Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19859 articles
Browse latest View live

GERALD HANDO AFUNGA NDOA NA MIRIAM KITENGE

$
0
0
Maharusi Gerald Hando na mkewe Miriam Kitenge wakiingia ukumbini.
Mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Joto la Asubuhi katika Kituo cha Radio cha Efm, Gerald Hando amefunga ndoa juzi Jumamosi, Agosti 20, 2026 na mpenzi wake, Miriam Kitenge.

Sherehe ya harusi hiyo iliyokuwa ya aina yake ilifanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip uliyopo maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya mastaa walihudhuria huku mwanamitindo maarufu, Sheria Ngowi akiwa ndiye mbunifu wa mavazi ya maharusi hao.

Hando ameuaga ukapera na kuanza kufurahia maisha mapya ya ndoa na mkewe Miriam kama walivyofanya mastaa kadhaa hivi karibuni wakiwemo mchekeshaji maarufu, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ wa Orijino Komedi na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Bwana Harusi Gerald Hando akiwa na marafiki zake Edward Urio na Sheria Ngowi.

WASSIRA AOMBA SERIKALI IZUNGUMZE NA CHADEMA YAISHE

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Chakula na Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wassira ameomba wasaidizi wa Rais John Magufuli kumshauri kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani ili kuepusha madhara yanayoweza kutokana na maandamano yanayopangwa kufanyika Septemba 1.

Wassira ameeleza kuwa washauri hao wanapaswa kufanya hivyo kwani bado nafasi hiyo ipo kuliko kuacha Rais aingie vitani na wananchi wake kwani madhara yatawapata Watanzania wote.

“Wazungumze ili wasimuingize Rais kupigana na watu wake kwa maana wote tutapoteza. Kwa nini uweke askari polisi wote hao, msimweke Rais kwenye vita na watu wake,” Wassira anakaririwa na Jambo Leo.

“Kinachohitajika ni wasaidizi wa Rais kumshauri ili kuhakikisha kuwa tofuati zilizopo baina yake na vyama vya upinzani haziendelei ili kuepusha madhara yanayoweza kuzuilika, itafutwe suluhu,” aliongeza.

Akizungumzia uamuzi wa Serikali kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano na maandamano, alisema kuwa tatizo linaweza kuwa ni aliyekuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.

Alisema kuwa hii inatokana na joto la uchaguzi lililokuwepo pamoja na nia ya Lowassa kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wapiga kura, kungeweza kuzua tafrani kubwa kwani alipata kura nyingi na alikuwa akidai ameshinda kwa asilimia 62.

“Ukiwaruhusu kufanya mikutano na ukwaambia kuwa atakayekuja kutoa shukurani ni Lowassa, ambaye amekuwa akipinga kushindwa ni sawa na kurejesha hali ya uchaguzi kipindi hiki,” alisema.

Alitaaka Serikali kutoa elimu ya wazi kwa umma kuhusu sababu zinazopelekea kukataza kufanyika kwa mikutano ili kuweka mambo sawa.

“Kama mimi hapa nimetaja sababu kwamba inawezakana kuwa ni Lowassa. Sasa na wao Serikali waseme tu tunapiga marufuku mikutano na maandamano… wataje [sababu]na kuzifafanua,” alieleza.

HAPPY BIRTHDAY BLOGGER MC BARAKA

$
0
0
Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwangu, Aug 23. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuishuhudia siku hii. Ni neema ambayo sistahili,Napaswa kutambua kwamba kila siku katika maisha yangu ni dhamana, niitumie kwa mambo mema,Nizingatie wajibu wa kuvitumia kikamilifu vipaji alivyonipa Mungu kwa manufaa ya wanadamu.

Siwezi kujivunia chochote nilichoweza kufanya, bali ni kumshukuru Mungu na kuendelea kumtegemea na kila ninaposherehekea kumbumbuku ya siku ya kuzaliwa kwangu, fikra zinanituma kufananisha mchango wangu Kimkoa na Kitaifa sawa na ule wa watu maarufu,Ukweli ni kwamba ninajitahidi lakini mchango wangu bado ni hafifu sana. Mengi nimefanya kupitia Bukobawadau Blog Media ninachoweza kusema ni kwamba changamoto ni kubwa sana!
I will always praise God.

