Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19859 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MPANGO MKAKATI WA WAFANYABIASHARA DUNIANI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli za kwa uadilifu (UNGC) uzinduzi huo umefanyika leo Januari 19,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha kitabu cha mpango mkakati baada ya kuzindua mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli za kwa uadilifu (UNGC) uzinduzi huo umefanyika leo Januari 19,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Jukwaa la mpango Mkakati wa Wafanyabiashara Tanzania Patrick E. Ngowi kushoto, Mwakilishi mkaazi wa Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez katikati na msaidizi wa Balozi wa Zurich Nchini Florence T. Mattli kabla ya kuzindua mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli zao kwa uadilifu (UNGC) uliofanyika leo Januari 19,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwenyekiti wa Jukwaa la mpango Mkakati wa Wafanyabiashara Tanzania Patrick E. Ngowi kabla ya kuzindua mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli za kwa uadilifu (UNGC) uliofanyika leo Januari 19,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Washiriki wa mkutano wa mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli zao kwa uadilifu (UNGC) uliofanyika leo Januari 19,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya Viongozi na Washiriki wa mkutano wa mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli zao kwa uadilifu (UNGC) uliofanyika leo Januari 19,2016, nje ya ukumbi wa mikutano katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na baadhi ya waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari baada ya kufungua mkutano wa mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa unaohimiza Wafanyabiashara Duniani kufanya shuhuli zao kwa uadilifu (UNGC) uliofanyika leo Januari 19,2016 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la mpango Mkakati wa Wafanyabiashara Tanzania Patrick E. Ngowi. (Picha na OMR)

TAARIFA ZA UPOTOSHWAJI ZA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA KIJITOUPELE

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 
KUHUSU UPOTOSHWAJI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA GAZETI LA MWANAHALISI KUHUSIANA NA UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA  KIJITOUPELE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inapenda kutaarifu Umma na Watanzania kwa ujumla kuwa Jimbo la Kijitoupele lililoko  Zanzibar ni miongoni mwa Majimbo hamsini(50) ambayo yalitegemewa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 25, oktoba,2015. 

Hata hivyo Jimbo hilo halikufanya uchaguzi wake wa Mbunge kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura badala Wapiga kura walishiriki katika kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Tume imefikia uamuzi wa kutoa ufafanuzi huu kutokana na taarifa iliyochapishwa na gazeti la MwanaHalisi toleo l Na.322 la Januari 18, 2016 katika ukurasa wake wa mbele likidai  “ NEC YAIBUA MAPYA” Habari hii si sahihi na inalenga kuupotosha umma na kuleta uchochezi miongoni mwa Wananchi.

Kwa ujumla maelezo yote yaliyopo katika taarifa hiyo yanaeleza kwamba, Tume imeanzisha Jimbio jipya, kwa mujibu wa taarifa ya gazeti husika ni Jimbo la Kijitoupele – Zanzibar.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda inasisitiza kuwa taarifa zilizotolewa na Gazeti la MwanaHALISI siyo za kweli, ni za uongo, uzushi, uzandiki na uchochezi. Kufuatia taarifa hiyo,Tume inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:
•          Tarehe 13 Julai, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari ikionesha Orodha ya Majimbo yatakayofanya uchaguzi wa Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na Jimbo la Kijitoupele lipo katika Orodha hiyo. Taarifa hii ipo katika tovuti ya Tume.
•          Katika Taarifa hiyo, Tume ilieleza wazi kuwa Majimbo ya Zanzibar yataendelea kuwa hamsini (50), ingawaje Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imeongeza majimbo manne na kuwa Hamsini na Nne (54).
•          Tulieza sababu ya kubaki na Majimbo hamsini (50) ni kutokana na matakwa ya Ibara ya 98 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ili kuongeza idadi ya wabunge kutoka Zanzibar inahitaji theluthi mbili ya Wabunge kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya Wabunge kutoka Zanzibar kuunga mkono mabadiliko hayo.
•          Tulieza kuwa, kipindi hicho Tume isingeweza kuandaa na kuwasilisha Muswada Bungeni kwa kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa linamaliza muda.
•          Katika taarifa hiyo, ilifafanuliwa kuwa, ili kubaki na majimbo Hamsini (50), kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, majimbo manne yaliunganishwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabuge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotoka Zanzibar.
•          Majimbo yaliyounganishwa ni:
1.         Jimbo la Bububu liliunganishwa na Jimbo la Mtoni, likaitwa jimbo la Bububu
2.         Jimbo la Mwera liliunganishwa na Mto pepo likaitwa jimbo la Mwera
3.         Jimbo la Kiembesamaki liliunganishwa na Chukwani likaitwa jimbo la Kiembesamaki
4.         Jimbo la Pangawe liliunganishwa Kijitoupele likaitwa Kijitoupele
•          Kwa mantiki hiyo Jimbo la Kijitoupele ni mojawapo ya Majimbo hayo (50) ambayo Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilisimamia na kuratibu Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge.
•          Tarehe 28 Oktoba, 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa taarifa kwa Umma kuwa, ilishapokea Matokeo ya Kura za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa kutoka Majimbo yote ya Zanzibar na siyo “siyo Matokeo ya Ubunge”

