Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19857 articles
Browse latest View live

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KITUO CHA KUZALISHA UMEME CHA KIKULETWA WILAYA YA HAI LEO

$
0
0
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kuzalisha umeme na kutoa mafunzo cha Kikuletwa ambacho nchi yake imetoa dala za Marekani milioni 5 kwaajili kukifufua kwaajili matumizi ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).
Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro,Anthony Mtaka,Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika wakikagua vyanzo vya maji eneo la Chemka vitakavyotukika kuzalisha umeme na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya Uandisi Umeme wa Chuo hicho.
Mhandisi wa Umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha,Merchior Urbanus (kushoto) akimwelekeza jambo Balozi wa Norway wakati akitembelea eneo la Kikuletwa.
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad akifurahia madhari ya Kituo cha Kikuletwa, amehaidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati hapa nchini.
Moja ya mitambo zamani iliyopo kwenye kituo cha Kikuletwa iliyowekwa na Mmisionari wa Kijerumani mwaka 1935 na baadaye kukabidhiwa kwa shirika la umeme nchini Tanesco kisha Chuo cha Ufundi Arusha baada ya kutotumika kwa muda mrefu.
Moja ya chanzo cha maji ambacho pia hutumika kama sehemu ya utalii kutokana na maji yake kuwa ya vuguvugu muda wote.
Balozi wa Norway nchini Tanzania ,Hanne -Marie Kaarstad(wa tatu kutoka kulia)Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika wakiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Wakuu wa Chuo hicho na maafisa wa Ubalozi wa Norway nchini katika picha ya pamoja leo.

Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

WAZIRI WA AFYA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI MWANZA

$
0
0
 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa MSD wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
 ---
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. UmyMwalimu amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni.

Katika hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, ameipongeza MSD kwa hatua hiyo nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na kuitaka MSD kukamilisha ufunguzi wa maduka mengine mawili yaliyosalia katika mikoa ya Arusha naMbeya, kwani hicho ni moja ya kipaumbele katika uongozi waserikali ya awamu yaTano.

Waziri huyo ameeleza kuwa Wizara yake imejiwekea malengo ya upatikanaji wa dawa nchini kutoka asilimia 70 kwa sasa kufika hadi asilimia 95.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema maduka mawili ya Arusha naMbeya yamemekamilika, na yanatarajia kufunguliwa hivi karibuni, na kwamba kwa  mikoa mingine wameshafanya  mawasiliano  na kwamba tayari MSD imefanya mazungumzo na viongozi wa mikoa Ruvuma, Rukwa, Singida, Dodoma, Geita, Kagera na Iringa kufungua maduka yao ya dawa ambapo MSD itawauzia dawa.

“Tutakachofanya, sisi (MSD) utawapa  utaalamu na  kuwawezesha utaalamu wa uendeshaji maduka hayo” alieleza Bwanakunu.

MWILI WA MAREHEMU ASHA BAKARI WAWASILI ZANZIBAR KWA MAZISHI LEO SAA NNE JANGOMBE

$
0
0
Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Mwili wa Marehemu Asha Bakari alifariki nchini Dubai akitokea matibabuni Nchini India. Marehemu anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kianga nje kidogo ya mji wa Unguja na Maiti itasaliwa katika msikiti Mkuu wa Kwamchina saa nne asubuhi. 
Mwili wa Marehemu ukiteremshwa katika ndege kwa ajili ya maandalizi ya mazishi jana saa nne asubuhi Jangombe Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Pandu Amaer Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud wakiwa uwanja wa ndege Zanzibar wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu
Ndugu na Jamaa wa Marehemu wakiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Uwanja wa Ndege wa Zanzibar leo jioni
Mwili wa Marehemu ukishusha katika gari baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar wakiubeba wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar. 
Wananchi wakiupokea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Wafanyakazi wa Uwanja huo jana jioni.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho na Viongozi wengine wa Serikali na Vyama vya Siasa na Wananchi wakiuombea dua mwili wa marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili Zanzibar leo jioni tayari kwa mazishi jana katika kijiji cha kiyanga. 
Ndugu na Jamaa wakiwa na huzuni baada ya kuupokea mwili wa marehemu leo jioni 
Wananchi wakishiriki katika kuombeleza msiba wa marehemu Asha Bakari Makamu Mwenyekiti wa UWT Zanzibar aliyefariki Nchini Dubain wakati akitokea Nchini India katika matibabu.
Ndugu na Jamaa na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuombea mwili wa Marehemu Asha Bakari baada ya kuwasili nyumbani kaka wa marehemu kwa ajili ya matayarisho ya mazishi leo katika mtaa wa jangombe  
Waombolezaji wakiwa katika msiba jangombe kwa ndugu wa marehemu wakisubiri taratibu za mazishi leo saa nne asubuhi.
Ndugu wa marehemu wakiomboleza msiba wa ndugu yao nyumbani kwao jangombe Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud akizungumza na Ndg wa c na mareheme baada ya kuwasili kwa mwili wa marehemu Jangombe kwa nduga zake kwa mazishi leo.

Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com

JK ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA MAHUSIANO YA KIMATAIFA OUT

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ( Kulia) akifatilia kitabu cha mahafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika Jijini leo Dar es Salaam. kushoto ni Prof Suh Chae-Hong Rais wa Chuo cha Chosun kilichopo Korea ya Kusini..

Maandamano ya wanataaluma katika Mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akifungua rasmi mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimtunuku Shahada ya ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimpongeza Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa katika mahafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dare s Salaam.
Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanataaluma na wageni katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika leo Jijini Dare s Salaam.

Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali kutoka Chuo kikuu Huria Tanzania.
---
Na Raymond Mushumbusi Maelezo


Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa wa mahusiano ya kimataifa Leo Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.

“Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt Kikwete.

Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.

Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.

Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu 25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu chuo kuanzishwa.

SAFELY TRAVEL IN DAR ES SALAAM CITY

$
0
0
Dar es Salaam is Tanzania’s commercial hub, the city has a population of 4 million people owing to the increasing number of immigrants and the government offices in the city centre. Accordingly, the high population and several business activities in the city cause the transport system to experience occasional hitches.
JovagoTanzania has recognized the variety of local transport ranging from using buses to bajajis and brings you the best means of transport to get around the city.

Daladala
These are the main mode of public transport in Dar es Salaam and the cheapest in terms of fare cost (it’s only Tsh 400 per route). Daladalas will allow you experience the local life of many Tanzanians within a short period of time as they always crowded with people from different economic positions. It is safe as you will not get into trouble alone but also you need to take caution especially when you have luggages.

Taxi
These are the private owned businesses, they often offer private services and vary in prices depending on the distance (from Tsh 5000/= for short town trips, but often calculated on the basis of Km and waiting charges), the cost for the taxis is normally high but also negotiable.

Bajaji
These are the most popular transports for the short trips and the best option during the rush hours, bajajis are less expensive compared to taxi (from Tsh 1000/= depends with the distance). If you take a bajaji, make sure you hold your luggage properly so it isn’t stolen but also remember that bajajis are always restricted in town (Posta and Kariakoo).

Motorbikes
It is the best option when there is a traffic jam, motorbikes are less expensive compared to bajaji and taxi but make sure you wear motorcycle helmet.

Car hire
This service is based on the agreements with the car owner; you can choose the type of car based on your budget and choice. It is safer but you need to be very careful since it is not your property. Before you choose any means of transport ensure you know the exact route to the destination. People (locals) are nicer in giving instructions when you are lost but you need to do this carefully and cautiously.

Ferry boats
This is the only transport to Kigamboni (across the Indian ocean), it works full time day and night but you need to be on time since the ferry services cater to a lot of people.

There are several key tips you need to keep in mind when about to board a local transport in the major cities of Tanzania. Buses drive fast and offer minimal comfort, you need to travel early in the day and avoid night travels. You can also find your specific taxi or bajaji driver (find someone you trust to help you in negotiations).

MAALIM SEIF AHANI MSIBA WA BI. ASHA BAKARI MAKAME

$
0
0

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akimfariji Mama mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,akibadilisha mawazo na Baba mzazi wa marehemu Bi. Asha Bakari Makame, pamoja na kaka yake Bw. Mbarouk Makame (mwisho kushoto), alipofika kwenye msiba huo Jang'ombe mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

AHUKUMIWA MIAKA 19 JELA KWA KUIBA MBUZI MKOANI MBEYA

$
0
0
Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.

MAHAKAMA ya mwanzo vwawa mjini wilayani Mbozi mkoani Mbeya imemuhukumu Patrick Moses(19) mkazi wa Ilembo  kutumikia jela miaka mitano baada ya kukiri kosa la kuiba Mbuzi mmoja mwenye thamanai ya Sh 85,000 mali ya Bahati Mtafya.


Akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo,lazima Mwaijega alisema kutokana kifungu cha sheria 268 na mshitakiwa kukiri kosa hivyo mahakama imeamuru mshitakiwa kutumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani anategemewa na familia yake,hata hivyo hakimu Mwaijega amesema kifungo hicho cha miaka mitano amepunguziwa pia kwa kuwa ni kosa lake la kwanza na kwamba.

Awali imeelezwa mahakamani na  mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa January 20,mwaka huu saa 11 jioni  mshitakiwa alivamia nyumbani kwa Bahati Mtafya (38) na kuiba mbuzi mmoja mwenye thamani ya Sh. 85,000 huku akijua kufanya vyo ni kosa kisheria namba 229 sura ya 16 kanuni ya adhabu.

Aidha mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wale wenye nia ya kutendakosa kama hilo kutokana na wimbi kubwa la vijana kujikita katika wizi na kuacha kufanya kazi halali.

Katika hatua nyingine mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani hapo kujibu tuhuma ya wizi wa kuku 23 wenye thamani ya Sh laki 4 mali ya Evance Mwakenja mkazi wa Ilembo Vwawa 

Imeelezwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa tukio hilo lilitokea januari 20 mwaka huu saa 8 usiku ambapo mshitakiwa aliiba kuku 23 wenye dhamani ya Sh.laki 4 mali ya Evance Mwakenja huku akijua kufanya hivyo nikosa kisheria.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka linalomkabili na hakimuwa mahakama hiyo Chirstina Mlwilo amesema shauli hilo litaanza kusikilizwa Januari 27 mwaka huu,pia hakimu huyo amesema dhamana kwa mshitakiwa ipo wazi kwa ahadi ya Sh.laki 4 pamoja na kuwa na  wadhamini wawili wenye vitambulisho vya mpiga kura. 

 Hata hivyo mshitakiwa ameludiswa maabusu kwa kushindwa kutimiza masharti  la dhamana pamoja na kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano ya wizi wa mbuzi.
mwisho.

TIGO WAZINDUA UDHAMINI WA MBIO ZA NUSU MARATHON MJINI MOSHI

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
 Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, akifafanua jambo   kwa waandishi wa habari kuhusu udhamini wa Tigo kwa mbio za Nusu Marathon mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga(watatu kushoto, ).akizindua mbio za Kilimanjaro Marathon kwa upande wa Moshi. Wengine ni wadhamini wakuu wa mbio hizo kutoka kushoto, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania-Kilimanjaro na Tanga, Richard Temba, Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Listone Metacha na Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya GAPCO, Caroline Kakwezi.Uzinduzi huo ulifanyika Kibo Palace Homes.
---

Mbio za Nusu Marathon 2016 zimezinduliwa jana mjini Moshi, huku ikiwa imebaki mwezi moja kabla za mbio hizo kufanyika.


Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari alisema mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.

“Tumeonelea ni vizuri kuzindua mbio hizi rasmi hapa Moshi ambako zitafanyika ili kuashiria kuwa mambo yamekamilika,” alisema.

“Tigo imeingia mwaka wake wa 2 kama mdhamini wa mbio za kilomita 21.2 hizi. Kwa mujibu wa Meneja huyo, wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Kilimanjaro beer 45, Gapco kwa km 10 viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt kwa km 5.

Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair na Keys Hotel.

Alisema Tigo imewekeza zaidi ya Sh Millioni 200 katika mashindano hayo na kuwa hapo badaye watatangazo mchanganuo mzima wa zawadi zitakazotolewa.

Alitoa shukrani za pekee kwa mkoa wa Kilimanjaro na chuo kikuu cha Ushirika MOshi (MoCu), zamani kikiitwa MUCCoBS kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Akizindua mbio hizo mjini hapa, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makung, aliwapongeza Kilimanjaro Premium Larger,Tigo wadhamini wengine na wandaaji kwa kujielekeza vyema kila mwaka, akiongeza kuwa mashindanoyametokea kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kimichezo ndani na nje ya nchi.

“Mashindano haya pia yamekwenda mbali zaidi katika kukuza utalii, kwani wanariadha wa kimataifa na wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hiyo kufaidisha uchumi wan chi,” alisema Makunga.

