↧
HAPPY BIRTHDAY BW. JUSTO LYAMUYA
↧
KAMPUNI ZINAZOWAJIBIKA KWA JAMII KUTAMBULIWA MACHI, 2015
Katibu wa Kamati ya Tathmini wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Ernest Mwamwaja (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni zinazowajibika kwa jamii kutambuliwa Machi mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii, Abraham Shempemba na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI mbali mbali zinazotoa huduma kwa jamii zinatarajiwa kutambuliwa na kutolewa tathimini ya uwajibikaji wake machi mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Ushauri wa Biashara, Dickson Hyera alisema lengo ni kurudisha sehemu ya biashara kwa jamii kama sehemu ya shukrani.
Alisema pia italeta faida nyingine ikiwa ni pamoja na kuleta mahusiano mazuri na kampuni nyingine ambapo matoko yatakayotoka yataleta hamasa kwa kampuni nyingine kurudisha sehemu yao ya biashara katika jamii.
Hyera alisema tafiti zinaonesha kuwa kampuni za nje ndo zinahusika zaidi katika jamii hususani katika masuala ya elimu, mindombinu, maji na huduma nyingine za kijamii.
"Tayari kunataasisi nyingine zimeshafanya marejesho hayo na nyingine hazijaleta hivyo nyingine zijitokeze kuonesha nia ya kushiriki ili ziweze kunufaisha jamii," alisema.
Aliongeza kuwa mchakato huo pia unalenga kutathimini kwa kulinganisha takwimu za mirejesho ambayo inafanywa na taasisi kuthaminisha na kung'amua kuhusu manufaa hayo na gharama zake.
Alisema madhumuni makubwa ya tathmini hiyo yanajumuisha kuona jinsi gani taasisi mbalimbali zinazojitoa kwaajili ya kusaidia jamii, kutambua na kuthamini wanaofanya vizuri, jinsi taasisi hizo zinavyochangia kufanya maisha ya wanajamii kuwa bora kwa kuzingatia idadi ya misaada ambayo inatolewa na thamani zake.
Naye Katibu wa Kamati ya Tathmini Ernest Mamwaja alisema kuna watu wananufaika lakini hawajui wamesaidiwa na nani hivyo watajua, pia wanaotoa msaada wanaweza kuleta nguvu katika maeneo ambayo manufaa yake ni makubwa.
Alisema tafiti ambazo zimeonesha kuwa kampuni ambazo zinarejesha kwa jamii zinamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na soko kupanda, hivyo lengo si kuangalia nani mshindi au nani amefanyanini ali ni kwaajili ya manufaa ya watanzania.
Alisema tafiti ambazo zimeonesha kuwa kampuni ambazo zinarejesha kwa jamii zinamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na soko kupanda, hivyo lengo si kuangalia nani mshindi au nani amefanyanini ali ni kwaajili ya manufaa ya watanzania.
↧
↧
KIJIWE CHA UGHAIBUNI
↧
DRFA YAJA KIVINGINE, YAMTAMBULISHA AFISA HABARI MPYA, YAFUNGUA OFISI
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam, Sanifu Kondo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano maalum wa kutambulisha Ofisi mpya ya Chama hicho na kumtambulisha Afisa habari mpya wa Chama hicho, ambaye pia ni Mtangazaji wa Efm, Omary Katanga. Katikati ni Mweka Hazina wa Chama hicho, Ally...(kushoto) ni Benny Kisaka ambaye ni Mjumbe wa DRFA katika mkutano mkuu wa TFF.
Afisa Habari mpya wa DRFA, Omary Katanga, akuzungumza na wanahabari wakati akitambulishwa rasmi katika mkutano huo leo.
---
1.UTANGULIZI
1.UTANGULIZI
Awali ya yote tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha katika ofisi za DRFA, Pamoja na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuona mwaka mpya wa 2015.
Pia tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mkubwa ambao tumekuwa tukiupata kutoka katika tasnia ya habari
2.OFISI YA DRFA
Tunapenda kuchukua fursa hii kuitambulisha kwenu ofisi ya chama cha mpira wa miguu ( DRFA), ambayo uongozi ulijifunga mkanda katika kuhakikisha kuwa tunakuwa na ofisi bora itakayo saidia kufanya shughuli za uendeshaji wa chama kwa ufanisi.
Ni ofisi ambayo tumeijenga kutokana na mgao wa Mapato ambao tumekuwa tukiupata kupitia mechi za ligi kuu zinazochezwa Dar-es- salaam.
3.UTAMBULISHO WA OMARY KATANGA KAMA AFISA HABARI.
DRFA Inapenda kuchukua fursa hii kumtambulisha rasmi mwanahabari Omary Katanga kuwa Afisa Habari wa chama .Wadau tunaomba mumpe ushirikiano wa kutosha katika kuupaisha mpira wa Dar es salaam.
4.KOZI ZA MADAKTARI WA MICHEZO NA UTAWALA.
Kutakuwa na kozi ya madaktari wa michezo ( sport medical) itakayoandaliwa na DRFA Kuanzia tarehe 23/02/2015- 27/02/2015.
Kutakuwa na kozi ya utawara kuanzia tarehe 20/04/2015 – 25/04/2015. Washiriki wa kozi hii watakuwa wajumbe wa kamati ya utendaji wa DRFA maafisa wa michezo wa manispaa watendaji wa vilabu vya ligi kuu vilivyopo DSM.
5.LIGI YA MKOA DAR ES SALAAM
Ligi ya mkoa wa Dar es salaam ambayo inayoshirikisha vilabu 36 inaendelea ambapo sasa timu 18 zitacheza hatua ya mwisho ambayo itatoa wawakilishi wa mkoa wa Dar es salaam katika ligi ya mabigwa wa mikoa ya TFF.
6.LIGI YA WANAWAKE YA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Ligi hiyo inawakilisha timu 9 zilizo kwenye ngazi ya mkoa. Ligi hii ilitakiwa kuanza 16/01/2015 lakini kutokana na kuanza kwa mashindano ya TAIFA ya wanawake busara ilituelekeza kusitisha ligi hiyo mpaka mwanzoni mwa mwezi wa February 2015.
7.PROGRAMU ZA VIJANA
DRFA imekuwa na utaratibu wa kufanya program za soka za vijana ambapo kila wiki ya mwisho wa mwezi tumekuwa na utaratibu wa kukusanya timu za vijana wenye umri wa miaka iliyo chini ya kumi na mbili (11 -12) na kumi na tano (11- 15) na kuzichezesha mechi mbalimbali katika kuhakikisha kuwa vipaji vya vijana hao vinatunzwa na kuendelezwa . Hii ni program endelevu ambayo chama kimeamua kuifanya.
8.UJENZI WA KITUO CHA MICHEZO
Bado DRFA inaendelea na mipango yake ya kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo . Tunaamini tutafanikiwa katika hili hasa pale tutakapopata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali hususani ndugu zetu wanahabari. Tumekuwa tukifanya mawasiliano na ofisi za manispaa juu ya suala hilo la upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya ujenzi huo.
↧
MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU TAKWIMU RASMI
Meneja Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe (katikati) akiwahutubia Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi yaliyofanyika leo mkoani Morogoro. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo na kulia ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Bw. Edward Kaluvya.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukua habari wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Dkt. Frank Mkumbo akiwa katika mahojiano na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro. (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO - MOROGORO)
Na Veronica Kazimoto, Morogoro.
Wito umetolewa kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kutoka vitengo mbalimbali vya Makao Makuu ya Jeshi hilo kuwahimiza maofisa waliopo chini yao kutumia takwimu mbalimbali zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili zisaidie katika kuandaa mipango na kutoa maamuzi mbalimbali ya kazi zinazofanywa na jeshi hilo.
Wito huo umetolewa leo na Meneja Tawala wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Gabriel Madembwe wakati akifungua Mafunzo ya Takwimu Rasmi kwa Maafisa wa Ngazi za Juu wa Jeshi hilo yaliyofanyika katika ukumbi wa Amabilisi uliopo mkoani Morogoro.
Madembwe amesema kuwa maafisa wengi katika Jeshi la Magereza wakijua umuhimu wa matumizi ya takwimu itasaidia kuleta mabadiliko hasa katika kupanga mipango yao kwenye maeneo yao ya kazi.
"Napenda kusisitiza kuwa ili mabadiliko yatokee sehemu yoyote ile; iwe nyumbani, kazini au katika jamii, ni lazima kuwepo na kichocheo cha mabadiliko hayo, hivyo ninyi mtakuwa kiungo muhimu katika kuleta mabadiliko yenye kutoa maamuzi kwa kuzingatia matumizi ya takwimu rasmi", amesema Madembwe.
Nae Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu Dar es Salaam Bw. Edward Kaluvya amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo kwa sasa wamekuwa wakitumia sana takwimu katika maeneo mengi ya kazi zao.
"Mafunzo haya yatatusaidia kujenga uelewa wa pamoja na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na uzalishaji, uhifadhi na utumiaji wa takwimu kwa usahihi katika kutoa maamuzi na kupanga mipango endelevu katika Jeshi letu la Magereza'', amefafanua Kaluvya.
Mafunzo haya ya siku tatu yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo jijini Dar es Salaam na yamefadhiliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupia Mpango Kabambe wa Kitaifa wa Kuboresha na Kuimarisha Takwimu Tanzania (TSMP).
Lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na mfumo imara wa kitaifa wa kuratibu, kukusanya, kuhifadhi na kusambaza takwimu nchini.
↧
↧
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMO KATIKA JUHUDI ZA KUHAKIKISHA UWEPO WA MADAKTARI BINGWA WA FANI MBALI MBALI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo katika juhudi za kuhakikisha uwepo wa madaktari bingwa wa fani mbali mbali wakiwemo wanaohusiana na maradhi ya mfumo wa utoaji wa haja ndogo katika kipindi kifupi kijacho.
Dk. Shein aliyasema hayo huko katika ukumbi wa Hoteli ya Breezes iliyoko Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja, katika mkutano maalum wa wataalamu wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo kutoka Uingereza ambao kwa mwaka huu wameichagua Zanzibar kuwa ni sehemu ya kufanyia mkutano wao.
Mkutano huo pia, umehudhuriwa na madaktari bingwa wa maradhi hayo kutoka Tanzania Bara, Dk. Shein alitoa shukurani kwa Jumuiya hiyo kwa kuamua kufanya mkutano huo hapa Zanzibar huku akieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwapata wataalamu wakiwemo wa maradhi yanayohusiana na haja ndogo na maradhi mengineyo.
Alisema kuwa juhudi za makusudi zimekuwa zikichukuliwa katika kuimarisha sekta ya afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa lengo la kupata Madaktari ili kuongeza utoaji huduma kwa wananchi ambapo kwa hivi sasa Daktari mmoja amekuwa akitibu watu 9,708.
Katika kuhakikisha idadi ya Madaktari inaongezeka Dk. Shein alisema kuwa kwa kupitia Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kukiimarisha Chuo chake cha Madaktari ambacho hivi sasa kina wanafunzi 99 wanaosoma kwa mwaka wa kwanza na wa pili.
Aidha, alisema kuwa Serikali inakiimarisha Chuo chake cha Afya kilichopo Mbweni Zanzibar ambacho kinatarajiwa kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) pamoja na kuhakikisha Hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmmoja inafikia lengo lililowekwa sambamba na ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Mkoani Pemba unaoendelea.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo, kutoa shukurani kwa juhudi zinazochukuliwa na Jumuiya ya Misaada ya Uingereza ya Uimarishaji wa programu za Afya hapa Zanzibar (HIPZ), kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutoa na kuimarisha huduma hizo katika hospitali za Makunduchi na Kivunge. “Natumia fursa hii kutoa shukurani kwa Dk. Ru McDonagh na madakatari wote kwa huduma wanazozitoa katika hospitali hizi....”,alisema Dk. Shein.
Aidha, alisema kuwa kuimarisha huduma za afya ni miongoni mwa vipaumbele vikuu vilivyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika juhudi za kupunguza umasikini katika jamii licha ya baadhi ya changamoto zilizopo ambazo kwa juhudi za pamoja na kwa mashirikiano ya washirika wa maendeleo ufumbuzi wake utapatikana.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza mafanikio yaliopatikana katika kuimarisha sekta ya afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sera katika sekta hiyo huku akieleza azma ya Serikali anayoiongoza kuangalia uwezekano wa kutoa huduma bure za afya kama ilivyotangazwa mara baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa historia ya Zanzibar na hatimae Aprili 26, 1964 ilipojiunga na Tanganiyika na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kutoa historia katika sekta ya afya hapa nchini kabla ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, baada ya Mapinduzi na hatua zinazochukuliwa hivi sasa.
Nao Madaktari bingwa wa maradhi ya mkojo walioshiriki katika mkutano huo wakitoa mada mbali mbali ikiwa ni pamoja na hatua zinazochukuliwa na Jumuiya hiyo kutoka Uingereza ya kitengo cha maradhi ya haja ndogo katika kuyatafutia ufumbuzi maradhi hayo nchini Uingereza sambamba na mafanikio yaliofikiwa.
Aidha, Madaktari hao walieleza historia ya maradhi hayo pamoja na kuonesha juhudi zilizochukuliwa nchini Uingereza tokea miaka ya 1800 pamoja na namna ya kutafuta tiba sambamba kuonesha tafiti mbali mbali zilizofanywa na Madaktari bingwa wa nchi hiyo.
Madaktari hao, walipongeza juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya na kuunga mkono azma ya Serikali katika kuhakikisha wataalamu wa kutosha wa maradhi hayo katika kipindi kifupi kijacho wanapatikana hapa Zanzibar.
Nae Dk. Roger Plail, akitoa neno la shukurani kwa Dk. Shein alieleza kufarajika kwao na uamuzi wa kuja Zanzibar kufanya mkutano huo wa wataalamu kutokana na mashirikiano mazuri yaliopo kati yao na Madaktari wa Zanzibar akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Saleh Mohamed Jidawi pamoja na uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja.
Kwa niaba ya Madaktari hao Dk. Plail alimpongeza Dk. Shein ambaye ni mtaalamu katika fani ya Patholojia, kwa kuwapa maelezo ya kina juu ya sekta ya afya hapa nchini, historia yake pamoja na juhudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha mafanikio zaidi yanapatikana huku wakitoa shukurani kwa mwaliko rasmi aliowapa wa chakula cha mchana hapo kesho (Ijumaa Januari, 22 mwaka huu) Ikulu mjini Zanzibar.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
↧
UFUNGUZI WA MAFUNZO KWA WATOA HUDUMA WA MRADI WA KFW JANA WILAYANI KOROGWE
Picha namba 06534 ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani almaarufu Maji Marefu akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya watoa huduma ya mradi wa KFW waliosajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) yaliyoanza jana kwenye ukumbi wa Mamba wilayani Korogwe.
Washiriki wa mafunzo ya watoa huduma ya mradi wa KFW waliosajiliwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kutoka Halmashauri mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye mafunzo hayo jana yanayofanyika kwenye ukumbi wa Mamba wilayani Korogwe. Picha na Oscar Assenga
NA MWANDISHI WETU, KOROGWE.
ZAIDI ya bilioni 6 zimetumika kuwalipia wakina mama wajawazito na watoto katika vituo mbalimbali vya afya katika mikoa ya Tanga na Mbeya ambao ni wanachama na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kupitia mradi wa (KFW).
Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Benki ya Maendeleo ya watu wa Ujerumani (KFW) ambao unatekelezwa hapa nchini katika mikoa ya Tanga na Mbeya.
Hayo yalibainishwa kwenye ufunguzi wa mafunzo ya watoa huduma wa mradi wa (KFW) juzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Daudi Bunyinyiga ambapo alisema kwa kiasi kikubwa mradi huo umevuka lengo la walengwa waliokusudiwa awali kuandikishwa katika mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) kupitia mradi huo.
