Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

AFYA YAKO: MTINDO BORA WA MAISHA-1

$
0
0
Mtindo bora wa maisha ni upi?

Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia ulaji bora, kufanya mazoezi ya mwili, kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku; kuepuka matumizi ya pombe na kuepuka msongo wa mawazo. Mtindo bora wa maisha ni muhimu katika kuendeleza na kudumisha afya ya mtu na kuzuia maradhi, hususan magonjwa sugu yasiyoambukizwa.

Lishe na ulaji bora

Je, kuwa na hali nzuri ya lishe kunanipa faida gani?

Unapokuwa na hali nzuri ya lishe ina maana kuwa chakula unachokula kimeupatia mwili wako nishati-lishe na virutubisho vyote muhimu ambavyo vinahitajika ili uweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. hii ni pamoja na ukuaji, ukarabati wa seli zilizoharibika au kuzeeka na kuimarisha mfumo wa kinga, ambazo kazi yake ni kuzuia na kukabialiana na maradhi. Hali nzuri ya lishe pia huimarisha mfumo wa akili ikiwa ni pamoja na uwezo wa kufikiria na kukumbuka. Kwa mfano, watoto wanapokuwa na hali nzuri ya lishe ufanisi wao katika masomo huwa mzuri.
Ulaji bora ni nini?
Ulaji bora hutokana na kula chakula chenye mchanganyiko wa angalau chakula kimoja kutoka katika makundi matano ya vyakula. Chakula hicho kinatakiwa kiwe cha kutosha kukidhi mahitaji ya mwili. Ulaji bora unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri, mzunguko wa maisha (mfano; utoto, ujana, uzee), hali ya kifiziolojia (mfano; ujauzito, kunyonyesha), kazi au shughuli na hali ya afya. Ulaji bora huchangia katika kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza maradhi, yakiwemo magonjwa sugu yasioambukizwa. Usikose tena kesho... somo la Mambo ya kukusaidia ili uweze kufanikisha ulaji bora.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>