MAGAZETI LEO: OPERESHENI UKUTA YAHAMIA DODOMA, SERIKALI, UKUTA CHADEMA WABADILI UPEPO WA SIASA

$
0
0

MISS UNIVERSITY 2016 AT TCC CHANG'OMBE SEPTEMBER 3, 2016

$
0
0

HATI ZA VIWANJA VYA BAYPORT ZAENDELEA KUTOLEWA KWA WAHUSIKA

$
0
0
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akimkabidhi hati mteja wao Mary Simon, baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Viwanja hivyo vinapatikana kwa njia ya fedha taslimu na mikopo maalumu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi na wajasiriamali. Kulia ni Meneja Mikopo wa taasisi hiyo, Nasibu Kamanda. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, katikati akizungumza jambo baada ya kumkabidhi hati mteja wao Mary Simon kushoto baada ya kukamilisha taratibu za kupata kiwanja cha Vikuruti, vilivyopo Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Mikopo wa Bayport Financial Services, Nasibu Kamanda.
Afisa Sheria wa Bayport Financial Services katikati akisisitiza jambo.
Mteja wa Bayport Financial Services Sixtus Kilenga kushoto akisaini kama sehemu ya kukabidhiwa hati ya kiwanja. Hati hizo kwa wateja walionunua viwanja vinavyopatikana kwa njia ya mkopo na fedha taslimu zinaendelea kutolewa kwa waliokamilisha taratibu zao.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana imeendeleza utaratibu wake wa kugawa hati kwa wateja wao walionunua viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa njia ya mikopo na fedha taslimu.

Mradi huo wa Vikuruti ulizinduliwa mwaka jana, ambapo baada ya kufanikiwa kwake, taasisi hiyo ikaanzisha miradi mingine mitano ambayo ni Kigamboni, Bagamoyo, Chalinze, Kibaha na Kilwa, huku ikiweka utaratibu rahisi na nafuu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Afisa Sheria wa Bayport Financial Services, Mrisho Mohamed, alisema kwamba kugawa hati kwa wateja wao ni mwendelezo wa huduma nzuri zinazotolewa na taasisi yao kwa ajili ya kuwakomboa wananchi katika suala zima la ardhi.

Alisema kwamba makubaliano yao ni kuhakikisha taasisi inasimamia sualaa la hati ili wateja wao wasisumbuke kutokana na mchakato mzima wa utendaji kazi wao unaotoa urahisi juu ya upatikanaji wa viwanja vyao vyenye hati.

“Tunaendelea na kutoa hati kwa wetu walionunua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, ambapo Watanzania wengi walichangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo, ambavyo ukiacha vya Vikuruti, wateja wetu pia wanaweza kukopa fursa hii ya ardhi kwa miradi yetu ya Kimara Ng’ombe (Bagamoyo), Msakasa (Kilwa), Tundi Songani (Kigamboni), Boko Timiza (Kibaha), Kibiki na Mpera (Chalinze) na Kitopeni (Bagamoyo).

Naye mteja wa Bayport aliyopewa hati yake, anayejulikana kwa jina la Mery Simon Anthony aliipongeza Bayport kwa kutoa huduma nzuri kiasi cha kumfanya amiliki kiwanja chenye hati, huku kikiwa hakina mlolongo wowote.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa sababu nimepata hati yangu kwa haraka na sijapata usumbufu wowote, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi katika miradi hii ya viwanja vya Bayport kwa sababu ni rasilimali nzuri,” Alisema.

Naye Sixtus Francis Kilenga alisema kwamba amefurahishwa na utaratibu mzima wa kupata kiwanja chenye hati, huduma zinazotolewa na Bayport, ambapo mteja hana jukumu lolote la kufuatilia hati katika maeneo yanayohusika.

“Utaratibu wa kununua kiwanja kasha ukapewa hati bila kufuatilia wizarani ni mpya, hivyo binafsi nimeufurahia na unaweza kuifanya Bayport kuwa moja ya ofisi zenye kujali muda na gharama za kiutendaji wa wateja wao,” alisema.

Bayport ni taasisi inayotoa huduma za mikopo ya bidhaa ikiwamo viwanja pamoja na fedha taslimu isiyokuwa na amana wala dhamana, huku taasisi hiyo ikiwa na matawi zaidi ya 82 nchi nzima kwa ajili ya kuwapatia Watanzania huduma bora.

