Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all 19907 articles
Browse latest View live

KIJANA NAMKUBALI: NCHIMBI

$
0
0
Agness Alinyikira Mwenda:
Kwa kweli shemeji huyu kijana ni mbunifuuuu na anajituma anastahili pongezi.

Fadhili Fabian Ngajilo:
Huyu na Kanumba wanastahili kuenziwa, wamenipa value sanaa, TZ tunaenzi wanasiasa tu, hawa wazalishaji tunawapuuza. Ni tatizo letu la colonial mindset, big up Diamond!

Joseph Mkirikiti:
Anajitambua, anafanya kazi, hana muda wa kujadili mambo ya kushindwa bali anaangalia fursa zilizo mbele yake. Hapigani vita vya kushindwa bali vita vya kushinda. Tupo pamoja.

Juma Homera:
Ni kijana shupavu na mpiganaji halisi anayetumia hekma na busara kufanya mambo yake mwenyezi mungu amjalie inshallah.

Sospeter Yusuph Chambo:
Mh. Vijana wanajituma ila tatizo hapa kwetu Sanaa inachukuliwa kama ni option tu hakuna sapoti ya kutosha hakuna waalimu vifaa vya mziki ghalama, ilitakiwa kuwa na majumba ya Sanaa kila mkoa na wilaya zake.

Joseph Lugakingira:
Mkuu safi Sana, Wachapa Kazi Wote Emmanuel John Nchimbi Kiongozi Asiyependa Makuu Very Humble.

Lida Lugano:
Kijana yuko vizuri kafanya muziki wa Tanzania ujulikane kimataifa zaidi! Big up Diamond usiwasikilize wanaokukatisha tamaa take as a challenge mtangulize Mungu.

YALE YALE: DAR SASA INATISHA SALUNI YA NGONO YAFUMULIWA

$
0
0

MKUTANO MKUU WA SABA WA CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA), JIJINI DAR

$
0
0
 Jaji Fredrick Wambali akitoa mada katika mkutano huo.
 Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.
Wanachama wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), wakiwa kwenye mkutano wao mkuu uliofanyika Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama kutoka mikoa yote.
Na Dotto Mwaibale

JAJI Mkuu Mohamed Chande, amewataka wanawake nchini kutoa taarifa katika ngazi husika pindi  wanapoombwa rushwa ya ngono ili sheria ifuate mkondo wake.

Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa saba wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA), alisema kunaidadi kubwa ya wanawake ndani ya jamii wanaoombwa rushwa ya ngono lakini wamekuwa wahoga kutoa taarifa.

"Katika rushwa ya ngono lazima sheria mahususi zichukuliwe,hivyo tunawasihi wanawake baada ya kufanyiwa matukio hayo wafikishe malalamiko mahakamani au sehemu husika na sheria itafuatwa," alisema Jaji Chande.

Kadhalika, serikali itaendelea kuboresha mazingira ya majaji wanawake ili kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea ndani ya mahakama katika ngazi zote.

Mwenyekiti wa TAWJA, Engera Kileo, alifafanua katika kesi za rushwa ya ngono mahakama kupitia kifungu cha 25,muhusika atakayebainika kujihusisha na kitendo hicho atatozwa faini au adhabu ya kifungo cha miaka 30.

"Mahakama imeweka adhabu hiyo kutokana na ongezeko la matukio  kufanyika ndani ya jamii na wanawake kujengewa woga wa kutoa taarifa kwa wakati, hivyo tunachokifanya kuangalia namna ya kuongeza adhabu kwasababu ngono imetawala katika sekta mbalimbali," alisema Kileo.

Lakini kwa sasa  chama hicho kinatoa elimu juu ya rushwa ya ngono katika jamii na matumizi mabaya ya ngono zembe ili kuwalinda na magonjwa ya kuambukizwa kama Maambukizi ya Ukimwi(VVu), na yale ya zinaa.

MBUNGE ABWAGIWA MTOTO KIKAONI DAR

$
0
0
Hawa Kundani (mwenye vazi jeusi), anayedai kuzaa na kutelekelezwa na mbunge wa Dimani, Abdallah Sharia Ameir, akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kuvamia kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kilichokuwa kikifanyika Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses .

Na Mwandishi Wetu.

Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Hawa Kundani amezua taharuki kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, baada ya kuvamia ghafla na kupiga kelele akidai kutelekezwa na mumewe ambaye ni Mbunge wa Dimani (CCM) visiwani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir.

Tukio hilo la aina yake lilitokea jana kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, na mwanamke huyo akiwa ameongozana na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio, Joyce Kiria aliingia na kusababisha mshtuko kwa wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa dini ya Kikristo waliokuwa wamealikwa hapo. Wakati huo walikuwa wakijadiliana suala la Mahakama ya Kadhi.