•          Tarehe 19 Desemba, 2015 Tume ilitoa orodha ya Majimbo ambayo hayajafanya Uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015 kutokana na hililafu mbalimbali, mojawapo ya majimbo hayo nane (8), jimbo la Kijitoupele - Zanzibar ni miongoni.
Ni vema wananchi wakafahamu kwamba, Tume ya Taifa ya Uchaguzi haianzishi na haijaanzisha Jimbo jipya la Uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015.
Hii inaonesha ni kiasi gani Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alivyodhamiria kuupotosha Umma kwani katika Makala/Taarifa hiyo hiyo ambayo anadai hakuna Jimbo la Kijitoupele (Unguja); anaeleza kuwa tarehe 25 Oktoba 2015 wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele walikosa fursa ya kumchagua Mbunge. Amemtaja Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI kuwa ni Wapiga Kura wa Jimbo la Kijitoupele, ambalo anadai eti Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeliibua miezi mitatu baada ya Uchaguzi.  Huu ni uongo na upotoshwaji wa makusudi kabisa.

Tume inapenda wananchi waelewe kuwa, hata kabla Tume ya Uchaguzi haijafuta matokeo wa Zanzibar, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa imesha tangaza kuahirisha Uchaguzi katika Majimbo nane (8) likiwemo la Kijitoupele kwa sababu za Vifo vya Wagombea na hitilafu mbalimbali. 

Jimbo la Kijitoupele la Zanzibar ni miongoni mwa majimbo nane (8) ambayo yaliahirishwa kufanya uchaguzi wa Wabunge tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo majimbo sita (6) ambayo ni Lushoto, Ulanga Mashariki, Masasi Mjini, Ludewa, Handeni Mjini na Arusha Mjini yaliahirishwa kutokana na vifo vya wagombea na majimbo mawili (2) ya Kijitoupele - Zanzibar na Jimbo la Lulindi – Masasi yaliahirishwa kutokana na hitilafu mbalimbali.

Hoja nyingine iliyotolewa na gazeti hilo ilihusu uteuzi wa Uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum. Ifahamike kwamba katika maamuzi yake kuhusiana na viti maalum, Tume imezingatia matakwa ya Ibara ya 78 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayoeleza kuwa, ili chama kilichoshiriki Uchaguzi Mkuu kipate Viti Maalum ni lazima kiwe kimepata angalau asilimia tano (5%) ya Kura zote halali za Ubunge.  Hivyo, Viti Maalum vilivyobaki haviwezi kugawanywa hadi hapo Jimbo la Kijitoupele litakapofanya Uchaguzi katika tarehe ambayo itaitangazwa  na Tume hapo baadaye.

Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alipaswa kufanya uchunguzi na uchambuzi wa kina kuhusu habari aliyoiachapisha ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Viongozi wa Tume ya Uchaguzi  ili wapate ufafanuzi wa Majimbo ya Uchaguzi na siyo kutoa Taarifa za uongo, uchochezi na upotoshaji kama walivyofanya.

Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI atambue uandishi wa habari ni zaidi ya kushika kalamu na kuandika, unahusisha uwezo wa kutafuta habari pande zote mbili ili kupata mizania ya habari anayoiandika, kufanya utafiti, kujiridhisha pasipo shaka kuwa habari anayoitoa ni sahihi.

Kwa kuwa Mhariri wa Gazeti la MwanaHALISI alikusudia kuupotosha umma kwa sababu anazozifahamu yeye mwenyewe kwa kutoa Taarifa zisizo sahihi, za uongo na uchochezi Tume ya Taifa ya Uchaguzi inamtaka Mhariri wa MwanaHALISI KUIOMBA RADHI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, UKURASA WA MBELE  WA TOLEO LIJALO KAMA ALIVYOFANYA KATIKA GAZETI HILO.
Kama wasipofanya hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi italichukulia Gazeti la MwanaHALISI hatua za Kisheria.

