Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania Taifa 2012/13 wakipitia kwa umakini majarida yanayo elezea Utalii Tanzania
---
Serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii,imeendesha semina ya washiriki wa Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo Katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.
Serikali kupitia Bodi ya Taifa ya Utalii,imeendesha semina ya washiriki wa Fainali za Taifa Miss Utalii Tanzania 2012/13 iliyo fanyika leo Katika ukumbi wa mikutano uliopo Makao makuu ya Bodi ya utalii Tanzania.
Akifungua Semina hiyo Ndugu Devotha mdachi pamoja na kuwakaribisha washiriki wote makao makuu ya Bodi ya Utalii Tanzania aliwaasa washiriki hao kujifunza na kuvielewa kwa kina vivutio vya utalii Tanzania ili wale watakao shinda na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia waweze kuitangaza vema Utalii wa Tanzania na nchi kwa Ujumla.
Nae mtoa mada Mkuu katika semina hiyo Ndugu Deogratias Malogo ambaye ni Meneja wa Utafiti na Maendeleo wa Bodi ya Utalii Tanzania aliwafahimisha warembo wa Miss Utalii Tanzania wa Fainali za Taifa 2012/13 kuwa secta ya utalii ni secta muhimu katika Uchumi na kuchangia pato la Taifa kila mwaka. Alisema Secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 20 ya pato la Taifa kila mwaka na zaidi ya asilimia 25 ya pato la taifa la fedha za kigeni kila Mwaka. Alisema Kidunia secta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 12 ya ajira zote Duniani.
Warembo hao walifundishwa Historia ya utalii Tanzania . Walifundishwa vivutio vya utalii Tanzania, Mbinu za kutangaza utalii wa Tanzania Kitaifa na Kimataifa, lakini aliwaelezea pia jitihada ambazo serikali kupitia bodi ya taifa ya utalii na Mamlaka nyengine za utalii nchini imekuwa ikifanya katika kukuza secta ya utalii na kutangaza vivutio vya utalii kitaifa na Kimataifa.
Nae Rais wa Miss Utalii Tanzania alitoa shukurani na Pongezi kwa Bodi ya Utalii Tanzania kwa juhudi kubwa wanazo fanya ya kuinua na kuendeleza secta ya utalii nchini. Alipongeza na kushukuru pia hatua ya bodi ya utalii, kwa kuendesha Semina Maalum kwa washiriki wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 na kusema kwamba semina hii itakuwa ni Dira na ufunguo kwa Miss Utalii Tanzania wa kutwaa mataji zaidi ya Dunia katika mashindano yote watakayo shiriki na pia katika kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani Kitaifa na Kimataifa.