Maelfu waliojitokeza kumzika marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wasanii wakijipanga kumzika marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki'.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' likiwasili makaburini tayari kwa maziko.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete akiwa ni mmoja ya waombolezaji waliojitokeza katika maziko ya msanii huyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam.
Mawasiliano ya hapa na pale.
Waombolezaji waliojotokeza katika maziko ya Msanii Sajuki wakiwa katika utulivu.
Mh. Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akidiliana jambo na wasanii.
Wasanii wakijipanga kupokea wageni.
Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe alikuwa ni miongoni wa waombolezaji waliojitokeza kumzika Marehemu Sajuki.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga kupokea jeneza la Marehemu Sajuki.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Sajuki likiingizwa makaburini.
Mchezaji wa Simba, Juma Kaseja akiingia makaburini pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm, Bwinga (kwanza kulia).
Ilikuwa ni mshike mshike kwa waandishi kila mmoja akitaka kupata picha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akiwa na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa wakati wa maziko ya marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki'.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
Waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki'
Maelfu ya waombolezaji waliojitokeza kumzika marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' leo katika makabiri ya Kisutu jijini Dar es Salaam.---
Awali marehemu Sajuki alipangwa kuzikwa saa tano za asubuhi, lakini ratiba ilibadilishwa na kuzikwa saa saba baada ya swala ya Ijumaa. Mazishi ya Sajuki yalivuta watu na kuwapa majonzi makubwa.
Wasanii wengi walijitokeza kuanzia nyumbani hadi makaburini kwa ajili ya kushiriki mazishi ya msanii huyo ambaye pia amesababisha arobaini ya mchekeshaji maarufu, Hussein Mkiety, Sharomillionea kusitishwa jana na kupangwa kufanyika leo kijijini kwao Lusanga.
Mara baada ya gari lililobeba mwili wa marehemu Sajuki kufika makaburini hapo, mkanyagano ulizidi kuwa mkubwa, hasa baada ya mashabiki kuvamia wakitaka kuubeba mwili huo na kuusindikiza katika nyumba yake ya milele.
Hata hivyo, waliokuwa kwenye jukumu la mipango ya mazishi, walielekea kufanikiwa kuwadhibiti watu hao wenye mapenzi mema na Sajuki, ingawa baadaye hali ilikuwa tofauti kidogo pale msukuamano ulipoibuka kila mmoja akitaka kukaa karibu na kaburi.
Hali hiyo ilisababisha malalamiko kutoka kwa waandishi waliokuwa wakichukua tukio hilo kwa ajili ya kuwahabarisha wadau na mashabiki wa sanaa wa Tanzania, juu ya safari ya mwisho ya msanii Sajuki, aliyefariki Dunia juzi.
Sajuki aliyeacha mke na mtoto mmoja, amefariki juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, huku akifanikiwa kuzikwa na watu mbalimbali, akiwamo rais, wabunge na wasanii wengine maarufu wanaotamba hapa nchini.
Viongozi ambao nao wameshiriki msiba huo ni pamoja na Mwigulu Nchemba, Naibu Katibu Mkuu wa Chama ha Mapinduzi (CCM), Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Ester Bulaya, Mbunge wa Viti Maalumu, Junuary Makamba, Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dkt. Makongoro Mahanga na wengineo.
Marehemu Sajuki alizaliwa mwaka 1986 Songea alipopata elimu ya msingi na sekondari, kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam na kujiunga moja kwa moja katika kundi la Kaole Sanaa Group na kuingia kwenye mchakato wa kutafuta jina kwenye tasnia hiyo.