Imetolewa na
Kailima,R.K
MKURUGENZI WA UCHAGUZI.

MWILI WA MBUNGE LETICIA NYERERE WAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM MAZISHI YAKE KUFANYIKA BUTIAMA MKOANI MARA KESHO KUTWA

$
0
0
 Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani  kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
 Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
 Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
 Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
 Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.

WANAFUNZI 686 WA CHUO KIKUU CHA ELIMU CHA KUMBU KUMBU YA DR. ABDULRAHMAN AL – SUMAIT WATUNUKIWA VYETI VYAO LEO ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwenye uwanja kwa ajili ya Mahfali ya 15 ya chuo hicho hapo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ambae alimuwakilisha Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein kwenye Mahafali hayo ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Hicho Dr. Abdulrahman Al - Muhailan na kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.


 Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait wakiingia kwa maandamano kwenye uwanja kwa ajili ya kupewa stashahada zao.
  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan akitoa salamu kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
  
 Balozi Seif kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Shein akimkabidhi zawadi mwanafunzi Bora wa Daraja la kwanza katika Fani ya Kiarabu na Dini Kijana Nuru Ally Nassor Muhanna.
 Balozi Seif Ali Iddi akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho Dr. Abdulrahman Al – Muhailan kwenye mahafali ya 15 ya chuo hicho hapo chukwani.
 Seif pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hicho Dr. Abdulrahman Al – Muhailan wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa mahfali ya 15 ya wahitimu 686 wa chuo hicho. Aliyepo kati kati yao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuni.


 Balozi Seif akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kubmu ya Dr. Abdulrahman Al – Sumait, Dr. Abdulrahman Al – Muhailan hapo Chukwani.Wa kwanza kulia anayeshuhudia maagano hayo ni Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Profesa Hamed Rashid Hikmany.



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein alisema Vyuo Vikuu Nchini licha ya kuendelea kutoa taaluma kwa vijana wa elimu ya juu lakini bado vina wajibu na jukumu kubwa la kuhakikisha wasomi wake wanatumia vipaji vyao katika kufanya tafiti kwenye maeneo mbali mbali.

Alisema tafiti hizo zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwa wasomi wachanga wanaoanza kupata taaluma kwenye Vyuo hivyo sambamba na kuliwezesha Taifa kupiga hatua za haraka za Maendeleo.

Dr. Ali Moh’d Shein alitoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 15 ya Wahitimu 686 wa digrii ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait kiliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Alisema kuimarika kwa eneo la utafiti kutatoa fursa kwa wananchi mbali ya kupata elimu katika kiwango cha juu lakini pia watapata mbinu na maarifa ya kukabiliana na changamoto zilizowakabili maisha yao ya kila siku.

Rais wa Zanzibar alisema mchango mkubwa unaotolewa na Vyuo vikuu hapa Nchini hasa vile vyuo vikuu Binafsi umesaidia ongezeko kubwa la Walimu wa skuli mbali mbali za Sekondari hapa Visiwani.

Mapema Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al Sumait Chukwani Profesa Hamed Rashid Hikmany alisema kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wa chuo hicho mwaka huu kimeongezeka mara dufu kutokana na mikakati mizuri iliyowekwa na Uongozi wa Chuo hicho.

Profesa Hikmany alisema malengo ya uongozi wa chuo hicho kwa sasa ni kuimarisha zaidi utoaji wa wanafunzi wenye kiwango bora zaidi utakaokidhi mahitaji ya taaluma kimataifa.

Akitoa salamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Elimu cha Kumbu kumbu ya Dr. Abdulrahman Al - Sumait, Dr. Abdulrahman Al - Muhailan alisema Uongozi wa Chuo hicho utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Sekta ya Elimu.

Dr. Al - Muhailan alisema hatua hii inalenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Wananchi wa Zanzibar na Kuweit kupitia sekta za mendeleo na ustawi wa jamii ambazo tayari zimeshaleta mafanikio makubwa kwa pande hizo mbili rafiki.

Jumla ya wanafunzi 686 wa fani za Sayansi, Sanaa, Lugha ya Kiswahili, Kiarabu mfunzo ya Dini ya Kislamu wamehitimu mafunzo yao na kukabidhiwa stashahada ya kwanza.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
19/1/2016.

RAIS DKT. MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Bwana Sylvester Ambokile na Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Utawala na fedha Bwana Piniel Mgonja   ili kupisha uchunguzi, kufuatia dosari alizozibaini Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Charles Kitwanga alipotembelea Idara ya Uhamiaji hivi karibuni.

