Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19676

JAMII YAASWA KUMRUDIA MUNGU - VIONGOZI WA DINI

$
0
0
 Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki , Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa akiongoza ibada ya Krismas katika Kanisa la Mt. Joseph, jijini Dar es salaam leo.
"Shkamoo....." Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki ,Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa akipokea salam kutoka kwa mtoto,mara baada ya Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mt. Joseph,jijini Dar es salaam leo.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dk. Alex Malasusa akiwatakia heri ya Krismas sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front,jijini Dar es Salaam leo.
---
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Katoliki, Dar es Salaam Eusebius Nzigilwa amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismas  watu wafuate njia ya mungu na sio njia ya Ibilisi ambayo inafundisha maovu.

Akizungumza leo baada ya Ibada ya Sikukuu ya Krismas ,Nzigilwa alisema watu wenye uwezo lazima wasaidie wasio na uwezo kwani Yesu alizaliwa katika pango la Bethelehem lakini watu wenye uwezo walimuacha kutokana na kuwa katika njia ya ibilisi.

Nzigilwa alisema suala la kuingiziwa fedha katika akaunti yake ambazo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow hawezi kulizungumzia kwa  sasa lakini siku zijazo atazungumzia suala hilo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19676

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>