Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (pili kulia) akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binilith Mahenge msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Afisa Usalama na Mazingira wa Airtel, Mazoya Ncheye (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Julius Ningu msaada wa moja ya fulana zilizotolewa na Airtel Tanzania, kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Juni 1-5 mwaka huu, mkoani Tanga, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa pili kushoto) na (kulia) ni Meneja Uthibiti wa Airtel, Calvin Simba
---
ASILIMIA 61 ya ardhi nchini imeharibika kutokana uharibifu wa mazingira ya ardhi katika vyanzo vya mbalimbali na kusababisha kuzama kwa baadhi ya viziwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Mhandisi Binith Mahenge wakati akitangaza maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yatakayofanyika Juni 5 mwaka huu mkoani Tanga.
Mahenge amesema Juni 5 ya kila mwaka iliamuliwa na Umoja wa Mataifa
mwaka 1972 kuwa Siku ya mazingira duniani kutokana na kuonekana baadhi ya vyanzo vinapotea kutokana na uchafuzi mazingira.
mwaka 1972 kuwa Siku ya mazingira duniani kutokana na kuonekana baadhi ya vyanzo vinapotea kutokana na uchafuzi mazingira.
Amesema mikoa ambayo imekuwa kame kutokana na uharibifu wa mazingira ni Dodoma, Shinyanga, Geita, Singida, Simiyu na Kilimanjaro huku kasi ya ukataji miti ikiwa inaongezeka na kufikia hekta 400, 000 kupotea kila mwaka nchini.
Waziri huyo ameunga mkono kwa Kampuni ya simu za mikononi Airtel
kuungana kuadhimisha siku ya mazingira kwa kuchangia kutoa elimu kwa
njia ujumbe mfupi.
kuungana kuadhimisha siku ya mazingira kwa kuchangia kutoa elimu kwa
njia ujumbe mfupi.
Afisa Mawasiliano na Matukio wa Airtel,Dangio Kaniki,amesema watatoa ujumbe mfupi kwa ajili ya kutoa elimu kwa katika kuhamasisha utuzaji wa mazingira na kutaka makampuni mengine yajitokeze kuunga juhudu za utuzaji wa mazingira.
Dangio,amesema ujumbe mfupi wataotoa katika utuzaji wa mazingira katika maadhimisho hayo ni zaidi ya Sh.milioni 90 ambazo Airtel ingepata kutokana na kutuma ujumbe huo.