Hawa akizungumza na gazeti hili alidai kwamba Ameir ni mume wake walifunga ndoa mkoani Arusha mwaka 1999 na kuzaa naye watoto wanne, lakini mmoja alifariki dunia.

“ Nashangaa amebadilika ghafla amekuwa mtu wa kuoa wanawake na kuacha mara kwa mara, hadi sasa ameshaoa wanawake wanne na kuwaacha mimi nipo tu, alinioa bado mdogo,” alidai Hawa.

Alidai kuwa watoto wengine wawili, mkubwa ana miaka tisa na mwingine miaka sita walichukuliwa na mumewe huyo akawapeleka kulelewa na mwanamke aliyemuoa jambo ambalo alidai linamuuma.

“ Naumia wanangu sijui wanaishi vipi, huyu niliyembeba ni mlemavu, hamtaki amekuwa akininanga kwa maneno mengi sana, mimi nimetoka naye mbali nilibadili dini kwa ajili yake, leo hii ananitesa, hanitaki anipe haki yangu ili niishi mwenyewe,” alisema Hawa.

Kwa upande wa mbunge hiyo Ameir alidai kwamba kesi yao ipo kwenye Mahakama ya Kadhi, akidai kwamba mwanamke huyo amekuwa akimdhalilisha kwa kupitia mtoto huyo mlemavu ambaye alikiri ni mwanaye.

“ Huyu ni mwanangu sishindwi kumhudumia, lakini sitaki fedha ziende kwa huyu mwanamke atazitumia kwa mambo yake mengine, mimi nilimpeleka kwa mama yake mzazi akakae naye huko lakini yeye hataki,” alisema Mbunge Ameir.

Akizungumzia tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes alisema ni tukio ambalo limewafedhehesha kwa kuwa hawakulitarajia.

“Tulivamiwa na wanawake kama wanne na wanaume wawili nafikiri mmoja alikuwa ni mpiga picha, mwanamke mmoja akawa anapiga kelele, tulitaharuki kwa sababu maaskofu walikuwa wameanza kutoa maoni yao,” alisema.

Alisema kwamba waliomba msaada kwa maofisa usalama wa ukumbi na walifika na kuwachukua wahusika hao, kisha kuwapeleka polisi kwa hatua zaidi.

TIMU YA WATAALAM KUTOKA WIZARA YA UCHUKUZI WATEMBEMBELEA KAMPUNI YA KUHUDUMIA MIZIGO, NDEGE NA ABIRIA YA SWISSPORT INAYOTOA HUDUMA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (JNIA) MWISHONI MWA WIKI

$
0
0
 Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, karatasi inayotumika kuonyesha aina za mizigo inayopakiwa kwenye ndege  wakati wataalam hao walipotembelea Kampuni hiyo,  mwishoni mwa wiki kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Meneja wa Huduma za Mizigo, ndege na Abiria wa Swissport, Stella Kitali, akiwaonyesha wataalam kutoka Wizara ya Uchukuzi, ngazi mbalimbali zinazotumika wakati abiria wanaposhuka kutoka kwenye ndege,  wakati wataalam hao waliotembelea Kampuni hiyo,  mwishoni mwa wiki kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 Moja ya magari yanayomilikiwa na Kampuni ya kudumia ndege, abiria na Mizigo ya Swissport, yanayotumika kushusha mizigo kutoka kwenye ndege, kama lilivyokutwa mwishoni mwa wiki wakati wataalam kutoka Wizara ya uchkuzi, walipotembelea kampuni hiyo kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni hiyo kwa ndege mbalimbali zinazotua katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).
 Moja ya magari yanayomilkiwa na kampuni ya kuhudumia mizigo, ndege na abiria ya Swissport, likitumika kuitoa ndege na kuiweka kwenye Barabara ya kiungio (tax way) kabla haijaondoka, kama lilivyokutwa mwishoni mwa wiki.
Ndege za mashirika mbalimbali zinazofanya safari zake kutoka Tanzania kwenda Nchi za nje, zikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Idadi ya abiria wanaowasili na kuondoka katika viwanja vya ndege nchini imeendelea kuongezeka kutoka abiria  2,172, 519  mwaka 2005 hadi abiria  4,670,380  mwaka 2013, sawa na  ongezeko la asilimia 14.8.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

MIGOGORO NDANI YA VYAMA YAIKERA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Hivi Karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la Migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta Taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea katika uchaguzi Mkuu wa nchi.


Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa za usajili.

Hivi sasa mfumo wa demokrasi ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki shughuli za chama.

Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro. 

Mojawapo ya Mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za chama.

Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, kuvisihivyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa.

