Maandamano yakiendelea barabara ya Ohio
Blass Bend ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandamano ya Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani na Miaka 66 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu. Maandamano hayo yaliyoanzia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima hadi Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam leo asubuhi yaliandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Maandamano yakiingia Makumbusho ya Taifa barabara ya Shabani Robert.
Wanaharakati Rose Mwalongo na Halord Sungusia wakipeana hi baada ya maandamano hayo kuwasili viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Ezekiel Masanja akitoa hutuba katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Profesa Geofrey Mmari.
Wawakirishi wa mashirika mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia akitoa mada katika maadhimisho hayo.
Wanakwaya wa Kwaya cha Mwalusanya ambao wapo chini ya LHRC wakitoa burudani za nyimbo za uhamasishaji.
Maofisa wa LHRC wakiwa kwenye maadhimisho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwajibikaji, Imelda Urio.
Wadau mbalimbali na wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wadau mbalimbali na wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Na Mwandishi Wetu.KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kiwango cha elimu ya haki za binadamu nchini bado kipo chini hali inayosababisha kukithiri kwa makundi ya ukatili wa kinjia nchini.
Kufuatia hali hiyo kituo hicho kinaishauri Serikali kujumuisha elimu ya haki za binadamu kwenye mfumo wa elimu rasmi inayotolewa nchini ili kupanua uelewa kwa jamii.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Kaimu Mkurungezi Mtendaji wa kituo hicho, Ezekiel Masanja wakati wa hitimisho la siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia duniani.
Akitoa takwimu za nusu mwaka dhidi ya vitendo vya ukatili wa jinsia Masanja alisema wanawake na wasichana 2878 walibakwa, vilvile vitendo vilivyoripotiwa polisi nchi nzima ni 3,633.
''Ukatili upo katika makundi mbalimbali kama vile mauaji ya vikongwe, albino watoto kubakwa lakini, ukatili, unyanyasaji ambao mara nyingi unafanywa na ndugu jamaa wa karibu ambao sio rahisi kuwatambua kwa haraka,'' alisema.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012 idadi ya watanzania waliopata elimu rasmi ni zaidi ya milioni 14 kati yao watu ni zaidi ya milioni 11 wamehitimu elimu ya msigi, wenye elimu ya chuo kikuu ni zaidi ya laki tatu 3.3.
"Hali hii inabainisha watu walio na elimu ya dhidi ya haki za binadamu ni wachache ukilinganisha na mahitaji changamoto inayotokana na mifumo ya elimu rasmi inayotolewa nchini ,"alisema.
Akizungumzia kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa mwakani alisema wananchi bado hawana uelewa wa kutosha dhidi ya katiba inayopendekezwa.
"Naiomba Serikali kutoa mwamko kwa wananchi kwa kusambaza kopi nyingi za rasimu inayopendekezwa kusudi kuwasaidia wananchi kuelewa nini wanaenda kupigia kura , "alisema.