Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Zantel, Bi Awaichi Mawalla, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya Bonus Balaa, Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Zantel, Zanzibar-Mohamed Mussa.
---
Ofa mpya inayotolewa kwa wateja wa Zantel, ya Bonus Balaa, ambayo inawawezesha kupata muda wa maongezi mara mbili ya salio waliloweka kwenye simu zao, imepongezwa na wateja wao kwa kuwasaidia kupunguza gharama za mawasiliano.
---
Ofa mpya inayotolewa kwa wateja wa Zantel, ya Bonus Balaa, ambayo inawawezesha kupata muda wa maongezi mara mbili ya salio waliloweka kwenye simu zao, imepongezwa na wateja wao kwa kuwasaidia kupunguza gharama za mawasiliano.
Wateja wengi wameonyesha kufurahia huduma hiyo, ambayo, kiupekee kabisa pia inawawezesha wateja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa salio hilo la ziada.
‘Gharama za maisha zimekuwa juu sana, lakini bado mahitaji ya mawasiliano, iwe kikazi au kifamilia yamezidi kuongezeka, hivyo tunashukuru kampuni ya Zantel kwa ofa hii ya kipekee’ anasema Aman Mgaya, mmoja wa wateja wa Zantel, Zanzibar.
Muda huo wa maongezi, ambao ni sawa sawa na ongezeko la aslimia mia moja, ambalo wateja wa Zantel watapata baada ya kuongeza muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi, utatumika ndani ya siku thelathini.
‘Tumeweka siku thelathini ili mteja wetu atumie pesa yake pale tu atakapojisikia kufanya hivyo na sio kumlazimisha atumie ndani ya siku moja kama ofa nyingine’ alisitiza Afsa Biashara Mkuu wa kampuni hiyo, Bwana Sajid Khan.
Wakati huo huo, wateja wa mtandao wa Zantel Zanzibar wameanza kujishindia zawadi katika promosheni kubwa ya ‘Kwangua na Ushinde’ inayoendelea kisiwani humo.
Katika promosheni hiyo ambayo mshindi wake atajinyakulia gari, huku wateja wengine wakijishindia zawadi za kila siku kama muda wa maongezi wenye thamani ya shilingi milioni moja, pikipiki aina ya Vespa, komputa ndogo (Huawei Media pads) pamoja na modemu za 3G.
Ili kushiriki katika promosheni hiyo, wateja wapya na wale wa zamani wa Zantel wanapaswa kuweka muda wa maongezi wa kuanzia shilingi elfu moja au zaidi ili kuingia kwenye droo hiyo.