KISOMO CHA KUMWOMBEA RASHID MKAKILE APONE HARAKA BOSTON, MASSACHUSETTS NCHINI MAREKANI

$
0
0
Ustadh Hemed (mwenye kipaza sauti) akiongoza kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile apone haraka kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015 mjini Boston jimbo la Massachusetts, Rashid Mkakile (hayupo pichani) alipata stroke alipokua kikazi jimboni hapo na kumpelekea kulazwa katika hospitali ya Beth Israel Deaconess Medical Center tangia mwezi wa Oktoba 2014 na baadae kuendelea na mazoezi ya mama cheza (Physical therapy) na kumfanya kuendelea vizuri na kesho Jumapili atarejea Dallas atapokua akindelea na mazoezi ya mama cheza na tunaomba muendelee kumtia kwenye maombi na sala zeni za kila siku. Kulia ni Salum mmoja wa mkazi wa Massachusetts na kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania jimbo hilo ambaye yeye na wenzake walikuwa mstari wa mbele katika kumsaidia Rashid Mkakile na kuhakikisha hayupo peke japo hapo Massachusetts ambapo Mkakile alikuwepo kwa kizazi sio jimbo analoishi.
Watanzania wa Massachusetts wakifanya kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile aendelee kupata nafuu kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015. mjini Boston jimbo la Massachusetts.
Kushooto n Mohammed Mkakile(mdogo wa Rashid), Rashid Mkakile na Eliud Mbowe wakifuatilia kisomo.
Ikota akifuatilia kisomo 
Eddy akitoa shukurani kwa niaba ya Watanzania wa Massachusetts.
Rashid Mkakile akitoa shukurani zake kwa Watanzania wa Massachusetts kwa kuwa karibu nae kwa muda wote tangia siku ya kwanza ya maradhi yake.
Ikota nae akitoa shukurani kwa niaba ya familia ya Rashid Mkakile.
Mayor Mlima akitoa shukurani kwa niaba ya Watanzania wa DMV na Massachusetts.
Watanzania wa Massachusetts na baadhi kutoka Michigan na DMV wakijumuika pamoka kwenye kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile aendelee kupata nafuu na hatimae kupona haraka.
Picha ya pamoja na Mkakile.

UFAHAMU MTANDAO WA MALEZI MAKUZI NA MAENDELEO YA WATOTO WADOGO TANZANIA (TECDEN)

$
0
0
unnamed
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Bruno Ghumpi
---
Mtandao wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Watoto Wadogo Tanzania – TECDEN ni chombo kinachoundwa na mashirikia mbalimbali yanayofanya kazi za kuhudumia watoto wadogo Tanzania. Mtandao huu ulianzishwa mwaka 2000 na kusajiliwa rasmi mwaka 2004.

Makao makuu ya Mtandao huu yapo Jijini Dar es salaam. Hadi kufikia mwaka 2014 Mtandao huu una jumla ya mashirika wanachama wasioungua 200 katika mikoa 14 ya Tanzania bara na Visiwani yanayotoa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.

Lengo kuu la Mtandao ni kuboresha huduma za watoto wadogo Tanzania ili waweze kukua na kufikia utimilifu wao.

Shughuli Kuu za Mtandao ni pamoja na:-

• Kufanya ushawishi na utetezi wa masuala yanayohusu uboreshaji wa huduma na kulinda haki za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na kushawishi maboresho ya sera na kufuatilia utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali inayohusu uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.

• Kuhamasisha jamii na watoa huduma kutambua umuhimu wa kuimarisha na kuwezesha watoto wadogo kupata mahitaji na haki zao za msingi. 

• Kuimarisha mifumo ya upashanaji habari na kuelimishana katika ngazi zote za huduma kwa watoto wadogo. 

• Kutafiti na kutumia matokeo ya utafiti katika kushauri uboreshaji wa huduma kwa watoto wadogo Tanzania.

Dhana ya Malezi Makuzi na Mendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)
Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ni istilahi ya jumla ya programu na vitendo vinavyoandaliwa kuwasaidia watoto (kuanzia mimba, kuzaliwa hadi miaka 8) ili kukua vizuri kimwili, kiakili, kijamii, kihisia, kimaadili na kiroho. Watoto wanahitaji kuchangamshwa katika nyaja na hatua zote za ukuaji, kiakili kwa michezo, kujifunza kuzungumza, kukaa, kutambaa, kutembea na kupatiwa fursa ya kuanza kujifunza mambo mbalimbali pamoja na utamaduni wao.

Utoaji wa huduma jumui za MMMAM.

Huduma hizi hujumuishwa ili kuwawezesha watoto wengi kupata huduma jumuishi za MMMAM zitolewazo na sekta mbali mbali katika mkabala jumui. Huduma hizi zinapaswa kupatikana kuanzia ngazi ya familia ,vituo vya afya ya msingi,vituo vya kulelea watoto mchana, vituo vya Malezi Makuzi ya awali ya mtoto vinavyomilikiwa na Jamii, madarasa ya awali na madarasa ya msingi hususani darasa la kwanza na la pili.

