Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19839 articles
Browse latest View live

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMUAPISHA MKURUGENZI MKUU MPYA WA IDARA YA USALAMA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimuapisha Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba akila kiapo cha maadili ya viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016. Kushoto akisimamia zoezi hilo ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju na Katibu Mkuu kiongozi Engineer John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.John Pombe magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 24, 2016

PICHA NA IKULU.

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA CANADA, THAILAND NA AUSTRIA LEO IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Canada Mhe Ian Myles Ikulu jijini Dar es salaam leo agosti 24, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Canada Mhe. Ian Myles Ikulu jijini Dar es salaam leo agosti 24, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Thailand hapa nchini Mhe. Prasottiporn Wetpraisait Ikulu jijini Dar es salaam leo agosti 24, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Austria hapa nchini Mhe. Harald Gunther Ikulu jijini Dar es salaam leo agosti 24, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Thailand hapa nchini Mhe. Prasottiporn Wetpraisait Ikulu jijini Dar es salaam leo agosti 24, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Austria hapa nchini Mhe. Harald Gunther Ikulu jijini Dar es salaam leo agosti 24, 2016

PICHA NA IKULU.

BARASS BINGWA AIRTEL RISING STARS MWANZA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dr. Leonard Masale (katikati) akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa Barass Sports Centre baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza juzi. Kushoto ni Meneja wa Airtel Kanda ya Ziwa Ezekiel Nengwa.
Wachezaji wa Barass Sports Centre kabla ya mchezo wa fainali dhidi ya Hamas ambapo walishinda 6-1 na kutwaa uchampioni wa Airtel Rising Stars mkoani Mwanza.
---
Timu ya wavulana ya Barass Sports Center imetawazwa kuwa bingwa wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Mwanza baada ya kuiadhibu Hamas Sports Center 6-1 katika mechi ya fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa DIT nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Mechi hiyo ilitanguliwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliozikutanisha timu za Nyamagana United na HHT ambapo Nyamagana waliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0. Goli hilo pekee lilifungwa na Khalifan Kamanga katika dakika ya 50.

Katika mchezo wa fainali, Hamas Sports Center ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata goli katika dakika ya 10 lililowekwa kimiani na Rogose Albert kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Barass Sports Center.

Kuona hivyo Barass walikuja juu na kulisakama lango la wapinzani wao kama nyuki na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 13 kupitia kwa Celuha Nehemia aliyefanya kazi ya ziada kupangua ngome ya Hamas kabla ya kuweka mpira wavuni.

Hamas walifanya mashambuli ya nguvu kwa nia ya kupata goli linguine lakini juhudi zao hakuzaa matunda na kujikuta wakifungwa goli la pili. Goli hili lilifunfuwa na mshambuliaji machachari Frank Osoro katika dakika ya 27.

Alikuwa ni Osoro tena aliyewainua mashabiki wa Barass Center baada ya kuwatoka walinzi wa Hamas na kufunga goli la tatu zikiwa zimebakia dakika mbili tu kabla ya kumaliza kipindi cha kwanza.

Barass walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la nne katika dakika ya 55 kupitia kwa Maseke Mabigi ambaye alishirikiana vizuri na washambuliaji wenzake na kuachia shuti iliyojaa wavuni hivyo kuwakatisha tamaa wapinzani wao.

Mabigi ambaye alikuwa mwiba mkali kwa walinzi wa Hamas alifanikiwa kufunga goli la tano katika dakika ya 63 kabla ya Deo Martine kuhitimisha karamu hiyo ya magoli kwa kufunga goli la sita mnamo dakika ya 77.

Mechi za mashindano hiyo zimewawezesha makocha kuchangua kombaini ya wavulana ambayo itawakilisha mkoa wa Mwanza katika fainali za Airtel Rising Stars ngazi ya taifa zinazotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia September 6 hadi 11.

Timu zitakazoshiriki fainali hizo zitatoka Ilala, Kinondoni, Temeke, Zanzibar, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mwanza na Arusha.

JENGO LA HOSPITALI LENYE THAMANI YA BILIONI 8.8 LAJENGWA JIJINI DAR

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul makonda leo ameonyesha picha za jengo kubwa la hospitali ya kinamama ambalo ujenzi wake tayari umeanza kwa msaada kutoka Serikali ya Korea Kusini na linatarajiwa kuzinduliwa na Rais Magufuli mwezi wa nne mwakani.

Jengo hilo litakalogharimu jumla ya shilingi bilioni 8 na milioni 800 litakuwa na uwezo kulaza wakinamama (wagonjwa) 160 kwa wakati mmoja na litakuwa na chuo kwaajili ya wanafunzi na tayari Madaktari kutoka Korea wamesha anzaa kutoa mafunzo ya magonjwa ya kinamama.

