Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

HEINEKEN YAZINDUA MICHUANO YA FOOSBALL KWA MARA NYINGINE NCHINI TANZANIA

$
0
0
KAMPUNI ya Bia ya Heineken, imezindua msimu wa pili wa kampeni ya michuano ya Foosball kwa nchi za Afrika Mashariki, ambayo itaanza kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa mbalimbali.

Heineken ambao pia ndio wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), imezindua mashindano hayo ambapo yatakua yakiendelea huku mashabiki wakifurahia kuangalia Ligi ya Mabingwa inayoendelea.

Akizingumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe, alisema kuwa wameamua kuzindua mchezo huo baada ya mashabiki kuhamasika zaidi.

Alisema kuwa michuano ya Foosball inafanyika kwa mara ya pili huku Tanzania kwa udhamini wa bia ya Heineken, baada ya kufanya vizuri mwaka jana.

Alisema kuwa michuano hiyo itaendana na mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, inayoendelea ili kuweza kuwaweka mashabiki wa soka pamoja.

"Foosball ambayo inachezwa na mashabiki wengi Ulimwenguni, umekua kati ya michezo inayokua zaidi kila siku na hivyo tumeamua kuzindua tena kampeni hii ili kuendelea kuongeza mashabiki wa soka " alisema.

Alisema kuwa kutokana na mafanikio makubwa waliyopata mwaka jana bia ya Heineken inayotambulika Kimataifa, wameamua kuboresha zaidi mchezo wa Foosball kwa ajili ya kuhakikisha wanafikia malengo.

"Kwa mwaka wa pili mfululizo Heineken inaendesha michuano ya Foosball, baada ya kufanya vizuri msimu uliopita, hivyo tunatarajia mashabiki wa soka wataongeza ufanisi zaidi kwenye msimu huu "alisema.

Alisema kuwa pia katika michuano italayokuwa inafanyika maeneo mbalimbali watakuwa wanagawa zawadi kwa washindi. Taarifa zaidi za kila siku kuhusu mashindano pia zinapatikana katika kurasa za kampuni ya Heineken za facebook ambayo ni www.facebook.com/Heineken na Twitter https://twitter.com/Heineken_TZ
Jina la Eneo
Tarehe  2014
1.      Jackie's
28 Machi
2.      Didi's
29Machi
3.      Corner bar
28 Machi
4.      Hisaje
19 Aprili
5.      Uhuru peak
4Aprili
6.      Samaki samaki city centre
4 Aprili
7.      Frisha's Arena
5Aprili
8.      Nanuku bar
29 Machi
9.      Kisuma
11Aprili
10.  Maisha club
11Aprili
11.  Igosi lounge
12Aprili
12.  Kwetu pazuri
12Aprili
13.  Brazil bar
18 April
14.  Liquid bar and lounge
18Aprili
15.  Catalunya
19Aprili
16.  Amsterdam bar
5 Aprili

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>