unganishi wa taarifa za Ardhi (ILMIS). Wanaoshuhudia pamoja naye; Kulia kwake ni Waziri nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Mhe. George Simbachawene, kushoto kwake ni Naibu wake; Mhe. Angeline Mabula katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akiwa amemaliza tukio la Uzinduzi wa Miradi ya upatikanaji wa picha za anga (Basemap) na mfumo unganishi wa taarifa za Ardhi (ILMIS) . Wanaoshuhudia pamoja naye; Kulia kwake ni Waziri nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Mhe. George Simbachawene, kushoto kwake ni Naibu wake; Mhe. Angeline Mabula na pembeni kabisa ni Katibu Mkuu wake; Dk. Yamungu Kayandabila katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi akisisitizia jambo wakati wa Uzinduzi wa Miradi ya upatikanaji wa picha za anga (Basemap) na mfumo unganishi wa taarifa za Ardhi (ILMIS) , katika Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwl. J.K. Nyerere, jijini
Dar es Salaam.

TIGO FIESTA YATIKISA MJI WA KAHAMA USIKU WA JANA

$
0
0
Msanii wa Bongofleva Baraka Da Prince akitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2016 lililofanyika katika uwanja wa Taifa usiku wa jana Mjini Kahama na kuwakutanisha wasaniii wengine nguli hapa nchini katika mziki wa kizazi kipya.Christian Bella akilishambulia jukwaa la Tigo Fiesta 2016 katika uwanja wa Taifa mjini Kahama usiku wa jana.
Chege Chigunda naye alitoa burudani ya kukata na shoka katika uwanja wa Taifa kwenye Tamasha la Tigo Fiesta 2016 Mjini Kahama usiku wa jana.
Chege Chigunda.
Jux akiwa na Dancer wake akitumbuiza wimbo wa Wivu katika jukwaaa la Tigo Fiesta 2016.
Maua Sama naye alipamba Tamasha la Tigo Fiesta 2016 katika Uwanja wa Taifa Mjini Kahama usiku wa Jana.
Rayvany naye akitumbuiza katika jukwaa la Tigo Fista 2016 ambapo aliwasimulia wananchi wa Kahama stori ya "KWETU" na jinsi anavyotafuta "KIKI"
Stamina akitoa michano katika jukwaa la Tigo Fiesta 2016 usiku wa jana katika Uwanja wa Taifa .
Maelfu ya wakazi wa Kahama na maeneo jirani wakishuhudia burudani mbali mbali toka kwa wasanii waliotumbuiza katika jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa jana.
Mashabiki.
IMOOOOOOOOOOOOOOO
Shanngwe zikiendelea katika uwanja wa Taifa wakati Tamasha la Tigo Fiesta likiendelea usiku wa jana Mjini Kahama.

WAKALA WA VIPIMO WAWAPIGA MSASA WAKULIWA JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA MIZANI

$
0
0
WAKULIMA WA KOROSHO KATIKA MKOA WA RUVUMA WAKIPATA ELIMU KUPITIA VIPEPERUSHI VILIVYO ANDALIWA NA WAKALA WA VIPIMO WAKATI WA ZOEZI LA UTOAJI ELIMU.
MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI MTWARA AUGUSTINE MAZIKU AKIWAONESHA WAKULIMA WA KOROSHO, MKOANI HUMO KUSOMA KWA USAHIHI MIZANI ILIYO HAKIKIWA NA WAKALA WA VIPIMO
ALFA MTUI AFISA VIPIMO MWANDAMIZI, AKITOA ELIMU KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI RUVUMA NAMNA YAKUTAMBUA MIZANI ILIYO HAKIKIWA NA KURUHUSIWA KUTUMIKA NA WAKALA WA VIPIMO.
MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI MTWARA BWANA AUGUSTINE MAZIKU AKIJIBU MASWALI KUTOKA KWA WAKULIMA WALIOKUWA WAMEFIKA KUPATIWA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MIZANI ILIYO HAKIKIWA NA WAKALA WA VIPIMO KABLA YA MSIMU WA UNUNUZI WA KOROSHO KUANZA.
MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO MKOANI RUVUMA BW. HALLET HASSAN AKITOA ELIMU KWA WAKULIMA WA KOROSHO MKOANI HUMO KABLA YA MSIMU KUANZA ILI KUEPUSHA KUZULUMIWA NA WANUNUZI WASIO WAAMINIFU. (Picha zote na Iren John).