TAARIFA YA NHC NAMNA INAVYOSAIDIA UPATIKANAJI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA SERIKALI WANAOHAMIA DODOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam kuhusu wadaiwa sugu wa pango katika shirika hilo moja ya wadaiwa waliotajwa ni Jengo la Club Billicanas ambali linadaiwa Bilioni moja, Kulia ni Meneja Mauzo wa NHC Bw. Itandula Gambalagi na katikati ni Muungano Saguya Meneja katika ofisi ya Mkurugenzi.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo Upanga kushoto ni Hamad Abdalla Mkurugenzi wa Miliki NHC na katikati ni Suzan Omari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NHC .
---
Serikali imeamua kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala inayoelekeza Serikali kuhamishia shughuli zake Mji Mkuu wa nchi yetu Mjini Dodoma. Shirika la Nyumba la Taifa linaunga mkono uamuzi huu wa kizalendo wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wenye lengo la kuharakisha maendeleo ya nchi yetu. Sisi katika Shirika la Nyumba tunaunga mkono uamuzi huu kwa sababu umetupatia fursa zifuatazo:-

Kuendelea kutekeleza jukumu letu la msingi la ujenzi wa nyumba katika mji wa Dodoma kwa ajili ya watumishi wa Serikali wanaohamia Dodoma
Kuliongezea Shirika soko la nyumba inazojenga kwa ajili ya kuwauzia wananchi
Kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya ujenzi wa nyumba
Kuongeza ajira kutokana na shughuli za ujenzi wa nyumba zitakazofanyika Dodoma

B: NAMNA SHIRIKA LILIVYOJIANDAA KATIKA KUSAIDIA UAMUZI HUU WA SERIKALI:

Shirika la Nyumba la Taifa kama chombo cha Serikali limejiandaa kuwezesha upatikanaji wa nyumba za watumishi wa Serikali kwa kufanya yafuatayo:-

Tumejenga nyumba za makazi 153 eneo la Medeli, Mjini Dodoma kwa ajili ya kuuza. Kwa sasa bado nyumba 97 zinaendelea kuuzwa kwa wananchi. Nyumba hizi kwa sasa zimepangishwa na kipaumbele kitapewa kwa wapangaji waliopo ndani, na wakishindwa basi zitauzwa kwa Watanzania wengine wenye uhitaji wa kumiliki nyumba. Katika mkataba wa upangishaji nyumba hizo, kulikuwa na kipengele kinacholiruhusu Shirika la Nyumba kuuza nyumba kama watahitaji kufanya hivyo.
Tumejenga nyumba 44 za gharama nafuu katika Wilaya ya Kongwa nje kidogo ya Mji Mkuu wa Dodoma ambazo tunaziuza kwa wananchi. 

Tumenunua ekari 236 ya benki ya ardhi katika eneo la Iyumbu, pembezoni mwa Makao Makuu ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Tutatengeza Master Plan ndogo ya “Satelite Center” ndani ya Main master Plan ya Dodoma inayoandaliwa na CDA. Tunatarajia kufanya ujenzi wetu katika eneo hili na pia kuwakaribisha wawekezaji wengine watakaotaka kuwekeza au kuendeleza ujenzi katika eneo hili.
Tumenunua ekari 7 eneo la Chamwino ambazo tutazitumia kujenga nyumba
Tumenunua ekari 4 eneo la Bahi, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba
Tumenunua ardhi ekari 4 eneo la Chemba, kwa ajili ya kujenga nyumba

Kupitia akiba ya ardhi tuliyo nayo Shirika linajiandaa kuanza ujenzi wa nyumba 300 hadi 500 ndani ya miezi 12 kwa ajili ya kusaidia makazi ya watumishi wa Serikali. Kipaumbele kitakuwa kuuza na baadhi tutaziacha kwa ajili ya kupangishwa.

C: NAMNA YA KUPATA FEDHA ZA UJENZI HUU

Ili kutekeleza kwa haraka ujenzi wa nyumba za watumishi Mjini Dodoma, NHC inatarajia kuwa na shilingi bilioni 60 zitakazopatikana kutoka katika vyanzo mbalimbali vya fedha vifuatavyo:-

Kuuza nyumba 97 za makazi eneo la Medeli ambazo kwa sasa tunazipangisha ili kupata kiasi cha shilingi bilioni 15 za kujenga nyumba mpya.

Kuendelea na uuzaji wa baadhi ya maeneo na viwanja vya Shirika vilivyo wazi Jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ili kupata kiasi cha shilingi bilioni 30 zitakazotumika kujenga nyumba mpya Mjini Dodoma. Uuzaji wa viwanja hivi ni muendelezo wa kuwezesha ukuaji wa miji haraka kama tulivyoanza na uuzaji wa maeneo yetu katika eneo la uwekezaji la Safari City Arusha.

Kufuatilia madeni sugu ya kodi ya nyumba kwa wale wote wanaodaiwa, madeni yanayofikia shilingi bilioni 15,052,877,606. Fedha hizi zitatumika kujenga nyumba mpya Mjini Dodoma. Tunawasihi wadaiwa wote ikiwemo taasisi za Serikali kulipa madeni yao ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe 25 Agosti, 2016 ili kuepuka adha ya kuondolewa katika nyumba wanazopanga. Lakini kwa wale waliopewa notisi za kulipa kodi, tunawataka wahakikishe wanalipa kodi zao ndani ya muda wa notisi walizopewa na kinyume na hapo tutawatoa kwenye nyumba na kuendelea na hatua nyingine za kisheria ikiwemo kukamata mali zao.

D: NAFASI YA SEKTA YA NYUMBA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

Uamuzi wa Serikali wa kuhamishia Makao Makuu yake Mjini Dodoma, unalenga kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa kitovu kikuu cha shughuli za kibiashara. Mpango kabambe wa Dar es Salaam mpya unaandaliwa na Serikali na utakuwa tayari mwezi Oktoba mwaka huu. Kwa vyovyote vile Mpango huu unalenga kuifanya Dar es Salaam iweze kubeba shughuli nyingi za kiuchumi na kibiashara. Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa tumejiandaa kuendelea na ujenzi wa nyumba bora za kuuza na majengo makubwa kwa ajili ya kupangisha wafanyabiashara Dar Es Salaam, kwa kuwa jiji hili litaendelea kuwa kitovu cha Biashara.