TIGO YAANZISHA MKAKATI WA HUDUMA KWA JAMII NCHI NZIMA KATIKA MSIMU WA FIESTA 2016

$
0
0
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bwiru Mkoani Mwanza wakiwa wamekalia madawati 60 waliyopewa na kampuni ya Tigo, wakati wa hafla iliyofanyika jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(wa tatu kulia) akimpa mkono Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya, kwenye hafla ya kukabidhi madawati 60 kwa Shule ya Msingi Bwiru jana.
•Shule 9 za msingi Mwanza zapokea madawati 385

Kampuni ya Simu ya Tigo Tanzania leo imeanzisha rasmi mkakati wake wa nchi nzima wa kutoa huduma kwa jamii kwa kuchangia madawati 385 yenye thamani ya shilingi milioni 64 kwa shule tisa za msingi mkoani Mwanza ambayo yatazinufaisha shule za msingi katika wilaya za Ukerewe, Nyamagana, Ilemela na Sengerema wakati wa msimu wa tamasha la Fiesta 2016 mkoani Mwanza

Kukabidhiwa kwa madawati hayo mkoani Mwanza ni matokeo ya juhudi zinazoendelea za Tigo za kuwekezaq katika elimu na hususani katika kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi za umma nchi ambapo mikoa 18 itanufaika katika msimu wa Fiesta 2016. Ikumbukwe kwamba kwa mwaka huu kampuni imeshachangia madawati 5,700 kote nchini na hivyo kuwa imewakalisha wanafunzi 17,000 ambao awali walikuwa wakikaa sakafuni.

Mkakati wa kutoa msaada wa madawati katika msimo huu wa Fiesta unajulikana, “‘Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora; Fiesta 2016 kwa Kishindo cha Tigo Elimu bora, Imooooo!’

Akizungumza katika sherehe za kukabidhi madawati hayo zilizofanyika katika Shule ya Msingi Bwiru Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ally Maswanya, alisema uhaba wa madawati katika shule za msingi unajulikana kama moja ya sababu zinazoathiri kujifunza pamoja na ufanisi wa wanafunzi katika shule zetu nyingi za msingi.

“Tumejikita katika kuhakikisha kuwa mazingira ya kujifunzia katika shule zetu za msingi yanaboreshwa na tunayofuraha kwamba Tigo inabadilisha kizazi cha baadaye am,bacho ni wanafunzi katika shule za msingi kwa kuhakikisha hawakai chini tena. Tunaamini kwamba msaada huu utaenda mbali katika kuwasadia wanafunzi kuzifikia ndooto zao za kuwa viongozi wa baadaye kutokana na kuondoka kwa bughudha na hivyo kujikita katika masomo,” alisema Maswanya.

Makabidhiano ya madawati hayo yalishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ambaye alisema kuwa madawati 385 yataboresha kwa kiwango kikubwa mazingira ya kujifunza kwa watoto katika mkoa huo na kuwataka watu wengine wenye mapenzi mema kujitokeza na kujiunga na juhudi hizo za kuondoa uhaba wa madawati uliobakia katika mkoa huo.

Mongela alizitaja shule zitakazopokea madawati hayo na idadi katika mabano kuwa ni Nakoza (29), Uhuru (40), Busangu (41), Bukongo (30), Nansio (30), Namagubho (30), Mkuyuni (65) Chambanda (60) na Bwiru (60) .

“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa kutuunga mkono katika juhudi zetu kwa kupunguza kiasi cha uhaba wa madawati katika shule za msingi mkoani Mwanza. Tunaamini madawati haya 385 yatatufikisha mbali katika kuwawezesha mamia ya watoto kuwa katika mazingira mazuri ya kujifunzia yanayotakiwa kwa ajili ya mafanikio katika elimu yao,” alisema Mongela.

NATAKA KURUDI UONGOZINI KUIONDOA CCM 2020 - PROF. LIPUMBA

$
0
0
#‎1. Aliyekuwa‬ Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ktk mkutano wa CUF na kuletea kusitishwa kwa mkutano huo.

‪#‎2. Akijibu‬ maswali kadhaa ya mwandishi wa Habari wa Azam Tv, Prof. Lipumba anasema ni kweli yeye kama mwenyekiti aliyejiuzuu hakualikwa wala hana vigezo vya kuingia ktk mkutano huo, lakini akiwa nyumbani alipata ujumbe wa simu ya mkononi kuwa anahitajika ukumbini na baadhi ya wanachama wanataka arudi katika nafasi yake.

‪#‎3. Baada‬ ya kupata ujumbe huo, Lipumba aliamua kuondoka nyumbani kwake na kwenda ukumbini,ambapo kimsingi kikatiba na kikanuni hakuwa na ruhusa ya kuingia, lakini kwa nafasi yake ktk chama alipaswa kuruhusiwa kuingia japo walinzi walimgomea wakisema haitajiki kwa muda huo, yeye alilazimika kuhakikisha anaingia ili kuweza kukidhi kiu ya wanachama waliomhitaji na wanaoona anafaa kurudia nafasi yake.

