Je asali inafaida gani kiafya?
Asali hutumika sio tu kama chakula bali baadhi ya watu hutumia pia kama dawa. Asali ina uwezo wa kuondoa chembe chembe haribifu mwilini na hivyo kuulinda mwili dhidi ya maradhi mbali mbali.
Asali ina virutubishi mbali mbali ikiwa ni pamoja na vitamin, madini na protini kwa kiasi kidogo. Vile vile asali ina sukari nyingi ambayo ni asilimia themanini(80%.
Kutokana na asali kuwa na sukari nyingi, asali ina nishati-lishe nyingi kama ilivyo sukari, hivyo ikitumika kwa wingi huongeza uzito wa mwili.
Asali iliyokomaa kwa kawaida ina kiasi kidogocha maji, chini ya asilimia ishirini (20%). Asali iliyoongezwa maji ina chacha mapema(inaharibika) na inaota ukungu (fangasi), ambao wakati mwingine hauonekani kwa macho.
Kwa kawaida asali iliyokomaa na isiyochanganywa majiikihifadhiwa vizuri haiharibiki kwa miaka mingi, bila hata ya kuweka kwenye jokofu.
Kiasili, asali ilikuwa ikitumika kwa sababu maalumuna kiasi kidogo tu, hivyo hatari ya kumwongezea mtu uzito haikuwepo. Mara nyingi mtu anayetumia asali alikuwa anatumia kijiko kimoja au viwili kwa siku na sio kila siku.
Hata hivyo, kumekuwa na imani potofu kwamba asali uweza kupunguza uzito wa mwili na hivyo husababisha walengwa kutumia sasli kwa wingi, hii si kweli .
Ikumbukwe kwamba asali inanishati-lishe kwa wingi ambayo huchangia kuongeza uzito wa mwili hivyo huweza kuleta madhara iwapo itatumika kupita kiasi.