Katika kutekeleza shughuli zake Mtandao wa TECDEN umekuwa ukishirikiana na mashirika mbalimbali ya wabia wa maendeleo ikiwemo shirika la Children in Crossfire kutoka nchini Ireland na shirika la Better Way Foundation kutoka nchini Marekani.

HUYU NA YULE... MAHOJIANO NA DR NA MAMA WILLIAMS

$
0
0
Karibu kwenye mahojiano ya Dr na Mama Williams.

Waasisi wa AHEAD Inc. Taasisi ambayo iliasisiwa mwaka 1985 na inajishughulisha kubadili maisha ya wengi nchini Tanzania kupitia Elimu, Stadi za Maisha, Afya ya Mama na Mtoto na pia kuzisaidia jamii mbalimbali..

Wamezungumzia mengi kuhusu namna walivyofika Tanzania kwa mara ya kwanza 1974. Kilichowapeleka, walivyoamua kubaki huko mpaka sasa, shughuli za Taasisi yao na mengine mengi

Karibu

Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production

Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

JUMATATU NJEMA; TANGA RAHA - TUNU ALIYETUKUKIWA

$
0
0

PICHA YA LEO

$
0
0

UJUMBE WA SIMANZI WA WAUZA ‘UNGA’ CHINA

$
0
0
Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Godfrey Nzowa.

Na Mwandishi Wetu, Gazeti la Mwananchi.

Magareza mbalimbali ya China, Hong Kong na Macau yamefurika Watanzania wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Wanakuja kwa makundi. Wake kwa waume, vijana kwa wazee, wenye elimu na historia tofauti za kimaisha... lakini kilichowaleta China, Hong Kong na Macau ni kimoja tu; biashara ya dawa za kulevya.

Hawa ni zaidi ya Watanzania 130 ambao wamefungwa katika magereza mbalimbali kwenye nchi za China, Hong Kong na Macau.

Ingawa wanadai kupata mlo mzuri, mahali pazuri pa kulala na fursa kadhaa katika magereza, lakini bado wamekosa kitu kimoja muhimu duniani; uhuru.

Faraja wanayoitegemea ni ya Mchungaji John Wootherspoon, raia wa Australia anayeishi China ambaye amepata kibali cha kutembelea magereza mbalimbali.

Wafungwa wa Kitanzania wapo katika magereza mbalimbali kama Shek Pik, Stanley, Loo Woo na Macau.

Fursa ya kukutana na wafungwa ilikuwa ndicho chanzo cha Wootherspoon kuona kuwa kuna idadi kubwa ya Watanzania katika magereza kuliko hata idadi ya wazawa wenyewe.

“Kila mwezi Watanzania wanne hadi sita walikuwa wakiingia magerezani na wengine wengi wakiwa rumande kwa makosa mbalimbali,” anasema

Wootherspoon ana kazi moja kubwa katika magereza hayo, ambayo ni kuwafariji kwa neno la Mungu.

“Ninapata nafasi ya kukaa nao kila siku na ninapowasikiliza, nimegundua kuwa wanajuta na wametumiwa tu na watu wenye ufahamu na biashara hiyo,” anasema

Wootherspoon, ambaye yupo nchini kwa sasa, anasema kuwa anachotaka ni kuwakataza vijana wengine kwenda China kwa kusafirisha dawa za kulevya.

Ujumbe wa majonzi kwa ndugu za wafungwa

Baada ya kuona hali imekuwa mbaya, Wootherspoon aliamua kuja Tanzania ili angalau awasaidie wafungwa hao kuwasiliana na familia zao. Kitabu maalum kidogo kilitayarishwa kwa kila mfungwa kuandika ujumbe kwa baba, mama, dada, kaka mume au mke. Ilikuwa ni lazima kila mfungwa aweke namba ya simu ili ujumbe uwafikie walengwa kule waliko. Januari Mosi, 2015, mchungaji huyo anatua na ujumbe huo katika ardhi ya Tanzania.

Haikuwa kazi rahisi kwa ndugu na jamaa za wafungwa hao kupokea ujumbe huo katika hali ya kawaida.

Siku ya kwanza, familia ya mfungwa wa kike ambaye alijifungua mtoto wa kiume akiwa gerezani, anafikishiwa na ujumbe.

Akibubujikwa machozi mama wa mfungwa huyo anasema hajawahi kudhani kuwa binti yake anaweza kusafirisha dawa za kulevya.
“Aliniaga kuwa anasafiri kibiashara kwa sababu alikuwa na duka la viatu, lakini katu sikudhani anayafanya hayo,” anaeleza mama huyo. Mzazi huyo, ambaye haikuwa rahisi kumbembeleza, anasema kuwa binti yake mwenye umri wa miaka 30 tu alikuwa ndiyo nguzo ya familia.

