Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ABSALOM KIBANDA, THEOPHIL MAKUNGA NA SAMSON MWIGAMBA WASHINDA KESI YAUCHOCHEZI

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru Meneja Uendelezaji Biashara wa Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Waliarwande Lema amesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa makala iliyoandikwa na Mwigamba na kuchapishwa Tanzania Daima ilikuwa ya uchochezi.
Akizungumza na Kajunason Blog muda mfupi baada ya kuachiliwa huru na mahakama hiyo mmoja wa waliokuwa wakituhumiwa katika kesi hiyo Absalom Kibanda amesema `kesi hiyo itakua ni mwanga kwa wanahabari na fundisho kubwa kwa watu wenye nia ovu ya kukandamiza vyombo vya habari.

"Kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuweza kusikiliza sala zetu, hakika kila kitu ni Mungu ndiye anayepanga... Tumeshinda na sasa tupo huru" anasema Kibanda.

Katika kesi hiyo, Makunga ameshtakiwa pamoja na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda na Mwenyekiti wa zamani wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Kwa pamoja, washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima ikiwa na maneno yanayodaiwa kulenga kuwashawishi wasiwatii viongozi wao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>