Makunga aliawataka wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanajiandaa vyema ili watwae zawadi nyingi zaidi kwa kadiri zilivyopangwa kwa kila mbio. Aliongeza kwamba wizara yake inaunga mkono kabisa ubunifu kama huo na kuzitaka kampuni nyingine kufuata nyayo hizo kwa kudhamini mashindano hayo kila mwaka.

Aliwapongeza wandaaji, Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa Executive Solutions, Chama cha Riadha Tanzania (RT) na wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha siku zote kwamba tukio hili linafikiwa .

“Mbio hizi zimeleta mwamko mpya katika riadha hapa nchini kwa kuwapa fursa vijana wetu wanaochipukia kuweza kujipima na wanariadha mashuhuri kimataifa. Changamoto hii imekuwa na faida kubwa,ambapo vijana wetu wameweza kutambua uwezo wao na kuweza kujiamini zaidi wanapokwenda kushiriki mashindano mbalimabli kwenye nchi za kigeni,” alisema.

Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, alisema kwamba kampuni yake imefurahishwa kupata fursa ya kudhamini mbio za nusu marathoni kwa kilimota 21 kwa mwaka wa pili mfululizo.

“Natoa rai kwa washiriki wajiandae vizuri ili safari hiituweze kunyakua mataji mengi,” alisema Kinabo.

Meneja Masoko wa Gapco Tanzania, Caroline Kakwezi, ambaye kampuni yake inadhamini mbio za kilomita 10 kwa wanaotumia viti vya magurudumu na wale wanaonyonga baiskeli kwa mikono ambazo wanazidhamini, alisema zimekua na mvuto mkubwa na ushindani mkubwa pia na kwamba katika mwaka wao wa tano katika udhamini wameshuhudia mbio hizo zikikua.

“Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono, safari hii tutatoa usafiri, malazi na chakura kwa washiriki wote kutoka Dar es Salaam katika mbio hizi za walemavu na yote haya hayawezekani bila ushirikiano tunaoupata kutoka kwa wateja wetu”alisema.

RIPOTI YA TATHMINI YA MAZINGIRA YA KISHERIA KATIKA MWITIKIO WA UKIMWI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA ZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC), Dk.Ali Ali (katikati), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa ripoti ya tahmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa ukimwi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo asubuhi.
 Viongozi hao wakiwaonesha wageni waalikwa na wadau mbalimbali ripoti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tacaids, Elizabeth Kaganda na kilia ni Dk.Bwijo Bwijo kutoka UNDP.
 Naibu Mkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP), Titus Osundina, akihutubia wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar (ZAC),Dk. Ali Ali (kushoto), Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa yaKudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango (katikati) wakimpongeza NaibuMkurugenzi Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaMaendeleo (UNDP), Titus Osundina baada ya kuhutubia.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na viongozi.
Wasanii wa Hisia Threatel Group kutoka Sandali Temeke jijini Dar es Salaam wakionesha igizo linalohusu ukimwi katika uzinduzi huo.

NYOTA WA KIKAPU WA MALAWI KUZIKABILI TIMU ZA DAR

$
0
0
 Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.


 Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
---
Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.

Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.

Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.

Karabani ambaye michuano yake ya mpira wa kikapu iko chini ya udhamini wa Sprite, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibua na kukuza vipaji vya vijana kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo michuano hiyo imekuwa ikifanyika. Vilevile michuano hii inatoa fursa ya kuendeleza ushirikiano baina ya maeneo mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi.

“Lengo letu ni kuanzisha michuano ngazi ya kanda mwishoni mwa mwaka huu, ambapo mabingwa kutoka Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe”, Karabani alisema na kuongeza kuwa uzinduzi wa michuano hiyo utafanyika nchini Malawi

Kwa upande wake, Meneja Biashara wa Coca-Cola nchini, Maurice Njowoka alisema anajisikia furaha kubwa kutokana na heshima waliopewa kuisapoti michuano hiyo hapa nchini na kusisitiza kuwa kampuni yake itaendeleza ushirikiano wake na wadau wa mchezo wa kikapu kuzidi kuutangaza mchezo huo.

“Sote tunafahamu kuwa mpira wa kikapu ni moja ya michezo maarufu na yenye nguvu nchini, hasa miongoni mwa vijana ambao wanahitaji aina hii ya msaada ili kuhamasika na kuweza kuendeleza vipaji vyao”, Njowoka alisema.