Msichana huyo ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 14 kwenye gereza la Loo Woo, China, ameiacha familia yake ikigubikwa na umaskini wa hali ya juu.

“Ameniachia watoto wawili, sina kazi wala biashara, watoto wanahitaji kusoma,” anasema
Ujumbe mwingine mrefu kutoka kwa mfungwa mwingine Hong Kong ulimfikia mama yake ambaye sambamba na umaskini, anaishi na Virusi vya Ukimwi.

“Mama najua unaumwa na nimekuachia mtoto, nisamehe sana lakini uniombee. Nilifanya hivi ili tuondokane na umaskini,” anasema katika ujumbe wa binti huyo kwa mama yake.
Mama wa mfungwa anaposoma ujumbe huo naye anaangua kilio mithili ya msiba.

“Amefungwa miaka yote hiyo, acheni nilie unadhani hadi atakapoachiwa nitakuwa hai?” analia mama huyo.

Kila mfungwa ana hadithi yake ya kimaisha lakini ilibainika kuwa wengi wanafanya hivyo kwa sababu za umaskini.

Kwa mfano, mfungwa mmoja aliandika ujumbe kwa mama yake, lakini akimweleza kuwa hali yake ya kiafya si nzuri kwani anaumwa.

Wootherspoon anamweleza mama wa mfungwa huyo kuwa binti yake amelazwa kwa wiki tatu na hali yake si nzuri.

Wafungwa wengine ni wasomi

Ujumbe mwingine kutoka kwa mfungwa mwanaume ulitumwa kwa mke wake. Yeye, katika ujumbe huo, anatubu kwa mke wake kuwa amefanya kosa lililomgharimu uhuru wake na furaha ya kukaa na familia yake. Mke wa mfungwa huyo baada ya kusoma ujumbe huo anaeleza kuwa anashangazwa na uamuzi wa mume wake kufanya biashara hiyo wakati ni msomi mwenye shahada.

“Ameniachia watoto watatu, wote wanataka ada za shule, wanataka kula, kuvaa. Yaani ninaishi maisha magumu mno hadi nafanya vibarua,” anasema.

Ujumbe mwingine wa matumaini unatoka kwa kijana wa miaka 27 ambaye anakiri kuwa aliwahi kukanywa na wazazi asifanye hivyo lakini alikaidi kwa kuwa mara ya kwanza alipofanya hivyo nchini Italia, alifanikiwa.

“Baba ulinikataza, lakini niliona itakuwa kazi rahisi kama nilivyofanya mwanzo. Nakupenda sana na mniombee nitoke salama. Msiwe na wasiwasi mimi mzima wa afya,” ameandika mfungwa huyo katika ujumbe aliotuma kwa baba yake.

Waliobeba mimba kama mbinu ya kusafirisha ‘unga’

Katika ujumbe huu kutoka China, Hong Kong na Macau, ndipo ilipobainika kuwa baadhi ya wasichana walitumia mbinu ya kubeba ujauzito ili kusafirisha kirahisi dawa za kulevya.
Mbinu hiyo ilifanyika hivi...

Baada ya mimba kufikisha miezi minne au mitano, ndipo msichana humeza kete za dawa za kulevya.

Kwa kuwa kipimo cha kujua iwapo mtu amemeza kete za dawa za kulevya ni X Ray, na wajawazito hawapimwi kwa njia ya mionzi, wanawake hao hupita bila kukaguliwa.

Hata hivyo wafungwa hao hawakujua kuwa mbinu hiyo hujulikana katika nchi nyingine, hali iliyosababisha wakamatwe.

Mjamzito anaweza kumeza kete hadi 30 na baadaye huzitoa kwa njia ya haja kubwa.

Lakini akiwa njiani hatakiwi kula chochote ili kuepuka kuzitoa kete hizo kwa njia ya kinywa au haja kubwa.

Kamishna wa polisi wa Kitengo cha Dawa za Kulevya, SACP Godfrey Nzowa anasema hapa nchini wapo raia wa kigeni ambao walitumia njia hiyo, lakini walikamatwa .

Nzowa anasema wanawake hao baadhi wameshazaa watoto ingawa mmoja wa watoto waliozaliwa amepata mtindio wa ubongo.

Alibeba ‘unga’ ili apate fedha ya matibabu ya mtoto

Baadhi ya wafungwa imebainika kuwa hushawishika kubeba dawa za kulevya kutokana na hali mbaya ya kiuchumi waliyonayo.

Kwa mfano ujumbe wa mfungwa mwingine unaeleza kuwa, aliamua kukubaliana na magwiji wa kuuza dawa za kulevya ili tu apate fedha za matibabu ya moyo ya mtoto wake nchini India.

“...Mtu mmoja ambaye ni rafiki yangu wa karibu alisema anataka anisaidie kwa njia hiyo, kwa hiyo akanipeleka kwa (jina linahifadhiwa), na akaniambia nikiufikisha Hong Kong nitapata Sh 25milioni...nikajua nikifanya hivyo nitapata milioni 11 ninazotakiwa kulipa ili binti yangu aende Apollo,” unasema ujumbe huo.

