Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi Communications ilizindua muonekano mpya wa gazeti lake la Mwananchi ambapo ilifanya halfa fupi katika ukumbi wa Mlimani City, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali, vyama vya siasa, wafanyabiashara, wadau wa habari na watu mbali mbali maarufu jijini Dar es salaam. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya Katiba, Balozi Joseph Sinde Warioba. Pichani juu anaonekana Mheshimiwa Warioba (Wa pili kutoka kushoto, akishiriki katika zoezi la uzinduzi wa gazeti hilo lenye muonekano mpya, pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Bi Zuhura Muro, huku Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando(kushoto), na Meneja Biashara na maendeleo, Bw Theophil Makunga(kulia) wakishuhudia
Mhariri Mtendaji wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, ambaye kwa sasa ni Meneja Maendeleo ya Biashara akieleza kwa kina kuhusiana na miaka 13 ya Gazeti la Mwananchi na mafanikio yake kwa waalikwa
Nasaha kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw Tido Mhando
MEZA KUU: Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi, Mgeni Rasmi Mh Warioba, na Mwenyekiti wa Bodi wa MCL Bi Zuhura Muro wakiteta jambo
Mwenyekiti wa Bodi naye alisema machache
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la mwananchi, Bw Dennis Msacky(kulia), akiwa na Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya MCL, Bakari Machumu na mtaalam wa ubunifu wa kurasa Bi Kelly Frankeny
Umeona mwenyewe, hapa ni kila sehemu ya ndani imefanyiwa marekebisho
Picha na watu mashuhuri
Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma kaskazini pamoja na katibu mwenezi wa Chama Cha mapinduzi, Nape Nnauye wakiteta jambo
MCL Team
Meza kuu ilipata nafasi ya kuperuzi, ...na kudadisi...
Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari, Dk Reginald Mengi akitoa nasaha zake
kelly Frankey, mtaalamu wa miundo mbali mbali ya gazeti la mwananchi naye alipata wasaa wa kujieleza mbele ya wageni waalikwa
Kila mtu alifurahi
Mshereheshaji alikuwa Taji Liundi, moja kati ta wakongwe katika tasnia ya utangazaji
Baada ya yote, Skylight Band ikamaliza mambo kwa burudani ya Nguvu! Picha Zote Kwa Hisani ya Mdimu Blog