Alisema kuwa wakati mradi huo ulipoanzishwa ulitarajiwa kuwahudumia akina mama wajawazito 80, 0000 katika kipindi cha miaka mitatu ya mradi huo wakati mpaka sasa umeandikisha na kuwahudumia akina mama wajawazito 190,631 kwa mikoa ya Tanga na Mbeya hivyo kuvuka lengo kwa asilimia 238.
Bunyinyiga ambaya pia ni Meneja wa Miradi inayosaidiwa na wahisani alisema kuwa kwa mkoa wa Tanga fedha zilizotumika zilizokuwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 958 ambapo mradi huo umeweza pia kutumi kiasi cha shilingi milioni 989.1 kwa ajili ya kununulia vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia, mashine za kutakasia vifaa zilizovyokwisha kugawiwa kwa mikoa ya Tanga na Mbeya.
Akizungumzia kuhusu mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) alisema kuwa Jumla ya Shilingi bilioni 1.5 zimelipwa katika Halmashauri mbalimbali ili kuwaandikisha akina mama hao na familia zao katika mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Alisema kuwa lengo la kuwaandikisha akina mama hao na familia kwenye (CHF) ni kuhakikisha wanapata huduma endelevu baada ya kumalizika kwa muda wa kupata huduma katika mfuko wa Bima ya Afya ambapo huduma hizo ni kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Katibu Tawala wilaya ya Korogwe Stanley Lameck ambaye alimuwakilisha Katibu tawala mkoa wa Tanga,Salum Chima alisema kuwa mpango huo wa KWF kwa mkoa umekuwa na mafanikio makubwa hasa ukizingatia kuwa kundi la walengwa wa awali wanawake na wototo ndio waliokuwa na changamoto kubwa ya huduma za matibabu tangu hatua za mwanzo za ujauzito hadi kujifungua.
Alisema kuwa kupitia mradi huo idadi ya wanawake wanaojifungulia katika vituo vyakutolea huduma imeongezeka kutoka asilimia 48 mwaka 2011 hadi zaidi ya asilimia 60 mwaka 2013.
Hata hiyo alisema kuwa vifo vya wakina mama vinayotokana na matatizo ya uzazi wakati wa kujifungua vimepungua kutoka 110 mwaka 2013 hadi kufikia 69 kwa mwaka 2014 ikiwemo kwa watoto wachanga chini a mwezi mmoja kutoka 275 kwa mwaka 2013 hadi kufikia 206 mwaka 2014.
↧
SHEREHE ZA KILELE CHA MIAKA 50 YA CBE ZAFANA ZAONGOZWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALLY IDD
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema (wa pili kutoka kulia) akiwatambulisha viongozi wa chuo cha CBE kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akipata maelezo kutoka kwa Bi. Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam juu ya namna chuo hicho kinavyowaandaa kuitumia elimu wanayoipata chuoni hapo pindi watakapomaliza masomo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akimuuliza swali Bi. Esther Kibua, mwanafunzi wa mwaka wa 3 wa chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Dar es salaam alipotembelea banda la maonesho la wanafunzi wa Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd akifafanua akifafanua jambo alipotembelea banda la maonesho la Idara ya Mizani na Vipimo la Chuo cha CBE leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya chuo hicho.Kushoto ni Mwalimu wa Idara ya Mizani na Vipimo wa Chuo hicho Bw. Faraja Nyoni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akiwahutubia wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe sherehe za miaka 50 ya CBE leo jijini Dar es salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya uongozi na Menejimenti ya CBE. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Na Aron Msigwa – MAELEZO Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd ameugana na wasomi mbalimbali, viongozi wa Serikali, wanafunzi na wananchi kuadhimisha miaka 50 ya Chuo cha elimu ya Biashara (CBE) tangu kilipoanzishwa mwaka 1965.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo jijini Dar es salam, katika viwanja vya chuo hicho na kutoa fursa ya mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd kutembelea mabanda ya maonesho yaliyokuwepo chuoni hapo ili kujifunza na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi wa chuo hicho.
Akiwahutubia wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo Balozi Idd ametoa Pongezi kwa uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kusimamia viwango vya taaluma zinazotolewa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uhaba wa vyumba vya mihadhara na miundombinu isiyotosheleza mahitaji halisi ya chuo.
Balozi Idd amesema kuwa Serikali itaendelea kukijengea uwezo chuo hicho ili kiweze kukidhi matarajio ya wananchi ya kuendelea kuwa chuo bora kinachozalisha wataalam wa fani mbalimbali huku akiahidi kukisaidia kupata dhamana ya Serikali ili kiweze kukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu yake.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa kuwakaribisha wageni mbalimbali chuoni hapo amesema chuo hicho sasa kinafurahia matunda ya mafanikio ya kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake .
Amesema yapo mabadiliko na maboresho makubwa yaliyofanywa na chuo hicho hasa ongezeko la udahili wa wanafunzi, ongezeko la fani za masomo na kampasi za chuo hicho kutoka 1 iliyokuwepo mwaka 1965 mpaka 4. Zilizopo Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya.
Prof. Mjema ameeleza kuwa chuo cha CBE sasa kinatimiza miaka 50 kikiwa chuo pekee Afrika ya Mashariki na katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kinachotoa wanafunzi wa shahada ya vipimo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1965 na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere , chuo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka kutoka wanafunzi 25 mwaka 1965 hadi 14,000 mwaka 2014.
Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa kozi za masomo na ngazi za mafunzo hadi kufikia shahada, kuongezeka kwa wakufunzi wenye shahada za uzamivu (PhD) chuoni hapo pamoja na chuo kuanzisha ushirikiano wa elimu na vyuo vikuu vingine nje ya nchi kikiwemo Chuo Kikuu cha Eastern Finland katika utoaji wa mafunzo ya shahada za uzamivu kwa kutumia TEKNOHAMA kwa nchi za SADC.
Aidha, katika kuhakikisha chuo hicho kinaendelea kuimarisha ubora wa elimu inayotolewa kwa wanafunzi na kuendana na mahitaji na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea nchini kuanzia mwaka ujao kitaanza kutoa mafunzo ya shahada ya uzamili katika masuala ya Gesi na Petroli.
↧
VIDEO MPYA: Y-TONY FT BARNABA - MAMA
↧
↧
UVCCM ZANZIBAR WAFANYA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO KUUNGA MKONO HOTUBA YA DR.SHEIN






↧
MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO
| ||
Mwanahabari wa Habari leo Iringa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard akitoka kutazama Kimondo |
Mgeni akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya |
Wanahabari wakitoka katika Kimondo kulia na Slvanus Kigomba (ITV) na kulia ni Iren Mwakalinga (TBC),nyuma yao ni ofisi ya makumbusho hayo |
Mhifadhi akionyesha jiko ambalo linatumika eneo hilo |
Nyumba ya wahifadhi wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya |
Mhifadhi msaidizi wa makumbusho ya Kimondo akiingia katika nyumba yake |
Hii ndio nyumba ya mhifadhi mkuu na mhifadhi msaidizi wa Kimondo Mbeya |
Mwanahabari wa ITV Iringa Slvanus Kigomba akijipumzisha kando ya Kimondo |
Mwanahabari wa Star Tv Iringa Mawazo Marembeka kushoto akiwa na mzee wa Matukio Daima katika Kimondo
Wanahabari wakimhoji mhifadhi msaidizi wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya Bw Mussa Nsojo |
Hiki ndicho kimondo kina tani 12 |
Afisa utalii kanda ya kusini Tanapa Bi Risala kabongo akiwa katika kibao cha Kimondo |
↧
UKITAKA JUA RAFIKI WAKWELI, NDUGU WA KWELI, JAMAA WA KWELI, JIRANI WAKWELI, PATA TATIZO
JIFUNZE. Thamani ya mwanadamu huonekana wakati ule akiwa na mchango katika jamii. Aidha kiuchumi, Kimawazo, Nguvu kazi, Kitaaluma na hata Kimichezo. Lakini kile kilichokufanya uwe na thamani punde kinapotoweka, ama potea, Nawe unasahaulika Mara moja.
Wanadamu tuliumbwa na kasumba moja mbaya kabisa. Siku zote tumekuwa tunathamini kilichopo Mbele yetu, na kupuuzia ama kusahau kilichopo nyuma yetu. Kwasababu tu, tunaamini uwepo wa macho mbele yetu, unamaanisha tutazame vya mbele tuu. Tunasahau kuwa tulipewa na uwezo wa kugeuka nyuma pia.
Ndugu, Rafiki, Jirani, Swaiba, Wapenzi, Geuka sasa mtazame alie nyuma yako. Mtazame maskini, omba omba, yatima, mjane, Mlemavu, hata Mgonjwa zaidi ya Mimi alie lala kitandani saa hii kwa maumivu makali asie jiweza, Na yeyote anaenyoosha mkono, wa uhitaji, Geuka na Rudi nyuma kamnyanyue, Muongoze Sehemu sahihi na salama. Na Mungu Atakubariki.
Ikumbukwe kua hata dk 1 ijayo katika maisha yako huwezi bashir nini kitajiri katika maisha yako. Mfano Sekunde zisizo zidi 30 siku napata ajali, Ziliweza nibadili ghafla toka mtu aliyekua akitembea tena kwa majivuno bila maumuvu yeyote, nakua mtu nisie weza japo geuka kitandani pekeangu mpaka sasa. Ninashinda nimelala kwa maumivu makali yakuvunjika Mguu. Sekunde hizo pia ziliweza haribu utekelezaji wa mipango yangu yote ambayo ilikua niwe naendelea itekeleza mpaka sasa, sekunde hizo hizo pia zimeweza nagawa na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki kwanamna tofauti tofauti.
Ikumbukwe kuwa Majengo ya Hospital kwa mwonekano wa nje Kwa mtu asie mgonjwa nimazuri na yana mvuto sana. Lakini punde unapokua na matatizo ya kiafya na kuingizwa mule utakutana na mazazingira mabaya sana yasiyo tamanisha hata kiduchu kuendelea kaa mule, nimateso, uchungu, maumivu hasa unapotizama yanayoendelea kwa wagonjwa waliopo jirani nawe wodini na wenye hali mbaya zaidi yako.
Jifunze kugeuka nyuma na kuwatizama wenye matatizo, na wenye uhitaj kama mimi nilivyo kumbukwa na Wasamaria.
Ni mtazamo wangu, na mawazo yangu tuu. Wala isikupe tabu kama inakugusa.