RATIBA YA MKUTANO WA WABUNGE WOTE PAMOJA NA VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE TAREHE 20 JANUARI – 25 JANUARI, 2016

$
0
0
Ofisi ya Bunge inapenda kuwafahamisha Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa ujumla kuwa,uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge utafanyika kesho Alhamisi tarehe 21 Januari, 2016, na kufuatiwa na Uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati husika pamoja na Kamati kupatiwa maelezo juu ya Wajibu, kazi na Mipaka ya kazi ya Kamati na kupokea na kujadili Mpango kazi wa Kamati unaoishia Juni, 2016.

Kwa kuzingatia Kanuni ya 111 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 siku ya Ijumaa tarehe 22 hadi Jumamosi tarehe 23 Januari kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na lengo la kuwafahamisha Wabunge kuhusu Kanuni za Kudumu za Bunge na Uendeshaji wa Bunge, Nadharia ya mgawanyo wa Madaraka katika Mihimili ya Dola, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Mambo Mengine ya Kiserikali.

Aidha, Kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ambacho wajumbe wake ni Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge chini ya Uenyekiti wa Mhe. Spika, kinatarajiwa kufanyika Siku ya Jumapili tarehe 24 Januari, 2016, ambapo Jumatatu tarehe 25 Januari, 2016 itakuwa ni siku mahususi kwa Wabunge kupata maelezo kuhusu Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano.

Ratiba ya Shughuli za Mkutano wa pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza
Jumanne tarehe 26 Januari, 2016 itatolewa baadae.

Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM
20 Januari, 2016.

NHIF YAKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WANACHAMA WA TBN

$
0
0
Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo. Meneja wa Mfuko wa Afya ya Jamii, Slivery Mgonza akimkabidhi Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii (Bloggers-TBN) kadi za Bima ya Afya kwa baadhi ya wanachama wa TBN. Kushoto ni Ofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa, Nicholaus Mwangomo.

WAZIRI WA ELIMU PROF. JOYCE NDALICHAKO AMELIAGIZA BARAZA LA MITIHANI (NECTA) KUONDOA MFUMO WA GPA NA KURUDISHA MFUMO WA DIVISION

$
0
0

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA (OUT) KUMTUNKU UDAKTARI WA HESHIMA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE, DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Profesa Elifas Bisanda akizungumza kuhusiana na mahafali ya 30 ya chuo hicho yatakayofanyika kesho (Alhamisi), Biafra jijini Dar es Salaam jana. Picha na Mugishagwe Zablon
---
Mugishagwe Zabon, Dar es Salaam.

Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), kesho Alhamisi kinatarajiwa kumtunku udaktari wa heshima Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika, viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Elifas Bisanda alisema licha ya Rais huyo mstaafu pia Rais wa Chuo Kikuu cha Chosun cha nchini Korea Kusini, Profesa Chae-Hong Suh nae atatunukiwa shahada hiyo ya heshima.

“Tutamtunuku Rais huyo wa chuo kikuu Chosan ambaye ambaye amebobea katika eneo la dawa za binadamu kwani tunafanyanae kazi hapa nchini” alisema na kuongeza kuwa Kikwete anapewa heshima hiyo kwa chuo kudhamini mchango wake kimataifa katika kutatua migogoro na ukuzaji uchumi kupitia uwekezaji.

Alisema kiuchumi Kikwete amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuvutia uwekezaji hali ambayo imechangia Marais wengi wakiwemo wastaafu wa nchi za Marekani na Ulaya kutembelea nchini akiwemo Rais Barack Obama.

Profesa Bisanda alisema Rais Kikwete amefanyakazi kubwa kuhakikisha sualuhu inapatikana katika migogoro mbalimbali ukiwemo ule wa baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya 2007-2008 ambazo zilisababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000.

“Wote tunakumbuka vurugu za baada ya uchaguzi nchini Kenya ambazo ziisaabisha vifo vya mamia ya raia wasio na hatia na mchango wake jinsi ulivyowezesha kupatikana kwa utengamano wa kisiasa nchini humo akishirikiana na Rais wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa” alisema Bisanda.

Alibainisha kuwa Profesa Chae-Hong Sun wa Chuo Kikuu Chosun cha nchini Korea ya Kusini ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia ustawi wa OUT ambacho pia kina matawi katika nchi mbalimbali za Afrika akiwa amejikita zaidi katika masuala ya dawa za binadamu

AIisema licha ya shahada hizo za heshima lakini pia wahitimu wapatao 69 watatunukiwa shahada za uzamili, uzamivu, stashahada na astashahada katika mahafali hayo ambayo yaitanguliwa na mengine kama hayo yaliyofanyika, Kampasi ya Kibaha mkoani Pwani.

