Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA DARAJA LA KIGAMBONI

$
0
0

Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigambonio Bw. Lin Tao kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) akionesha jinsi ambavyo daraja la kigamboni litakavyoonekana baada ya kukamilika. Kulia kwake ni Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Miundombini Bw. Hussein Mativila. Daraja hilo kutoka Kurasini mpaka Kigamboni takribani kilometa moja litakuwa na njia sita kwa ajili ya magari. Daraja hili linajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka kwa Bw Lin Tao (katikati) kulia kwake (mwenye tai nyekundu) ni Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji. Wa kwanza kulia (mwenye suti nyeusi) ni Meneja wa Mradi kutoka NSSF, Bw Karimu Mataka.
Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa daraja la Kigamboni. Mbele yake ni Menaja wa Mradi kutoka Kampuni ya ujenzi wa daraja hilo (CRCEG-MBEC JV)
Moja ya nguzo inayosukwa katikatika ya maji ya bahari huku kukiwa na bomba la pembeni linalotoa maji nje ya eneo linalosukwa nondo na zege kali.
Mhandisi wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Aldelsomond Elthag kutoka Arab Consulting Engineers (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Maduka Kessy (mwenye tai nyekundu), kulia kwake ni Mhandisi Omari Athumani kutoka Tume ya Mipango wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo.

Picha zote na Joyce Mkinga,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>