‪#‎4. Prof‬ Lipumba anasema hakuna mwana-CUF anayeijua CUF kama yeye na wala hakuna mwana-CUF toka Tanzania bara na hata visiwani ukitoa Maalim Seif aliyeweza kuwatetea Wazanzibar kama yeye, akitolea mfano wa kudai haki ya mwaka 2001 na harakati nyingine za kuwasemea na kuwatetea Wazanzibar. Lipumba anasema yeye ndiye kiongozi aliyezunguka Tanzania bara na visiwani na kufahamiana na viongozi wa ngazi zote na ndio hao wanaomtaka arudi katika nafasi yake.

‪#‎5. Akijibu‬ swali la kuwa "anatumiwa na Watu kuivuruga CUF", Prof Lipumba anasema hawezi kuihujumu CUF kwa sababu yeye ndio sehemu ya waasisi wa chama hicho na amekipigania kwa miaka mingi ndani ya jasho na damu, hivyo kuwataka viongozi wa CUF Taifa kutumia hekima na kuacha maamuzi ya wanachama wanaotaka yeye arudi na kuchukua nafasi yake na kuendeleza harakati za kuindoa CCM madarakani kuelekea 2020.

‪#‎6. Prof‬ anasema bado ana imani kuwa wanachama wanataka yeye arudi na ndio maana hata baada ya kuwa yeye si sehemu ya mkutano kikatiba na kikanuni, bado kuna wanachama walimpigia simu afike ukumbini na kujuwa hatima yake ya kurudia nafasi yake.

Source: Azam TV.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WA NCHI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni akisaini kitabu kabla ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini Kim Yong Su mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini Kim Yong Su mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

MKUU MPYA WA WILAYA YA ARUSHA MHE. GABRIEL DAQARRO AAPISHWA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akiapa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akisaini hati ya kiapo cha Mkuu mpya wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Fabian Daqarro (kulia) wanaoshuhudia ni Katibu Tawala mkoa, Richard Kwitega na Afisa wa Itifaki, Mukhsin Khasim.
Viongozi mbalimbali katika Jiji la Arusha wakifatilia tukio hilo.
Mwenyekiti wa CCM na Mbunge mstaafu wa Longido, Lekule Laizer(kushoto) akimsikiliza Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM wilaya ya Arusha DC, Mathias Manga.
Mkuu mpya wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akitoa shukrani zake baada ya kuapishwa.
Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na usalama kati ya Tanzania na China, Kulia ni Msaidizi wa Balozi, Wang Fang. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiangalia vipengele mbalimbali vinavyohusu ushirikiano juu ya masuala ya ulinzi na usalama, wakati wa mazungumzo yaliyomhusisha Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing(kulia). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong. Mazungumzo hayo yalifanyika leo,jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong(kulia), Msaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania, AI Zhuan(katikati) na Katibu wa Balozi, Dong Zhenyu(kushoto), wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(hayupo pichani), wakati wa mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na usalama kati ya Tanzania na China. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na usalama kati ya Tanzania na China. Mazungumzo hayo yalifanyika leo, jijini Dar es Salaam.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA MILLICOM GROUP IKULU ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zanztel (katikati) Bw. Mauricio Ramos, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom Group" (wa pili kulia) na (kushoto) Ndugu Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zantel ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo na Rais leo 23/08/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, akifanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group Mauricio Ramos alipofika Ikulu Mjini Unguja, Zanzibar kwa mazungumzo Jumanne 23 Agosti 2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zantel (katikati) Bw. Mauricio Ramos, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom Group" (wa pili kulia) na (kushoto) Ndugu Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo na Rais leo 23/08/2016.
Mkurungenzi Mtendaji wa Millicom Group Mauricio Ramos akiwa kwenye ya pamoja na wanafanya kazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za kampuni hiyo Zanzibar.
Mkurungenzi Mtendaji wa Millicom Group Mauricio Ramos akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na wanafanya kazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za kampuni hiyo Zanzibar.

WAZIRI WA AFYA AZINDUA BODI MPYA YA UDHAMINI HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakati akizindua bodi mpya ya udhamini wa hospitali hiyo Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Dk.Charles Majinge na Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Michael John.

Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Dk.Charles Majinge (kushoto), akizungumza katika uzinduzi wa bodi atakayoiongoza.

Wafanyakazi wa Hospitali hiyo wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Usikivu wakati waziri akizungumza nao.

Maofisa uuguzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru (kushoto), akiwa kwenye uzinduzi huo. Kulia ni Mjumbe wa bodi hiyo, Esther Manyesha na Dk. Ellen Mkondya Senkoro.