Aidha, asilimia takribani 70 ya rasilimali za Shirika la Nyumba la Taifa ziko katika Jiji la Dar es Salaam hivyo kulipa Shirika nafasi nzuri ya kushirikiana na Serikali katika kulipanga upya Jiji la Dar es Salaam. Niwatoe hofu wananchi na wateja wetu kuwa wasiogope kununua nyumba zetu kwa hofu ya kukosa biashara, badala yake watarajie kuliona jiji la Dar Es salaam litakalokuwa bora zaidi kwa ajili ya shughuli za kibiashara. Tunatarajia yafuatayo katika jiji letu

Tunatarajia kuwa Dar es Salaam mpya itakuwa na ufanisi mkubwa kwa kuwa sasa usafiri wa kutoka eneo moja kwenda jingine utakuwa mwepesi kuliko hivi sasa.
Hali ya Jiji hili inabadilika kupitia mpango kabambe unaokuja na kuwa kitovu kikuu cha biashara.
Pia hii itakuwa fursa nzuri kwa Uongozi wa Jiji pamoja na wakazi wake, kujipanga vizuri ili kuwa na jiji la kibiashara litakaloshindana na majiji ya kibiashara ya nchi zingine.

Sekta ya Ujenzi itanufaika zaidi katika maamuzi haya na matokeo yake yatainufaisha nchi katika maeneo yafuatayo:-

Kuongeza ajira kubwa kupitia sekta ya nyumba ambayo inagusa wakandarasi, mafundi ujenzi, wafanyakazi kwenye mabenki, wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi na samani, mama lishe na watoa huduma wengine.

Ujenzi mkubwa utasaidia kuchochea uwekezaji na ukuaji wa viwanda vinavyohusiana na mambo ya ujenzi kwa kuwa mahitaji na soko lake vitakuwa na uhakika.

Fursa hii itaongeza wigo wa kodi na mapato mbalimbali ya serikali, kutokana na faida kubwa ya washirika mbalimbali wa sekta ya ujenzi.

Kuongeza upatikanaji wa nyumba bora nchini. Nchi yetu ina upungufu mkubwa wa nyumba unaofikia takribani nyumba milioni tatu na nusu na mahitaji ya nyumba kwa mwaka yanaongezeka kwa nyumba laki mbili. Hivyo, kila kunapokuwa na fursa ya kuchochea ujenzi wa nyumba, kama ilivyo fursa hii ya serikali kuhamishia shughuli zake za kiutawala Mjini Dodoma, daima inakuwa ni nafasi murua na sahihi kuitumia kupunguza pengo hilo la nyumba ambalo linazidi kuongezeka kila mwaka.

Ujenzi huu mkubwa utasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. Kwa sasa sekta ya ujenzi inachangia katika ongezeko la kukua kwa uchumi kwa asilimia 24 kwa mwaka. Fursa ya ujenzi mkubwa inayotokana na uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma kwa vyovyote vile utapaisha mchango wa sekta ya ujenzi na nyumba kwa takriban asilimia 30 kwa mwaka.

Kwa hiyo, tunatarajia kuuona mji wa Dodoma ukibeba shughuli za kiutawala za Serikali wakati Dar Es Salaam ikibaki kuwa Jiji la Kibiashara na hivyo kufanya mgawanyo huo kuwa na manufaa na maslahi mapana kwa Taifa letu.

IMETOLEWA NA:
NEHEMIA KYANDO MCHECHU
MKURUGENZI MKUU

MAGAZETINI LEO: LOWASSA ASEMA JINAMIZI LAKE LINAITESA CCM, MBOWE NAE KUFILISIWA

$
0
0

MKUU WA MKOA WA SIMIYU ATOA UFAFANUZI SAHIHI WA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka,
Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia) akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) wa kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
---
Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa ufafanuzi wa agizo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata mkoani humo, ambalo Serikali ya Mkoa ililitoa tarehe 17 Agosti, 2016 katika kikao ambacho alipokea Vishikwambi (tablets) 637 kutoka EQUIP Tanzania (Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini) kwa ajili ya Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu Kata.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshaji wa agizo hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii., kuwa
Mkuu wa Mkoa ametangaza kuwavua madaraka Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata wote wa Mkoa huo; hali iliyopelekea baadhi ya Walimu wakuu na Waratibu kukosa ari ya kufanya kazi, kwa kigezo cha kusubiri kuvuliwa madaraka.

Mtaka amesema Mkoa ulipokea taarifa za takwimu za wanafunzi hewa, vyumba vya madarasa, idadi ya walimu na idadi ya madawati, baada ya kupokea taarifa hizo ulionekana utofauti mkubwa wa takwimu hizo ndipo Serikali mkoani humo, ikaahidi kupitia mapungufu ya udanganyifu wa takwimu hizo kwa kila shule na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Walimu wakuu na Wakuu wa Shule waliodanganya idadi ya wanafunzi.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepata bahati ya kuwa na Mradi wa EQUIP Tanzania ambao umewawezesha waratibu kupata pikipiki na posho, walimu wakuu wamepewa vishikwambi kwaa jili ya utunzaji wa takwimu, hivyo Serikali inao wajibu wa kuangalia mahitaji ya Mkoa katika elimu ambapo alielekeza yafanyike mabadiliko ya Walimu wakuu Msingi, Sekondari na Waratibu wa mkoa mzima.

