Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la nchi ya Ujerumani akipokea zawadi ya picha yenye vinyago kutoka kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Taarishi mara baara ya kufanya naye mazungumza wakati waziri huyo alipotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya dunia ya Utalii ya ITB yanayofanyika katika jengo la Mense Berlin jijini Berlin nchini Ujerumani Bodi ya Utalii Tanzania TTB inaongoza ujumbe wa makampuni zaidi ya 43 ya utalii yanayoshiriki katika maonyesho hayo leo.Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Taarishi wakati alipofanya mazungumza naye katika banda la Tanzania katika maonyesho ya utalii ya ITB yanayoendelea jijini Berlin Ujerumani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Taarishi kushoto akizungumza na Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani wakati alipotembelea banda la Tanzania kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki na wa pili ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula. Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Dirk Viebel Waziri wa Uchumi, Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani baada ya kuwasili katika banda la Tanzania. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Taarishi akiagana na Dirk Viebel Waziri wa Uchumi , Ushirikiano na Maendeleo wa Shirikisho la Ujerumani baada ya kufanya naye mazungumzo katika banda la Tanzania.Baadhi ya Wafanyakazi wa wa Taasisi mbalimbali serikali zinazofanya kazi ya utalii nchini Tanzania wakiwa katika maonyesho hayo tayari kwa kazi ya kupokea na kutoa maelezo kwa wageni mbalimbali wanaotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya ITB yanayofanyika Jengo la Mense Berlin nchini Ujerumani.
↧