Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19902

MWANAMUZIKI WA ITALY MWENYE ASILI YA TANZANIA, CHANTAL SAROLDI KUTUMBUIZA HOTELI YA MEDITERRANEO MEI 30, 2015 JIJINI DAR

$
0
0
Mwanamuziki Chantal Saroldi muitaliano mwenye asili ya Tanzania (kushoto), akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Mei 28, 2015. Kulia ni Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto.
 Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Sccoto (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, kuhusu tamasha la muziki litakalofanyika hoteli ya Mediterraneo iliyopo Kawe, jijini Dar es Salaam ambapo mwanamuziki huyo atatoa burudani.
Mkurugenzi wa hoteli ya Mediterraneo ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Samantar Abdinur Lusuf (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni  mwanamuziki Chantal Saroldi  na mmoja wa wakurugenzi wa hoteli hiyo, Alas Abdinur.
 Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Sccoto (wa pili kulia), akiwa meza kuu na mwanamuziki huyo. Kulia ni mpiga kinanda wa mwanamuziki huyo Gianluca Tagliazucchi na wakurugenzi wa hoteli hiyo waandaaji wa tamasha hilo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mkurugenzi wa hoteli ya Mediterraneo ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Samantar Abdinur Lusuf (wa pili kulia), akimuaga Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Sccoto mra baada ya mkutano kumalizika.

Picha na  Cathbert Kajuna/Habari na Dotto Mwaibale.

Mwanamuziki wa miondoko ya Jazz kutoka nchini Italia Mwenye asili ya Tanzania Chantal Saroldi anataraji kutumbuiza  katika hafla maalumu ya kusherehekea Siku ya Taifa la Italia ambapo raia wa Italia waishio nchini  watajumuika pamoja kwenye viunga vya ubalozi wa Italia ili kusherehekea Siku hiyo.

Mwanamuziki  Chantal Saroldi  mwenye asili ya Italia na Tanzania  alizaliwa nchini Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro akitokea kabila la Wachaga.

Chanty yupo nchini kwa ajili ya ziara maalumu ya muziki ambapo  kesho anatarajia kutumbuiza katika hoteli ya Mediterraneo ya jijini Dar esalaam na Juni 2 atatumbuiza katika hafla maalumu inayoandaliwa na ubalozi wa Italia nchini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Taifa hilo.

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Luigi Scotto,  alisema kuwa katika kuzingatia kuwa mwanadada Chantal ni mwanamuziki mahiri waratibu wa sherehe hizo wamemchaguliwa kuja kutumbuiza katika hafla hiyo kwa kuwa ni nembo muhimu inayoziunganisha nchi mbili hizi za Tanzania na Italia.

Katika hatua nyingine mwanadada huyo alisema kuwa anajilaumu kwa kutojifunza lugha ya mama yake ambayo ni kiswahili, huku akibainisha kuwa mikakati ni  kujifunza lugha ya Kiswahili.

Mwanamuziki huyo amewahi kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo tuzo ya dhahabu katika kipengele cha uhariri na uandishi wa nyimbo ikitolewa na Disc Festival.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19902

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>