Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje.
Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima kabla ya kuondoka nchini kuelekea Hague
Ruto ambaye ni rais kwa muda naye pia anakabiliwa na kesi katika mahakama hiyo ya ICC.
Mawakili wa Kenyatta wanasema kuwa kesi hiyo inapaswa kufutiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
Majaji wa mahakama hiyo hata hivyo watathmini kauli kutoka kwa pande zote mbili. Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa pia kutangaza tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Kenyatta.
ICC imemtaka Kenyatta kujibu madai ya upande wa mashitaka kuwa Kenya inakataa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu kesi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye atakuwa rais wa kwanza aliye mamlakani kufika mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu anazodaiwa kutenda baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Mahakama hiyo inasama kuwa Kenyatta alihusika katika kupanga na kufadhili ghasia za kikabila baada ya uchaguzi uliozua utata mwaka 2007/08 Zaidi ya wakenya 1,000 waliuawa kwenye gasia hizo.
Mwezi Septemba, mahakama iliahirisha kesi dhidi ya Kenyatta baada ya upande wa mashitaka kusema kuwa Kenya imekosa kutoa ushahidi unaotakikana na mahakama hiyo.
Mashahidi wa upande wa mashitaka wamejiondoa katika kesi hiyo. Mamia ya wabunge wa Kenya wanatarajiwa kuambatana na Kenyatta kama ishara ya kumuunga mkono.