“Nililisema mwanzo na leo nalirudia tutafanya mabadiliko makubwa kwa Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari na Waratibu Elimu kata kwa kujiridhisha na maendeleo ya shule zetu, idadi ya walimu waliopo, idadi ya wanafunzi, kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na mazingira ya shule ; lakini tutatoa upendeleo kwa shule 10 bora katika kila wilaya kwa Mitihani ya Kitaifa ya Darasa la IV, VII Kidato cha II na IV , hiki ni kipimo kimojawapo cha walimu wa kuendelea nao. Nasisitiza hakuna mtu atakayeonewa wala kufedheheshwa”, alisema Mtaka.

Mtaka amesema azma ya Serikali ni kuibua vipaji vipya vya viongozi wa Elimu katika ngazi ya Wilaya ambapo alisema ameshaagiza Maafisa Elimu wa Wilaya kuwasilisha taarifa ya walimu waliojiendeleza katika ngazi shahada ya kwanza na shahada ya uzamili ili watakaokuwa na sifa waweze kuteuliwa katika nafasi za Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata ambao watafanyiwa upekuzi (vetting) na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Sanjari na hilo , Mkuu huyo wa Mkoa amesema Walimu wakuu na Wakuu wa shule wa zamani ni tofauti na wale wa sasa, kwa kuwa sasa hivi wamekuwa maafisa masuuli wa shule zao ambapo wanapokea fedha za Elimu bila malipo kupitia akaunti za shule zao, hivyo ni lazima wapatikane watu waadilifu, wenye sifa na uwezo wa kuongoza shule na kusimamia fedha za Serikali.

Akichangia katika kikao hicho Afisa Elimu (Msingi) Wilaya ya Meatu, George Lowasa ameshauri Uchambuzi wa watu watakaoteuliwa ufanyike katika umakini mkubwa ili wapatikane watendaji wazuri na kuhusu utoaji wa takwimu sahihi alishauri kuwe na utaratibu wa kuziboresha kila (robo) baada ya miezi mitatu ili kuwa na takwimu sahihi pale zinapohitajika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema Uteuzi huo utazingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uteuzi ambapo hakuna mtu atakayeonewa au atakayependelewa.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amesema atawachukulia hatua Maafisa wale wanaolalamikiwa na walimu kwa kuwatolea lugha mbaya kila wanapotoa huduma kwa walimu hao katika Halmashauri za Mkoa huo.

Naye Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema ameshauri baada ya mabadiliko ya wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu Kata kufanyika wale ambao wataonekana hawana sifa za kuendelea kushika nafasi hizo waondolewe kwa staha, ambapo aliomba Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa ikishirikishe chama hicho katika masuala yote muhimu ya kuendeleza sekta ya Elimu, kwa kuwa wanamsaidia mwajiri katika usimamizi wa utendaji kwa walimu.

Kikao hicho cha wadau kilichofanyika mjini Bariadi na kimewahusisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Maafisa Elimu kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ngazi ya Mkoa na Wilaya.

MHE. FREEMAN MBOWE AJIBU MKURUGENZI NHC KUHUSU MADAI YA KUDAIWA, ASEMA 'HAWAMDAI'

$
0
0
Nimepata taarifa ya mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Waandishi wa habari kuhusu kilichoitwa "wadaiwa sugu" wa NHC ambapo katika orodha hiyo kampuni ambayo nina hisa ya Mbowe Hotels Co.Ltd imeorodheshwa kama mdaiwa anayedaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja.

Nakiri kuwepo kwa mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi baina ya Kampuni hii na NHC. Aidha kampuni hii imekuwa ikilipa kodi stahiki kwa NHC kwa mujibu wa makubaliano yetu ya kibiashara.

Kumekuwepo na ukakasi wa muda mrefu kuhusiana na mkataba wetu wa umiliki, uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili unaochagizwa na msimamo wangu wa kisiasa.

Haki na Uhuru wetu wa kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara kwa mara katika mazingira yanayoambatana na Vitisho kiasi ambacho Maamuzi kadhaa hayafanyiki kwa hofu ya kisiasa kwamba "Itakuwa kumwongezea nguvu Mpinzani".

Hivyo, ningependa umma wa Watanzania uelewe kuwa sidaiwi na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC).

Kufuatia utata huu wanasheria wa Kampuni wanashughulikia jambo hili kwa taratibu za kibiashara na kisheria.

Naomba kuweka wazi kwa yeyote anayehusika. Sitafungwa fikra, sitafungwa mdomo na sitaacha kuutetea Ukweli, Haki na Demokrasia katika nchi hii kwa misingi ya "kulinda kinachodhaniwa ni maslahi yangu ya kibiashara".

Wafanyabiashara wengi wanafungwa fikra na midomo ndani ya nchi hii kwa kuogopa hila na ghiliba za watawala.

Ni heri kufa masikini nikiwa nimesimamia ukweli, kuliko kuishi tajiri niliyetawaliwa na ubinafsi, woga, hofu na ubatili.

Natambua kuna jitihada za kutumia kila silaha na kila hila dhidi yetu katika Kipindi hiki.

