Siku ya Tarehe 4 Mwezi wa 10 mwaka 2014 haitakaa isahaulike kwa wakazi wa Mwanza na Vitongoji vyake... Hii ni siku pekee ambayo Mwanza nzima ilihamia JEMBE BEACH almaarufu kama JEMBE NI JEMBE ambako Tamasha kubwa sana Tanzania linalofahamika kama INSTAGRAM PARTY lilirindima siku hii...
Kufikia saa 4 Jembe ni Jembe tayari ilikwishafurika na watu kutoka kona mbalimbali za Jiji la Mwanza walikuwa wakifurahia muziki maridhawa kutoka kwa MADJ watano wakali kabisa...
Deejay VASLEY all the way kutoka DSM wengi tunamjua akiwa anapiga SAMAKI SAMAKI, Deejay D'Ommy Kutoka Times FM DSM, wakiungana na Ma-DJ watatu wakali kutoka JEMBE NI JEMBE, Deejay Frank,Deejay KFlip na Deejay Davy, waliwasha moto wa hatari na kukata kiu ya wakazi wa Mwanza ambao hawajawahi kupata burudani kali yenye ladha tofauti namna ile.
MARA GHAFLA, Katika kile ambacho hakikutegemewa Mwanamuziki wa RnB, BEN PAUL akapanda jukwaani na kuanza kupiga acapella za nyimbo zake kali kali zoteee huku akitoa zawadi kwa washindi mbalimbali ambao walijishindia Simu za Mkononi kutoka kampuni ya TIGO.
Haikuishia hapo tu, Wanamuziki wawili kutoka TAMADUNI MUSIC, Stereo Singasinga au CHUNDABADI na Songa wakapanda jukwaani na kuangusha Hip Hop za kutosha na kuwafanya watu washindwe kabisa kukaa kwenye viti vyao Mwanzo mpaka mwisho wa Shoo...
Wakadhani imeisha, kumbe bado WAKAZI alikuwepo... SHILOLE aka Shishi Babe alikuwepo na Mwanadada JOKATE alikuwepo na wananchi wa Mwanza wakapata nafasi adimu ya kupiga Stori na Picha na masupastaa hawa ambao kwa hali ya kawaida wasingeweza kuonana nao ana kwa ana popote pale.
Hiyo ndio INSTAGRAM PARTY... Ni mwendo wa SURPRISE... Watu hawajui nini kinakwenda kutokea bali wanashangaa kukutana na watu ambao hawakuwategema kabisa..
MBEYA MKO TAYARI??
DODOMA JE?
ARUSHA??
Mnajua kwamba TEAM FORBES wanaleta INSTAGRAM PARTY hivi karibuni??
Kaeni mkao wa kula maana hii ni zaidi ya Party Tanzania
Tungependa kuwashukuru Wadhamini wetu wote kwa kuweza kutupa Sapoti ya hali ya juu kuhakikisha Party za Instagram zinafika kila mkoa Tanzania, Shukrani ziwaendee pia TIGO TANZANIA, PIGEON HOTEL, PHOTOSPOT STUDIOS, JESTINAGEORGE BLOG, BLOGU YA WANANCHI, SEIF KABELELE BLOG, KAJUNASON BLOG, VK DESIGNS, P-MONEY, MKITODOTCOM, AIM GROUP na JEMBE BEACH SWAHILI DIGITAL, DALALI ONLINE.