Haikuwa rahisi kwa mke wa mfungwa huyu kusoma ujumbe mrefu kutoka kwa mume wake.

Kabla hata hajaelezwa kuhusu hali ya mume wake, alianza kulia na baada ya kuusoma anaangusha kilio zaidi.

Licha ya kujuta na kueleza hisia zao, wengi walionyesha kukumbuka mila na tamaduni zetu kama vile vyakula, muziki wa kizazi kipya na muziki wa dini.

Wanauza chakula gerezani kujipatia fedha

Baadhi ya wafungwa wa Tanzania katika magereza hizo wanasoma na wengine kuuza chakula ili kujipatia kipato.

Ili kujipatia fedha wameamua kuuza mlo wao wa mchana wanaogawiwa gerezani hapo kwa raia Hong Kong au China na wazungu.

Kwa kawaida katika magereza hayo, kuna milo mitatu, asubuhi, mchana na usiku hivyo wafungwa wa kike huuza mlo wa mchana kwa wafungwa wenzao ambao hawatosheki na sahani moja huuzwa kwa Dola 2 ya Hong Kong ambayo ni sawa na Sh 3,460.

“Hapa magereza tunakula mara tatu kwa siku, lakini ili kujipatia fedha tunawauzia chakula chetu mara nyingi cha mchana wafungwa wengine ambao wanaona chakula wanachopewa ni kidogo na hakiwatoshi,” alisema mfungwa mmoja kupitia barua aliyoituma.

Watanzania hao wanazitumia fedha hizo kununulia vitu vidogo vidogo kama sigara, mafuta ya kujipaka na baadhi wanazihifadhi na kuwatumia ndugu zao nchini.

Wootherspoon anasema wanaofanya biashara ya chakula gerezani wengi ni wafungwa wa kike na wakati wafungwa wanaume wao huuza chakula chao mara chache.

“Chakula chao mara nyingi ni wali na kipapatio cha kuku, au makaroni na kunde, lakini mara nyingi wafungwa hao huuza mlo wao wa mchana,” anasema Wootherspoon.

Wafungwa hao wanaeleza zaidi kuwa siku za sikukuu kama Christmass, wanapewa wali na mapaja ya kuku.

Wafungwa wanaonunua chakula hupata fedha zinazoingizwa kwenye akaunti ya magereza na ndugu zao.

Fedha inakuja kwa jina la mfungwa anayenunua chakula na baadaye mchakato hufanywa wa kuzihamisha kwenda kwenye akaunti ya mfungwa anayeuza.

Pamoja na kuuza chakula, wafungwa hao wengi wanasoma masomo mbalimbali ikiwemo, lugha za Kiingereza, Kichina, kutengeneza viatu, kushona, kutengeneza kompyuta na ufugaji.

Akizungumza kuhusu maisha ya wafungwa hao magerezani Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ali, anasema uamuzi wao wa kusoma ni jambo jema hasa wakati wanapokuwa kwenye wakati mgumu kama walio nao.

“Kama wanasoma wanafanya jambo zuri badala ya kutoka gerezani wakiwa hawana chochote,” anasema

USIMHUKUMU MTU YEYOTE… SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE

$
0
0
Daktari aliingia hospitalini kwa haraka sana baada ya kuitwa kwa shughuli ya Upasuaji wa haraka, alipokea simu haraka, na kuvaa nguo za kazi na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha upasuaji.

Wakati akielekea kwenye chumba cha upasuaji alimkuta Baba wa mtoto anazunguka huku na huku karibu na chumba hicho akimsubiria Daktari.

Baada ya kumuona tu, Baba mtoto akapayuka: “ Kwanini umechelewa kuja? Hufahamu kama maisha ya Mtoto wangu yapo hatarini? Hivi unayajua majukumu yako?”

Yule Daktari alitabasamu na kumwambia: “ Samahani sana, Sikuwa Karibu na Hospitali na nimejitahidi kuja kwa haraka sana baada ya kupokea simu kutoka hapa hospitalini… Na kwakuwa nimeshafika ningekuomba upunguze jazba na hasira ili nifanye shughuli yangu” “Punguza hasira?!

Hivi ingekuwaje kama Mwanao ndiye angekuwa chumba cha upasuaji sasa hivi, ungeweza kupunguza hasira? Kama mwanao ndiye angekuwa anakufa sasa hivi ungefanyaje?” Yule Baba aliongea kwa hasira sana.

Yule Daktari alitabasamu tena na kumjibu: “Daktari hawezi kurefusha maisha ya Binadamu. Nenda katulie na umuombee mwanao, sisi tutajitahidi kadri kwa uwezo tulionao kwa Baraka za Mwenyezi Mungu”

“Kutoa Ushauri kwa vitu visivyo wahusu ni rahisi sana” Alinong’ona yule Baba mwenye mtoto.