Uzinduzi ukiendelea.

Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia uzinduzi huo.

UKOSEFU WA MAARIFA YA VIPINDI VYA MABADILIKO YA MWILI KUNAATHIRI MAKUZI BORA KWA VIJANA

$
0
0
Mwezeshaji Herman Mathias kutoka UNESCO akitoa somo kwa washiriki wa Shule za Sekondari Sengerema.

Washiriki wakichangia mawazo na uzoefu wao kuhusu changamoto zinazowakabili.


Kijarida kilichoandaliwa kama matokeo ya nadharia kwa vitendo.

Wanafunzi washiriki wakifanya zoezi la viungo wakishirikiana na Mwezeshaji Herman Mathias.

Wanafunzi wa Shule za Msingi Pangani wakiwa katika ziara ya kutembelea kituo Redio Jamii Pangani FM wakati wa mazoezi.

Picha ya pamoja wanafunzi wa Shule za Msingi Boza na Kikokwe Pangani, walezi, wajumbe wa kamati za shule na viongozi kutoka Wizara ya Elimu.

Ukosefu wa maarifa na taarifa sahihi wa vipindi vya mabadiliko maisha ya vijana husababisha uwezekano wa kupotoka kimaadili kwa kufanya mafunzo kwa vitendo na kuathiri makuzi bora.

Akitoa mafunzo kwa wanafunzi wanaounda vikundi vya kutayarisha vipindi vya redio kwa ajili kupaza sauti zao kuieleza Jamii kuhusu hali zao mashuleni, mamlaka mbalimbali, majumbani na katika Jamii wilayani Sengerema na Pangani, Afisa Mtaalam masuala ya Afya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Herman Mathias alisema kwamba changamoto nyingi zinazoathiri makuzi ya kimaadili kwa vijana ni kutopewa maarifa na taarifa sahihi jinsi ya kutumia miili yao bila kuathiri ndoto zao.

“Vijana wengi wameshindwa kufikia ndoto zao kutokana na kutomaliza shule kwa sababu hawajui namna ya kufanya maamuzi sahihi kutumia fursa walizo nazo”, alisema Herman Mathias.

Ili kufikia malengo ya ndoto zao Afisa huyo wa UNESCO alisema vijana wanahitaji kusoma kwa bidii na kuhitimisha mzunguko wa elimu, kuwa na tabia njema kwa kuepuka vishawishi vya mtaani hususan kuvuta bangi na matumizi ya vileo, utoro na matumizi ya lugha mbaya.

Alizitaja tabia njema nyingine pamoja na kuepuka tabia za kimapenzi yanayoweza kusababisha magonjwa ya zinaa, maambikizi ya virusi vya UKIMWI na ujauzito na upatikanaji wa malezi yanayojali nafasi na muda wa mtoto na kuweka mazingira rafiki ya kuishi na kusoma, afya bora kwa kutougua hovyo magonjwa mbalimbali na kuwa msafi wakati wote hali inayompa fursa kijana kushiri katika shughuli zote za kijamii na kielimu na kuwataka wazazi na walezi kufuatilia mwenendo wa kijana shuleni na katika Jamii.

Zaidi ya asilimia 52 ya vijana hawana elimu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na afya ya uzazi.

Alisema kwamba mambo hayo yote yanawezekana kuepukika kwa sababu yako ndani ya uwezo wa vijana wenyewe na wazazi pia.

Wakichangia uzeofu wao unaowakwamisha kufikia ndoto zao, vijana hao walizitaja changamoto zinaowakumba katika kipindi cha makuzi ambazo ni mimba za utotoni zinazosababishwa na ukosefu wa elimu ya uzazi kuanzia shuleni na au katika familia, umaskini unaosababisha wasichana kutoka nje na kujiingiza katika matendo ya kimapenzi kwa kutafuta mahitaji mbalimbali muhimu na matamanio kukidhi matakwa yao kimaisha na makundi rika ambayo huchangia katika kushawishiana na kufundishana mabaya.

“Zaidi wa watoto 6,000 wanaacha masomo kutokana na ujauzito na mara nyingi waalimu wamekuwa hawaripoti taarifa za mimba badala yake huripoti utoro peke yake, lakini wanafunzi wanaelewa hali halisi na kuweza kueleza ukweli”, alisema Herman Mathias.

Changamoto nyingine ni tamaa inayopita kiasi kwa kuona baadhi ya marafiki zao wanakuwa na vitu vizuri ambavyo wengine huvikosa hususan simu za mkononi, viatu na nguo nzuri, kubakwa na matumizi mabaya ya mawasiliano ya utandawazi na vifaa vya kielektroniki zinazopatikana kwa njia zisizo halali.

