Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto) na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (wa pili kutoka kulia) wakizindua huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sunil Colaso. Na Mpigapicha Wetu.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine wanaofuatia ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sunil Colaso na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo. Na Mpiga picha Wetu.
---
• Wateja kupata kifurushi cha dakika 25 kupiga simu kwenda India
• Ofa hii inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki,
Kampuni ya Bharti (“Airtel”) inayoongeza kwa kutoa huduma za
mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza uzinduzi wa ofa itakayowawezesha wateja wa Airtel Tanzania kupiga simu kwenda nje kwa gharam nafuu zaidi.
Ofa hii inaendelea kuonyesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kuendelea
kuwanganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano na kuwapa huduma bora zenye gharama nafuu. Uzinduzi huu unafatia utambulsho wa huduma kabambe ya Airtel yatosha iliyofanyika week chache zilizopita.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwn. Sunil Colaso alisema ”baada ya uzinduzi wa mafanikio ya huduma yetu ya Airtel yatosha. leo tunazindua ofa ya mawasiliano ya gharama nafuu na kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia
,marafiki na washirika wa kibiashara walioko nje ya mipaka ya nchi.
Kwa kiasi cha chini cha hadi shilingi3, 000 sasa wateja wa Airtel
wanaweza kupiga simu India masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Ofa hii
itampatia mteja dakika 25 za muda wamaongezi kwa muda wa wiki nzima.
Aliongeza “Hii ni ya kwanza kutoka Airtel, na tunaendelea kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima huduma bora, za uhakika na
gharama nafuu za mawasiliano wakati wote. Tumesikiliza kile wateja
wetu wanachokitaka na kutengeneza ofa inayokidhi mahitaji yao hivyo
tutaendelea kutekeleza dhamira kwa watanzania ya kuleta huduma zenye ubunifu, bora na gharama nafuu ambazo kwa uhakika zitaleta uhuru wa kuongea nje ya mipaka. Ofa hii itawawezesha wateja wanaosafiri au kuwasiliana na India iwe kimasomo, kibiashara , wanaotembelea India kimatibabu kuwa na mawasiliano na familia zao kwa gharama za kiushindani zilizo nafuu zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo wa kuleta mapinduzi ya mawasiliano katika soko la Tanzania.