DAKTARI wa meno Anord Rimo umri wa miaka kati ya 30 hadi 40 wa hospitali ya Sabasaba manispaa ya Morogoro amekutwa amejinyonga katika nyumba ya kulala wageni ya Camel iliopo Kihonda mjini hapa.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 22 saa 10 alfajiri katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
Kamanda huyo alisema kuwa Daktari huyo alikuwa amepanga katika nyumba hiyo ya kulala wageni kwenye chumba namba 2 na kwamba alikutwa amejinyonga dirishani kwa kutumia foronya za mto pamoja na taulo.
Alisema kuwa usiku wa kuamikia siku hiyo marehemu huyo alikwenda katika sehemu ya mapokezi ya nyumba hiyo ya kualala wageni na kufanya fujo zilizokuwa huku akionyesha sehemu zake za siri kuwa hazifanyi kazi.
Kamanda huyo alisema kuwa marahemu huyo alikuwa peke yake katika chumba hicho na haikufahamika mara moja anaishi wapi hku chanzo cha kujinyonga kwake bado hakujajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi zaidi.
Wakati huo huo msichana Dorosia Michael (15) alifariki dunia Mei 17 mwaka huu huko eneo la Sultani manispaa ya Morogoro baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge.
Kamanda Shilogile alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 17 mwaka huu huko Sultani nyumbani kwa Masud Ramadhani ambako msichana huyo alikuwa akifanya kazi.
Alisema kuwa chanzo cha kujinyonga msichana huyo bado hakijajulikana na polisi wanaendela na uchunguzi zaidi huku wakisubiri taarifa za madaktani juu ya uvumi uliopo kuwa msichana huyo kabla ya kujinyonga alibakwa.