KAMATI YA KURATIBU MISS TANZANIA YAJITOA KWENYE MASHINDANO

$
0
0
PI1
Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya kuratibu Miss Tanzania ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino International Agency, kushoto ni Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo na kulia ni Mjumbe wa kamati Gladys Shao .
PI2
Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Miss Tanzania Joketi Mwegelo akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Kamati hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili mfumo ili kubadilisha muonekano wa mashindano ya urembo (Miss Tanzania) kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Pinto.
PI3
Waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mashindano ya Miss Tanzania, Juma Pinto (hayupo pichani) alipokuwa akitoa sababu za kujitoa kwa kamati katika mashindano hayo. PICHA NA Beatrice Lyimo-Maelezo
---
Lilian Lundo- Maelezo, Dar es Salaam.

Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.

“Tumekuja kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya kamati kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.

Pinto aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.

Kamati hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano hayo.

Kutokana na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.

Aidha, Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na walioonesha nia ya kuwasaidia, amewataka kuendelea kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio kamati.

MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR SALIM JECHA AMETANGAZA KUWA UCHAGUZI VISIWANI HUMO UTAFANYIKA MACHI 20, 2016

$
0
0

RAIS MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA WAHITIMU CHUO CHA MAFUNZO YA KIJESHI MONDULI

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi katika viwanja vya Chuo hicho.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia gwaride lililokuwa likipita mbele yake  kutoa heshima.
 Gwaride la Wahitimu likipita kutoa heshima mbele ya mgeni rasmi  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Meja Generali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi aliyefanya vizuri  O/Cdt. Mmang’anda katika Mafunzo hayo. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya hawapo pichani
.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akisoma jarida  la Ngome baada ya kukamilika zoezi la
kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi.
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Wananchi. 
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na watoto waliofika kushuhudia tukiohilo la kuwatunuku Kamisheni Maafisa Wapya wa Jeshi. Picha na IKULU

DKT. REGNALD MENGI ASHIRIKI CHAKULA CHA MCHANA NA WATU WENYE ULEMAVU UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE, DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi (kushoto), akizungumza na Cosmas Anthony ambaye ni mlemavu wa miguu kwenye tafrija ya chakula cha mchana aliyoiandaa maalumu kwa watu wenye ulemavu iliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo mchana.
 Mwanamuziki wa kizazi kipya, Beny Paul (kulia), akipagawasha kwenye tafrija ya chakula cha mchana maalumu kwa watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam leo.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi akitoa hutuba fupi kwenye tafrija hiyo.
 Wafanyakazi wa IPP waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali katika tafrija hiyo.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Dk. Regnald Mengi, akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivawata), Ummy Hamisi kwenye tafrija hiyo.
 Dk.Mengi akimpa chakula mmoja wa walemavu aliyehudhuria hafla hiyo.
 Dk.Mengi akimpa chakula mmoja wa walemavu aliyehudhuria hafla hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye tafrija hiyo.
 Tafrija ikiendelea.
 NI furaha tu katika tafrija hiyo watu wamekula na kunywa.


 Dk.Mengi akiteta jambo na mtoto mwenye ulemavu Roida Undule.
 Dk.Mengi akisalimiana akina mama waliohudhuria hafla hiyo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mchungaji Alphonce Temba akiomba kabla ya kuanza kwa tafrija hiyo.

EDWIN HAMLI NA ISABELLA MUSHI WAMEREMETA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
???????????????????????????????????? 
Mdau Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakipozi kwa picha mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe na kufuataia na hafla ya kukata na shoka kwenye ukumbi wa Water Front jijini Dar es salaam usiku huu, hafla hiyo imehudhuriwa na ndugu marafiki na jamaa wa maharusi katika kufanikisha.???????????????????????????????????? 
Mdau Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakivishana pete wakatia walipofunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe leo.???????????????????????????????????? 
baadhi ya wasimamizi wa harusi hiyo wakishiriki ibada ya harusi hiyo kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe jijini Dar es salaam.???????????????????????????????????? 
Mdau Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakipozi wakiwa na waimamizi wao mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe.???????????????????????????????????? 
Mdau Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakionyesha vyeti vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe.???????????????????????????????????? 
Mdau Chilumba akiwa mna wageni waalikwa wengine waliohudhuria katika hafla hiyo.???????????????????????????????????? 
Mdau Kombe pamoja na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo.???????????????????????????????????? 
Maharusi Edwin Hamli na Mkewe Isabella Mushi wakipozi kwa picha kwenye ukumbi wa Woter Front mara baada ya kufunga ndoa yao takatifu kwenye kanisa katoliki la Chang'ombe.???????????????????????????????????? 
Bi. Harusi Isabella Mushi na waalikwa wakicheza muziki kwenye ukumbi nwa Woter Front.???????????????????????????????????? 
Mdau Kombe akiserebuka pamoja na wageni waalikwa wengine katika hafla hiyo.???????????????????????????????????? 
Mdau Chilumba wa pili kutoka kulia na Hassan Mabuyu wa pili kutoka kushoto wakiserebuka kwa muziki.???????????????????????????????????? Kutoka kulia ni mdau Willy Mwenyekiti wa kamati Kombe mjumbe wa kamati, Merkior mjumbe na Gasper mjumbe wakipozi kwa picha.

