Hali ndivyo ilivyo mpaka sasa japo juhudi za uokoaji zinaendelea. Jengo lilikuwa la ghorofa 16, na kwenda chini zilikuwa ni ghorofa 3.
Umati wa watu ukiwa umefurika eneo la tukio.
Jengo moja la ghorofa 16 lilipo jirani na msikiti wa Shia katika mtaa wa idra ghand, jijini la Dar es salaam, limeporomoka leo majira ya saa mbili na nusu asubuhi.
Mpaka sasa watu wapatao 17 wameokolewa huku wawili wakiwa wamepoteza maisha, na juhudi za ziada zinaendelea kufanywa ili kuokoa wengine wengi waliofukiwa na kifusi hicho.
Mkuu wa mkoa wa jiji la Dar es Salaam, Mh. Said Meck Sadick pamoja na viongozi wengine mbalimbali wapo bado eneo la tukio hivi sasa akishirikiana na wadau wengine wa vyombo mbali mbali vya Ulinzi na Usalama, kuhakikisha uokoaji unafanyika kwa wakati. Ambapo Jeshi la kujenga taifa limewaleta vijana wapatao 150 kusaidia shughuli za uokoaji.
Chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo hakijafahamika mpaka sasa, kwani kila mtu yupo kwenye hekaheka za uokoaji.
Majira ya saa saba mchana rais Jakaya Kikwete alitembelea eneo la tukio na kuwapa pole wafiwa.