Mwisho, Natoa rai kwa wanachama na wapenzi wa Haki katika Taifa hili, wasiogope. Haki itaweza kucheleweshwa kwa muda tu, lakini kamwe haiwezi kuzuiwa. Binadamu akikufungia mlango Mungu wa Haki atakufungulia dirisha.

Ubatili ni wa mpito lakini Haki ni ya milele.

Imetolewa
Leo Jumatano Agosti 24, 2016 
Na: Freeman Aikaeli Mbowe
Mfanyabiashara.

BEI YA BADAFU LEO

$
0
0

FURAHIA BURUDANI YA LIGI YA BUNDERSLIGA, CHINA NA SERIE A KUPITIA STARTIMES PEKEE

$
0
0
Ni msimu wa Ligi kuu ya Ujerumani ijulikanayo kama Bundesliga inayotarajiwa kuanza tarehe 26 August 2016 kwa miamba ya Bayern Munich kukipiga na SV Werder Bremen.

Burudani ya Michuano ya Ligi ya Bundersliga utaipata kupitia startimes pekee. Burudika na michuano ya ligi kuu ujerumani na italy kupitia startimes pekee.

Pia utaweza kupata burudani ya ligi kuu ya China kupitia Startimes Pekee.

Nunua sasa dekoda ya Startimes kwa bei ya Shilingi 34,000 tu.

WANAFUNZI WA UALIMU WALIOKOSA CHUO CHA UDOM WAPANGIWA VYUO VYA UALIMU VYA SERIKALI

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dar es Salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewapangia vyuo wanafunzi wa programu maalum ya ualimu chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambao hawakupata nafasi ya vyuo katika awamu ya kwanza, walioagizwa kuomba mafunzo kulingana na sifa zao kupitia Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE).

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Leonard Akwilapo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu wanafunzi wanaosoma stashahada maalum ya ualimu wa sayansi chuo kikuu cha Dodoma.

“Mtakumbuka tuliagiza kwamba wanafunzi ambao walikosa sifa za kujiunga na ualimu wa sayansi waliombwa kuomba mafunzo yanayolingana na ufaulu wao kupitia NACTE, Lakini baada ya taarifa hiyo tulipokea maombi mengi kutoka kwa vijana hawa wakiomba kupangiwa vyuo moja kwa moja na Wizara, wizara imetafakari na kuamua nao wapangiwe vyuo vya Serikali,” alifafanua Dkt. Akwilapo.

Aliendelea kusema kuwa, wanafunzi ambao waliachwa awamu ya kwanza na kupangiwa katika awamu ya pili ni wanafunzi 290 ambao walikuwa wakisomea programu ya stashahada ya ualimu wa sekondari na wanafunzi 1,181 ambao walikuwa wakisomea stashahada ya ualimu wa msingi.

Dkt. Akwilapo amesema kuwa Wizara imeamua kuwapangia wanafunzi hao vyuo kutokana na kuonyesha nia ya dhati ya kusomea ualimu ambapo wanafunzi hao wamepangiwa vyuo vya ualimu vya Marangu na Tabora.

Aidha, Dkt. Akwilapo ameeleza kuwa wanafunzi hao watajigharamia masomo yao kulingana na viwango vya ada vilivyowekwa na Serikali. Pia amewataka kutembelea tovuti ya wizara ya hiyo ambayo ni www.moe.go.tz ili kuona vyuo walivyopangiwa.

Mnamo tarehe Mei 28, 2016 Serikali iliwarejesha nyumbani wanafunzi 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum ya Ualimu wa Sayansi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Katika mchujo wa awamu ya kwanza wanafunzi 382 ndio waliokuwa na sifa ya kuendelea na masomo chuo kikuu cha UDOM na wengine 4,586 walipangiwa vyuo vya ualimu vya Serikali.

HANDING OVER CEREMONY FOR AMBULANCE PROJECT AT MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL

$
0
0
Ambulances which were given to Muhimbili Hospital
Ambassador of Japan, Yoshida handed over the keys to Minister for Health, Community Development, Gender, Elders and Children Hon. Ummy Mwalimu.
Group photo with staffs of Emergence Medicine Department (EMD).
Minister for Health, Community Development, Gender, Elders and Children, Hon. Ummy Mwalimu made a speech.

The Government of Japan has been extending support to local communities in various sectors including health, education and water supply under the Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP) scheme since 1991.

On 23rd August, 2016, a Handing-over Ceremony was held at Muhimbili National Hospital for the project of equipping two ambulances funded by the Government of Japan under the GGHSP scheme in the Japanese Fiscal Year 2014.

UMOJA WA WANAWAKE VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA WAPINGA MAANDAMANO YA KUVUNJA AMANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania (UWASATA), Cecilia Augustino akifafanua jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kupinga maandamano ya UKUTA. Kulia ni Katibu wa umoja huo Mwajuma Naty na Makamu Mwenyekiti Zaitun Hokororo.

Hussein Makame - MAELEZO

Umoja wa  Wanawake Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania (UWASATA), umepinga  maandamano yasiyo na ukomo yaliyotanganzwa na Chama cha Demokrasia na  Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwa hayana tija kwa wananchi na Tifa kwa  ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  leo, Mwenyekiti wa umoja huo Cecilia Augustino, alisema maandamano hayo  yanaashiria uvunjifu wa amani ambayo ni urithi wa Taifa la Tanzania.