MAGAZETINI LEO; MUUAJI POLISI NI KOMANDOO... VIGOGO CHADEMA WAKAMATWA

$
0
0

KAMANDA SIRRO ATANGAZA KULA SAHANI MOJA NA WANANCHI WATAKAOANDAMANA SEPTEMBA MOSI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kamanda Sirro akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Magari ya polisi yenye zaidi ya askari 80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha Kati, yakielekea Vikindu kwa ajili ya Operesheni saka majambazi.
Askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kuelekea Vikindu kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa ujambazi.

Na Dotto Mwaibale

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Simon Sirro ametangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

“Jeshi la polisi mkoa wa Dar es Salaam tumejipanga vizuri siku hiyo nawaomba wananchi wasidhubuti kujitokeza kuandamana siku hiyo kwani watakiona cha moto” alisema CP Sirro.

Sirro alisema tayari jeshi hilo lina taarifa za kiinteligensia kuwa kuna vijana wanapewa fedha kwa ajili ya kuandamana na kufanya fujo Septemba mosi.

Aliwasihi wananchi hasa vijana kutoingia barabarani Septemba mosi na kuwaachia wachache wenye nia ya kuletafujo.

“Ni rai yangu wale wananchi wazalendo wan chi hii wasiopenda kupambana na jeshi lao la polisi ambalo linawalinda na kulinda mali zao siku hiyo wasiingie barabarani,” alisema.

Aliwakaribisha wanao taka kuingia barabarani na kupambana na jeshi hilo na kuwa watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

“Sisi tupo vizuri na tupo imara hasa kwa wale wanaopenda kuvunja sheria kwa makusudi wata wajibika kwa mujibu wa sheria, hivyo suala la utiiwa sheria bila shuruti ni la msingi sana,” alisema Sirro.

Alisema jeshi hilo limejiandaa kwa wananchi wachache ambapo alibainisha wananchi wengine hawana haja na maandamano hayo huku akibainisha vijana wachache wenye shida kupewa fedha na viongozi kwa lengo la kuandamana.

“Jiulize hiyo 40,000 unayo pewa kuingia barabarani na matokeo yake ukavunji kama mguu hiyo 40,000 ina thamani gani kwani… kwa hiyo mimi kama kiongozi wenu wa jeshi la polisi na sisitiza na ninaelekeza tuwaache wale wenye sababu zao binafsi waingie barabarani,” alisema.

Katika hatua nyingine Kamanda Sirro alisema askari zaidi ya 80 wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wameondoka kwenda vikindu na maeneo mengine wilayani Mkuranga mkoani Pwani kufanya operesheni ya kuwasaka watu wanaodhaniwa kujihusisha na ujambazi.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMSIMAMISHA KAZI AFISA MAENDELEO YA JAMII WA JIJI KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

$
0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani J. Kihamia amempuzisha kutekeleza majukumu yake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji Bi. Mwantumu Dosi kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake hivyo kukiuka kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.

Mkurugenzi Kihamia ametoa taarifa hiyo leo tarehe 27.08.2016 baada ya kukamilisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kufanya tathmini ya miradi iliyopitiwa na Mwenge na kugundulika kwa dosari zilizojitokeza katika moja ya mradi ambao uko chini ya Idara hii.

