Na Cathbert Kajuna, Morogoro
WAANDISHI wa Habari za michezo na Maofisa mbalimbali hapa nchini, wameaswa kuhakikisha wanatumia vema mafunzo waliyoyapata katika Semina iliyofikia tamati jana Mjini Morogoro.
Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala wa Mkoa Msaidizi Lameck Noah (pichani) ambaye amewataka kufanya hivyo ili kuleta ufahamu na mabadiliko makubwa kwa wananchi mbalimbali wapenda michezo.
“Nyie waandishi ni watu ambao mnanafasi kubwa katika jamii na msipofanya hivyo michezo itadolola sana hapa nchini ili michezo yetu iweze kufikia ngazi ya Kimataifa zaidi,”alibainisha.
Noah aliwataka wanahabari kuacha kuegamia katika mchezo wa Soka pekee na kuangalia michezo mingine ambayo inaweza kuwapatia vijana ajira.
Pia aliwataka wanahabari kuachana na habari za kishabiki ususani kwa timu kongwe za Simba na Yanga na kudai kuwa inaharibu maadili ya fani yao.
Aliongeza kwa kuwaomba waratibu wa Semina hiyo, Britsh Cuncel kwa kusaidiana na Baraza la Michezo Taifa (BMT) kutoishia hapa na kuwataka kuendelea na semina kama hizo mpaka Mikoani.
Mwezeshaji wa semina hiyo toka Baraza la Michezo Taifa, Jacob Nduye akitoa machache.
“Nawaomba msiishie hapa, mwende mpaka Mikoani na nakabidhi vyeti hivi kwenu iwe ni chachu katika mabadiliko,”aliongeza.
Semina hiyo ya Siku tatu ilishirikisha waandishi wa habari za michezo pamoja na Maofisa mbalimbali hapa nchini ilianza Jumanne ya wiki hii na kufikia Tamati jana jioni Mjini Morogoro.
Waandishi wa Habari na Maofisa habari wakipokea vyeti.
Mmiliki wa Blog hii, Bw. Cathbert Angelo Kajuna akipokea t-shirt kutoka kwa wakufunzi wa semina hiyo, Sauda Simba (kushoto) mara baada ya kushinda bahati nasibu iliyochozeshwa baada ya mafunzo kuisha.
Semina hiyo iliyoratibiwa na Baraza la michezo Taifa (BMT) kwa kushirikiana na British Cuncel lilifunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro MariaMbora Nkya ambaye aliwataka waandishi kuepuka kuandika habari za uchochezi.