Matumizi mabaya ya utandawazi hushawishi vijana kuiga utamaduni wa kigeni hususan kuvaa nguo zisizo na maadili na vitendo vingine vinavyoenda kinyume na maadili ya Mtanzania na malezi yanayowapa vijana uhuru mkubwa wa kufanya mambo yao bila kurekebishwa au kuingiliwa na wazazi na walezi ni changamoto inayochangia kupotosha maadili katika makuzi ya kijana.

Ndoa za utotoni zinazosababishwa na mila na desturi zinazoendelezwa katika Jamii kwa kiasi kikubwa zinachangia kufifisha vijana kufikia malengo ya ndoto zao na mimba za utotoni husababisha ulemavu wa mwili na akili na pia vifo kwa mama na mtoto.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 179 zilizokubaliana kutekeleza Mkakati wa Utekelezaji Mkutano wa Kimataifa wa Tatu na Maendeleo wa Cairo (UNFPA) mwaka 1994 wa harakati za maendelezo ya haki za uzazi, uzazi wa mpango, uzuiaji wa maambukizi ya VVU/UKIMWI, uwezeshwaji wa wanawake na maendeleo mengine yanayohusiana na hayo kulinda utimilifu wa kibailojia, kisaikolojia wa namna ambavyo mfumo wa uzazi unafanya kazi. Haki hizo zikipotea mtoto ana haki ya kupaza sauti kudai.

UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Redio Jamii ya wilaya ya Sengerema na Pangani, iliendesha warsha za kuwajengea uwezo vijana wa shule za Sekondari wilayani Sengerema na Shule za Msingi wilayani Pangani kupitia vikundi rika maarifa na ujuzi wa elimu ya afya ya uzazi na makuzi yao kupitia redio Jamii ili waelimike kabla ya kuandaa vipindi.

Afya ya uzazi inahusisha mfumo wa uzazi wa mtu na via vya uzazi kwa watu ambao unajumuisha uzazi na ujinsia, kuingia utu uzima, mahusiano, mimba, maambukizi ya virusi vya UKIMWI/UKIMWI na dawa za kulevya.

Pamoja na elimu ya afya ya uzazi, vijana pia waliweza kupata mafunzo ya msingi ya uandishi wa habari na utangazaji ili kuandika na kutayarisha vipindi vya redio, vijarida na midahalo kwa ajili ya kuwasiliana kutoka rika moja hadi jingine kuelimishana, kukemea, kudai na kukumbushana haki zao.

Elimu rika kupitia vikundi vya vijana katika redio ni mpango wa majaribio katika wilaya ya Sengerema na Pangani ambao mafanikio yake yataendelezwa katika sehemu nyingine hususan Kahama, Isaka, Micheweni, Simanjiro na Loliondo.

Vikundi hivyo ni fursa ya kuwajengea misingi ya ajira ya uandishi wa habari iwapo wataitumia vizuri kwa kushirikiana na vituo vya redio Jamii vilivyoteuliwa kuandaa na kutayarisha vipindi, kushirikiana na wenzao kurekodi majadiliano na kuwa wabunifu wa kuandaa vijarida kwa ajili ya kutoa elimu rika kuhusu afya ya uzazi na malezi.

AIRTEL MONEY YAGAWA BILLION 3 KWA WATEJA NA MAWAKALA

$
0
0
Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kugawa gawio la faida ya shilingi billion 3 kwa wateja wa Airtel Money na mawakala wake nchi nzima ikiwa ni faida yao kutokana na kutumia Airtel Money kuanzia Januari hadi juni mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Asupya Nalingigwa jana.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa gawio la faida la kila kiasi cha shilingi billion 3 kwa wateja wake wa Airtel Money na mawakala wakubwa na wadogo nchi nzima

Airtel imetoa gawio la faida kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi juni mwaka huu ambapo kila mteja atalipwa sehemu ya faida kulingana na kiasi cha salio lake katika akaunti yake ya Airtel Money kila siku

Akiongea na waandishi wa habari , Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “Tunayofuraha kutoa gawio la faida la shilingi bilioni 3 kwa wateja wetu na wakala nchi nzima. Tunaamini gawio hili la faida litawawezesha wateja wetu kutatua mahitaji yao ya kifedha na hivyo kuthibitisha dhamira yetu ya kuendelea kutoa huduma za kifedha”