Mradi huo ni kikundi cha vijana wanaojishughulisha na Uselemara pamoja na Uchomeleaji kinachojulikana kama Mbeshere Umoja Group kilichopo Kata ya Olorieni kiligundulika kuwa na wananchama waliovuka umri wa miaka 35 ambao hawastahili kunufaika na Mikopo ya Vijana kwa mujibu wa Sera.

Mwenge wa Uhuru katika Jiji la Arusha ulikimbizwa tarehe 24.08.2016 na Kikundi hicho kilikua ni miongoni mwa miradi iliyokua inapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambapo wanachama wake hawakizi vigezo. Wanachama hao walikua wameandaliwa kupewa Hundi ya TSH Milioni tano kama ishara ya kuunga mkono jitihada zao zakuboresha maisha. Mkimbiza Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg. George Jackson Mbijima alisitisha zoezi hilo baada ya kugundua dosari za umri kwa baadhi ya wanachama.

Kupumzishwa kutekeleza majukumu ya Mkuu wa Idara hii kunafuatana na masharti ya kukabidhi Ofisi kwa Mratibu wa Tasaf Bi. Tajiel Mahega ambaye kwa sasa atakua Kaimu Mkuu  wa Idara hii mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji la Arusha.
27 Agosti,2016

MISS ILALA TALENT SHOW 2016 ILIVYOBAMBA NDANI YA HIGH SPIRIT - DAR ES SALAAM

$
0
0
Warembo 15 wanaowania taji la Miss Ilala 2016, usiku wa kuamkia leo walichuana vikali katika kutafuta mrembo mwenye kipaji ambapo warembo wote walishindana kwa kuonesha vipaji vyao vya ubunifu, uchezaji muziki na uimbaji wa nyimbo mbalimbali.
Hii ndio tano bora ya Warembo wenye Vijapaji kutoka Miss Ilala 2016.
Washiriki mbalimbali wakionesha ujuzi wao kulingana na vipaji walivyo jaaliwa.
Washiriki mbalimbali wakionesha ujuzi wao kulingana na vipaji walivyo jaaliwa. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI.
Washiriki mbalimbali wakionesha ujuzi wao kulingana na vipaji walivyo jaaliwa.
Washiriki mbalimbali wakionesha ujuzi wao kulingana na vipaji walivyo jaaliwa.
Washiriki mbalimbali wakionesha ujuzi wao kulingana na vipaji walivyo jaaliwa.
Mashabiki wakishangilia
Wapenzi na Mashabiki wa sanaa ya Urembo nchini wakifuatilia shindano hilo.

PICHA YA LEO

$
0
0
Aliyekuwa mgombea wa UKAWA kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Waziri Mkuu wa zamani, Mhe. Edward Lowassa akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo kwenye Jubilei ya dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu awamu ya tatu, Mhe. Benjamin Mkapa na Mke wake Mama Anna Mkapa.

SIMBA YATOA SARE YA 0-0 NA JKT RUVU

$
0
0
Meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi (kulia), akiteta jambo na Kiungo wa timu hiyo Mwinyi Kazimoto baada ya kuisha mechi yao dhidi ya Jkt Ruvu,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib (kulia),akiwania mpira na beki wa Jkt Ruvu, Nurdin Mohammed,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchemzo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo (kulia),akivutwa jezi na beki wa Jkt Ruvu, Nurdin Mohammed,katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchemzo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
Mashabiki wa Simba wakiwa wameduaa baada ya timu ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Jkt Ruvu, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchemzo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.
---
KOCHA msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema kuwa kikosi chake kilicheza vizuri sema mapungufu katika safu ya ushambuliaji yameinyima ushindi timu yake.

Simba imelazimishwa suluhu ya kutokufungana na JKT Ruvu katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mayanja amesema kuwa bado wanajipanga kuweza kuhakikisha wanashinda kwenye michezo yao inayofuata.

Katika mchezo wa awali Simba walitoka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Ndanda na baada ya matokeo haya wanasalia na alama nne huku kwenye michezo mingine Azam amefanikiwa kushinda 3-0 dhidi ya Majimaji ya Songea mchezo ulipigwa uwanja wa Chamazi.

Mtibwa Sugar nayo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Ndanda huku Mwadui Fc wakitoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 1-0.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA JUBILEI YA DHAHABU (MIAKA 50) YA NDOA YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA NA ANNA MKAPA JIJINI DAR

$
0
0
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu Francis toka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam jana Jumamosi Agosti 27, 2016
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam jana Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukrani wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yake na na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam jana Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za pongezi wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam jana Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe wakati akiwasili kuhudhuria  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani  tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani  tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  wakiwa tayari kwa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  na wageni waalikwa akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli  katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 MC Mavunde akipiga kinanda wakati wa  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

  Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya waumini na wageni waalikwa   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Wanakwaya katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Kiongozi wa kwaya  katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa    katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo  katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Bw. Nicholaus Mkapa, mtoto wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa  akisoma somo la kwanza   katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongea na wana familia, waumini na wageni waalikwa katika  Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni waalikwa  wakiwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akimvisha pete Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akivishwa pete na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakifurahia jambo baada ya zoezi hilo
 Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" hao wenye furaha 
  Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro  Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" . Kulia ni  Balozi Anthony Nyaki aliyesimamia harusi yao siku kama ya leo miaka 50 iliyopita. Matron alikuwa Marehemu Lucy Lameck.
  "Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wanaketi baada ya ukumbusho wa viapo vya ndoa yao katika  kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016

 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akiongea na kadamnasi 

  Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni wakiendelea na misa
 Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa
 Sir Andy Chande akiungana na waalikwa katika misa hiyo
 Mohamed Dewji na mkewe wakiwa katika misa hiyo
 Mstari wa mbele
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg Philip Mangula na mkewe pamoja na wageni wengine
 Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa
 Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi, Maspika wastafu Mzee Pius Msekwa na Mama Anne makinda na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue
 Sehemu ya waalikwa
 Jaji Mkuu mstaafu Mhe. Barnabas Samatta na mkewe pamoja na waalikwa wengine
 Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Marten Lumbanga na mkewe pamoja na Waziri mstaafu Profesa Philemon Sarungi na mkewe Mama Sarungi
 Waalikwa
 Wageni waalikwa 
 Waalikwa
 Sehemu ya waalikwa
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiongoza wana familia kupeleka matolea altereni
 Kwaya 
 Sehemu ya waalikwa
 Waalikwa
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa 
 Misa ikiendelea
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa 
 Misa ikendelea
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mama Anna Mkapa
Mama Janeth Magufuli na Mama Maria Nyerere wakiwatakia amani Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa.
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati malumu ya ndoa kutoka Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakionesha hati yao  maalumu kutoka  Vatican
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa na hati yao kutoka Vatican
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiongea 
 Kila mtu anafurahia mafundisho ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
 Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea zawadi kutoka Paroko ya Upanga ya Mt. Imakulata 
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimia na kuwapongeza Mzee Mkapa ma mkewe
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akifurahiajambo
 Wote wanafurahia hotuba ya Rais Dkt John Pombe Magufuli 
Rais Dkt John Pombe Magufuli  
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo akitambulishwa kanisani hapo
 Ni wakati wa kupata picha za kumbukumbu ambapo Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa wanaanza na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu 
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo akimpongeza Mama Anna Mkapa
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Martin Shoo Mhe Benjamin William Mkapa
 Picha na viongozi wastaafu na wana familia 
 Picha na waliosoma na Mzee Mkapa
 Picha na kamati ya maandalizi

 Picha na viongozi wastaafu
 Picha na viongozi wastaafu na walio kazini
 Picha na watoto wa kutoka Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Kibaha (Kibaha The EOTF Orpham Centre) 
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipozi na Sir Andy Chande.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja viongozi wa dini na viongozi wastaafu na wake zao wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam jana Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakikata keki katika hafla ya chakula cha mchana waliyoandaa baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Viewing all 19839 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>