Mkemia Alfred Aloyce kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sampuli ya jiwe la dhahabu iliyotayarishwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara ili kubaini kiasi cha madini ya dhahabu kwenye jiwe hilo.
Meneja wa Maabara kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) Mhandisi Mvunilwa Mwarabu akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mashine ya kupimia kiwango cha madini inayoitwa Atomic Absorption Spectroscopy (AAS) walipotembelea Maabara ya Wakala huo jijini Dar es Salaam jana.
Madini ya ujenzi aina ya kokoto zilizo tayari kwa matumizi ya ujenzi wa aina mbalimbali. Kupitia TMAA Madini hayo kwa sasa yanaipatia Serikali zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa mwaka.
Waandishi wa habari waliotembelea ofisi za Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) wakipata maelezo kuhusu mafanikio ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini katika ukusanyaji wa mirabaha ya madini kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa wakala huo Bw. Bruno Mteta.
Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Usafirishaji kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) Bw. Conrad Mtui akiwaeleza waandishi wa habari mikakati ya ukusanyaji wa mirabaha ya madini ya ujenzi wakati walipotembelea kituo cha ukaguzi wa madini hayo kilichopo wilayani Bagamoyo.
Mashine ya Kuyeyusha sampuli za Madini(Fusion and cuppelation Funances) inayotumika kwenye Maabara ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA)
Picha na Fatma Salum-MAELEZO
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Jumla ya shilling billion 5.2 za kodi katika madini ya ujenzi nchini zimeokolewa kwa kukusanywa na Wakala wa Ukaguzi wa madini Tanzania (TMAA) kutoka mwaka 2009 hadi hadi sasa.
Hapo awali fedha hizo zilikuwa zinapotea kutokana na kuwasubiri wachimbaji wenyewe wajekulipa jambo ambalo lilileta udanganyifu mkubwa katika ulipaji kwani kwasasa kwa upande wa kanda ya mashariki.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Udhibiti na Ukaguzi wa Madini Injinia Conrad Mtui wakati wa ziara na waandishi wa habari ya kwenye Mgodi wa Madini ya Ujenzi huko lugoba Mkoani Pwani.
Aidha Injinia huyo amesema kwamba wampata mafanikio makubwa kwani baadhi ya migodi mikubwa kama Geita Mining Limited, Kampuni ya Resote Tanzania Limited ,Pangae Minerals limited na Wiliamson Diamond Limited inayomiliki mgodi wa almasi wa Mwadui kuanza kulipa kodi jambo ambalo Taifa litazidi kuongezeka katika mapato.