
-Historia yake.
Samuel John Sitta alizaliwa Desemba 18, 1942 huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora. Sitta alisoma Shule ya Msingi Urambo kati ya mwaka 1950 – 1953, kisha alikwenda Wilaya ya Sikonge mwaka 1954 - 1957 na kuendelea na masomo ya “Middle School” katika shule ya “Sikonge Middle School”. Baadaye mwaka 1958 – 1963 alianza masomo ya sekondari Shule ya Wavulana Tabora yaani “Tabora Boys” kidato cha I – IV na cha V – VI.
Mara tu baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Sitta alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kusomea Shahada ya Sheria (L LB) mwaka 1964,Mwaka 1965 Rais wa Serikali ya wanafunzi UDSM na kuhitimu mwaka 1971.
Baadaye mwaka 1976 Sitta aliamua kujiendeleza kielimu katika masuala ya Usimamizi nchini Uswisi kwenye Chuo Kikuu cha IMEDE ambako alihitimu Stashahada ya Juu ya Usimamizi mwaka huohuo 1976.
Chini ya mfumo wa chama kimoja na Mpaka sasa Mfumo wa vyama vingi , Sitta amekuwa kiongozi wa juu serikali aliyebahatika kuwepo kufanya kazi na Marais wa awamu zote tangu ya kwanza ya Hayati Baba wa Taifa mpaka ya sasa awamu ya nne ya Mh.Jakaya Kikwete,Sitta akiwa mbunge Miaka 30 Mpaka sasa 2015, mkuu wa mikoa ya Iringa na Kilimanjaro 1987-1993 na Waziri wa Ujenzi ,Waziri Ustawishaji Makao Makuu na Waziri wa Katiba na Sheria 1978 -1995 katika nyakati tofauti na ameendelea kuwa mbunge Urambo Mashariki miaka 30: 1975-1995 ,2005-2010 Spika wa Bunge la Tisa na waziri wa Afrika Mashariki 2010,Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba 2014 Waziri wa Uchukuzi 2015.
MAFANIKIO.
(a)-Ujenzi wa Salender Bridge 1980
-Uwanja wa Ndege wa J.K.Nyerere, Dares Salaam 1981
-Ujenzi wa Daraja la Kirumi -Mara 1982
- Ujenzi wa Barabara ya Morogoro -Dodoma 1983
-Ujenzi wa Barabara ya Makambako -Songea 1984.
(b)-Sheria zilizoanzisha mashirika ya Reli,Bandari, Ndege, baada ya Jumuiya ya EAC kuvunjika 1977.
(c) -Akiwa Spika wa Bunge la Tisa 2005-2010 alisimamia mkutano mkuu wa Kwanza nchini wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola.
-Alikuwa Rais wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola 2009.
-Spika aliyesimamia mabadiliko makubwa ya kanuni yaliyoimarisha Uhuru na demokrasia ya Bunge 2005-2010.
MBIO ZA URAIS
Samuel John Sitta alianza mbio za urais “kimyakimya” tangu alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa (2005 – 2010).
Hata alipoliongoza Bunge la Katiba mwaka 2014, mara nyingi Sitta alionekana kama mtu mwenye shauku kubwa na urais na alipohojiwa, mara kwa mara, juu ya urais alionyesha ana ndoto hizo. Mara kadhaa, alilalamika kuwa wala rushwa wakubwa wanampiga vita kwa sababu ni msafi pia mwenye uzoefu na Taifa letu la Tanzania ktk nyanja ya Uongozi .
Nguvu yake
Sitta ni kiongozi mwajibikaji kwa namna moja. Majukumu mengi ambayo amekuwa akipewa anayasimamia hadi mwisho bila kujali athari zake. Alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa alisimamia mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa Bunge jambo ambalo lilimpa sifa kubwa.
Na hata anapokabidhiwa mamlaka ya uwaziri amekuwa mtu anayethubutu bila kuogopa na uthubutu hakuuanza majuzi; aliuanza enzi zile za Mwalimu Nyerere miaka ya 1965 alipokuwa Rais wa Umoja wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Sitta ni kiongozi mzoefu na ni mmoja wa watu waliopata kufanya kazi na marais wote wanne waliopata kuongoza Tanzania. Chini ya Nyerere na Mwinyi amekuwa Waziri wa Maendeleo, Waziri wa Kazi na Waziri wa Katiba na Sheria. Wakati wa Mkapa aliteuliwa kuongoza Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wakati wa Kikwete ameshikilia Nyadhifa nyingi zaidi Spika wa Bunge la Tisa 2005-2010,Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki 2010-2015,Mwenyekiti wa Bunge la Katiba 2014,Waziri wa Uchukuzi 2015. Huu ni uzoefu wa kujivunia kwa mtu anayetaka kuongoza nchi.
Moja ya mambo yanayoweza kumbeba Sitta katika kupenya mchujo wa CCM ni kukijua chama chake vizuri. Sitta ni mmoja wa vijana wa zamani waliokulia ndani ya TANU kadi yake alichukua mwaka 1960 na baadaye CCM na amepata uzoefu wa kutosha katika awamu zote nne za uongozi wa nchi jambo linalomfanya awe kwenye nafasi ya kujua changamoto za taifa na labda namna ya kuzitatua.
Pia, kwa kiasi kikubwa utendaji wake haujaambatana na kelele za kashfa kwenye maeneo mengi alikopita.
Kama CCM inahitaji wagombea wasio na kashfa za fedha za umma Sitta anaweza kuwa mmoja wao.
Kundi la Sitta ndani ya CCM katika kusaka urais halina nguvu kubwa, si kati ya makundi yanayosigana kweli kweli. Hali hiyo inamfanya abakie kama chaguo rahisi la kuikoa CCM ikiwa chama hicho kitazikimbia kambi kubwa za urais zilizo ndani ya yake lakini kikahitaji mtu mwenye uzoefu mkubwa. Jambo hili likitokea litaweza kumbeba Sitta.
Hakika, Sitta ana sifa mchanganyiko sana, ni kiongozi thabiti, anayethubutu, mchapakazi, mwadilifu, mtata na mwenye malengo makubwa ya utumishi wa kisiasa na Taifa kiujumla.
Kila la kheri Viwango na Kasi Chuma Cha Pua S.S Mh.Samuel John Sitta.
Imeandaliwa na James Rock Mwakibinga (Mwandishi).