Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

JK AKUTANA NA WAKONGWE WA MUZIKI IKULU

$
0
0
Mwanamuziki Mkongwe kutoka bendi ya The Kilimanjaro Band a.k.a Wananjenje,Waziri Ally akizungumza jambo na Rais Kikwete Ikulu mapema leo walipokwenda kumpongeza kutokana moyo wake mkunjufu aliounesha kwa kuwajali wasanii wa aina zote
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Desemba 21, 2012 amepokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaaam kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.
Pichani kulia ni Rais Kikwete akipokea maneno ya sukurani kutoka kwa Mwanamuziki Mkongwe wa bendi ya The Kilimanjaro Band a.k.a Wananjenje kwa niaba ya wasanii wa filamu na wanamuziki waliofika Ikulu leo,jijini dar.
Mwanamuziki Mkongwe wa bendi ya The Capital Mzee King Kikiii akipeana mkono na Rais Jakaya Kikwete huku baadhi ya wanasanii wa filamu na muziki wakishuhudia tukio hilo mapema leo,wakati wasanii hao walipokwenda kumpongeza Rais kwa kuwajali.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wasanii wa Filamu na wanamuziki wakongwe mapema leo Ikulu jijini Dar,walipokwenda kumpongeza Rais kwa kuwajali. PICHA NA IKULU.
---
Serikali imeanza kutoa Nishani kwa wasanii kwa vile inatambua umuhimu wao katika jamii.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wawakilishi wa sanaa mbalimbali nchini waliofika Ikulu leo asubuhi kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kuwatambua na kuwapa heshima kubwa ya Tuzo na Nishani wasanii katika siku ya sherehe za Uhuru za tarehe 9 Disemba, Ikulu, Dar-Es-Salaam.

“Tumetoa Nishani kwa vile wasanii wanatoa mchango mkubwa, tumeanza kutoa nishani mwaka huu na tutaendelea kutoa miaka ijayo kwani kwa kuitambua sanaa, mnawapa moyo wasanii kuendelea kujituma na kuwa wabunifu zaidi” Rais amesema na kuongeza, “Tumeingiza Nishani ya Wasanii na Watafiti maana nao wanafanya kazi kubwa sana ya kutafiti mazao na mbegu mbalimbali ambazo zinaongeza tija katika kilimo nchini”.

Katika kumbukumbu ya kusherehekea miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara mwaka huu, Rais Kikwete alitunuku nishani kwa makundi mbalimbali ya watu waliotoa mchango mkubwa katika jamii na waliotumikia taifa kwa uadilifu.

Rais alitoa Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mara ya kwanza kwa wasanii nchini ambapo Bi. Fatma Baraka Khamis (Bi Kidude) kupitia Baraza la Sanaa Zanzibar, Kiongozi wa Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo, Kiongozi wa Zamani wa Bendi ya Dar Intrenational Marehemu Marijan Rajab walipata tuzo hiyo.

Wengine ni Msanii wa maigizo na filamu nchini Marehemu Fundi Said (Mzee Kipara) na Mwanariadha mkongwe John Steven Akwari.

Rais amewataka wasanii kushirikiana na serikali lakini pia wawe mstari wa mbele katika kupigania haki zao na sio kusubiri serikali tu iwafanyie hivyo.

Wasanii hao wamefika Ikulu wakiongozwa na Bw. Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group.

Wengine ni Addo Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Injili, Bw. Juma Ubao Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania (CHAMUDATA), aliyewakilishwa na Hamza Kalala.

Bibi Shakila Said, Mkongwe wa Muziki wa Taarab Nchini, Bi Carola Kinasha Msanii wa Muziki , Mzee King Kiki msanii wa Muziki wa Dansi Mwana FA, msanii wa Kizazi Kipya na Bw. Waziri Ally , msanii wa Muziki.

Wawakilishi hao pia wamemshukuru Rais kwa msaada wa hali na mali anaotoa kwa wasanii mbalimbali wanapopata matatizo ambao hivi sasa wapo katika hatua mbalimbali za matibabu ya afya zao hapa nchini na nchi za Nje.

“Haya mengine ninayafanya tukama wajibu wa kibinadamu kwa vile nina nafasi ya kufanya hivyo na pale tunapokua na uwezo tunasaidia kama binadamu wenzetu” Rais Amesema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles