Vijana waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,katika kaburi alilozikwa leo katika viwanja vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi, akiongoza sala wakati wa mazishi ya Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja leo.
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi, aliyezikwa leo katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope, Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
ASkofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa leo katika viwanja vya kanisa Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Rais wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja. Picha kwa hisani ya Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.