Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema wakimsikiliza miliki wa Nyumba ya kulala wageni United State na bar, Laurent Kasiga iliyopo Mbagala Rangi tatu, Dar es Salaam ambayo iliteketea kwa moto uliotokana na roli la mafuta lililopinduka na kuwaka moto wakati vijana wakiiba mafuta.
Mkuu wa Moa akikagua Nyumba hiyo ya kulala wageni iliyokuwa na vyumba 32.
wananchi wakiangalia athari za moto huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiangalia tenki la lori hilo.
Lori hilo lilivyoteketea kwa moto uliosababishwa na mshumaa.
Moja ya maduka ya vifaa vya pikipiki lililoteketea
Wafanyabiashara wa mchele waliokuwa na fremu katika eneo hilo wakiwa katika majonzi baada ya mzigo wao kuungua moto na kuharibika kabisa.
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar.
Watu wa tano wamethibitishwa kufariki dunia kufuatia na ajali ya moto iliyotokea jana maeneo ya Mbagala baada ya lori la kubeba mafuta (PETROLI) kupinduka.
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo kamishna wa polisi kanda maalum, Suleiman Kova amesema kwamba lori hilo lilibeba kemikali aina ya petrol lita 38 elfu yenye thamani ya Dolar elfu 36 na lilikuwa linaelekea Kamapala, Uganda.
Aidha kamanda Kova amewatoa hofu wazazi kuhusiana na Uvumi wa gari aina ya Noah kuhushwa kuwateka watoto wadogo amesema kwamba hakuna jambo hilo ni uvumi tu na Mtu mmoja wanamshilikia kwa kusambaza taarifa hizo zinazowatia hofu wananchi kwa sasa.
Hata hivyo ajali ya moto iliyotokea jana imesababisha kuunguza nyumba ya wageni iliyopo Mtoni Mtongani, kuteketea kwa pikipiki saba pamoja na maduka matano ambapo thamani ya vitu vilivyopo kwenye maduka hayo ni Shillingi million 197.