Chuo hicho ambacho kina matawi takribani nchi nzima, kilianzishwa mwaka 1992 hadi hivi sasa kimeishatoa wahitimu zaidi ya 26,763 katika fani na ngazi mbalimbali za kitaaluma.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AONESHA UMAHIRI WAKE WA KUSHONA

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia Cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es salaam Januari 20, 2016.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi wa hali ya juu.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

PROFESA MWANDOSYA ATOA MHADHARA CHUO KIKUU CHA ULINZI (NATIONAL DEFENCE COLLEGE) JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Waziri Mstafu Profesa Mark Mwandosya akitoa  Mhadhara Chuo Kikuu Cha Ulinzi (National Defence College) jijini Dar es salaam. Mada ilihusu  changamoto za kiulinzi na usalama zinazotokana ushirikiano katika mabonde ya kimataifa ya majishirikishi. Waliohudhuria ni maafisa wa ngazi za kati na juu wa vyombo vya ulinzi na usalama, na wanafunzi wengine wa Chuo hicho kutoka Kenya, China, Namibia na Malawi.

 Waziri Mstaafu Profesa Mark Mwandosya akiagana na wakufunzi wakuu baada ya kutoa mhadhara huo. Kutoka  kulia ni Meja Jenerali Omar; Mrs Lucy Mwandosya; Profesa Mwandosya, na Brigadia Mwaseba.
Mwisho.

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU LETICIA NYERERE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete nyumbani kwa Baba wa Taifa  Msasani Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho  wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji mume wa marehemu Bw. Madaraka Nyerere wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimfariji Mama Maria Nyerere wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Marehemu Leticia Nyerere aliyefariki mwishoni mwa wiki Nchini Marekani alikokuwa akitibiwa leo Januari 20, 2016. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

AUAWA KISA LAKI 7, MOSHI

$
0
0
 Wakazi wa Kijiji cha Kindi Tarafa ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, wakiwa kwenye  mazishi ya marehemu Eugeni Mboro mfanyabiashara wa mahindi aliyeuawa kwa kukatwa na shoka nyuma ya shingo yake na kuporwa sh700,000.
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Anthony wa Padua, Kijiji cha Kindi Tarafa ya Kibosho Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro, Padri John Senya, akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Eugeni Mboro mfanyabiashara wa mahindi aliyeuwa kwa kukatwa na shoka nyuma ya shingo yake na kuporwa sh700,000.

Na Woinde Shizza, Moshi

WANANCHI wa Kijiji cha Kindi Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wamesema ili kukomesha mauaji ikiwemo tukio la kukatwa na shoka nyuma ya shingo kwa Eugeni Mboro kwa sababu ya sh700,000 wauaji hao wachukuliwe hatua.

Mkazi wa kijiji hicho Richard Massawe alisema jana chanzo cha kifo hicho ni sh700,000 alizokuwa nazo Mboro baada ya kuuza mahindi yake ndipo baadhi ya watu aliokuwa nao kupanga njama za kumuua na kuzichukua fedha hizo.

“Tunaomba serikali ichukue hatua kwani Mboro alikuwa ni mjasiriamali mdogo anayeibukia hapa Kindi na asiyekuwa na tatizo na mtu ila hao kina Gasto na Kisimati walishikwa na tamaa ya kumuua ili wachukue pesa,” alisema Massawe.

Mjomba wa marehemu Joseph Mwacha aliiomba serikali kuchukua hatua kwa wahusika wote wa mauaji hayo kwani ndugu yao hakudhulumu kitu cha mtu ila ni roho mbaya zilizosababisha kifo hicho na kumpora sh700,000 zake.

Hata hivyo, akiongoza ibada ya mazishi hayo, Paroko wa kanisa katoliki parokia ya Anthony wa Padua, Padri John Senya, aliwataka wakazi wa eneo hilo kupiga vita matukio ya uuaji kwa mtu asiye na hatia.

“Tunapaswa kubadiliwa jamani watu Kindi kwani itafikia siku mtu ukisema umetoka Kindi watu watakuangalia mara mbili mbili hivyo unasema umetoka Kibosho badala ya kutaja eneo hili tulipozaliwa,” alisema Padri Senya.

Kwa upande wake, kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Ramadhan Mungi alisema mwili wa Mboro ulikutwa kwenye shamba la Michael Makabili huku akiwa na jeraha nyuma ya shingo lililotokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali.

