Zaidi ya dollar laki moja zimetolewa kwa makampuni manne ya kitanzania kwa kuendeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini.
Pesa hizo zimetolewa baada ya kufanyika kwa mashindano mashindano katika kampuni za watu binafsi ambapo kampuni mia tatu zilishindanishwa.
Akizungumza mara baada ya kutoa zawadi hizo Waziri wa nishati na madini Proffesa Sospeter Muhongo amesema kwamba kwasasa wanashirikiana na Marekani katika miradi hii midogo ambayo inafanyika katika vijiji vya ndani.
Naye Mkurugenzi wa Tanesco Injinia Felchesmi Mramba amesema kwamba kwasasa wamejipanga zaidi kupeleka umeme vijijini kwa kushirikiana na makampuni binafsi.
Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Lung’ali Natural Resources ambayo ni moja ya washindi Padre Luciano Mpoma amesema kwamba kwasasa wataweza kuhudumia vijiji 15 vilivyopo mkoa wa Iringa na hadi sasa wamefikia asilimia 88 kumalizia mradi huo.
Hii ni mara ya kwanza Tanzania kushiriki katika shindano hilo la Power Afrika Off-Grid energy ambapo Washindi waliochaguliwa walionesha biashara mpya ya kutoa nishati endelevu kwa wakazi wa pembezoni mwa miji mikuu.
Kampuni zilizoshindani Jamii Power Limited, L’s Solution Limited, Lung’ali Natural Resources Company Limited na Space Engineering Company Limited