Alisema wamefikisha tamko lao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji  Francis Mutungi na kumtaka msajili kutoacha chokochocko hizo ziendelee  kwani zitasababisha kutoweka kwa amani nchini.

“Sisi wanawake  viongozi wa vyama vya Siasa Tanzania tunapinga azimio la maandamano  yasiyo na kikomo yanayoandaliwa na chama cha Chadema, hakika maandamano  hayo hayana tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla” alisema Hokororo na  kuongeza:

“Mheshimiwa Msajili, chokochocko hizi zinazofanywa na baadhi ya viongozi wa kisiasa zikiachwa tu bila ya kukemewa tunaamini  tunu yetu ya amani ambayo ni urithi wetu tulioachiwa na waasisi wetu  itatoweka” .Aliongeza kuwa hatma ya maandamano hayo ni kuingia kwenye  machafuko na hatimaye mauaji na mateso kwa wanawake, watoto na walemavu, mambo ambayo hawatakubali yatokee.

Alibainisha kuwa wanawake viongozi wa vyama vya siasa wanaamini kuwa siasa ni kushindana kwa hoja  na si uvunjifu wa sheria kwa njia ya maandamano yasiyo na tija kwa  wananchi na Taifa.

Aliliomba Baraza la Vyama vya Siasa kuhakikisha  linawajibika katika kulinda demokrasia, amani na ustawi wa jamii nzima  ya Watanzania. Katika hatua nyingine, umoja huo unaojumuisha wanawake  viongozi wa vyama 22 vya siasa nchini, umeomba kufanya kongamano la  amani lenye lengo la kuhamasisha amani na utulivu nchini.

Hivyo, Hokororo aliwaomba viongozi wakuu wa nchi kuanzia Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, wadau wa amani na  mashirika binafsi kushirikiana na umoja huo kufanikisha kongamano hilo.

“Hakika tunaumia wanasiasa wanapokuwa chanzo cha migogoro na vurugu kwa  Taifa letu.Hivyo tunamuomba Rais wetu tunajua ni msikivu aweze kuona  namna nzuri ya kutafuta suluhu ya mgogoro huu wa kisiasa” alisema  Mwenyekiti Cecilia Hokororo.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji  Francis Mutungi, tayari ameitisha Baraza la Vyama vya Siasa Agost 31,  mwaka huu ili kutoa fursa kwa pande vyama husika kukaa meza moja na  kujadili tofauti zilizopo na kuzipatia ufumbuzi.

Naye Makamu  Mwenyekiti wa umoja huo Ziada Athumani alisema wanaunga mkono hatua hiyo kwani ndio njia muwafaka ya pande husika ili kufikia muwafaka kwa njia  ya amani.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, wanawake  viongozi wa vyama vya siasa waliwakilishwa na wenzao kutoka vyama vya  Demokrasi Makini, ADA TADEA na Chama cha Umoja wa Demokrasi ya Vyama  Vingi (UMD).

WABUNGE WA VYAMA VINNE WAKUBALI KURUDI BUNGENI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya vyama vinne vyenye uwakilishi bungeni vitarejea bunge lijalo kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili sintofahamu kwa vyama hivyo katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zanzibar, Said Issa Mohamed akizungumza na waandishi habari juu ya maazimio ya viongozi wa dini jana katika mkutano uliofanyika leo Makao Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI.
Waandishi wakimsikiliza Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia leo Makuu ya chama NCCR -MAGEUZI jijini Dar es Salaam.

(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.)
---
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

VYAMA vinne vyenye uwakilishi bungeni vimesema kuwa watarejea bunge lijalo kutokana na ushauri wa viongozi wa dini waliokaa kujadili sintofahamu kwa vyama hivyo.

Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI, James Mbatia amesema viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa katika majadiliano hayo kwa kuweka masilahi mapana ya taifa.

Amesema kuwa kurudi katika bunge lijalo mpaka wabunge wote wa vyama wakutane na kuweza kufikia mwafaka huo kutokana na ushauri wa viongozi hao.

Mbatia amesema kuwa kuna vitu vingine huwezi kuangalia katika katiba huvyo unahitaji busara zaidi kwa kuangalia masilahi mpana ya taifa.

Amesema kuwa NaibuSpika, Dk.Tulia Ackson anatakiwa kuweka busara katika kuongoza bunge na kuacha taratibu kanuni za bunge pamoja na katiba.

Aidha amesema kuwa viongozi wa dini wameshauri vyama kurejea bungeni na kutaka masuala yao wanayoyataka kikatiba yatatuliwe.

MIILI YA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI MBANDE-TEMEKE YAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yaliyobeba miili ya askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,bada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ibada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni , akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa ndugu wa askari waliouawa baada ya kuvamiwa na majambazi katika eneo la Mbande, Temeke ,ibada hiyo ya kuaga miili ilifanyika katika Viwanja vya Kambi Kuu ya Polisi iliyopo barabara ya Kilwa,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi .Ibada hiyo ya kuaga ilifanyika katika Viwanja vya Polisi vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu, akizungumza wakati wa maombolezo na kuaga miili ya askari waliouawa katika eneo la Mbande, Temeke baada ya kuvamiwa na majambazi.Ibada hiyo ya kuaga ilifanyika katika Viwanja vya polisi vilivyopo barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

