Quantcast
Channel: HABARI NA MATUKIO
Viewing all articles
Browse latest Browse all 19576

ZAIDI YA WAGONJWA 250 WAKOSA HUDUMA KUTOKANA NA KUFUNGWA KITUO CHA TIBA ASILIA CHA FOREPLAN KILICHOPO ILALA BUNGONI, DAR

$
0
0
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Zaidi ya Wagonjwa 250 wamekosa huduma kutokana kufungwa Kituo cha Tiba Asilia cha Foreplan kilichopo Ilala bungoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumuza na Kajunason blog ofisini kwake Mmilikiwa wa kituo hicho Dk Juma Mwaka amesema kwamba kituo hicho kilifungwa bila ya yeye kupewa nafasi ya kujieleza kama sababu walizoleta zipo sahihi au si sahihi.

Aidha Dkt Mwaka amesema kwamba suala hilo alilipeleka katika vyombo vya sheria na mahakama iliamuru kituo hicho kifunguliwe lakini bado hadi sasa wafungaji hao hawajafungua kituo hicho.

Kwa upande wa Mratibu wa Taifa wa tiba asilia na mbadala katika Idara ya Tiba Wizara ya Afya Dkt Liggy Vumilia amesema kwamba walimhushisha kuhusiana na mapungufu yaliyopo katika kituo hicho kabla ya kufungwa kna sababu kubwa ya kufunga ni kutangaza huduma ambazo anatoa jambo ambalo amesema lipo kinume na sheria kwa sekta hiyo kujitangaza.

Kituo hicho kimefungwa toka tarehe 6 ya mwezi huu na hadi sasa suala hilo lipo mahakamani ambapo sababu kubwa ya kufungwa kwa kituo hicho ni kujitangaza pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho kutokuwa na sifa za kufanya kazi hapo jambo ambalo Mmilikiwa kituo hicho amepinga madai yao kuwa hayana mantiki.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 19576

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>