Kamanda Mungi alisema pia marehemu aliibiwa fedha zake sh700,000 na wanawashikilia watuhumiwa wawili kwa uchunguzi akiwemo Gasto Costa (25) mkazi wa kijiji cha Kindi na mtu mwingine ambaye hakumtaja jina lake.

“Huyu mtuhumiwa Gasto tulifanya upekuzi kwenye nyumba yake na kukuta kuna shuka lenye damu na nguo za marehemu Mboro ila huyu mtuhumiwa mwingine bado tunaendelea na uchunguzi juu yake,” alisema Kamanda Mungi.

JK ATEULIWA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0

WAFANYAKAZI WA TBL MBEYA WAPATIWA ELIMU YA JINSIA

$
0
0
po1
Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba akitoa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini
po2
Afande Prisca akiwazungukia washiriki wakati wa semina
po3
Baadhi wa wafanyakazi wa TBL Mbeya wakimsikiliza afande Prisca wakati huo huo wakipata chakula cha mchana.
po4
Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni.
---
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group katika kiwanda cha Mbeya leo wamepatiwa semina kuhusiana na masuala ya jinsia naMkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba.

Katika semina hiyo wafanyakazi waliweza kujua masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kijinsia ambapo pia walipata fursa ya kuuliza sheria na masuala ya jinsia kutoka kwa mkufunzi huyo kutoka Jeshi la Polisi.

Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki mafunzo hayo walisema kuwa yameweza kuwafumbua macho kujua masuala mbalimbali yatakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku wanapokuwa sehemu za kazi na katika maisha ya kawaida na familia zao wanapokuwa wameishatoka kazini.

MWANASAIKOLOJIA ANTI SADAKA AWAFUNDA WANAWAKE WA JIJI LA MWANZA

$
0
0

Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza.
Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa  na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano  Foundation  yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani  wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa   kwenye Mafunzo hayo.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mkoani Mwanza kuchangamkia FURSA zinazowazunguka mapema iwezekanavyo. Alisisitiza umuhimu wa usafi wao binafsi na mazingira yao ya kazi kupewa kipao mbele kwa sababu usafi humlinda mteja asipate breakout ya ngozi yake na kuridhika na huduma yake yaani "Smart You & Environment."
Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Mwanza kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. Baada ya washiriki kupata mafunzo ya biashara na urembo watapatiwa  MIKOPO kutoka Taasisi ya Manjano  Foundation  kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Mwanasaikolojia Anti Sadaka Akiwa katika Picha ya Pamoja na wanawake wa Mkoa wa Mwanza waliojitokeza  kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali  yanayoendeshwa  na Taasisi ya Manjano Foundation.
Washiriki wa mafunzo hayo  wameushukuru uongozi wa Taasisi ya Manjano  Foundation kwa kuwakumbuka na kuwaletea Mradi huo jijini Mwanza. Wakieleza zaidi wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu matumizi sahihi ya vipodozi lakini walikosa elimu hiyo ya kuwa Makeup Artists.

YALIYOMKUTA MDAU: KUWENI MAKINI MNAPOSAFIRI

$
0
0
"Jana nikiwa safarini tumepatwa na tukio lisilo la kawaida! Kumbe hizi ajali zingine ni nguvu za kichawi chawi tu. 

Ni hivi jana tumefika Tinde kwenye mizani ya tanroads kuna mzee akalalamika kuwa kaibiwa laptop, ikabidi gari igeuze tuelekee kituo cha police si mbali kutoka hapo! 

Police wakaamuru kila abiria atone na begi lake kwa upekuzi! Ila tukiwa singida kuna jamaa alipanda na hakuweka begi lake chini yaani mda wote alikuwa amelipakata na alikuwa siti ya jirani yangu tu.

Sasa kwenye upekuzi tulishuka nae ila begi akaliacha chini ya siti, upekuzi ulipoisha askari wakaingi ndani ya basi wakashuka na begi mbili, moja ilipata mwenyewe ila nyingine ikakosa mwenyewe, yaani moja ya ile begi mwenywwe alikua sister mmoja hivi na alijitetea kuwa alichemka kuitoa juu ya keria (zile za ndani) ile nyingine ikabidi ifunguliwe... lahaulaah! 

Kilichokutwa ndani ni tunguli,vibuyu, sufuria, vitambaa vyeusi na vyekundu, ugali na nyoka wakubwaa wawili.

Sadick Hamis - Kahama - Dar es Salaam.

DC KINONDONI KUONGOZA UPIMAJI WA MAGONJWA YA MOYO BURE VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR, JANUARY 23, 2016

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa mwito kwa wananchi hasa wa Wilaya ya Kinondoni na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupimwa maradhi ya moyo bure katiza zoezi litakalofanywa na madaktari kutoka taasisi hiyo litakalofanyika viwanja vya leaders kesho kutwa January 23, 2015. Kushoto ni Meneja wa Taasisi hiyo, Salome Kassanga na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Meneja wa Taasisi hiyo, Salome Kassanga (kushoto), akimuelekeza jambo DC Makonda. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa Taasisi hiyo, Dk.Peter Kisenge.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

 Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kesho kutwa anatarajia kuongoza wananchi wa wilaya yake na wakazi wengine wa jiji la Dar es Salaam katika upimaji wa magonjwa ya moyo utakaofanywa bure na madaktari kutoka Taasisi  ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),  katika viwanja vya Leaders Club. 

Upimaji huo utatoa fursa ya kubaini wagonjwa wa wilaya hiyo kwa kuwa wananchi wengi hawajui magonjwa ya moyo yanaweza pia kusababishwa na shinikizo la damu na ni chanzo kikubwa cha   magonjwa ya macho,upungufu wa nguvu za kiume, kiharusi, figo na kutokuzaa.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi alisema kutokana na umuhimu wa wananchi kujua afya zao na kupatiwa matibabu mapema kesho wataungana na Makonda katika kuwapatia vipimo wakazi wa kinondoni.
 
Alisema ugonjwa wa moyo ni hatari na asilimia kubwa ya wagonjwa hao wanatembea na kufanya kazi zao kwakuwa ugonjwa huo hauna dalili hivyo haja ya kila mmoja kupima na kujua afya yake ni muhimu.
 
“Pia wengi wanaougua shinikizo la damu hawajua wanaweza kuwa na magonjwa ya moyo na  kujikuta wakisababisha kuua figo,macho,nguvu za kiume,kuugua kiharusi na kukosa watoto upimaji huu ni hatua nzuri kwa wananchi wa kinondoni hivyo tumeridhia kuwapima na kuwapatia matibabu bure,”alisema.
 
Alisema taasisi hiyo itakuwa kamili katika kila sekta kesho kutwa viwanja vya Leaders Club ili wananchi wenye magonjwa yanayoshabihiana na moyo waweze kupewa tiba katika hospitali za wilaya hiyo ikiwemo Mwananyamala na wale walioathirika na ugonjwa wa moyo waweze kutibiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Profesa Janabi alisema pia watahakikisha madaktari wa ushauri wanatoa elimu ipasavyo juu ya kuepuka ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu ambao hauna tiba na jinsi ya kuzingatia lishe.
 
“Ni muhimu kujua ongezeko la matumizi ya vyakula vya wanga kwa wingi pia ni hatari katika kuongeza uzito hivyo kusababisha shinikizo la damu,”alisema
 
Kwa upande wake Makonda aliwataka wananchi kuelewa kuwa ugonjwa wa moyo ni hatari na matibabu yake ni gharama hasa kwa wale wanaosafirishwa nje ya nchi hivyo ni vyema kuitumia fursa hiyo kesho.
 
Alisema serikali imeona haja ya kuboresha afya za wananchi ili kukuza uchumi na hatua hiyo ya kusaidia upimaji wa bure itapunguza hatari ya ugonjwa huo kwa watu wengi wanaopoteza maisha kila siku.

OJADACT WALAANI SHERIA YA MAGAZETI YA MWAKA 1976. WAMWOMBA MAGUFULI KUINGILIA KATI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo +BINAGI MEDIA GROUP 

Chama cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Nchini OJADACT, Kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi yake ya kufanyia marekebisho sheria kandamizi kwa vyombo vya habari nchini, aliyoitoa wakati wa Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.

Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko, ametoa ombi hilo hii leo mbele ya Wanahabari Jijini Mwanza, wakati akielezea hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali dhidi ya vyombo vya habari vinavyokiuka sheria katika utendaji wake wa kazi.

Soko alitolea mfano Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kupitia sura ya 229 kifungu cha 25 (1), kinachompa Mamlaka Waziri waHabari kulifungia gazeti lolote linalotoa habari zenye ukakasi, kuwa ni ishara ya ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini, kwa kuwa kuwa sheria hiyo haitoi nafasi kwa chombo kinacholalamikiwa kujitetea ikizingatiwa kwamba Serikali ndiyo mlalamikaji na wakati huo huo mtoa hukumu.

