Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi DAVID MISIME (SACP) anawashukuru wananchi wa kondoa kwa jinsi walivyotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha kumkamata mwanamke aliyeiba mtoto mchanga wa siku moja tarehe 20.01.2014 huko katika maeneo ya Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
Mtoto huyo wa jinsia ya kiume alizaliwa tarehe 19.01.2014 huko katika zahanati ya Thawi. Mama yake mzazi SALMA S/O ZUBERI, mpare, mkazi wa kijiji cha Mwembeni, Kata ya Changaa - Kondoa, alipatwa na matatizo ambayo yalimlazimu kuhamishiwa katika hospitali ya Wilaya ya Kondoa. Wakati mama huyo akiwa anapatiwa matibabu na daktari alibidi mkwe wake aitwaye HADIJA D/O SAID awe anambeba mtoto huyo mchanga. Alitoka naye nje na ndipo akakutana na AMINA D/O JUMANNE MWASI, 22 Yrs, mkazi wa Mningani, Kondoa mjini, alianza akuongea na nyanya wa kichanga hicho cha siku moja baada ya kuzoeana na mwanamke ambaye alijieleza kuwa amelazwa hapo hospitali kutokana na ujauzito aliomba kumshika au kumpakata mtoto huyo.
Mama mkwe huyo alitoka kwenda kutafuta chakula ili mgonjwa atakapomaliza matibabu aweze kula. Baada ya muda alirudi akashangaa kutokumwona mama ambaye naye alikuwa amejifanya ni mjamzito haonekani, alijaribu kumtafuta maeneo mbalimbali na kuuliza watu mbalimbali bila mafanikio ndipo akaamua kutoa taarifa Polisi.
Kwa vile taarifa zilikuwa zimetolewa maenoe mbalimbali wananchi wema walimtilia mashaka mwanamke aliyeiba mtoto na andipo kwa ushiriano mkubwa baada ya kumfuatilia kwa karibu sana Polisi wakafanikiwa kumtia mbaroni tarehe 29.01.2014 wakati alipompeleka motto huyo hospitali ya Wilaya kwani mtoto alianza kuugua.
Baada ya mahaojiano alikubali kuwa alimuiba mtoto huyo na hata uchunguzi wa kitaalamu umebaini mwanamke huyo hajajifungua siku za karibuni.
Ninatoa wito kwa wananchi kutokuamini watu wasiwafahamu kwa asilimia mia, hata kama wanalugha nzuri kiasi gani pia nawatahadharisha wanawake waliokosa watoto kwa muda mrefu utatuzi wake sio kuiba watoto wa watu wengine.
DAVID MISIME – SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA.