Napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia maandalizi mema ya mwaka mpya. Mungu atupe nguvu na neema zaidi katika mwaka 2013.
Mwaka 2012 tutaukumbuka kwa mengi yapo mema na mabaya. Naomba nikuombe radhi wewe kwa lolote ambalo niliwahi kukukosea, nawe kama ulinikosea sina tatizo nawe tangu sasa. Pia naomba nitoe shukrani zangu kwa wote waliohusika katika mafanikio yangu ya kimuziki. Naamini wengi mlikuwa mstari wa mbele katika kunishauri, kunipongeza na hata kunikosoa nilipokosea.
Shukrani nyingi ziwafikie radio presenter, Dj's, Radio na TV zote Tanzania na Afrika naamini bila nyinyi kuzicheza nyimbo zangu basi nisingefika hapa.
Waandaaji wa magazeti mlikuwa mstari wa mbele katika kuona nafika mbali kwa kuandika habari zangu na kufika hata vjijini. Nachukua fursa kuwashukuru pia. Blogs mbalimbali. Mlikuwa mstari wa mbele kwa kuandika habari na kupost hata baadhi ya show zangu ambazo mmenipa heshima ya kufika mbali zaidi na kusikika hata nje ya nchi mchango wenu ni mkubwa japo siwezi kuwataja wote.
Pia Requester wa media sina cha kuwalipa nawashkuru sana sana na nitabaki kuwaheshmu kwani mmetoa mchango mkubwa sana kwa kuomba nyimbo zangu media na zikachezwa na amini ni mchango mkubwa sana katika game hasa kwetu wasanii nitabaki kuwaheshimu na kuwathamini siku zote. Bila kuwasahau wasanii wenzangu walikuwa nami bega kwa bega kunishauri na kunisaidia kwa chochote. Pia ma dj wa club mbalimbali, mmekuwa chachu ya mziki wangu pale mlipoonesha ushirikiann wenu kwangu. Pia Waandaaji wa (show) matamasha madogo na makubwa nawashukuru sana kwa kuniamini na kukubali kufanya kazi na pamoja nami.
Siwasahau maproducers wa video na Audio na studio mbalimbali kwa kunifanyia kazi za uhakika na jamii ikanikubali kwa kazi hzo. Wote kwa pamoja naamini sasa ni kama ndugu. Nawaomba muonyeshe tena moyo huo na mwaka ujao 2013 na mingine kwani kaz nzur ni yenye kushirikiana. Msisite kama ntawakosea naomba msisite kunikanya na kunisamehe. Napenda wote na kuwajali.
Nawatakia mwaka mpya.
Ni mimi. Dayna Nyange (mkali wao)