MORO KIDS WASHINDA AIRTEL RISING STARS MOROGORO

$
0
0
Mshambuliaji wa timu ya Angrikana Saidi Mohamed akidhibitiwa kikamilifu na beki wa timu ya Moro Kids Ibrahim Yohana katika pambano la fainali ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo moro kids ilinyakua kombe hilo baada ya kushinda 1-0.
 Mchezaji wa timu ya Moro Kids Ibrahimu Ally mwenye jezi nyeupe wakiwania mpira na mchezaji wa timu ya Angrikana Baraka Omary katika mchezo wa fainali ya Airtel Rising Starkwenye uwanja wa Jamhuri Morogoroo. Moro Kids ilinyakua kombe hilo kwa ushindi wa 1-0.
 Kapteni wa timu ya Moro Kids Abdul Rashid akipokea kombe la mshindi wa kwanza wa mashindano ya Airtel Rising Stars kutoka kwa mgeni rasmi ambae ni Meya wa Manispaa ya Morogoro pascal kihanga, Moro Kids imenyakua kombe hilo baada ya kuifunga timu ya Angrikana 1-0.
Wachezaji wa timu ya moro kids wakishangilia baada ya kunyakua kombe la mashindano ya Airtel Rising Stars kwa kuifunga timu ya Angrikana 1-0 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro jana.
---
Timu ya vijana ya Moro Kids imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya kufanya kazi ya ziada na kuishinda timu ngumu ya Angrikana 1-0 katika mchezo wenye upinzani mkali uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana.

Goli hilo la ushindi liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Nyamawi Juma katika dakika ya 22 baada ya kuwazidi mbio walinzi wa Angrikana na kuachia shuti kali lililotinga wavuni. Goli liliibua nderemo na vifijo kutoka kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushangilia timu yao.

Angrikana walijibu mapigo kwa kufanya mashambulizi mfululizo ambayo hata hivyo hayakuweza kuzaa matunda. Kipingi cha pili walikianza kwa matumaini ya kupata goli la kusawazisha lakini hadi dakika ya mwisho matokeo yalibaki kuwa 1-0.

Akikabidhi kikombe kwa washindi, Meya wa manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza Morogoro Kids kwa mafanikio makubwa na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa kujituma huku wakifuata maelekezo ya walimu wao. “Kwa kufanya hivyo kutawaweka katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto zenu za kufanikiwa katika maisha kupitia soka”, alisema.

Aliwataka viongozi wa soka mkoani Morogoro pamoja na makocha kuhakikisha wanachagua vijana wenye vipaji ili kuuwakilisha vyema mkoa wa Morogoro kwenye fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi to 11.

Wakati wa mechi hizo za mkoa makocha walipata fursa ya kuwatathimini uwezo wa kila mchezaji na kuchagua vijana wenye vipaji kuunda kombaini ya mkoa. Mikoa mingine ambayo tayari imeshaunda vikosi vyake ni kwa fainali hizo ni Ilala, Kinondoni, Temeke and Mwanza.

Fainali hizo za kila mwaka itazikutanisha timu za wavulana na wasichana kutoka mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Washiriki wengine watatoka Mwanza, Morogoro, Mbeya, Lindi, Arusha na Zanzibar.

CUF YA TANGANYIKA NA CUF YA ZANZIBAR!

$
0
0
 Na Hamidu Bobali.

Sikusudii kujibu mapigo lakini ni vyema kujikumbusha. Nimestaajabu sana kilichoandikwa na gazeti la Jambo Leo kuhusu hatma ya chama chetu, yakinukuliwa maelezo ya Naibu Katibu Mkuu Bara wa chama, Bi. Magdalena Sakaya.

Hoja za kukizushia chama chetu kuwa ni:
1. Chama cha Waislamu,
2. Chama cha Waarabu,
3. Chama cha Zanzibar,
4. Chama cha wapemba,
5. Chama cha Maalim Seif,

Zote zilikuwa ni propaganda chafu zilizoenezwa na CCM wakitumia kitengo cha propaganda cha usalama na miaka yote zimekuwa zikigonga mwamba na chama kinazidi kuchanja mbuga.

Leo haya ni mapyaaa! Hoja hizi kushabikiwa na kiongozi wa ngazi ya juu wa chama, Naibu Katibu Mkuu, ambaye chama hiki kimemuamini na kumpa ubunge wa viti maalum akitokea serikalini mwaka 2005 - 2010, akapewa ubunge wa viti maalum mara ya pili na chama hiki mwaka 2010 - 2015, akagombea ubunge jimbo la Kaliua, Tabora, akaungwa mkono na ushirikiano wa UKAWA, akawa mbunge wa kuchaguliwa 2015 - 2020.

Uzanzibar na ubara si ajenda ya chama chetu hata Siku moja, agenda zetu siku zote ni kuwaunganisha watanzania. Leo hii kusikia Maneno haya kutoka kwa kiongozi wangu wa juu nimefadhaika sana. Sijui ni nini kimempeleka kwenye mitego hii.

Yawezekana kiongozi wangu hajui " core objective of our party", "The civic united Front " Kutugawa wazanzibar na wabara sisi watu wa maeneo ya pwani huku maana yake ni kutuachanisha undugu, nje ya siasa sisi ni ndugu

Wito wangu kwa wana CUF wote, TUSIKUBALI KUGAWANYIKA KIRAHISI RAHISI NAMNA HII

Hamidu Bobali (MB),
Mwenyekiti JUMUIYA YA VIJANA YA CUF (JUVICUF),
Mbunge wa Jimbo la Mchinga (CUF),
25.08.2016.