Nimeamua jaribu weka wazi hili, kwa kuwa kwawkipindi kidogo nilicho kitandani sasa nimeweza jionea napia jifunza mambo mengi sana na hata ambayo sikuwahi fikiri wala yajua kabla. Nimeweza Gundua aina ya marafiki, ndugu, jamaa, watu wangu wa karibu, majirani, na hata watu pia nisio wajua juu ya mchango wao na mwitikio wao katika tatizo langu. Siwezi zungumzia hapa lakini picha yote nayo moyoni mwangu.
Mwisho kabisa napenda kuwashukuru wote walio niokota, nikimbiza hospitali, waliotoa magari yao kunipeleka huku nakule mpaka leo. Wanao niwezesha kiuchumi, walio nikumbuka kupitia mitandao ya kijamii, txt, calls, Maombi na sala na hata walio kuja niona macho kwa macho nawashukuru sana. Nawakumbuka wote hata kama ni wengi napia nathamini nakutambua michango yenu. Sitoasahau kiukweli, pia naomba mzidi niombe nizidi imarika kiafya.
Mwisho kabisa napenda kukwambia mtu wangu, Ukitaka jua rafiki wakweli, ndugu wa kweli, jamaa wa kweli, jirani wakweli. Pata tatizo. Majibu yote utayapata hapo.
↧
DK. JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA UPATANISHI WA CHAMA CHA SPLM YA SUDAN KUSINI, JIJINI ARUSHA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Mhe Cyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, Rais Salva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Yoweri Museveni leo kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mjane wa Mwenyekiti wa Zamani wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng Garang de Mabior Jumatano kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal,, Naibu Rais wa Afrika Kusini, Mhe Cyril Ramaphosa, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Kikwete, Rais Salva Mayardit Kiir, wa Sudani ya Kusini, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Makamu wa Rais wa Zamani wa Sudani ya Kusini Dkt Riek Machar. PICHA NA IKULU
↧
↧
INDABA 2015, A PLATFORM TO OPTIMISE AFRICAN TOURISM BUSINESS GROWTH
South African Tourism CEO, Mr Thulani Nzima: “Every single INDABA element must give exhibitors an unrivalled and effective platform to showcase their products and services, and to do business. INDABA belongs to them”
South African Tourism is working to make sure that INDABA 2015 exceeds the business expectations of both exhibitors and buyers.
South African Tourism Chief Executive Officer, Mr Thulani Nzima says: “INDABA is the single biggest platform for African tourism businesses to come and meet global buyer delegates. This tradeshow attracts the cream and the best cross section of the African tourism and travel trade which in turn, attracts the best buyers in the world to INDABA.”
INDABA 2015 takes place at the Inkosi Albert Luthuli International Convention Centre from 09 to 11 May, 2015.
INDABA Early Bird registrations for exhibitors closed on 30 November 2014. Over 400 exhibitors have confirmed their places on the tradeshow floor. Applications for the INDABA buyer lounge have opened, and registrations are now open for both hosted- and non-hosted buyer applicants. For more information, visit: www.indaba-southafrica.co.za/.
The already very useful online diary system will be refreshed to ensure INDABA 2015 delivers an optimal number of exhibitor and buyer connections. INDABA 2014 saw increased use of the matchmaking system, with 4.4 meetings per participant scheduled as opposed to 3.3 meetings per participant in 2013. In 2015, there will be better matching of exhibitor offerings to the individual business interests of buyers. The system will also incorporate search filters to help exhibitors easily and quickly identify buyers of most relevance to them.
Nzima also says: “Every single element of INDABA will give exhibitors an unrivalled and effective platform to showcase their products and services, and to do business. There would be no INDABA if it were not for the exhibitors, and the larger African and South African travel and tourism trade. INDABA belongs to them. This is the biggest team of African trade exhibitors in the world who come to Durban each year to do business.”
↧
FURAHA YA UTIAJI SAINI MAKUBALIANO YA KUNGANISHA CHAMA CHA SPLM CHA SUDANI KUSINI JIJINI ARUSHA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akikaribisha viongozi na wajumbe katika mkutano huo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo akisoma muhtasari wa mazungumzo hayo.
Sehemu ya ukumbi wa mkutano huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini wa Mhe. Salva Kiir Mayardit
Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt.
Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015
usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana
nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto
jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiongea
Dkt. Riek Machar akiongea
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Bw. Bw. Deng Alor Kuol wakifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini.
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Kikwete na Bw. Dkt Kuol wakipiga makofi wakati Rais Salva Kiir
Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini.
Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini.
Naibu Rais wa Afrika ya Kusini Mhe Cyril Ramaphosa
akiongea na kupongeza hatua iliyofikiwa
akiongea na kupongeza hatua iliyofikiwa
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika
mkutano huo
mkutano huo
Wajumbe wa kundi la SPLM in Opposition(SPLM-IO).
Sehemu ya wajumbe wa kundi
la SPLM in
Opposition (SPLM-IO)
Kila mtu alisimama kumshangilia Rais
Kikwete
Kikwete
Wajumbe wa kundi la SPLM
Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders –
FD)
Furaha kwa kila mtu
Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo akisoma dondoo za makubaliano
Meza kuu katika picha ya pamoja na kundi linalojulikana kama SPLM in Government
(SPLM-IG)
Picha ya pamoja na kundi la SPLM in Opposition(SPLM-IO)
Picha na Sekretareti ya mazungumzo hayo.