RAIS DK. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA VITAMBULISHO VYA TAIFA, DICKSON MAIMU

$
0
0
 
Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.

Aidha, baada ya utenguzi  huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

TBS YATEKETEZA BIDHAA ZA MAREKANI, CHINA

$
0
0
 Katapila likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziharibu bidhaa mbalimbali zikiwemo pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam.  Bidhaa hizo zenye thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa  na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA ZOTE  NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


---
Na Charity James

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa hafifu na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka nchini Marekani na China.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo,Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes.

Alisema miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwaajili ya biashara.

"Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.

Alisema bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni hafifu au kuisha muda wake.

Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na kuongeza wafanyabiashara ndio walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini hivyo ni vizuri wakafuata sheria kukwepa tatizo hilo.

MTANDAOWA TIGO 4G LTE KUPANUKA HADI MOSHI

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa 4G mjini moshi pia udhamini wa Tigo katika mbio za Kili NusuMarathon ambapo mbio hizo zitafanyika Februari 28, Wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali imetangaza mpango wake wakupanua huduma ya intaneti ya 4G hadi Moshi ifikapo Februari mwaka huu. Huduma hiyo ilizinduliwa kwanza jijiniDar es Salaam mwanzoni mwa mwaka jana na baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro, kwa ufanisi na hivyo kuufanya mtandao wa 4G kuwa mpana na wakasi nchini Tanzania.

Ikichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi karibuni kwenye sekta Ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia huduma ya intaneti, teknolojiaya 4G LTE inakasi takribani maratan ikilinganishwa na teknolojiaya 3G Ambayo inatumiwa na watoaji wengine wahuduma hiyo kwenye soko la Tanzania.

Akizungumza kwenye mahoajiano maalum na vyombo vya habari kwenye ofisiza Tigo mjini Moshi pempezoni mwa uzinduzi rasmi wa mbio za kila mwaka za masafa za Kilimanjaro Marathon, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kusambazwa kwa mtandaowa 4G kuna fanyika ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo wa kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ilikuwawezesha kuendesha maisha ya kidijitali.

“Mpango wa kupanua mtandao wa Tigo wa 4G hadi Moshi kwa mara nyingine umeonesha sio tu kwamba Tigo inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, balipia kujikita kwake Kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwaWatanzania wengi kadri iwezekanavyo,”alisema Wanyancha na kubainisha kuwa kuwalengo kubwa la kampuni hiyo ya simu ni kuhakikisha huduma hiyo inaenea nchi nzima ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2016.

Akizungumzia mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo Tigo ni mdhamini mwenza, Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali aTigo imeamua Kuwaunga mkono wanamichezo wa umekwa wake hapa nchini ilikuwasaidia kufikia malengo yao ya muda mrefu katika maisha.Wanyancha alihitimisha kuwa tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dola milioni 120 kwa mwaka kwenye upanuzi wa mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao ya 4G na 3G na mkongo wa mawasiliano na hali kadhalika kuongeza idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MH.GEORGE SIMBACHAWENE AMVUA MADARAKA MKURUGENZI WA MANISPAA YA DODOMA KWA KUKIUKA AGIZO LA SERIKALI LA 'ELIMU BURE'

$
0
0

WAZAZI MKOANI MWANZA WASIKITIKA ELIMU BURE KUWABAGUA WANAFUNZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA

$
0
0
Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima.
---
Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.

Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.

Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.

Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango
mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.
Viewing all 19857 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>