Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MWISHO UREJESHAJI FOMU SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO NI LEO OKTOBA 10, 2014

$
0
0
Vijana katika biashara ya uuzaji samaki. 
Vijana katika biashara ya uuzaji samaki.
Vijana katika biashara ya uuzaji samaki. Vijana katika biashara ya uuzaji samaki.Vijana katika biashara ya uuzaji mapambo mbalimbali 
Vijana katika biashara ya uuzaji mapambo mbalimbaliVijana katika biashara ya ukaangaji na uuzaji samaki. 
Vijana katika biashara ya ukaangaji na uuzaji samaki.

WAKATI siku ya mwisho ya urejeshaji wa fomu kwa vijana watakao shiriki Shindano la Mashujaa wa Kesho ukiwadia na dirisha la upokeaji fomu hizo kutarajiwa kufungwa leo Oktoba 10, 2014 majira ya saa nane ambapo idadi ya vijana waliorejesha fomu hizo imeendelea kupanda. 

Akizungumzia zoezi hilo jana mchana, Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Erick Mchome aliwataka vijana waliochukua fomu zao kuzirejesha mapema ili kujipatia fursa ya kushiriki katika shindano hilo ambale linaweza kuwakwamua vijana kiuchumi. 

 Akifafanua zaidi, Erick Mchome alisema dirisha la kupokea fomu za Shindano la Mashujaa wa Kesho linatarajiwa kufungwa rasmi na kuwataka vijana wachangamke kabla ya muda huo kufungwa.

Alisema bado kuna idadi kubwa ya fomu ambazo hazijarejeshwa na vijana waliochukua fomu hizo na kuwataka kufanya hivyo kabla ya muda wa zoezi hilo kufungwa hapo kesho.

“Vijana waliorejesha fomu mpaka leo (jana) ni takribani vijana 200. 

Waliochukua fomu tangu siku ya uzinduzi Septemba 3, 2014 ni zaidi ya vijana 1000. Hivyo natoa wito kwa vijana ambao bado hawajarejesha na wanataka kuingia kwenye ushindani huu kurejesha fomu zao kwa wakati,” alisema Mchome.

Zoezi zima la urejeshaji fomu litafikia tamati siku ya Ijumaa Oktoba 10, 2014 kabla ya saa nane mchana na baadaye kufanyika mchujo wa kupata vijana 40 watakaoingia hatua ya pili kabla ya kutangazwa washindi watano ifikapo mwezi wa 12. 

 Aidha alivitaja vituo vya kurejesha fomu mkoani Mtwara kuwa ni pamoja na Naliendele Agricultural Institute, Tanzania Institute of Accountancy, VETA, Chuo cha Utumishi, Chuo cha Stella Maris Pamojana Pride FM.

Naye Mhadhiri wa Chuo cha Stella Maris ambaye pia ni Mratibu wa shindano hilo kituo cha chuo hicho, Justin Lusasi aliwataka vijana kutokata tamaa katika ushiriki kwani kitendo cha kushiriki pekee katika shindano hilo na kuingia hatua ya pili ni faida kubwa kwao kwa kuwa watapata fursa ya kujifunza jinsi ya kuaanda mipango ya biashara. 

 “Napenda kuwasihi vijana wote warejeshe fomu zao, wala wasikate tamaa kwani kwa kila atakayefanikiwa kuwa miongoni mwa washiriki 40 watakaoingia katika hatua ya pili, atapata faida kubwa...watapata nafasi ya kujifunza masuala ya biashara kama vile namna ya kuandika mipango ya biashara, utekelezaji na usimamizi wa biashara,” alisema Lusasi. 

Shindano la Mashujaa wa Kesho linaloendeshwa mkoani Mtwara linalenga kuendeleza ujasiriamali kwa vijana mkoani Mtwara linaratibiwa na kampuni ya uchimbaji gesi ya Statoil Tanzania. Washindi watano watapatikana ambapo mshindi wa kwanza atajishindia kitita cha dola za Kimarekani 5,000 na dola 1,000 kwa washindi wengine wanne. Washindi wanatarajia kutangazwa Desemba, 2014.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>