Rais Kikwete na Mzee Malecela wakipongezana baada ya kufanikisha mazungumzo na hatimaye makubaliano ya viongozi wa SPLM
Rais Kikwete akishukuru vikundi vya ngoma za utamaduni vilivyokuwapo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kumsindikiza baada ya mkutano wa mafanikio.
MKATABA wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM) ulitiwa saini usiku wa jana, Jumatano, Januari 22, 2015, katika sherehe ya kufana iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Mkataba huo unaojulikana kama Agreement on the Re-unification of Sudan People’s Liberation Movement umepongezwa kuwa ni hatua muhimu katika kulitoa taifa changa la Sudan Kusini katika hali ya machafuko, vita vya wenyewe kwa wenyewe, kutoelewana na kutoaminiana, mambo ambayo yameligubika taifa hilo tokea mwishoni mwa 2013 wakati kutokuelewana kulipozuka ndani ya SPLM na hatimaye katika Serikali ya nchi hiyo.
Baada ya siku nzima ya mawasiliano na majadiliano baina ya pande zinazovutana ndani ya chama hicho pamoja na viongozi wa nchi jirani na rafiki na Sudan Kusini, viongozi watatu wa vikundi vinavyopingana ndani ya SPLM walitia saini Mkataba huo muhimu sana.
Viongozi waliotia saini ni Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition(SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Sherehe hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Wengine walioshuhudia tukio hilo muhimu ni Rais wa Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri Kaguta Museveni; Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya; Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo na Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo.
Mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo yalianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya Rais Kikwete na Chama cha CCM kuombwa na Rais Kiir Mayardit kukubali chama hicho tawala cha Tanzania kutumia uzoefu na ujuzi wake wa miaka mingi wa uongozi na siasa kujaribu kuleta suluhu ndani ya SPLM.
Mazungumzo hayo ya kutafuta suluhu ambayo yamefanyika kwa awamu mbili, ya kwanza yakiwa yamefanyika Oktoba mwaka jana na pili yakiwa yameanza mwanzoni mwa mwezi huu, Januari 2015, yameongeza thamani kwenye mazungumzo mengine yanayofanyika Addis Ababa, Ethiopia chini ya usimamizi wa taasisi ya IGAD na yanayojadili jinsi ya kurejesha amani nchini humo.
Viongozi wa SPLM wanaamini kuwa kwa sababu mgogoro wa kisiasa nchini mwao ulianzia ndani ya chama hicho na kwa sababu SPLM ndicho chombo pekee ambacho kinawaunganisha wananchi wote wa Sudan Kusini, basi busara inaelekeza kuwa suluhu ianze kutafutwa ndani ya chama hicho.
Mkataba wa jana, kimsingi, unalenga kuweka mazingira ya kujenga utulivu, maelewano, amani na umoja wa kudumu ndani ya chama hicho na nchini humo kwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mambo ya msingi yaliyokubaliwa kuhusu shughuli za siasa, uongozi na oganisheni ya chama hicho yanafanyika bila kukawia.
Mkataba huo pia unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinabuni na kutekeleza sera za kuondokana na ukabila, makundi yenye mitazamo finyu na mwenendo wa kijeshi katika siasa za Sudan Kusini.
Aidha, Mkataba huo unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinafanya mageuzi ya kuanza kujenga utamaduni wa kuvumiliana na ujenzi wa misingi ya demokrasia.
Mkataba huo pia unataka watu wote ambao walishiriki katika mauaji na umwagaji damu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wasiruhusiwe kugombea wala kushika nafasi ya uongozi wa umma ndani ya chama hicho.
↧
AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE YA SEKONDARI KITETO MANYARA
Wanafunzi wa shule ya sekondari kiteto wakionyesha vitabu baada ya kukabithiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel chini ya mradi wake wa Airtel shule yetu wenye lengo la kuchangia katika sekta ya elimu nchini.
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepiga jeki jitihada za serikali za kuhamasisha masomo ya sayansi kwa kutoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara.
Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni 1.5 unahusisha vitabu vya fizikia, hisabati, baiolojia na kemia kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma masomo hayo katika shuleni hiyo.
Akipokea msaada huo Diwani wa kata ya Central wilayani Kiteto Mh Yahya Masumbuko, amesema shule nyingi wilayani hapo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu vya masomo ya sayansi licha ya kwamba kuna uhaba pia wa walimu wa masomo hayo.
“Ni kweli kwamba uhaba wa vitabu unakwamisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza kwa ufasaha masomo ya Sayansi wilayani Kiteto hali inayorudisha nyuma ukuaji wa elimu ya sayansi wilayani hapa”. Alisema Mh Masumbuko.
“Uhaba wa vitabu ni moja ya changamoto, lakini uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi pia ni kikwazo kikubwa kwa utoaji wa elimu ya sayansi kwa wanafunzi wetu hapa wilayani” aliongeza Mh Masumbuko.
Aidha Diwani huyo ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel kwa kuona umuhimu wa kuboresha masomo ya sayansi ambayo ufaulu wake umekuwa mdogo hali ambayo inayotoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa umakini zaidi.
“Msaada huu utaongeza hamasa kwa wanafunzi wetu kujifunza masomo ya sayansi hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kuona umuhimu wa kusaidia shule hii na hasa vitabu vya sayansi” alieleza Mh Masumbuko.