“Tumejipanga kuwawezesha wateja wetu kwa kupitia huduma na bidhaa tunazozitoa. huduma ya Airtel Money imelenga kuleta unafuu na kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini hususani ya maeneo ya pembezo mwa nchi. Aliongeza Mmbando

Mpaka sasa Airtel imeshatoa kiasi cha shilingi billion 10 kwa wateja na mawakala wa Airtel money tangu 2014

Huduma ya Airtel Money inawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea pesa, kulipia bili, kununua vifurushi, kuamisha pesa na kutoa pesa kutoka benki pamoja na kutoa mikopo isiyo na dhamana kupitia huduma ya Airtel Timiza ambayo inatoa mikopo ya haraka, rahisi kwa wateja na mawakala

Mpaka sasa mtandao wa mawakala 50,000 wa Airtel Money nchini Tanzania wanaweza kutumia huduma hii. Theluthi moja ya mawakala wote wa Airtel Money hutumia Timiza, na baadhi ya mawakala sasa hivi wanakidhi vigezo vya kupata mikopo hadi Shilingi milioni moja.

TIGO YAKABIDHI MADAWATI NDANI YA MSIMU WA FIESTA WILAYANI KAHAMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya (kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Kahama Mjini. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa shule za wilayani humo ndani ya msimu huu wa fiesta.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Mungula wakiwa wamekaa kwenye madawati baada ya kuyapokea madawati 235 kutoka kwa Kampuni ya Tigo Wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Ally Maswanya (wa kwanza kulia ) akiwa amekaa kwenye madawati baada ya makabadhiano anayefuatia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu kwenye hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Kahama Mjini. Jumla ya madawati 235 yalitolewa kwa shule za wilayani humo ndani ya msimu huu wa fiesta.

JESHI LA POLISI LAHUSISHA TUKIO LA KUUAWA KWA POLISI MBANDE NA 'UKUTA'

$
0
0
Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tukio la mauaji ya askari wanne katika Benki ya CRDB Tawi la Mbande yaliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KUFUATIA mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka wahusika wote kujisalimisha.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.

Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia alipiga mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.

Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.

"Katika tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha mbilo aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.

Alisema katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi Srptemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.

AAR YATOA VIFAA VYA USAFI KWA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Meneja Masoko kampuni ya bima ya afya AAR Insurance Bi. Tabia Masoud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akikabidhi vifaa vya usafi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda kama programu yao endelevu ya kusaidia jamii na kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakua safi. Mwisho kulia ni Afisa Afya mkoa wa Dar es salaam, Denis Kanzola na mwisho kulia ni Msimamizi wa Fedha, Geofrey Masiga wa kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda akikabidhiwa baadhi ya vifaa mbalimbali vya usafi na Kampuni ya bima ya afya AAR Insurance Tanzania kama sehemu ya mpango wake kusaidia jamii na kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakua safi. Mwisho kulia ni Afisa Afya mkoa wa Dar es salaam Denis Kanzola, na kushoto ni msimamizi wa fedha Geofrey Masiga wa kampuni hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mheshimiwa Paul Makonda akimshukuru Meneja Masoko wa kampuni ya bima AAR Insurance Tanzania Bi Tabia Masoud kwa msaada wa vifaa mbalimbali vya usafi kama mpango wake kusaidia jamii, Kulia ni Afisa Afya Mkoa wa Dar es salaam Denis Kanzola na mwisho kushoto ni msimamizi wa fedha Geofrey Masiga wa kampuni hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo amepokea msaada wa vifaa vya usafi kutoka kampuni ya bima ya AAR Insurance Tanzania ikiwa ni ni msaada uliolenga kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi.

Ikiwa ni sehemu ya mpango wake kusaidia jamii, kampuni hiyo ya bima ya afya imetoa msaada wa matoroli 5, mabuti , reki , mafyekeo , mafagio , machepe , glovu na magudulia ya takataka 50 ambapo vifaa hivyo vitagawiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na uchafu.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Masoko wa AAR Bi Tabia Masoud alisema msaada huo pia umezingatia mojawapo ya vipaumbele vya serikali iliyopo madarakani ambapo inataka kuboresha utunzaji wa mazingira na uhifadhi wa takataka.

Alisema kwamba msaad huo umelenga zaidi kutatua tatizo la ukusanyaji na uhifadhi wa takataka katika jiji la Dar es salaam. Tunalenga kuwa na mkakati endelevu wa wa kusaidia kampeni za uhamasishaji, ushiriki wa jamii na kupunguza tatizo la takataka katika jiji la Dar es salaam.