Upasuaji ulifanyika kwa masaa kadhaa mara tu baada ya kumalizika Daktari alitoka akiwa anafuraha, “Asante Mungu! Mtoto wako amepona!” Kama una swali lolote utamuuliza Nurse!!” Bila ya kumsubiri Baba Mwenye mtoto kujibu chochote aliondoka kwa haraka kwenye eneo la upasuaji.

“ Kwa nini ni mkorofi sana huyu Daktari? Yaani hawezi hata kusubiri kidogo nimuulize maendeleo ya mwanangu” Baba wa mtoto alimjadili akiwa na nurse baada ya Daktar kuondoka.

Nurse akamjibu, huku akitokwa na machozi:
“Mtoto wake alifariki jana kwenye ajali ya gari, alikuwa katika mazishi ya mtoto wake wakati tunampigia simu aje Hospitali kwa ajili ya upasuaji wa mtoto wako. 

Amefanikiwa kuyaokoa maisha ya mtoto wako, kwahiyo ameondoka kuwahi mazishi ya mtoto wake.”

HEKIMA:
1. “USIMHUKUMU MTU YEYOTE…. SABABU HUYAJUI MAISHA YAKE NA KIPI
KILICHOMKUTA KWENYE MAISHA YAKE.

SARAHA - TANESCO

$
0
0

CXC AFRIKA YAMPIGA TAFU SIBOKA

$
0
0
Msanii wa nyimbo za asili Tanzania Engele Yange anatarajia kurekodi nyimbo yake jijini Mwanza katika Ziwa Victoria ili kuendeleza kutangaza utalii wa nchi. Nyange atakuwa na kundi lake Mjini Mwanza kwa wiki mbili ya mwezi huu.

Yange ni ameimba nyimbo nne za makabila manane ya Kikerewe,Kihaya,Kijita.Kisukumapamoja  na   Kikulya.

Katika Mkoa wa Mara aliimba katika video kwa kabila la wajita video hizo ni mbili zitaanza kuruka mapema Februari  mwaka  huu.

Siboka(mfalme)ameushukuru Uongozi wote wa CXC AFRIKA LTD. Unavyotoa misaada mbalimbali kwa wasanii wa hapa nchini Kupitia Mkurugenzi Wao  Charles Hamkah.

TUTAKUKUMBUKA DAIMA MZEE WETU, JAMAL SINGOI

$
0
0
Ilikuwa ni tarehe 20.1.2011 majira ya saa 3 asubuhi siku ya Alhamis, marehemu baba yetu mpendwa Jamal Singoi ulivuta pumzi ya mwisho ukiwa mikononi mwangu..nakumbuka kama imetokea jana... siwezi kuandika mengi kwani huenda nikamkufuru mwenyezi Mungu ambaye alinipa bahati ya kipekee kuwa na mzazi kama wewe na zaidi kukupa uhai wa kuniona nikikua na ukapata nafasi ya kuwaona wajukuu zako ambao ilikuwa ndoto yako kuwaona... 

Namshukuru Mungu kwa kunipa bahati ya kipekee kuwa nawe akichukua pumzi yako ya mwisho... anyway a thousand words wont bring you back neither with a million tears because we have cried... your always in our mind and forever in our heart. We miss you everyday of our lives. 

Pumzika kwa Amani till we meet again... R.I.P comrade Jamal Singoi.

BARAZA LA WATUMIAJI HUDUMA SUMATRA LASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA MIAKA 40 YA CHUO CHA NIT JIJINI DAR

$
0
0
Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri  akitoa maeklezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange (kulia) wakati alipotembelea banda la SUMATRA katika maonesho ya kuazimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa chupo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) kwenye viwanja vya chuo hicho jana. Kushoto ni Afisa wa Baraza hilo la Sumatra, Doatha Kabyemela.
Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Monica Mwamunyange (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Usafirishaji  (NIT) Mhandisi Priscilla Chilipweli baada ya kupokea maelezo ya kina na yanayoeleweka ipasavyo kuhusu shughuli za baraza hilo kutoka kwa  Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri.
Maafisa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, wakitoa elimu kwa wananchi.
 Wananchi wakipata elimu katika baraza hilo.
 Maafisa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, wakitoa elimu kwa wananchi.
 Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akielezea takwimu za utafiti uliofanywa na baraza.
Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akitoa elimu kwa vijana.

