Msanii Mkali wa Sanaa ya uigizaji kutoka Rocky City Mwanza Masele Malekela amesema kuwa atahakikisha sanaa ya uigizaji Mwanza inasimama na kupendwa na wadau wa sanaa uigizaji almaarufu Filamu kwa sababu umechoka na sanaa ya Mwanza kuonekana si kitu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, Msanii Masele amesema kuwa muda umefika kwa wadau na wapenzi wa filamu kuondoa fikra potovu kwamba wasanii wa Mwanza hawawezi kuigiza muvi nzuri.
Amesema kuwa kumekuwepo na dhana iliyojengeka katika ufahamu ya baadhi ya Wadau kwamba Mwanza hakuna waigizaji wazuri na hivyo kutonunua kazi zao.
Pia ametaja baadhi ya changamoto wanazokutana nazo wasanii wa Mwanza kuwa:
Ø Uchanga wa soko la filamu za Mwanza.
Ø Maeneo ya kufanyia shutingi.
Ø Uelewa mdogo wa Tanzania wa kuamini kila anayefanya sanaa ni Malaya na anakuwa na tabia mbaya.
Ø Sapoti kutoka kwa wadhamini ni ndogo sana hasa hapa jijini Mwanza hivyo inapelekea wasanii wengi wenye vipaji kutoka Mwanza kushindwa kuonesha uwezo wao katika sanaa.
Ø Baadhi ya waongozaji filamu wana tabia mbaya kama kuwataka kimapenzi wasanii wa kike.
Pia ameeleza mafanikio ya ambayo anatarajia kuyapata kuwa ni:
Ø Kuwa msanii mkubwa na kutambulika kimataifa.
Ø Kujenga heshima katika soko la filamu Mwanza.
Ø Kuifanya sanaa kuwa kazi na sio kitu cha ziada kwa msanii.
Ø Kuwainua wasanii wa Mwanza nitakapopata mafaniko kisanaa.
Amewaomba wadau, wapenzi wa Filamu kumkubali na kuwa tayari kupokea Filamu yake Mpya iitwayo RAFAEL ambayo inatarajiwa kuingia sokoni katika sikukuu ya Pasaka.
Kwa yeyote anayemwitaji mpigie kupitia 0767 028400 Zaidi mtazame kupitia www.matukiomedia.blogspot.com