Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Silvanus Kigomba akiuliza swali kwa Mzee Philip Mangula wakati wa mkutano huo.Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifafanua zaidi swali la mwandishi huyoMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi huo ambapo amesema CCM ni waumini wa Amani na kwamba katika jimbo la Kalenga hagombei Godfrey Mgimwa bali kinachogombea ni Chama cha Mapinduzi kwani ungekuwa ni ukoo wa mgimwa unagombea basi ungeona akina mgimwa woote wako mbelea wakipiga debe ili washinde lakini kwa sababu ni CCM inagombea ndiyo maana utaona viongozi na wana CCM mbalimbali wakishiriki katika kampeni hizo ili kukipatia ushindi chama chao.Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza nabaadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kabla ya kuelekea Ifunda ambako atapiga kambi huko.