DORIS MOLLEL KATIKA UZINDUZI WA BWENI LA KWANZA KWA WATOTO WA JAMII YA HADZABE, SINGIDA

$
0
0
Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati alipohudhuria kwenye hafla ya ufunguzi wa bweni jipya maalum kwa watoto wa jamiii ya hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilaya ya Mkarama mkoani Singida. Uzinduzi wa bweni hili ni matunda ya jitihada za Serikali ya wilaya hiyo na mkoa wa Singida kuwahamasisha watoto hao kuhudhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya Ndg Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (Wa kwanza kushto).
Mlezi wa watoto wa jamii ya Hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilayani Mkarama mkoani Singida akimpongeza Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel baada ya kumteua kuwa ‘balozi wa elimu’ wa watoto wa jamii ya Hadzabe kwenye shule hiyo. Doris ambaye ni Miss Singida na Kanda ya Kati 2014/15 alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na mkuu wa Wilaya Ndg. Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk. Paseko Kone (mwenye suti nyeusi).
Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akikabidhi Blanketi kwa watoto wa jamii ya Hadzabe waliojengewa Bweni na Serikali ya Wilaya na Mkoa wa singida katika shule ya msingi Munguli Wilayani Mkarama ikiwa ni jitihada za Serikali kuwahamasisha kuduhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Akishuhudia tukio hilo ni Dk. Paseko Kone, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

AJIRA ZA VIJANA WANAOAJIRIWA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZAONGEZEKA

$
0
0
Ofisa Habari wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kassim Nyaki (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu Msaidizi, Idara ya Ajira Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Malimi Muya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitoa taarifa kuhusu kuongezeka kwa vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa umma. Kushoto ni Ofisa Habari, Kassim Nyaki.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale.

SERIKALI imesema ajira za vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa Umma imeongeza kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2010-2014 huku wanawake wakionesha kuongoza.

katika hatua nyingine serikali  inatarajia kuajiri vijana 7,210 nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015-2016.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi  Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma     Umma, Malimi Muya, alisema nafasi za ajira 7,210 zimetengwa kwa  ajili ya vijana wa kitanzania.

"Tunatarajia kuongeza ubunifu na ufanisi mkubwa katika sekretarieti ya ajira kwa sababu tunaamini vijana wana uzoefu wa kutumia  vifaa vya teknohama," alisema

" Takwimu zinaonesha kunaongezeko la ajira kwa vijana wanaoajiriwa katika utumishi wa umma kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2010-2014 huku wanawake wakiongoza.

Tangu Sekretarieti ya ajira kuanza mchakato wa ajira katika Utumishi wa umma tumepokea jumla ya maombi ya kazi 191,844 kati ya hayo waliyoita kwenye usahili walikuwa waombaji 71,124.

"Hadi kufikia Desemba 2014 jumla ya waombaji kazi 12,858 walipangiwa vituo vya kazi na kati ya hao wanaume walikuwa 7,598 sawa na asilimia 59.1,wanawake walikuwa 5,260 sawa na asilimia 40.9," alisema Muya.

Katika waajiriwa 12,858 waliopamgiwa vituo vya kazi vijana wenye umri wa miaka 26-30 walikuwa 6,346 sawa na asilimia 49.5 kwa msingi huo ndani ya miaka mitatu utumishi wa umma umeajili vijana mwenye ongezeko la asilimia 57.5,"alisema.

Muya alifafanua kuwa idadi ya wanawake walioajiliwa katika utumishi wa umma imekuwa ikiongezeka kutoka mwaka hadi mwaka.

"Mwaka 2010 wanawake walioajiliwa katika sekretarieti ya ajira walikuwa  aslimia 27.7 wakati mwaka 2013-2014  wanawake walifika 49.4 hili ni sawa na ongezeko la asilimia 41.1 wakati wanaume wakiwa na ongezeko la asilimia 27.9,"alisema.

Katibu msaidizi huyo,alitoa rai kwa wanafunzi  kuyapenda masomo ya sayansi ili kusaidia tumme kupata watalamu wa sayansi kwani tume inauhaba mkubwa wa watalamu wasayansi.

"Tumme inauhaba wa watalamu wa sayansi kama vile wahandisi wa petroli,watalaam wa mifugo,wahandisi wa kilimo na wengine wengi,"alisema.

Aidha katibu huyo alisema aliotuma maombi ya kazi na kufanyiwa usahili Desemba 2014 tangazo la kupangiwa vituo vya kazi litatolewa kabla ya mwisho wa mwezi Januari kuisha.

ZAINABU 'IKOTA' MHAMILA ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

$
0
0
Zainabu 'Ikota' mhamila 'Super D' akiwa katika pozi uku akiwa na keki yake
Zainabu 'Ikota' mhamila 'Super D' akiwa katika picha ya pamoja na rafiki zake siku ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa
Zainabu 'IKOTA' Mhamila kushoto akimlisha keki mama yake mzazi Asha Kamnyanga wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika juzi nyumbani kwao buguruni Lozana.
Zainabu 'Ikota' mhamila 'Super D' akiwa katika pozi.
Viewing all 19907 articles
Browse latest View live