TIGO YAFUNGUA DUKA LA KISASA WILAYANI MASASI

$
0
0
Afisa tawala wa wilaya ya Masasi Lincoln Ben Tamba akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa duka la tigo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi kulia kwake ni meneja wa kanda ya kusini wa tigo Nderingo Materu na na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles na anayefuatia ni Meneja huduma kwa wateja kanda ya Pwani, Isaack Shoo katika sherehe za ufunguzi zilizofanyika mapema wiki iliyopita wilayani Masasi.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles akiongea na wananchi wa Masasi mara baada ya ufunguzi wa duka la tigo Masasi katika hafla ya ufunguzi iliyofanyika katika wilaya ya Masasi mapema iliyopita.
Afisa tawala wa wilaya ya Masasi Lincoln Ben Tamba akihutubia wananchi wa Masasi mara baada ya hafla ya ufunguzi wa duka la tigo wilayani hapo ,mapema wiki iliyopita.
Baadhi ya wafanyakazi wa duka la Tigo Masasi wakifuatilia kwa makini hafla za ufunguzi wa duka la Tigo wilaya ya Masasi mapema wiki iliyopita.

MAGAZETINI LEO; UKAWA, ACT WATAKA MAGUFULI AFUTE SIASA... LIPUMBA NA WENAKE KUTIMULIWA CUF

$
0
0


JACQUELINE MENGI AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KWA KUKARABATI NA KUNUNUA VITABU VYA MAKTABA

$
0
0
Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kushoto) akiwa ameongoza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kushoto), Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi na uongozi wa shule hiyo kwa pamoja wakiimba na wanafunzi wa shule ya Msingi Kinondoni.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa maktaba ya vitabu aliyoipa jina la Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika hatua za kumuenzi marehemu baba yake ambaye aliyemjengea misingi mizuri ya usomaji wa vitabu wakati wa makuzi yake
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akionyesha wageni waalikwa picha mbalimbali za awali kabla ya kukarabati maktaba hiyo.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi kwa pamoja wakizundua nembo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi wakipeana mikono na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.
Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akimwonyesha baadhi ya vitabu Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda vinavyopatikana katika maktaba hiyo.
Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule hiyo wakati akiondoka shuleni hapo.
---
Na Mwandishi wetu

Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha sasa na baadae, Jacqueline Mengi kupitia Taasisi yake ya Dk. Ntuyabaliwe ameamua kuunganisha nguvu kwa serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Magufuli kwa kusaidia kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa kufanya marekebisho ya maktaba katika shule ya msingi Kinondoni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ambao uliambatana na uzinduzi wa Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe, Jacqueline amesaidia kufanya ukukarabati wa maktaba katika shule hiyo na kuweka vitabu ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka baba yake Dk. Ntuyabaliwe kutokana na kupenda kwake kusoma vitabu.

Alisema baba yake alikuwa akiamini zaidi katika vitabu hivyo alipenda hata watoto wake wasome vitabu na anachokifanya yeye kwa sasa ni kuendeleza juhudi ambazo alikuwa akiifanya baba yake ya kuona watu wakisoma vitabu na matarajio yake ni kuona vitabu hivyo vikiwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuwaongezea uwezo wa kufaulu katika masomo yao ya darasani.

"Ndoto yangu ya muda mrefu leo imetimia, kila mtu ambaye alikuwa akimfahamu baba yangu Dk. Ntuyabaliwe alikuwa akifahamu kuwa alikuwa anapenda vitabu na hata sisi alituzoesha kusoma vitabu na hata kuanzishwa kwa taasisi hii ni sehemu ya kumkumbuka yeye,

"Naamini kuwa usomaji wa vitabu unaweza kumsaidia mtu kufika mbali hata kama sio katika elimu unaweza kumsaidia kwa jambo lingine hata katika maisha ... ndoto yangu ni kuona watanzania wote wanapenda kusoma kama baba yangu alivyokuwa anapenda kusoma vitabu," alisema Jacqueline.

Nae mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda alisema sio jambo rahisi serikali kuweza kumaliza changamoto zote zilizopo na kupitia watu wenye moyo kama wa Jacqueline ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kunaweza saidia upatikanaji wa elimu bora.

Alisema kupitia maktaba hiyo anaamini ipo siku kutatokea mtu ambaye atakuwa na msaada kwa Tanzania ambaye wakati akisoma alikuwa akitumia maktaba ambayo imefanyiwa ukarabati na Jacqueline Mengi.

"Nimeona hali ambayo ilikuwa awali katika eneo hili na niseme tu Jacqueline atakuwa na yeye aliguswa na hali hiyo na nitumie fursa hii kumshukuru sana kwa msaada ambao ameutoa, shule inatakiwa kutoa elimu bora lakini ili kufikia malengo hayo kunahitajika kuwe na nyenzo za kutosha ambazo zitasaidia malengo ya kielimu kufikiwa," alisema Mapunda.

Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga alimshukuru Jacqueline Mengi kwa msadaa wa kukarabati maktaba ya vitabu ili wanafunzi kujisomea, maktaba ambayo awali hawakuwahi kuwa nayo.

"Tunakushukuru sana kwa maktaba hii sasa wanafunzi wataweza kujisomea, tunafahamu juhudi za Dk. Mengi katika kusaidia elimu kwa kutoa madawati sasa na wewe umemuunga mkono tunawashukuru kwa hilo," alisema Ntenga.
Viewing all 19839 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>