Mordichai aliongeza kwamba utupaji taka ovyo katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam ni tatizo kubwa hivyo upatikanaji wa vifaa kama magudulia ya kukusanyia takataka ni hitaji la haraka kwa wakazi wa maeneo hayo. “Tumedhamiria kusaidia jitihada za serikali kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi na kuhakikisha tunakuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya kampeni hii”, alisema Tabia Masoud.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema: “Kuanzia wakati tunapozalisha takataka mpaka wakati takataka hizo zinatupwa lazima wote tukumbuke kwamba ni jukumu la kila mmoja wetu kuhifadhi taka vizuri. Nawashukuru AAR Insurance Tanzania, kwa kusaidia jitihada zetu za kuwa na Dar es salaam safi.”

KOREA KUSINI YATOA BILIONI NNE KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa
wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa
cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akisalimiana na wadau wa utalii, Zainabu Ansel, Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Zara (katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy Chamburo. (kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa.
Moja ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake Prof, Dkt Bernhard Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog Kanda ya Kaskazini.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na serikali ya Korea ya Kusini imeanza mchakato wa ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kutunza tarifa za mienendo ya Wanyamapori kitakachojulikana kama Serengeti Internatinal Media Centre.

Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .

Tayari serikali ya Korea Kusini imeshatuma wajumbe wake kuja nchini tanzania kujionea eneo kitakapojengwa kituo hicho na kukamilisha taratibu nyingine muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung amesema mradi huo ni mwendelezo wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.

Akizungumza na ujumbe huo mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti Wiliam Mwakilema amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.

Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance amesema ujenzi utaanza mwezi october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi 14.

WATANZANIA WARAHISISHIWA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA TEKNOLOJIA

$
0
0
Pamoja na kuwepo kwa maendeleo ya kasi katika nyanja mbalimbali lakini sekta ya teknolojia inabaki kuwa moja ya njia ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo kwa kurahisisha kazi nyingi kufanyika kwa haraka.

Kwa kutambua hilo, kampuni inayohusika na utoaji wa huduma zinazohusiana na teknolojia ya EnGenius imeingia katika makubaliano na kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia ya Red Dot ili iweze kusambaziwa vifaa na huduma mbalimbali ambazo zinafanywa na Red Dot katika nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao akizungumzia kazi ambazo wanazifanya na mipango ya kutoa bidhaa bora kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kampuni ya EnGenius ambayo inatoa huduma kama za internet wireless, radio frequency (RF) technology na kusambaza bidhaa mbalimbali kama kompyuta imesema kuwa imefanya maamuzi ya kuingi katika makubaliano na Red Dot ikiamini kuwa ni moja ya njia sahihi ambayo itawawezesha kuwafikia wateja kwa karibu zaidi.

Akizungumzia makubaliano hayo, Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao alisema kampuni ao kwa sasa inahitaji kujitanua katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia hivyo wameungana na Red Dot ili waweze kukuza biashara yao zaidi.

"Tumeingia makubaliano na moja ya wasambazaji wakubwa wa Red Dot na tunaamini watatusaidia EnGenius kufikia malengo yetu ya kuwa wauzaji wakubwa wa bidhaa za kiteknolojia kwa Afrika Mashariki, tunafahamu kuwa ni wasambazaji wakubwa na atatusaidia kukuza biashara yetu," alisema Hsiao.

Na Rabi Hume, modewjiblog.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution akielezea jinsi ambavyo wamejipanga kufanya kazi na EnGenius. (Picha zote na Na Rabi Hume, modewjiblog.com)

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani alisema kuwa ni ushirikiano mzuri ambao wameanza kuufanya na EnGenious na wana mipango mingi kuhakikisha malengo ambayo yamewekwa yanafikiwa.

"Tuna taraji mafanikio makubwa, Red Dot ni kampuni ya kitanzania ambayo inafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki kwahiyo tunatazamia ushirikiano huu utakuwa na faida," alisema Bharwani.
Meneja Mkuu wa Red Dot Distribution Tanzania, Rajesh Adiani akifungua halfa ya uzinduzi wa makubaliano kati ya Red Dot na EnGenius kwa kuelezea shughuli ambazo wanazifanya.
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa EnGenius, Alishan Zaidi akilelezea huduma ambazo wanazitoa za kiteknolojia na usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia kama kompyuta na kamera za usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani na Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao wakipongezana baada ya kuingia rasmi katika makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia bidhaa ambazo zinatolewa na EnGenius.
Baadhi ya wageni waaliakwa waliohudhuria halfa ya makubaliano ya Red Dot Distribution na EnGenius.
Viewing all 19859 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>