Nimegundua adui wa maendeleo kwa sisi wanaume ambao ni single ni Wanawake, nasema hivi kwasababu nina mifano hai na limenitokea mimi binafsi nimekuja kungundua hili late japo sasa ninaweza kujipanga upya,
unakuta unajitolea kwa msichana ups and down ukimsaidia au kusaidiana kwa namna fulani ili sikumoja mtimize ndoto zenu.
LakinI mwishowe mnaishia kiajabu ajabu tu na kinachoumiza zaidi ni pale mwenzio anapokuchukulia kama buzi bila kujali unachomtendea au kukumbuka kuwa mnasafari ndefu kati yenu inauma sana unapokuja kugundua haya, tena unakuta mtu huyo huyo anafanya kazi lakini hujawahi kuona hata senti tano yake au zawadi hata yakusingizia toka kwake lakini chaajabu wewe mwanaume unajituma hata saa nyingine unajinyima sana ilimradi tu kumfurahisha mwenzio bila kujali apatacho au kipato chake, najua pia kuna wanawake wanatumiwa na wanaume lakini janga hili linatukumba sisi wanaume tulio wengi kuliko wao. Sasa basi kwa vijana wenzangu tuache kulea tujipange na kile kidogo tupatacho ili tujenge maisha yetu kwanza na ndiyo mengine yafuate.
Kwasababu unajitolea sana kwa mtu hadi unasahau kuinvest mwishowe unakuja kushtuka kuvuta shuka kumesha kucha wakati mwenzio hawazi wala kujali kuhusu wewe anajali kula bata kuvaa vizuri kifupi anajali maisha yake tu! mwishowe unapoachwa unabaki na maumivu na kulipiza visasi kwa wengine ambao hawakustahili eti kisa ulitendwa.
Nachokiona maisha bado yapo na yanaendelea ila tukumbuke tu! unapokosea na ukagundua ulipokosea basi tayari huo ugonjwa umeshagundulika na tiba yake ipo, pia tusilipize visasi kwakutendwa na mmoja bali tusonge mbele kwa kumuweka muumba wetu mbele kwa kila tufanyayo kwani na yeye atatubariki, natamani kuandika kwa kirefu sana lakini nisikuchoshe bali naamini kijana mwenzangu nimekukumbusha kitu siku hii ya leo.
Jiulize,Tafakari na chukua hatua!
Mungu atuongoze sote single meeeeeeeen!