“Sisi wa Kiteto tunaendelea na jitihada za kuhakikisha wanafunzi wetu wanajifunza masomo hayo na ndio maana hata mgao wa walimu tulioupata tumeuelekeza katika ufundishaji wa masomo ya Sayansi. Alimalizia Mh Masumbuko.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kiteto wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwawezesha kupata vitabu vitakavyowasaidia katika masomo yao.
Msaada huo wa vitabu vya masomo ya hisabati,kemia,fizikia na Bailojia utasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye shule hiyo ya wilayani Kiteto mkoani Manyara.
Airtel shule yetu ni mpango endelevu uliodumu kwa takribani miaka 10 iliyopita mpaka sasa zaidi ya shule za sekondari 1300 nchini zimeidika na msaada wa vitabu chini ya mradi huu.
Tutaendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunaboresha sekta ya elimu na kutoa kipaombele kwenye masomo ya sayansi ili kuwa na wanasayansi wengi nchi ambao kwa sasa ni changamoto katika shule nyingi na nchi kwa ujumla alisema Meneja mauzo wa Airtel kanda ya kati Bwana Hendrick Bruno
↧
MAHOJIANO NA JHIKOMAN KUHUSU WIMBO WAKE MPYA...AFRICA ARISE
Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania
Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage.
Amezungumza mengi kuuhusu
Karibu usikilize hapa chini
Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja
↧
↧
FRIDA FELIX AWEKA HADHARANI HISTORIA YA MAISHA YAKE KIMUZIKI
Mwanasheria na mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Frida Felix kwa mara ya kwanza aliweza kutua katika ofisi ya Rumafrica baada ya kupata mwaliko na utawala wa ofisi hiyo. Ujio wake ulikuwa ni kwaajili ya kutaka kujua historia fupi ya maisha yake kimuziki.
Katika clip hii kuna mambo mengi sana aliweza kuyaeleza ambayo wewe ukiyasikiliza yatakusaidia sana.
Frida Felix
Frida Felix kwa asilia anatokea Songea ila maisha yake yote yuko Dar es Salaama, na kwa sasa akichukua stashahada (degree) yake ya Uanasheria katika chuo kilichopo maeneo ya Ubungo katika Jengo la Mawasiliano Tower.
Huduma yake ya uimbaji ilianza mara tu alipopata ufahamu kuwa anaweza kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji nikimaanisha akiwa mdogo sana. Frida Felix Frida Felix amezaliwa katika familia ya Wakristo na amekuwa akiishi maisha ya Ukristo tangia akiwa mdogo mpaka sasa yuko ndani ya Ukristo akimtumikia Mungu.
Katika maisha yake ya Ukristo amesema kuna mambo mengi ameyaona yakifanyika katika maisha yake na mpaka leo anaitwa Mwimbaji Frida, na ndio maana anazidi kumtukuza huyu Mungu wetu kwasababu anamtendea yaliyo mema katika maisha yake.
Frida Felix Mwimbaji huyu mbali na uimbaji wake pia ana ndoto kubwa sana kuwa mwigizaji wa kimataifa, hii ni kutokana na kutambua kipaji chake hiki akiwa mdogo sana, ameshawahi kufanya uigizaji akiwa shuleni na alikubalika sana na walimu wake na wanafunzi wake kwa uigizaji mzuri.
Mwimbaji huyu ni mwimbaji wa kipekee sana ukikutana naye na kuongea naye, hasa alivyo na heshima na utii. Malengo yake ya sasa ni kumalizia albamu yake ambayo bado iko jikoni.
Akiongea na Rumafrica amesema anaamini kwa asilimia 100 ujumbe aliopewa na Mungu utafanyika tiba katika maisha yako kama utausikia na kuufanyia kazi. Frida Felix Nisikumalizie uhondo wa historia ya maisha ya mwimbaji huyu mahili Tanzania na Afrika nzima, sasa ninaomba umsikilize akiimba na akielezea historia ya maisha yake.
↧
BUNGE LA TANZANIA KUANZA VIKAO VYAKE JUMANNE JANUARI 27 - FEBRUARI 7, 2015 DODOMA
↧
MFALME WA SAUD ARABIA KING ABDULLAH AFARIKI DUNIA
Marehemu Mfalme Abdullah bin Abdulaziz enzi za uhai wake.
Mfalme Abdullah bin Abdulaziz akiwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
---
MFALME wa Saudi Arabuia, Abdullah bin Abdulaziz amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.
Mfalme Abdullah aklikuwa amelazwa hospitalini kwa matibabu ya maradhi yalikuwa yakimkabili tangu m, wezi Desemba mwaka jana.
Kufuatia kifo chake Mdogo wake aitwaye, Salman, 79, amemrithi katika ufalme huo.
Kifo chake kilithibishwa jana katika matangazo katika televisheni ya taifa ambapo ilikuwa ikitolewa mistari Quran ambayo hutolewa tu endapo kuna kifo cha mtu mzito katika familia ya kifalme.
Mazishi ya Mfalm,e Abdullah yanataraji kufanyika leo kwa kufuata tamaduni za kiislamu ambapo mtu hutakiwa kuzikwa ndani ya saa 24 tangu kifo chake.
Viongozi mbalimbali Duniani akiwemo Rais Barack Obama ametuma salamu za rambi rambi.
↧