“Sheria ya Magazeti ni mbaya kwani haitoi nafasi kwa upande wa pili kujibu, huku serikali ikiwa ndiyo mlalamikaji na hapo hapo hakimu (Unfair game). Alitanabaisha Soko na kuongeza kuwa OJADACT inalaani matumizi ya sheria ya magazeti nchini ya mwaka 1976.

Wakati OJADACT ikitoa ombi hilo kwa Rais Dkt.Magufuli, baadhi ya Waandishi wa Habari Jijini Mwanza walikiri kuwepo kwa sheria zenye ukandamizaji wa Uhuru wa habari nchini ambapo wameomba sheria hizo kurekebishwa ili kukuza haki ya kutafuta na kutoa habari katika jamii.

Vyombo mbalimbali vya Habari nchini hususani Magazeti, vimekuwa vikikabiliwa na sheria kadhaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa ya kwamba zinakiuka misingi ya uhuru wa habari ambapo ni hivi karibuni Serikali imelifungia gazeti la Mawio kuchapisha habari zake kutokana na kuchapisha taarifa zilizoelezwa kuwa na mkanganyiko katika jamii.
Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.
Wanahabari
Kulia ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG.
Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG
Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG
Kutoka Rock City Jijini Mwanza, Mimi ni GB Pazzo wa Binagi Media Group.

MAELFU WAJITOKEZA KUMPOKEA MAGUFULI ARUSHA

$
0
0
 Ngoma za asili zikiwa zinatumbuiza katika uwanja wa KIA mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutua na ndege uwanjani hapo
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki  Magufuli
Na Woinde Shizza,Arusha
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa nchi ya Tanzania  ni tajiri na inarasilimali nyingi ,ila baadhi ya matajiri ambao ni mafisadi ndio wanasababisha nchi yetu kuonekana maskini  hivyo amehaidi kula nao sahani moja.
Aliyasema hayo  leo  wakati akiongea na wananchi wa  mkoa wa Arusha waliojitokeza  barabarani kumpokea  huku wakimuomba aendelee kutumbua majipu.
Alisema kuwa nchi ya Tanzania inarasilimali nyingi  ila kunabaadhi ya matajiri ambao wanapenda kujilimbikizia fedha wamekuwa wakifanya ufisadi na kusababisha baadhi ya wananchi kuendelea kuwa maskini  pamoja na nchi yetu kuonekana maskini.
“nasema hivi kuanzia sasa nipo tayari kulala mbele na mafisadi wote na pia nawapa onyo kali wale walimu ambao bado wanatoza ada mashuleni iwapo nitagundua mwalimu yeyote  anaetoza ela nahaidi ivi nitalala nae mbale ,na katika hili  sitalifanyia masiara ata kidogo”alisema Magufuli
Aidha aliwaambia wananchi kuwa kuanzia sasa elimu ni bure kuanzia shule ya msingi adi sekondari na serekali imeshaweka mipango hiyo tayari na imeanza kutumika.
Magufuli aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuendelea kufanya kazi na kusema kuwa wakati wa kampeni umeisha , mambo ya siasa yameisha sasa ivi ni wakati wa kufanya kazi tu na sio kitu kingine.
“nasema ivi sasa ivii ni wakati wa kufanya kazi kama nitaendelea kutumbua majipu kila mahali na sitawaonea huruma mtu yeyote mimi kazi yangu kubwa ni kufanya kazi tu na wananchi napenda kuwambia fanyeni kazi kwani hapa ni kazi tu”alisema Magufuli.
Alisema yote aliyoyaahidi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla ikiwemo ujenzi wa barabara za Arusha, kulipa fidia za wananchi na kufuta ada ya shule za msingi na sekondari yanatekelezwa.
Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watanzania kumuombea ili aendelee kuwashughulikia wote wanaofanya ubadhilifu wa fedha za umma kupitia kampeni yake ya kutumbua majipu.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake haitawabagua watanzania kwa dini zao wala makabila yao na wala haitawabagua kwa milengo ya vyama vyao na kanda zao na kuwataka watanzania wote  kuiweka mbele Tanzania na kushirikiana kuiendeleza.
Rais magufuli alipokelewa na mamia  ya wananchi  mbalimbali ambao walijitokeza barabarani ambapo pindi tu alipotoka katika kiwanja cha kia wananchi walikuwa wemejitokeza wengi mpaka ikamlazimu kufika katika baadhi ya maeneo na msafara wake kusimama ili wananchi waongee nae,sehemu ambazo aliweza kusimama ni pamoja na kikatiti ,usa river  pamoja na Tengeru .
Viewing all 19859 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>