Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

ASKOFU MKUU WA KANISA KATORIKI, MUADHANA POLYCUP CARDINAL PENGO AWAOMBA WAUMINI WAWE WATULIVU, ASEMA MAREHEMU PADRI MUSHI KUZIKWA FEBRUARI 20, 2013

$
0
0
Kanisa katoliki nchini limetoa tamko kufuatia kifo cha Padri Evaristus Mushi, ambapo limewataka waumini wa kanisa hilo popote walipo kuwa watulivu na kufanya maombi ya amani kwa nchi katika kipindi hiki cha maombolezo.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki nchini Muadhama Polycup Cardinal Pengo amesema kifo cha Padre Mushi ni pigo kwa kanisa na Taifa kwa ujumla na ni ishara ya kutoweka kwa amani hivyo suala hilo linapaswa kufanyiwa kazi mapema kabla halijasababisha madhara zaidi kwa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Cardinal Pengo amevitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kuwatia mbaroni wote waliohusika na mauaji hayo.

Cardinal Pengo  amesema viongozi mbalimbali wa kanisa katoliki wataungana na waumini wengine February 20 mwaka huu katika mazishi ya Padre Mushi huko Zanzibar huku misa kubwa ya kuomba amani ikipangwa kufanyika siku hiyo katika kanisa katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19575

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>