Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar.
Wito umetolewa kwa wananchi nchini kuichangia sekta ya elimu na sikuichaia serikali peke yake ili iweze kutoa wanafunzi bora na wenye uwezo mkubwa kielimu na kijamii.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Jenista Mhagama wakati akiwatunuku hati za utambuzi wachangiaji wa miradi ya elimu nchini leo jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mhagama amesema kwamba anatumaini utaratibu huo wa uchangiaji elimu utapokelewa vizuri na mashirika, kampuni, Taasisi na watu binafsi ambao bado hawajachangia wachangie ili kuongeza upatikanaji wa elimu na maendeleo ya kweli kwa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Rosemary Lulibuka amesema kwamba wachangiaji hao waliotunukia hati hizo watapata faida mbalimbali ikwemo punguzo la kodi kwa wale wanaofanya biashara.
Naye mwakilishi wa shirika la nyumba Tanzania (NHC) Rosemary Omary ambao wao ni moja ya kampuni zilizo tunukiwa hati hiyo amesema kwamba wao kama jamii waliguswa na suala zima la ujenzi wa mabweni ya watoto wakike na wakanunua mabati ya shilling million 20.
Mfuko huo ulianzishwa kupitia sheria ya bunge namba 8 ya mwaka 2001.